Uongozi, hatima ya nchi

raiswenu

JF-Expert Member
Apr 20, 2018
794
1,429
Nakumbuka siku ya tarehe 17/02/2024 nilikuwa nimekaa nikitazama luninga, kunatukio lilikuwa linaendelea, nilikuwa nikiangalia tukio hilo kwa huzuni, tukio hili lilinikumbusha miaka 24 iliyopita, kipindi nipo mdogo kabisa kijiji kizima tulikuwa tumekusanyika kwa bwana mmoja pale kijijini ambaye ndiye pekee alikuwa anamiliki luninga, watoto, vijana kwa wazee tulikuwepo pale kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, nchi yote ilikuwa katika simanzi, watu waliacha shughuri zao ili kuomboleza msiba wa mtu tuliyempenda sana.

Kwa sasa tumepitia hali kama hii mara kadhaa kwa kuondokewa na wapendwa viongozi wetu, lakini pamoja na kuondokewa na viongozi hao nchi bado ipo na mara wanapoondoka nchi inapata viongozi wengine, viti walivyovikalia vinapata watu wengine wa kuvikalia, hapa tunapata ujumbe gani? Viongozi ni binadamu, watapita, ila nchi itabakia, madaraka yatakwisha ila nchi itabaki.

Kwa mantiki hiyo basi uongozi ni nafasi aliyopewa mtu kuleta mabadiliko katika jamii yake (A leader is one who knows the way, goes the way and shows the way-John C. Max). Inawezekana kabisa siku moja hiyo nafasi ukapewa wewe unayesoma uzi huu, na ndio msingi wa mimi kuandika uzi huu na siyo kuzungumzia vifo vya viongozi. Ila ni kukumbusha mambo kadhaa kabla mwisho wako haujaja kama waliokutangulia.

Kuna msemo unasema “Good men must die, but death can not kill their names.” Kufa au kuishi kwa jina lako kunaanza pale watu wanaposambaa kwenye kaburi lako. Siku hizi kijana akiingia kwenye ofisi ya umma, anataka atajirike ndani ya muda mfupi sana, na hata ukisikiliza mazungumzo yao iwe chuoni au katika vijiwe vya kahawa, utaona mitazamo yao, ni upigaji mwanzo mwisho, kwa kifupi hata jamii yenyewe kiongozi ambaye ni mwizi anaonekana ndio mjanja kwenye macho ya jamii hii ambayo imekosa elimu sahihi, na hata akitokea kiongozi ambaye anamisimamo inayoenda tofauti na wizi na ufujaji wa mali ya umma, atapigwa vita na hakuna atakaye kuwa tayari kumlinda.

Kwenu wadogo zangu, viongozi wa kesho, hata ujikusanyie mali nyingi kiasi gani, kuna siku utaziacha huku nyuma watu wakizitumbua, lakini pia utaacha jina baya ambalo hakuna atakaye taka kulisikia, na hutakuwa na msaada kwa jamii yako.

Kumbuka wewe ni wa mda mfupi ila nchi ni ya milele, kwa kifupi uhai wako una kikomo ila uhai wan chi hauna kikomo, Kwa kifupi kama maisha yako hayana manufaa kwa nchi yako na jamii yako bora hata usinge zaliwa, unamkumbuka Mobutu Sese Seko aliye itawala Zaire akisaidiwa na Marekani kuanzia mwaka 1967 hadi 1997 ambaye makampuni ya uchimbaji wa madini yalikuwa yanamfanyia muamala kwenye akaunti yake binafsi ya benki kama malipo ya ushuru, ambaye mpaka anafariki anakadiliwa kuwa na utajiri wa dora za kimarekani kati ya bilioni 1 hadi 5, ambaye pesa zake nyingi zilifia kwenye mabenki ya nje huku yeye akizikwa genini na watu wachache huku washirika wake wakishindwa kushiriki mazishi, kwa kifupi mazishi yake hayakuwa na hadhi ya kiongozi wa taifa.

Unamkumbuka Moise Kapenda Tshombe aliyejitwalia uongozi katika Jimbo la Katanga lililokuwa na utajiri wa madini ya shaba, tin na Uranium, huku akipewa ulinzi na uberigiji na Ufaransa na huyu ndiye alimshikilia Patrice Lumumba (R.I.P) hadi mauti yanamkuta, mwisho wa siku aliondoka akiiacha Congo yenye vita vilivyogoma kuisha. Mifano ipo mingi

Jitathmini basi kabla hujawa kiongozi. IFANYIE KITU NCHI YAKO, MAANA WEWE UTAPITA NCHI NA VIZAZI VYAKO VITABAKI. Mpumzike Kwa amani viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom