Namna ambavyo Uhuru wa nchi za Afrika umepoteza uhalisia wake

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Umofia kwenu

Tatizo kubwa la Afrika lilianzia pale wale waliopigania UHURU wa nchi hizi kujipa nafasi ya utakatifu na kuamua kujimilikisha nchi wao, jamaa zao na vizazi vyao.

Uhuru wa nchi za Afrika ni Uhuru wa Viongozi kujifanyia watakavyo bila kuwajibika wala kuwajibishwa popote na yeyote.

Majeshi na Usalama wa Afrika maana yake ni ulinzi na usalama wa viongozi ama watawala. Wamekuwa ni programmed robots kufuata kila amri ya mtawala ama kiongozi wa nchi husika bila kujali wala kutafakari athari zitakazojitokeza kwenye muktadha mzima wa uhuru, usawa na haki. Leo tunajadili NIA ya rais wa Senegali kuhairisha uchaguzi ambao ulipaswa kufanyika March lakini akausogeza hadi Desemba 15 na hali hiyo imezua sintofahamu kubwa sana nchini kwake. Tumeshuhudia wanausalama wa nchi hiyo wakiwakamata wabunge na viongozi wa kisiasa wanaopinga amri hiyo wakiwa Bungeni live.

Tunashuhudia nchini Tanzania ambapo, Baada ya uhuru tukaunda mfumo wa kifo wa CCM ambapo rais anayetokana na chama hiko amepewa na Katiba ya Nchi nguvu za kipekee za uungu za kujiamulia chochote na kufanya lolote bila kuhojiwa wala kuwajibishwa na yeyote. Hata zile haki za raia za kikatiba zimekuwa zikitolewa kama fadhila huku sifa na utukufu vikienda kwa rais kuwa ndiye ameridhia jambo ambalo Katiba imeweka wazi kuwa ni Uhuru na Haki za raia.
Mfano,
  1. Kwa amri ya rais anaweza kuruhusu ama kuzuia maandamano,
  2. Kwa amri ya rais anaweza kuruhusu ama kuzuia mikutano ya kisiasa nchini
  3. kwa amri ya rais anaweza kuzuia ama kuruhusu TAKUKURU kushughulikia mafisadi wanaomulikwa na ripoti ya CAG
  4. Kwa amri ya rais anaweza kumtoa mkuu wa mhimili kama Bunge madarakani kwa sababu ya kuhitilafiana kauli ama mitazamo ya kitaifa
  5. Kwa amri ya rais asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao inayotoa nafasi za uhuru wa maoni, kuwa na utambulisho feki ili kujilinda dhidi ya vikosi halali vya serikali ambavyo havilali vikiwasaka wanaokosoa legacy ya rais.
  6. Kwa amri ya rais anaweza kuamuru mtu kufunguliwa shtaka lolote hata kama hakutenda kosa hilo ama akalifuta atakavyo yeye.
  7. Kwa amri ya rais anaweza kuamua kuruhusu ama kukatalia bajeti halali iliyopitishwa na Bunge kutekelezwa ndiyo maana mpaka wasaidizi wake waandamizi hawaishi kumtukuza kwa kuwapatia fedha (ya umma) kukamilisha jambo fulani. tumeona hilo hata kwenye msiba wa Laigwanan Lowassa ambapo Fredrick Lowassa aliuambia umma kuwa familia inamshukuru sana rais kwani alisababisha maisha ya baba yao yawe marefu zaidi ya uhalisia.... Tumeona kwenye kauli za mawaziri, wabunge na hata waandamizi wakiwaambia wananchi kuwa hela zao za kodi zinazotumika kwenye maendeleo zimetolewa na rais.
ukifuatilia kwa umakini, utagundua kuwa kuna mambo mengi sana Afrika yanaikwamisha kusonga mbele. Kinachotakiwa sasa ni uwepo wa Katiba ya Wananchi ambayo kila kiongozi anayeapa anapaswa kuitunza, kuilinda na kuwajibika kwa katiba, Pia katiba za nchi za Afrika hususan Tanzania zinapaswa kuwepo na kipengele cha ulinzi wa Katiba ili kuondoa ombwe la kukosekana kwa utawala bora.

Tanzania, kupitia Katiba yetu ya sasa tumetenganisha vyombo vya ulinzi na usalama visishiriki siasa lakini kwa uwazi tena mchana kweupee CCM chini ya rais kumekuwa na matumizi ya vyombo vya dola kuingilia michakato ya kisiasa na ambapo tumeshuhudia hata teuzi za kisiasa zikitolewa kwa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa madarakani ama kustaafu.

Leo, ukisimama ndani ya Tanzania na kusifia viongozi wa juu wa kisasa hususan chama tawala unaonekana ni mzalendo hata kama kiongozi ama viongozi hao hawafai kuendelea kushika ofisi za umma kutokana na misconducts zao. Ukienda kinyume na mawazo ama mtazamo wa watawala utaitwa kila majina n a unaweza hata kufilisiwa ndani ya Tanzania

Afrika iamke
Afrika ijivumbue
Afrika isimame kama mzazi
Afrika iwakumbatie watoto wake

Msanii

CC: Retired Erythrocyte Lucas mwashambwa raraa reree min -me Chizi Maarifa dronedrake Pascal Mayalla MalcolM XII Paul Alex Papaa Mobimba BIG Africa To yeye
 
Back
Top Bottom