Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,756
Kuanzia wakuu wa vyombo vya usalama, idara, wasomi wabobevu plus thinktanks na manguli wa hoja mitandaoni na jamii wamejikita kwenye vision ya NANI ATAGOMBEA 2025, wengine akina Pascal Mayalla wameenda mbali zaidi kutabiri ama.kujadili nani anafaa kugombea 2030.
Kiashiria kikubwa cha nchi iliyokosa muelekeo ni kama yanayoendelea Tanzania. Wasomi wanajivua utu wao kwa kushabikia ama kufanyia uchawa wa wagombea na possibly contestants. Hebu angalia hii video hapa chini uone aibu kidogo
Hatuna vipaumbele zaidi ya kurasa za ilani ambazo zimekaa kisiasa zaidi ya utaalam. Hatuna serza za taifa bali za vyama. Hatuna taasisi zinazosimama kama nchi bali zote ni matawi ya chama tawala.
Miradi kama SGR, MNHP na kadhalika imetawaliwa na mitaguso ya kisiasa ambapo badala ya kujikita kufanikisha tunaangalia inamjengaje mtu aweze kugombea tena.
Watu kama Lucas mwashambwa wanahesabiwa uzalendo wao kwa kuishi kama machawa waandamizi.
Nchi haina hata kiwanda cha kutengeneza sindano za kushonea, hatuna viwanda vya baiskeli na tumebaki tunaagiza mitumba na kuwauzia wananchi, nchi yenye madini ya quartz haina hata kiwanda cha kutengeneza kifaa chochote cha simu, hatuna viwanda vya pembejeo mtambuka za kilimo. Nchi inayoendeshwa kwa kushindanisha wanafunzi kupitia mitihani badala ya kupambanisha fikra bunifu kwa maendeleo mtambuka.
Nchi ambayo inatumia pesa nyingi kuagiza silaha huku ikiweka sheria kali dhidi ya raia anayeonekana anaweza kufanya ubunifu wa silaha......
Tuna wataalam wengi wa tiba mbadala na wapo treated kama walozi badala ya kuwa na programs za kuzalisha dawa zetu na wakayi huo huo soko la tiba limejazwa na dawa za asili kutoka nje ambazo zimekuwa packaged na endorsed na serikali zao.
Hii nch imepoteza mwelekeo kama Taifa, tunaishi kama kikundi cha watu wasiojitambua wanaoongozwa na wasiojitambua waandamizi. Yaani inafika mahala kila anayekosoa fikra za watawala anageuzwa kuwa muasi na adui wa taifa na tishio la usalama wa viongozi ambao kimsingi ni mzigo kwa Taifa. Angalia sheria lukuki kandamizi ikiwemo ya Makosa ya Mtandao na zinginezo zinazotoa haki kwa viongozi bila kuwawajobisha.
Hatuna la kujivunia zaidi ya Amani ambayo serikali imeshindwa kutumia amani hiyo kulileta Taifa pamoja na kuchechemiza maendeleo na uhuru kamili wa kifikra.
Teuzi zote anazofanya mkuu wa nchi zinaelemea kwenye KUSAIDIANA kuondoa hofu ya kupata mpinzani wa ndani.
Tuna Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo kisheria wanalazimika kuwa watii kwa chama na siyo kwa wenye nchi. Tuna jeshi la polisi ambalo linatumika kisiasa tofauti na kikatiba, limekuwa linaua ua raia watakavyo bila kuwajibishwa. Mataifa jirani (Rwamda) wanaingia nchini watakavyo na kuwanyakua wakimbizi waliokimbia kukandamizwa huko kwao, na haya yanafanyika mbele ya taasosi zetu za ulinzi na usalama. Hautakaa usikie Balozi wa Rwanda au yule wa Palestina ambaye anahamasisha chuki kupitia nyumba za ibada in their favor wakiitwa kujieleza ama hatua kuchukuliwa.
Rais anasimama kwa kujiamini kuwananga raia anaowaongoza ambao yeye ni sehemu yao kwamba HAWANA UFAHAMU KUHUSU KATIBA. Ujasiri huo unatokana na nchi kupoteza muelekeo maana kauli hiyo ilipaswa kuhojiwa na Bunge (oops halina guts hizo).
Mtanzania mwenzangu, ni mambo gani zaidi unayaona kama ashirio kuwa Tanzania inayumba kama nchi?
Ukitaka kuishi vizuri Tanzania hakikisha unakuwa chawa pro max wa mtawala mkuu na wasaidizi wake hakika mema ya nchi yatakuwa kwako