Naunga mkono Zitto kuwania urais - Kigwangalla

AshaDii,
Mkuu nakusikia sana lakini kwa nini ZZK afikirie hawezi kuchaguliwa?..Ina maana anajua fika kajenga maadui ndani ya chama laa sivyo kila mmoja wa anayo nafasi yake. Mbona Dr.Slaa hakutaka kabisa kugombea Urais na alipendekezwa mbele ya kina Mbowe?..tena Chama kilichelewa sana kumtangaza mgombea kiasi kwamba watu walianza kuingiwa wasiwasi. Na zaidi ya hapo walitaka kuungana nguvu na CUF wakachomoa tena kwa mara ya nyingine lengo likiwa ni kuutafuta ushindi kwa wananchi sio nani atakuwa ama atagombea Urais na haki yake yeye.

Na hata Dr.Slaa alipopendekezwa bado kuna wananchi kibao walilalamika kuona Dr.Slaa analiacha jimbo lake la Karatu wazi hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza hata jimbo hilo. ZZK alifanya nini? alikuwa hajui atagombea jimbo gani mpaka dakika ile mara tunasikia Kinondoni mara kama vile kachanganyikiwa. akatuweka roho juu watu kwa muda kabla hajarudi Kigoma, unakumbuka!..

Kwa hiyo, mkuu wangu ZZK kutangaza azma hiyo ana lake jambo na kama nilivyosema sisi wengine tumejaribu sana kumtetea ktk maswala mengi tu lakini imefika mahala tunachoka maana haiwezekani iwe ZZK tu kila siku ndiye awe chanzo. Binafsi yangu najua fika ya kwamba CDM hawezi kumshinda CCM kirahisi..Na sidhani kama Dr.Slaa anaweza kutuletea ushindi isipokuwa CHAMA ndicho kinatakiwa kuweka maandalizi ya ushindi ktk ushindani ujao..Nimewadokeza ktk waraka wangu japokuwa nimezua Mtafaruku mkubwa kwa washabiki wake ambao wanaamini tutashinda tu kwa vyovyote vile..

Kwa hiyo namsoma sana ZZK anapotokea, na pengine niseme Hivi Kina Kobello wanadhani nimelala usingizi kumbe nayajua mengi kuliko wanavyodhania na ushauri wangu unatokana na kutazama pande zote maana ZZK, Dr.Slaa na Mbowe wote hawa sii kitu ikiwa CDM itayumba..Umaarufu wa muda unaweza kuwa kilio chao kesho. CDM ndio mpango mzima na ili chama kiwe makini ni lazima utokane na uongozi bora..

Moja kubwa ambalo ningependa kulisema leo ni kwamba CDM isome alama za wakati, miaka mitatu haiko mbali sana na chama kinatakiwa kujiandaa mapema kwa uchaguzi wa mwaka 2015. Kuna makosa makubwa yanafanyika hadi leo ktk maandalizi. CCM wameanza uchaguzi wao na karibu wanapaliza hivyo watajipanga kuelekea 2015, CDM wao bado wanajikweza mavyeo badala ya kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo na kktk maandalizi. Jamani hata World cup ipo mwaka 2014 maandalizi tayari yameshaanza.. Kuna sababu ama haja gani CDM ya mtu mmoja kubeba vyeo vitatu hadi vinne kiasi kwamba wanashindwa hata kukabiri mambo mengine muhimu wakati vijana wengine wapo?...Kw amwendo huu ndio maana watu kama ZZK wanaonekana wao ndio CDM wao ndio wabora zaidi wenye kufaa kugombea Urais maana ukitazama meza kubwa ndio wao tu kila mahala...CDM Jipangeni mapema kuelekea 2015..

- Nasubiri Makombora ya wasojua maana...
 
Last edited by a moderator:
Toka Zitto atamke hili hata wiki haijaisha... Samahani Lukansola, nisaidie sababu nyingine ambayo ni kigezo cha wewe kuona hafai zaidi ya hii.

