Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu) Mhe. Joyce Ndalichako amesema kuwa malalamiko ya wafanyakazi kuhusu makato ya mishahara yao yanashughulikiwa kwa kuwa serikali sikivu ya awamu ya 6 imesikia kilio chao.
Waziri amewataka wafanyakazi kuviamini vyama vyao kwa kuwa vimewasemea vizuri na sasa wataangalia upya makato haya ya tozo.
Amesema kuwa serikali itakuja na jawabu sahihi, waondoe wasiwasi na waendelee kuchapa kazi kwani hoja zao zote zitafanyiwa kazi.
Ili kusisitiza hoja hii, waziri ametanabaisha kuwa serikali iliwapandishia madaraja tena kwa mserereko na baadhi iliwabadilishia muundo wao wa kazi. Amewaomba wafanyakazi wote kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuijenga nchi.