Nawakumbusha wanaJF, Russia alipeleka Jeshi kumlinda Nicolas Maduro ila Marekani kashindwa kumlinda Rais wa Ukraine

Wanaopiga ngoma ya vita humu ndani sana sana ni vijana ambao hawaelewi madhara ya vita hata wakati Tanzania anapigana na Uganda mwaka 1978/1979 walikuwa hawapo duniani hivyo hawajui vita ni kitu gani na hawajui kwamba kufuatia hivyo vita na Uganda ndio Tanzania ilipata kilema cha kudumu kiuchumi.
Halafu sasa wanajifanya wajuzi wa maswala ya vita,ukisoma comment zao unaishia kucheka tu.
 
Vipi kuhusu Syria, Iraq, Libya, Afghanistan huko hakuna watu mkuu maana kote alipeleka majeshi. Au wewe na USA kuna watu mnaona wanastahili kufa wengine hawastahili?
 
Mmarekani anachoangalia ni adhari kwa kwake na kwa dunia, uwezo wa kumpiga mrusi anao tena wakutosha tu, tatizo lipo baada ya kumpiga matokeo yake ndio yanayoogopesha.

Mungu azidi kuwaongoza kwa busara na hekima kwani ata wahenga walisema ni bora nusu shari kuliko shari kamili.
huo uwezo upo mdomoni au kwa vitendo?kama kampiga sadam na gadafi na bado duniani mambo yanaenda,ampige na mrusi.alafu uone ulaya itakavyofutika ndani ya dk sifuri...
 
Wewe unaongea nini? Hujui unacho ungelea eti uwezo anao wa kumpiga lakini eti litakalo tekea baada ya kumpiga ndo anacho uogapa, kwamatiki hiyo US hana ubabe wakumpiga Mrusi kabisa, Russia imepakana na US kama hujui US ndo atakae lia vibaya akiingia kwenye hiyo vita.
uko sahihi,wengi hawajui kuwa north korea na russia zipo karibu na marekani,hawajui dunia ni kama mpira,zamani ilikuwa kutoka urusi mpaka marekani,ni sawa na kutoka airport mpaka kariakoo..
 
Marekani itateketea alafu Urusi ndio haitateketea?!
Wote watateketea kuna siraha za sumu nk hivyo siku zote marekani ataipisha urusi kwenye maslai mapana ya mrusi na mrusi atampisha marekani kwenye maslai mapana ya marekani ila wanaweza kuchapana nje ya nchi zao tu ,marekani hawezi dhubutu kushambulia urusi hata siku moja maana huo utakuwa mwisho wao wote
 
Ukrane kalivunja daraja lake , hakuna tena warusia kuingia ukrane na waliopo watarudi russia wakiwa maiti.
Kazi ndio inaanza.
Rafiki nchi kubwa kama USA na Russia na wenzao daraja sio issue, Nimeshindwa kuweka picha .ila Search kupitia YouTube

Andika hivi.
"Russian army pantoon brdge" utaona maajabu ya dunia
 
Moscow to New York ni zaidi ya km 8,800.

Je ,ni karibu?View attachment 2130748
Babu nakutilia mashaka kwamba uelewi geography huu umbali Ni za miji na mji unazungumzia nchi kwa nchi ..mji wa New York na moscow lazm kuwe mbali babu ila Russian na Americans Ni mataifa yalioko karibu tu Ni bahar ndio imewatenganisha
 
Russia kapakana na Marekani kivipi mkuu? Russia ni far east wakati Marekani ipo west zaidi na umbali kutoka Marekani hadi Russia ni kilometres za kufa mtu.

Urusi ipo karibu na nchi za Ulaya tena ulaya ya mashariki sasa unaposema ipo karibu na Marekani kidogo nashindwa kuelewa.

Hata tofauti ya masaa tu Urusi siku inaanza kubadilika kisha baada ya masaa zaidi ya 10 ndo siku hiyo hiyo inabadilika Marekani.
kwa taarifa yako zamani kabla russia hajamuuzia marekani ardhi yake,umbali kati yao ulikuwa sawa na kutoka airport mpaka kariakoo,,,fatilia mambo,dunia ni duara kama mpira,sio flat kama karatasi...
 
We huna akili kabisa,hiyo screen shot inasema hizo kilometa ni kutoka New York to Moscow,sasa wenzako wanakuuliza umbali wa Russia to USA maana yake unatakiwa kuchukua closest point between them ndo upime.

Acha kukariri na jifunze kutafakari ulichoulizwa.Sasa nakurahisishia,Kuna sehemu inaitwa Alaska (ipo Marekani).Google kama ulivyofanya distance between Alaska to Russian Boarder kisha urudi hapo kuendeleza ubishi
 
Nipime kwa kutumia nini? Kwasababu inavyojulikana ni kwamba Urusi ipo mashariki ya mbali na Marekani ipo magharibi sasa umbali wa mashariki ya mbali na magharibi ni karibu?

Tofauti tu ya masaa ni kubwa mno kati ya Marekani na Urusi halafu niamini eti ni nchi jirani? Kwa maana hiyo New Zealand ambayo nayo ipo mashariki ya mbali tuseme ipo jirani na Marekani?
wewe utakuwa ,,muha,,sio kwa ubishi huo
 
US alishaambiwa akiijaribu Urusi basi Alaska itakuwa bahari(kama kumbukumbu ziko sawa).
Na ikumbukwe Alaska ilinunuliwa toka USSR
Ata mabom yote ya dunia nzima yapigwe alaska, haitoungana na bahari, thats the fact, fanya calculation ya energy held by nuclear weapons utajua
 
Ramani naijua vema tangu darasa la 4 na huu uongo wao kwamba dunia ni kama tufe sijui mviringo.

Tafuta kwenye vyanzo vyako vya kuaminika uone umbali halisi kati ya miji ya New York Marekani hadi Moscow Urusi ni kilometres ngapi?
Bila shaka wewe ni miongoni mwa zile division four za 28 zilizokuwa zinapewa go-ahead kipindi fulani.

Unapima umbali wa nchi hadi nchi kwa kuzingatia point zipi? Yani kwakua kutoka Dar(Tz) kwenda Kampala( UG) ni Km nyingi ndo useme kuwa Tz na UG sio majirani?? Vipi safari yangu nikiamua kuifanya from Bukoba to Kampala??

Ukitaka kuona ujirani wa Russia na America pima kuanzia mwisho wa Russia na Mwanzo wa Marekani kutokea upande ambao zimepakana.

Unakataa Dunia sio duara, kwahiyo dunia ni Flata surface, unatumia vigezo vipi?
 
Back
Top Bottom