Licha ya hivyo, hio kauli hapo sijaipata kwa kweli umeitoa wapi, so far nilivyomsoma ni kuwa hatagombea Ubunge sababu kazi aliyofanya katika nafasi ya ubunge inatosha... Take note; sio sababu hio hapo in blue...


AshaDii nimemsikia Zitto kwenye kipindi cha amplifaya ya clouds FM kwa maneno yakw akisema hayo, ni bahati mbaya tu kuwa sitaweza kuweka uthibitishi hapa kwa sababu sina, na tena mapema siku hiyohiyo nilimsikia katika kipindi cha asubuhi cha redio (siikumbuki). kama kuna mdau alisikia naomba anisaidie kuweka kumbukumbu sawa.
Alisema ameshakuwa mbunge kwa miaka mitatu na hana tena nia ya kugombea kwa sababu nilizozitaja hapo juu.

Kinachonifanya nione kuwa hafai ni kwa sababu; kwa mtazamo wangu namuona kama mtu asiyeamini katika team spirit, katika some of his statements amekuwa akijibrand ki u-mimi zaidi ya sisi. mimi huamini kiongozi mzuri huwa anatokea hajipandikizi na kupiga kelele ili ku attract attention ya watu. naona kama ni mapema sana kwa yeye kuanza kuwania nafasi hiyo. pili dadangu hivi wewe hushangai kwa nini awe zitto tu 'anayepingwa' na si wengine kama kina Mnyika, Mdee, Nassari, kwani hata nao ni vijana na ninaamini upstairs wako vizuri tu?


 
Zitto Zuberi Kabwe... The man himself! Mimi napenda kusoma tu vile wadau ambavo wanawaka moto na kutoa maneno ya hasira dhidi yake wakisikia huyu mkuu katamka kugombea.. Huwa natamani ningekuwa najua siasa kama wao (ambao wapo against) ili nielewe vipengele hivi.

  1. Hawapendi sababu anaungwa mkono na CCM wengi na maybe sababu inaonekana anapatana na baadhi kama vie Makamba Jr.? (Imagine Makamba Jr. katamka kua Zitto ni mwanasiasa ambae he is impressed by)
  2. Hawapendi sababu ni tishio kwa anayetazamiwa kugombea kwa chama hicho ambaye ni Mh. Dr. Slaa?
  3. Hawapendi sababu wanaona hafai na wala hana sifa za uongozi? AMA
  4. Hawapendi sababu ipi hasa? Kwanini watu wanachanganikiwa sana wakisikia Zitto in the lines of Presidency?

Kama kuna mtu wa kujijibu hayo kwa kina na ufasaha nitashukuru saana.
Amegeuka kuwa power monger...kiongozi mzuri atachaguliwa tu. Kwa nini kuhangaika hivyo????? Tunaogopa the secret behind...and it is obvious kwamba anataka kuvuruga chama na kuleta makundi yale ya mamvi...
 
wegi wanafuata mkumbo wa mawazo hawajui siasa ya Tanzania na hasa siasa ya CDM, wanamuandama zzk kwasababu fulani anampinga bila kuwa na mtazamo chanya. Tumefungwa fikra na viongozi wa CDM tumekuwa wendawazimu.
 
Amegeuka kuwa power monger...kiongozi mzuri atachaguliwa tu. Kwa nini kuhangaika hivyo????? Tunaogopa the secret behind...and it is obvious kwamba anataka kuvuruga chama na kuleta makundi yale ya mamvi...

wegi wanafuata mkumbo wa mawazo hawajui siasa ya Tanzania na hasa siasa ya CDM, wanamuandama zzk kwasababu fulani anampinga bila kuwa na mtazamo chanya. Tumefungwa fikra na viongozi wa CDM tumekuwa wendawazimu.
 
wegi wanafuata mkumbo wa mawazo hawajui siasa ya Tanzania na hasa siasa ya CDM, wanamuandama zzk kwasababu fulani anampinga bila kuwa na mtazamo chanya. Tumefungwa fikra na viongozi wa CDM tumekuwa wendawazimu.

