Naunga mkono Zitto kuwania urais - Kigwangalla

Sasa huo umoja mbona mnaupinga humu? na kama unafikiria ishachukuliwa, basi you ain't seen nothing yet!
Yaani mwana CCM akimuunga mkono Zitto mnaona kuna mushkeli .. dah! yaishe bwana.
Bila shaka yaishe.. Utamsifiaje mke wa mwenzako wakati mkeo yupo? Makosa kama haya ndio maana hata yeye kaenguliwa huko CCM....
 
Naendelea kujiuliza sana, hivi ni kwa nini wafuasi wa CDM wanaumia sana wakisikia tu ZZK anautaka Urais? Kwani kuna ubaya gani? Kama wanauhakika kwamba Slaa anakubalika zaidi ya ZZK si watulie tu? wakati ukifika umaarufu wa Slaa utamfanya amshinde ZZK ndani ya vikao vya chama na Slaa atakuwa mgombea. Na mimi binafsi kujitokeza hadharani kumuunga mkono haimaanishi eti nina mkakati wowote mimi na chama changu wa kuwavuruga CDM, mimi huo ni mtazamo wangu na sijatumwa na mtu na wala sijajadiliana na kiongozi yeyote faragha ama kwenye mikutano halali ya chama chetu ambayo mimi ni mjumbe, sasa woga wenu CDM unatokea wapi? Nawashauri mheshimu demokrasia, mmuache ZZK agombee na mumshinde kidemokrasia - japokuwa jambo moja ni lenye uhakika sana, kwamba yeyote mtakayemsimamisha 2015 atashindwa tu na CCM! Ni bora hata kama mtakuwa na akili ya kumuweka ZZK ama kijana yeyote yule wa CDM ili kumuandaa kushinda uchaguzi 2030 huko labda, kama chama kitakuwa hakijafa tu!
Mh Kigangwalla, naomba nianzie ulipoishia. Kitu kimoja nina uhakika nacho, mabadiliko Tanzania ni lazima(inevitable) yatokane na CUF, CDM, au Dovutwa,mbadiliko yanakuja.

Mwanasheria mkuu Werema ambaye ni jeuri na asiyesikia ameushangaza umma aliposema, malalamiko ya wananchi kuhusu mambo kama mikataba yasipuuzwe. Werema hakumaanisha mikataba, alichokuwa anamaanisha ni kuwa 'malalamiko' ya wananchi kuhusu hatima ya nchi yao yasikilizwe! kuna kitu alikiona.

Inapotokea wanakijiji wanaoishi kwa dola moja kutoa kiwanja, kununua mabati na matofali ili kujenga ofisi ya CDM wanachokisikia hapo lipo jambo! Inapotokea wananchi wanamzomea waziri mkuu tena wiki mbili baada ya mwananchi mwingine kumwagiwa bomu,hapo lipo jambo! Inapofikia mahali FFU wamesimama na PM anazogolewa mchana, kipo kitu.

Unaposema CCM itashinda tu! Tunakuangalia kwa kupoteza matumaini, wewe kama kijana unapaswa kuiona hatari iliyo mbeleni kwa wepesi zaidi. Kama yupo mwana CCM anayepata usingizi kwa kauli yako,sina shaka na maradhi yanayomkabili, nina shaka kama anapata matibabu sahihi!

Kuhusu ZZK, naungana na jmushi1 kukuuliza mbona CCM wakisikia fulani anataka kutamka nia, mtu huyo anaitwa pembeni na kuonywa? Iweje uzuri uonekane kwa ZZK na si Sitta au Lowassa, Membe au Mwakyembe?

Sioni tatizo kwa ZZK kuwania nafasi hiyo, sioni tatizo kwake kutangaza nia, naliona tatizo kwa utaratibu wa kanuni zake akiwa ndani ya chama chenye kanuni na taratibu. Kwahiyo anafanya jambo sahihi kwa njia isiyo sahihi!

Utaratibu wa ZZK unalenga kudhoofisha jitihada za CDM katika kujieneza. Ni utaratibu utakaofanya watu wafanye kazi kwa 'kujipanga' na si kama chama kilivyopanga!

