Nawezaje kuwa na tabia ya mkono wa birika? Natoa sana kwa watu na nahonga sana. Uhongaji utanifilisi

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,465
17,306
Wakuu habari za jioni.

Wakuu naomba kukiri mimi usingekua uhongaji labda ningekua namkaribia msukuma kwa mpunga lakini sijui ni pepo nimelogezewa la kuhonga ama namna gani.

Wakuu, inapokuja swala la kuhonga kwa kweli hua sijiulizi mara 2, kama ninacho natoa tu.

Hili sio kwa wanawake tu, hata kwa watu wengine, nikiwa nacho natoa sana kwa watu. Nadhani nimekua na roho nzuri kupita kiasi, mimi sio mtu wa kumuomba kitu ninacho nikakunyima. Hata nikijikaza nikakunyima roho itaniuma sana.

Na mbaya zaidi naona kama kuna watu wananijua na wana take advantage of my kindness. Nimekua too kind na I can't help.

Wakuu naombeni msaada hii tabia ya kutoa na kuhonga sana inanimaliza. Nawezaje kua na mkono wa birika.

Ahsante.
 
Hakuna atakaeweza kubadili moyo au tabia yako kwa maneno machache ya jf Ila kama Mungu akikupa nafasi ya kujua rangi halisi za watu. Utajuta hata kwa nini uliwahi juta kwa watu wasio na utu

Mkuu katika hii dunia, kila binadamu ni mwema na mzuri kwako pale unapowafaidisha hivyo, wanyime au uwaombe wao kama hutojiona mjinga kwa kudhani kila mtu ana moyo kama wako
 
Fanya kitu kimoja hii ni kwa ndugu zako au marafiki.

Akikuomba 1000 mpe 400 atakasirika achana nae.

Akitaka kukukopa 50000 mpe 20000 yaani pesa unayoombwa usitoe yote au nusu yake wewe toa pungufu.

Ukiweza hapo basi umewin mchezo.

Mademu sio wake zako sasa hiyo ni jukumu lako na akili yako wala haitakiwi kuepo na Coacher wa kukufundisha.

Mtu ambaye unatakiwa umpe pesa yote ni mkeo tu na sio vinginevyo.

Kwa mzazi labda kama upo peke yako kwakwe ndio unaweza kufanya hivyo lakini kama mpo wengi wala usitoe pesa yote hata kama unajiweza vipi kwamaana utaleta ubaguzi na chuki kwa ndugu zako.

Mimi ishanikutaga hiyo mambo lakini kwa sasa naendelea na hilo darasa la kutoa pesa pungufu.

Nilikuwa ni muongaji mzuri sana kwa malaya.

Na nilikuwa mtoaji sana kwa ndugu na marafiki lakini kwa sasa asee hahahahhahha ULIMWENGU UNAZUNGUMZA NA SISI TUWE MAKINI KATIKA UTOAJI WETU WA PESA.
 
Hakuna atakaeweza kubadili moyo au tabia yako kwa maneno machache ya jf Ila kama Mungu akikupa nafasi ya kujua rangi halisi za watu. Utajuta hata kwa nini uliwahi juta kwa watu wasio na utu

Mkuu katika hii dunia, kila binadamu ni mwema na mzuri kwako pale unapowafaidisha hivyo, wanyime au uwaombe wao kama hutojiona mjinga kwa kudhani kila mtu ana moyo kama wako
Mkuu mimi natamani sana kuwa na roho mbaya, mnyimi ila ndio siwezi.
 
Mkuu mimi natamani sana kuwa na roho mbaya, mnyimi ila ndio siwezi.
Jaribu siku moja moja kuomba msaada hata kama shida una uwezo wa kuzimaliza mwenyewe ili uwajue watu wako..

Mimi nilipigwa na reality kipindi nina uhitaji serious kiasi kwamba, nimeingia stage two, kwa sasa kusema sina au hapana nimeanza kuzoea Ila ni kwa baadhi ya watu tu. Bado napambana
 
kuwa na Mkono wa birika ni kipawa kama vile kipawa cha mpira,kukimbia na
kuimba.
Kuhonga ni uzwazwa kama vile kuuziwa madini feki.
 
Wakuu habari za jioni.

Wakuu naomba kukiri mimi usingekua uhongaji labda ningekua namkaribia msukuma kwa mpunga lakini sijui ni pepo nimelogezewa la kuhonga ama namna gani.

Wakuu, inapokuja swala la kuhonga kwa kweli hua sijiulizi mara 2, kama ninacho natoa tu.

Hili sio kwa wanawake tu, hata kwa watu wengine, nikiwa nacho natoa sana kwa watu. Nadhani nimekua na roho nzuri kupita kiasi, mimi sio mtu wa kumuomba kitu ninacho nikakunyima. Hata nikijikaza nikakunyima roho itaniuma sana.

Na mbaya zaidi naona kama kuna watu wananijua na wana take advantage of my kindness. Nimekua too kind na I can't help.

Wakuu naombeni msaada hii tabia ya kutoa na kuhonga sana inanimaliza. Nawezaje kua na mkono wa birika.

Ahsante.
Kazi kweli kweli una roho nzuri kama niliyokuwa nayo zamani, ila mimi sikuwa mhongaji. Nilikuwa mwepesi kukopesha na kusaidia. Ila baadae niligundua Binadamu wagumu sana, unaowapa pesa muda fulani wewe ukiwa na changamoto, kila siku hawana hela na wanabiashara na kazi.

Nikasema tutaenda sawa, sasa hivi nimejifunza roho ngumu kama jiwe, sitoi pesa Bora hiyo pesa niitunze itanisaidia au nipeleke out watoto. Ninatoa pesa Kwa watu wenye msaada kwangu tuu, sio wale wanaosubiri kupokea.

Na wakati mwingine kwa washkaji au watu wanaonizunguka akikomaa sana wala sisumbuki. Alitaka 50,000/= hata kama ninayo Nampa elfu Tano na tena namwambia asirudishe. Alitaka laki tusisumbuane Namkadiria tu. Binadamu hawana shukrani.

Ila pia lazima kuna Wana ambao mnabebana, hao tembea nao tu. Mtaji ukiyumba atakupa mchongo, na wewe halikadhalika utambeba.
 
Kuhonga ni afya mkuu!
 
Attachments

  • 20231213_091800.jpg
    20231213_091800.jpg
    28.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom