Nchi yangu Tanzania kwa nini naipenda ikiwa chini ya JK

mambomoto

JF-Expert Member
May 10, 2011
326
236
Kwa sababu zifuatazo

  1. Ni nchi yangu ambayo ukiongelea Ufisadi unahatarisha amani na utulivu.
  2. Ni nchi ambayo rasilimali za nchi zinaibiwa mkihoji kwa nini mtaambiwa mnahatarisha amani na utulivu
  3. Ni nchi ambayo milipuko kambi za jeshi inaua raia mkihoji mtaambiwa mnahatarisha amani na utulivu
  4. Ni nchi ambayo viongo wanakwiba mali za umma kwa wingi mkiuliza mtaambiwa mnahatarisha amani na utulivu
  5. Ni nchi ambayo bunge chini ya chama tawala miswada inapitishwa kwa ushabiki wa chama na si maslahi ya umma ukiuliza unahatarisha amani
  6. Ni nchi ambayo Rais ameonekana kushindwa na hajui kwa nini watu wake ni maskini mkiuliza mtahatarisha amani na utulivu
  7. Ni nchi ambayo wezi kama wa EPA wanaambiwa warudishe pesa na mkiuliza mnahatarisha amani na utulivu
 
Nchi ambayo ni shamba la bibi,wageni wakitakakuchukua madini,wanyama pori,magogo na gesi wanachukua kiulain tu.! Bila masharti.
 
Nchi pekee ambayo serikali ina mzigo wa kuwazika kwa nguvu hata ndugu wa marehemu "majambazi" kwa kudaiwa walivamia mgodi lkn wezi wa mabilioni ni watuhumiwa tu walisahaulika!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Du!!!!!!!!!
 
nchi ambayo asilimia themanini ya wananchi wake hasa waishio vijijini ni mbumbumbu wasiojua kusoma na kuandika na ndio hao wanaorubuniwa wakati wa chaguzi. Ukiuliza unahatarisha amani na Utulivu.
 
Back
Top Bottom