Ni utaratibu huo ndio unaoitesa CCM, je watu wakae kimya ili ifike mahali tunasikia kambi A na B? Ni utaratibu huo ndio umeanza kuzaa mitafaruku ndani ya BAVICHA!watu wakae kimya kwasababu ZZK amekuja na siasa zisizo za mazoea kama anavyotetewa na washauri wake? Siasa mpya na za kisasa ni zile zinazolenga kudhoofisha chama?

Nyerere hakusema watu watangaze nia mapema siku uchaguzi ukiisha tu, alimaanisha watoe muda wa watu kuwafahamu kwa undani. Leo ni 2012, tuna miaka takribani 3! Kwa CV yangu Nguruvi3 nahitaji watu wanifahamu kwasababu hata uwepo wangu haujulikani, kwa 'Fame' ya ZZK hivi anahitaji miaka 3 kweli?
Hata kama ninahitaji watu wanitambue nitanya hivyo kwa kujenga ili niitwe kama mwashi mzuri si mwashi mwenye kauli nzuri na anayejulikana

Kinachotia shaka zaidi si nia yake kutangaza ni 'controversy' zake katika mambo ya chama, kuanzia kumalizika timbwili na Mbowe hadi bungeni(KUB) hadi sasa. Amekuwa na matukio yanayotia shaka zaidi kuliko matumaini.

Imefika mahali wanachama wanamwangalia kwa mshangao hata kama anachokifanya ni sahihi.
Amekuwa kinyonga na inakuwa shida kujua anasimamia wapi?
Kinachomtuhumu hapa kama nionavyowasoma wachangiaji si azma ya kutangaza ni mwenendo wake usioeleweka.
 
..Kuhusu ZZK, naungana na jmushi1 kukuuliza mbona CCM wakisikia fulani anataka kutamka nia, mtu huyo anaitwa pembeni na kuonywa? Iweje uzuri uonekane kwa ZZK na si Sitta au Lowassa, Membe au Mwakyembe?
Kwa mfano ni nani alitaka kutamka nia akaitwa pembeni?
 
ZZK kwa mtazamo wake anajitambulisha kama MGOMBEA BINAFSI ambaye anakitumia chama tu kufikia malengo yake yeye. Well, hatuna mgombea binafsi na hivyo watu wengi wanaompa support wanshindwa kuelewa kwamba ndani ya chama kuna kanuni zake..Na kama unakumbuka niliandika mada ya ushauri wangu kwa ZZK kabla hata hajatangaza nia hii lakini wapi jamaa hata hakuisoma au alisoma akaipuuza na kufanya yale yale yanayomletea leo matatizo leo hii. Kwa nini alifanya hivyo? anajua mwenyewe na hivyo tunapomsema ktk haya ni kutokana na maamuzi yake mwenyewe..

Mkuu Mkandara has it occurred to you kuwa inawezekana kabisa Zitto anatambua fika kwa hali ilivotete ndani ya chama chake cha CDM in relation to his position na reputation ni to his disadvantage... Kuwa anaelewa kamwe hawezi kuwa nominated na chama chake kuwa mgombea wa chama? Sijui... BUT Thinking out loud ni kuwa Zitto kaamua kuweka hili mapema kabisa kuwa ana niya ya kugombea ili hata ikifika wakati muafaka wa kutangaza hata asipotangazwa akatangazwa mwingine ilete maswali ya msingi na mazito (hasa kama atakae kuwa nominated kugombea sio Dr. Slaa); ya kwa nini Zitto hajakuwa nominated... Na better yet, ikawa ni sababu ya msingi kwake kufaya maamuzi makubwa ya yeye kuchukua a loud step...

Umeziungumzia swala la ZZK kukusikitisha sana kila anapokuwa mbali na wenzake.. Hili ndio neno la LEO kmkuu wangu kwani sisi tunapingana na ZZK kwa sababu gani?.. ZZK anaitafuta IKULU kwa udi na Uvumba wakati anajua fika kwamba pale sii mahala pa kukimbilia isipokuwa unajipanga. Na angeweza sana kufika kama angesikiliza watu lakini sisi wengine huonekana wahuni tu wa mtaani hatujui kitu kwa sababu tunavaa baseball cap, Tshirt na raba.

