Rais Samia: Sitangazi hadharani kiasi cha Ongezeko la Mshahara ili wafanyabiashara wasipandishe bei

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) leo tarehe 01 Mei, 2023 mkoani Morogoro.



Rais amewasili uwanjani akiambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson pamoja na Viongozi wengine wa Kiserikali na Vyama vya wafanyakazi.

Kauli Mbiu ya mwaka huu ni Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi. Wakati ni Sasa.”

Kinachoendelea sasa ni maandamano ya vyama vya wafanyakazi wanapita mbele ya Rais na Meza kuu wakiwa na Mabango yenye jumbe mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa anazungumza;
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa amesema tangu Rais Samia aingie Madarakani, wafanyakazi 7108 mkoani humo wamepandishwa madaraja huku wengine 2030 wameajiriwa kupitia ajira mpya na kibali kingine cha kuajiri watu 3861 tayari kimeshatolewa.

IMG_6991.jpeg

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Abubakar Mwassa
Aidha, mkoa huo kwenye mwaka huu wa fedha umepanga kuanzisha ranchi mpya 4 pamoja na kufufua mashamba mengine makubwa ili kuongeza ajira kwa vijana.

Amemshukuru Rais Samia kwa uongozi mzuri na anatumaini chini ya Utawala wake Maslahi ya wafanyakazi nchini yatazidi kuboreshwa.

Katibu Mkuu wa TUCTA anazungumza;
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Hery Mkunda amesema wafanyakazi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa jitihada anazofanya Rais Samia kwenye nyanja zote za maisha.

IMG_6990.png

Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi TUCTA, Hery Mkunda
Amesema Kauli Mbiu ya mwaka huu waliibuni kuonesha nia ya kuwawezesha wafanyakazi wapate haki zao, mikataba ya ajira na mishahara iliyo bora ili kuongeza tija na ufanisi kwenye maeneo ya kazi.

Kwa niaba ya Wafanyakazi, amemshukuru Rais Samia kwa kufanya mambo makubwa yanayowagusa. Ametoa ahadi ya kuendelea kuwa watiifu huku wakijituma kwenye maeneo ya kazi.

Mwaka jana ongezeko la Mshahara lilikuwa 23.3% likigusa wafanyakazi wa kika cha chini cha Mshahara, amesema wanaendelea kupiga magoti na kubisha hodi ili aendelee kuwafikiria.

Ameomba kitengo cha Idara ya Kazi kilicho chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kiboreshwe na kuongezewa wafanyakazi, ameishujuru Serikali kwa kuboresha afya kwa watanzania kupitia mpango bima ya afya kwa wote.

Rais Samia anazungumza;
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewashukuru waandaji wote wa Maadhimisho ya mwaka huu kwa kuwezesha yafane na yaende kama yalivyopangwa.

Amesema Mei Mosi ni siku ya kutambua mchango na kutoa heshima kwa wafanyakazi kwa kazi kubwa wanayofanya ndani ya taifa. Umadhubuti wa Taifa hili upo kwa sababu ya wafanyakazi.

Pamoja na kudai mishahara bora, uadilifu na weledi kazini ndio utaleta maisha bora kwa wafanyakazi.

Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya kazi serikalini na katika sekta binafsi zipatikane ajira zenye usalama na ajira za staha kwa wote. Pia, madai yote ya mwaka jana yametekelezwa kwa zaidi ya 95%

Rais Samia amesema pia nyongeza ya Mishahara ya mwaka sasa itarejeshwa, watu watapandishwa madaraja na vyeo pamoja na kuongeza posho japo hatasema hadharani ataongeza kwa kiasi gani.

Amesisitiza “Kwa hiyo ndugu zangu wafanyakazi, kile watu walichozoea tukiseme hapa ili wapandishe bei madukani mara hii hakuna, tunakwenda kufanya mambo polepole, kupandishana jinsi tulivyosema, wasione tumeongezeana kitu gani ili mwenendo wetu wa bei uwe salama. Kwahiyo mambo mazuri yapo, ila hatutayatangaza hapa”

Kuhusu malalamiko ya makato ya kodi, Raia Samia amesema hilo ameliacha kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi na Mawaziri husika ili walitazame kwa pamoja na kulipatia majibu.

Baada ya Mkutano huu, Waziri Mkuu atazungumza na waajiri ili kutatua kero ya uwasilishaji wa michango ya wanachama.

Madai ya malipo ya Bima yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 kama sheria inayotaka ili wafanyakazi wanufaike.

Akizungumzia kuhusu Maslahi ya walimu upande wa teaching allowance, Rais Samia amelichukua na ataenda kulifanyia kazi, pia amemuagiza Waziri wa Elimu kuhakikisha walimu wanapewa mafunzo ya matumizi sahihi ya vishikwambi walivyopatiwa, na utaratibu unafanyika ili baadae kila mwalimu awe na kishkwambi chake.
 
Leo kwa kweli naona tofauti nikiangalia Mei mosi za jiwe na hili la mwaka hii ni kimbuga

Rais ni mfariji na mtia moyo ingawa hata kama hali ni ngumu

Mimi sitegemei makubwa sana lakini kwa kutumia maneno matamu watu hufurahi

Kitu kimoja ambayo siipendi mshahara haja ongeza na madaraka siyo hisani ya Rais

Lakini kama angeongeza mishahara alistahili sifa hizi.

Jambo moja kwa walimu sikuipenda badala ya kuweka bango la kikokotoo wao wanasema Sema neno 2025

Lakini pia tuseme tu watumishi Wana imani sana na Rais hilo linaonekana kwa wazi
 
Back
Top Bottom