Ipo hivi, niliingia mgogoro mkubwa na mke wangu chanzo ni kuwa; kuna siku nilikuwa nimekaa sitting room simu yangu ipo mezani mara sms ikaingia wife akawa ameona akaenda kuchukua simu ili asome, mie nikawahi nikampokonya simu kabla hajasoma nikihofia inaweza kuwa ni sms kutoka kwa mchepuko.
Baada ya hapo alikasirika sana akahama na chumba, ikapita wiki tukiwa hatuongei akawa amepata safari kikazi ya wiki moja. Akiwa huko tukawa tunasalimiana kwa simu huku akijulia watoto hali lakini cha kushangaza aliporudi tu akabadilika akawa tena haongei na mimi na anaendelea kulala kwa watoto.
Sasa kuna siku akiwa anaoga nikaenda kuchukua simu yake nilichokiona kimenikatisha sana tamaa. Nikakuta SMS akichati na mtu ambaye nahisi waliokuwa nae huko alikokuwa ameenda wakiitana kabisa wapenzi, sikuweza kumuuliza kwakuwa tulikuwa hatuongei.
Baada ya mwezi suluhu ikapatikana ndipo nikamuuliza kuhusu hiyo SMS, kwakweli alikuwa mkali sana alibaki kuniambia unafikiri kila mtu anawaza umalaya kama wewe na nitarudi tena kulala kwa watoto ukiendelea kuniudhi na nani kakwambia ushike simu yangu?
Ilibidi nibaki mpole na kuanzia hapo anaficha simu hataki niiguse, pia kanitamkia kuanzia sasa sitashika simu yako na wewe usiguse yangu.
Kwakweli siku zinayozidi kwenda naona namchukia na yale mapenzi tuliyokuwa nayo hayapo tena. Nikiwaza watoto nashindwa kufanya maamuzi maana tuna watoto wanne.
Naombeni mnipe njia ya kupitia changamoto hii.