Mkuu, nasikitishwa kwa picha inayoonekana kuwa inaonesha Zitto yupo mbali na Chama chake, ila sina maana kuwa huo umbali naona ni sababu ya Zitto or CDM. Ndio maana kuna mahala hapo nyuma katika one of my posts niligusia kuwa lazima kuna kitu hapo kati kati ndani ya chama chao... Bahati mbaya ama nzuri lawama zote hutupiwa Zitto, hivyo umbali wake mara nyingi unaangaliwa kwa kumlaumu badala ya kujaribu kutafakari tatizo, sababu na chanzo kama ni yeye, Zitto, viongozi wenzie ama viongozi wakuu wa chama.

Asmuchas ni mchanga sana katika siasa na ni ngumu kuelewa nini kinajiri hasa chini ya carpet, uzuri ni kuwa naelewa kwa yale juu ya surface. Na uzuri wa CDM wote katika utendaji, malengo, sera zao, mikakati yao na mengine mengi KASORO yako kubwa ni mbili kuu! Moja wapo SO over-confident na lingine ni kwa wale wa chini (yaani wafuasi, wanachama, wanaharakati wao) na tabia ya ushabiki, wao hawaoni kuwa CDM ama mwana CDM yeyote (hasa akina Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Madamed Slaa, Mnyika, Lissu) hawawezi kufanya kosa lolote na hawatakiwi kukosolewa lolote lile ILA ZZK tu! Hii tabia huwa nachoka kabisa na kunishangaza, na hili ndilo nilitaka nijue hasa kwa nini hawamkubali ZZK. Na hii imedhihirishwa zaidi na pale ambapo Madame Slaa alifanya blunder ya kutoa taarifa ya vitisho vya kuangamizwa kwa Dr. Slaa na wapinzani wake. Hakuna waliokuja ku support kuwa kweli Madame hapo kavuka mpaka, na ilitakiwa a delegate hio habari kwa chama... Ila rusha makosa ya ZZK... Moto unawaka. So comfusing...

Hata hivyo Mkuu wangu Mkandara, nimekupata sana, na NASHUKURU kwa kunielewesha your side of the coin. Appreciated.
 
Zitto Zuberi Kabwe... The man himself! Mimi napenda kusoma tu vile wadau ambavo wanawaka moto na kutoa maneno ya hasira dhidi yake wakisikia huyu mkuu katamka kugombea.. Huwa natamani ningekuwa najua siasa kama wao (ambao wapo against) ili nielewe vipengele hivi.

  1. Hawapendi sababu anaungwa mkono na CCM wengi na maybe sababu inaonekana anapatana na baadhi kama vie Makamba Jr.? (Imagine Makamba Jr. katamka kua Zitto ni mwanasiasa ambae he is impressed by)
  2. Hawapendi sababu ni tishio kwa anayetazamiwa kugombea kwa chama hicho ambaye ni Mh. Dr. Slaa?
  3. Hawapendi sababu wanaona hafai na wala hana sifa za uongozi? AMA
  4. Hawapendi sababu ipi hasa? Kwanini watu wanachanganikiwa sana wakisikia Zitto in the lines of Presidency?

Kama kuna mtu wa kujijibu hayo kwa kina na ufasaha nitashukuru saana.
kuna himaya mbili hapa kuna wanaotishiwa kunyang`anywa nchi na chadema na wale wanotaka nchi ambao ni chadema je ukifanya utafiti wako kimahesabu zaidi ni wangapi walioserious wanachadema wanaomuunga zitto mkono kugombea? je zitto kwenye jamii ya watu wa kawaida kabisa imani yake kwao iko sawa na zitto wa mwaka 2007? mimi nachoona si zitto kuwa tishio kwa chadema bali ni zitto kuamua kuchakachua image ya userious wa chadema mbele ya jamii na jamii iamini chadema hawana msimamo wa kimsingi na dira thabiti bali kulumbana katika nafasi za uongozi for sure na hii ndio kazi anayofanya zitto
 
kigwangala unaunga mtu mkono ambaye unajua hatashinda ili mshinde tena sio? sasa ukijua hata kauli yako inaweza kuempress watu wasiokuwa na mwelekeo hata usingesema basi washawishi ccm zitto aje agombee huko! kama ni mzuri kama mnavyodai
 
Kumjadili Zitto ni sawa na kukosa kazi ya kufanya, ila kwakuwa hapa ni sehemu ya mijadala basi nawatakia mjadala mwema. ila mwenye notebook na aandike maneno haya, Zitto Kabwe kamwe hawezi kushinda Ubunge wa Kigoma kaskazini 2015.

Siongelei Urais kwa sababu mpaka dakika hii Zitto anaidharau katiba ya nchi ambayo yeye anataka aje aape kuitii. kijana ameshalewa sifa za kijinga na 2015 Zitto atakuwa na miaka 39, sasa yeye ndio msemaji wa Watanzania kwamba tupitishe katiba kuruhusu under 40 kugombea Urais kwa matakwa yake? Muogopeni sana huyu mpuuzi.
 
Ok swali jepesi,nitajie kiongozi yeyote wa ccm aliyetangaza kugombea urais this time.Sasa hivi ni muda wa kujenga chama.Tena hata wenye kuutaka urais hawasemi,ni wapambe wao ndo wanaongea.
Ningeshangazwa watu kushtushwa endapo ungekuwa ni muda wake.

Pili,mbali na muda,wote wanao muendorse,ni wa ccm,shangaa kwanini hawasemi so and so ndiyo wenye kufaa kugombea huko ccm,badala yake ni chadema.Kwao kuna discipline,ndo maana wanashangilia na kuchochea hayo yasiyo na discipline kwa wapinzani wao.

Ni very unnatural kwa mwana ccm kupendekeza mgombea mzuri kwa mpinzani wao.That's just common sense.


Jmushi1 kwa jinsi ninavyoelewa (maybe am wrong) ni kuwa hasara ya kutangaza kugombea Uraisi mapema mno ni kubwa sana kuliko faida zake... Moja ya sababu ni kuwa it is so damaging kwa mgombea hasa katika swala la kufufua what lies in the abandoned closet.

Yoote ulioeleza hapo nimekupata na kwa kiasi kikubwa nakubaliana nayo... Ila naomba nikuulize, wewe ni mzuri wa kutambua wa nini kinajiri katika siasa. I know am not that good YET mimi na wewe tanaelewa vizuri sana hayo ambayo umeeleza na mengine mengi yalitolewa na wengine wengi kwa nini Zitto anachemka kujitangazia kuwa yupo tayari kugombea urais, na kuonesha yupo serious kaeleza kuwa hatagombea ubunge tena....

Tukiweka hayo yote pembeni na kujiengua kana kwamba hili walitazama kwa mara ya kwanza... Swali; Hivi kweli unadhani kuwa Zitto haelewi hayo? Kwamba mimi, wewe na wengine wote wanaomkosoa tunaelewa zaidi kuliko yeye? Siamini... Mie nathubutu kusema we are asking the wrong questions hapa... La msingi coming to the bottom of this nadhani inatakiwa kuuliza kuwa Zitto ana malengo gani? Niya yake ni nini hasa? Anatuma ujumbe gani na strategy yake kubwa ni kufanya nini? Hii ya kulaumu na kukosoa kuwa ana makosa/msaliti na the like naona kama zina diverge maswala ambayo ni msingi kuangaliwa kwa undani ili kumuelewa vema malengo yake in the long run.
 
Kumjadili Zitto ni sawa na kukosa kazi ya kufanya.


Hapa Matola kwa mtazamo wangu utakuwa umekosea... Kuna kila haja, yeye ni public figure.. Moja ya viongozi ambao wapo so controversial, mmoja wa figure head CDM ambae tokana na maoni ya wengi anaonekana anaenda kinyume na taratibu za chama chake.

Hio kauli nilo ku-quote inakuwa kama vile inalenga kuonyesha kuwa huyu mtu hana umuhimu; swala ambalo litakuwa ni kujidanganya... Wanasema 'actions speak lounder than words' nitaelewa kuwa ZZK hatakiwi CDM pale tu atakapokuwa 'Chagulani'd' else hapa inabaki tu kuwa politics... Na hilo ni moja ya misingi ya ZZK kujadiliwa.
 
Hapa Matola kwa mtazamo wangu utakuwa umekosea... Kuna kila haja, yeye ni public figure.. Moja ya viongozi ambao wapo so controversial, mmoja wa figure head CDM ambae tokana na maoni ya wengi anaonekana anaenda kinyume na taratibu za chama chake.

Hio kauli nilo ku-quote inakuwa kama vile inalenga kuonyesha kuwa huyu mtu hana umuhimu; swala ambalo litakuwa ni kujidanganya... Wanasema 'actions speak lounder than words' nitaelewa kuwa ZZK hatakiwi CDM pale tu atakapokuwa 'Chagulani'd' else hapa inabaki tu kuwa politics... Na hilo ni moja ya misingi ya ZZK kujadiliwa.
Pole sana, hujui Zitto ni jinsi gani ameumiza mioyo yetu hasa mimi Matola ambaye niliacha shughuri zangu kwenda kumlaki pale alipofukuzwa Bungeni, sikujuwa kama anaweza kucheza Double Agent Game.

AshaDii naona unatumia nguvu nyingi sana bila sababu, tatizo la Zitto si kutaka Urais bali ni kuwasaliti Watanzania na kuwa kibaraka wa JK ili kuisambaratisha Chadema. kamwe Zitto hawezi kusamehewa kwa usaliti huu. usidhani kila ambaye yupo hapa nyuma ya keyboard yupo kwa ajili ya porojo au propaganda na ndio maana tunatumia majina Fake.

Zitto amenasa kwenye mtego wa system na hana namna ya kujinasuwa, ni lazima afanye kazi atakayoagizwa otherwise wanamlipuwa dakika mbili tu, nashangaa sana watu sijui kwa nini mnakuwa na uelewa wa hali ya juu lakini mnashindwa kuhoji mawasiliano ya Zitto na Usalama wa Taifa ni ya nini? hwbu jiulize kwanza kabla hujapoteza energy zako kumuongelea a dead snake.
 
kuna himaya mbili hapa kuna wanaotishiwa kunyang`anywa nchi na chadema na wale wanotaka nchi ambao ni chadema je ukifanya utafiti wako kimahesabu zaidi ni wangapi walioserious wanachadema wanaomuunga zitto mkono kugombea? je zitto kwenye jamii ya watu wa kawaida kabisa imani yake kwao iko sawa na zitto wa mwaka 2007? mimi nachoona si zitto kuwa tishio kwa chadema bali ni zitto kuamua kuchakachua image ya userious wa chadema mbele ya jamii na jamii iamini chadema hawana msimamo wa kimsingi na dira thabiti bali kulumbana katika nafasi za uongozi for sure na hii ndio kazi anayofanya zitto

Zitto wa sasa sio wa 2007, nor kiongozi yeyote yule, hawezi akabaki hivo hivo lazima abadilike aidha for the better or worse. Ila kinachofanya hili zoezi kuwa gumu ni nini kipimo hasa cha kupima kuwa Zitto anakubalika kwa kiasi gani ndio tatizo... Tupime kwa wafuasi wa CDM, CCM ama wananchi?

Hapo in blue... Ni moja ya maeneo ambayo hufanya hili la kutazama ZZK liwe interesting... Kwa nini wanamuacha?? Hapa alaumiwe Zitto ilaumiwe CDM?
 
Kwa jinsi taasisi ya urais ilivyofanywa ionekane kama kupiga debe tu, kuna siku hata vichaa wa Milembe wata tangaza nia ya kuutaka
 
Pole sana, hujui Zitto ni jinsi gani ameumiza mioyo yetu hasa mimi Matola ambaye niliacha shughuri zangu kwenda kumlaki pale alipofukuzwa Bungeni, sikujuwa kama anaweza kucheza Double Agent Game.

AshaDii naona unatumia nguvu nyingi sana bila sababu, tatizo la Zitto si kutaka Urais bali ni kuwasaliti Watanzania na kuwa kibaraka wa JK ili kuisambaratisha Chadema. kamwe Zitto hawezi kusamehewa kwa usaliti huu. usidhani kila ambaye yupo hapa nyuma ya keyboard yupo kwa ajili ya porojo au propaganda na ndio maana tunatumia majina Fake.

Zitto amenasa kwenye mtego wa system na hana namna ya kujinasuwa, ni lazima afanye kazi atakayoagizwa otherwise wanamlipuwa dakika mbili tu, nashangaa sana watu sijui kwa nini mnakuwa na uelewa wa hali ya juu lakini mnashindwa kuhoji mawasiliano ya Zitto na Usalama wa Taifa ni ya nini? hwbu jiulize kwanza kabla hujapoteza energy zako kumuongelea a dead snake.

Hiyo polee nastahili Matola, nimekiri toka post yangu ya kwanza (1[SUP]st[/SUP] post) kuwa sielewi kabisa na nataka nieleweshwe na niridhike kuwa nimeelewa. Nikaeleza wazi kabisa, hivyo anae nielekeza kikubwa anielekeze kama Mtanzania yeyote wa chini asie na uelewa kabisa kwa manufaa ya kuelewa.

Situmii nguvu Matola, nasimamia lile ambalo linanisumbua na kutaka kujua. Na sina tabia ya kukimbia sababu tu ya kuagree to disagree unless ionekane hakuna hatma ya suala lenyewe. Najua hukubali katika kumjadili ZZK na ni moja ya kiongozi ambao unaona hawafai wala hawana tija kabisa. Ukiwa mzalendo wa kweli na a devoted CDM naomba kama hujatali uwe wazi na uniambie ni kwa nini hawajibishwi? Je ni yoyote kati ya haya?


  • ZZK ni moja ya nguzo za CDM bila yeye inakufa?
  • Ama kuna mahala iliwekwa wazi katika maandishi huko nyuma kuwa no matter afanye kitu gani hairuhusiwi kum'wajibisha?
  • Ama ni mmoja wa wale viongozi wenye VETO Vote ndani ya chama?

Nikiichukulia jinsi CDM ilivyo sasa, ni chama kilicho jijenga kikiwa na viongozi wengi kwa sasa ambao ni potential, wana jina tayari na kuifanya kazi yao vilizuri. Nina imani kubwa sana katika vyama pinzani CDM (kwa sasa) ndio pekee inaweza kukomboa Tanzania kwa kuweza wang'oa CCM katika uongozi kwa ngazi ya Rais. Na naamini pia hili linawezekana hata Zitto asipokuwepo.

Narudi kwenye swali, kwa nini hawajibishwi akatolew kabisa katika chama? Au sababu ndio moja ya zile ni ngumu kuweka wazi na damaging ikijulikana? (If that then kweli kabisa naachana na hii kitu na kuachia ngazi). Swala hapa sio namtetea ZZK, ila natka kuelewa...
 
zitto alikuwa mpambanaji wa kweli,..lakini baada ya kujumuishwa na jk kwenye tume ya madini kabadilika..."jk kafanya mambo mengi kigoma,.kupitia upya mikataba ya madini kutawafukuza wawekezaji,.nitagombea urais 2015(in 2012),.kila safari za mara kwa mara na jk..waliozaliwa kabla ya uhuru hawawezi kuleta maendeleo nchini etc etc etc
 
AshaDii sina haja ya kuquote post yako, ila kama shida yako ni kuelewa basi kama una masikio na usikie, usidhani Zitto ni mjinga kiasi hicho wa kusema tu awajibishwe.

Kwanza kabla sijakwenda mbali mimi si mwanachama wa Chadema wala chama kingine chochote, Zitto kama ana turufu au kura ya Vetto uliyoiuliza ni turufu ya Propaganda za udini ambazo Zitto mwenyewe ameshiriki kuziratibu kwa umahiri mkubwa akishirikiana na CCM via Usalama waTaifa.

CCM is Dead big snake, inahaha kwa namna yoyote ibaki madarakani iwe kwa njia haramu au halali wao hawajali hilo, kinachotakiwa ni kushika dola, sasa kumuwajibisha Zitto kwa sasa ni kuingia kichwa kichwa kwenye mtego wa CCM huku wakishirikiana na Cuf zitaenezwa Propaganda za ajabu kwamba Chadema ni adui wa Waislamu, wakati hata huo Uislamu wenyewe wa Zitto ni Uislamu jina.

Kitu ambacho hata Zitto mwenyewe anakijuwa the time will tell & time will decide itself, lakini for sure this Young Man alianza vizuri na anamaliza vibaya na kwa wale wanaojitambulisha kama wafuasi wa Zitto badala ya kuwa wafuasi wa Chadema, watashangaa huyu jamaa akiwaacha kwenye mataa na kwenda kufanya PHD yake Ujerumani.

Nadhani kama nitakuwa nimekujibu swali lako ni kwamba Zitto anapaswa kumspare kwa maslahi ya muda maalum ya Chama, sawa na wanavyomspare Shibuda, ni kwamba 2015 atafute ustaarabu wake si Chadema tena.
 
Last edited by a moderator:
I stand to be corrected, huyu Kingwangala si mwana CCM?!

If So kwanini asiunge mkono mgombea mmojawapo wa chama chake CCM?
Kwanini yuko happy kuunga mkono mgombea wa upinzani? Mimi ningemuomba
awe BOLD ENOUGH aseme yeye anamuunga mkono mgombea yupi huko CCM? Hizi
light touch politics za kuunga mgombea kwakuwa ni mwanamke au kijana awapelekee
WANAO NUNULIWA NA VITUMBUA SIO JF HOME OF GTs HATUDANGANYIKI NG'O


Jaribu kwingine!
 
Na Suleiman Abeid, Shinyanga | Majira

MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dkt. Hamis Kigwangala, ametangaza kuunga mkono dhamira ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, ya kutangaza kuwania urais mwaka 2015.

"Naunga mkono Bw. Zitto kwa dhamira yake ya kutaka kuwania uongozi wa juu kabisa katika nchi yetu japokuwa yuko CHADEMA na mimi niko
CCM," alisema Dkt. Kigwangwala.

Dkt. Kigwangwala alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia wanafunzi wa Sekondari ya Shinyanga, iliyopo wilayani Kishapu mkoani hapa, wakati wa mahafali ya 46. Katika mahafali hayo, Dkt. Kigwangwala alikuwa mgeni rasmi.

Mbunge huyo alisema vijana wanaomaliza masomo yao wasipokuwa na malengo ya kuwa viongozi wa nchi itakuwa hatarini kujikuta ikikosa vijana makini.

Hapo ndipo alipotolea mfano Bw. Zitto, akisema alisoma naye shule moja, ambapo tangu akiwa masomoni alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi.

“Binafsi nampongeza kijana mwenzagu Zitto (Kabwe), maana tangu tukiwa shuleni alikuwa na malengo ya kuwa kiongozi, sasa hivi ametangaza nia yake ya kutaka kuwania urais wa Tanzania mwaka 2015, ameniwahi hata mimi natamani siku moja nitakuwa rais, lakini leo hii hapa sitangazi nia hiyo,” alisema Dkt. Kigwangwala na kuongeza;

“Muda wake bado, ipo siku nitatangaza dhamira hiyo, akijitokeza kijana nitamuunga mkono...kwa hiyo namuunga mkono Zitto kwa dhamira yake ya kutaka kuwania uongozi wa juu japo naelewa hawezi kutushinda CCM.”

Ili taifa liendelee kupata viongozi, Dkt. Kigwangwala alisema hakuna sababu ya vijana waliopo mashuleni kubaki na dhana kuwa masuala ya siasa yanahusu wanasiasa waliopo madarakani au watu wazima peke yake, badala yake waanze kujiwekea malengo yatakayowawezesha kushika uongozi wa nchi.

Aliwataka vijana watakaobahatika kuingia katika siasa na kupata nafasi za uongozi kujiepusha na siasa za makundi ambazo hivi sasa zinaitafuna nchi.

“Epukeni makundi yanayohujumu Serikali na hatimaye kutaka uongozi wa nchi yetu, hakikishesni mnawakwepa wanasiasa wa aina hiyo, maana hawafanyi siasa kwa malengo ya jamii, hawafanyi siasa kwa malengo ya umma wanafanya siasa kwa malengo ya kutunisha matumbo yao,"alisema Dkt. Kigwangala.

Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangala alijitolea kuichangia shule hiyo msaada wa vitanda vyenye thamani ya sh. milioni tatu, kabati mbili kwa ajili ya chumba cha wanafunzi wasioona, na vifaa mbalimbali vya michezo.

................. Sipendi kusikia wanaoutamani urais katika kipindi hiki, inanisumbua kuona ni kama kuanzisha malumbano yasiyokuwa na msingi.... muda ukifika hiyo haina taabu lakini kwa sasa binafsi naona muda bado
 
Back
Top Bottom