Mkuu Baba Clara,
Tufafanulie hizo Siasa za Tz, hasa CDM maana Zitto alipendwa sana na wanaCDM hadi kufikia gari yake kusukumwa alipofukuzwa Bungeni, sasa hivi kwa nini hali imekuwa kinyume hata kabla ya kutangaza kugombea Urais? Kilichobadilisha wanaCDM ni kipi hasa?
Pia kinachowafanya baadhi ya WanaCCM kumpenda Zitto kwa sasa ni kipi hasa? Why this U-TURN kwa CDM na CCM (hata JK kusafiri naye huku akiacha M4C ikiendelea)?
Usiishie tu kutoa mawazo ya jumla jumla kuwa watu hawajui siasa za Tanzania/CDM huku wewe unayedai kujua nako husemi unachokijua, kazi kwako sasa!
 
Last edited by a moderator:
wegi wanafuata mkumbo wa mawazo hawajui siasa ya Tanzania na hasa siasa ya CDM, wanamuandama zzk kwasababu fulani anampinga bila kuwa na mtazamo chanya. Tumefungwa fikra na viongozi wa CDM tumekuwa wendawazimu.

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009 SHIDA Salum, mama mzazi wa SHIDA Salum, mama mzazi wa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha Maendeleo na Demokrasia
(CHADEMA), Zitto Kabwe,
ameibuka na kusema mwanaye
anatumiwa kukivuruga chama chake. Akizungumzia taarifa
zinazoandikwa na baadhi ya
magazeti kuhusu kinachoitwa
mgogoro wa uongozi katika
CHADEMA, kati ya Zitto na
viongozi wenzake, Shida alisema, “hakuna mgogoro pale,
kuna kikundi cha watu
wanaotaka kumtumia
mwanangu kufanikisha mambo
yao.” Akizungumza na gazeti hili juzi
jijini Dar es Salaam, alidai kuna
watu walio nje ya CHADEMA
wanakula njama za
kumgombanisha mwanawe na
viongozi wenzake. Alisisitiza, “kuna baadhi ya
wanasiasa ndani ya CHADEMA
wanaotumiwa na walio nje
kugombanisha viongozi.” Akaongeza, “Mambo ya
uchaguzi yalikwisha kitambo na
Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumaliza tofauti zake
na Mbowe (Freeman Mbowe)
ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee
wa uenyekiti.” Shida aliwatuhumu watu walio
nje ya CHADEMA akisema ndio
wanaopandikiza mbegu za
chuki kwa lengo la kuwavuruga.
Hata hivyo, hakuwataja. Alisema kila mwenye akili
timamu anajua kinachotafutwa,
na nani mkweli na yupi
anasingiziwa. “Angalia wanaoandika haya.
Kweli Zitto anaweza kutetewa
na magazeti ya Habari
Corporation yanayomilikiwa na
Rostam Aziz halafu ukaamini
kile kinachoandikwa?” alihoji. Aliongeza, “Rostam yupi? Ni
huyu tunayemjua au mwingine?
Kwa wema upi alionao kwa
chama chetu.” Wiki iliyopita magazeti ya Rai
na Mtanzania yalinukuu taarifa
zikidai kuwa zimetolewa na
Shida, kwamba anataka
mwanawe aondoke kwenye
chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa
“kumwepuesha na yaliyomkuta
Chacha Wangwe.” Katika kujibu hilo, Shida
anasema, “Mimi na Zitto tunajua
katiba ya chama chetu.
Tunafahamu taratibu za
kuendesha chama. Yeye ni naibu
katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini
maana ya uongozi, hivyo
hatuwezi kukurupuka
barabarani. “Kwamba kama kuna
malalamiko au tuhuma
mathalani juu ya uteuzi wa
wabunge wa viti maalum, basi
sote ni sehemu ya hicho
kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya
hatuhusiki na tukatuhumu
kupitia vyombo vya habari, tena
magazeti yanayomilikiwa na
mwanachama wa CCM.” Shida alisema anajua kwa
mapana chanzo cha yote
yanayoandikwa na jitihada za
kutaka kumgombanisha Zitto na
viongozi wenzake, hasa Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti
wake, Freeman Mbowe. “Yote haya tunafahamu chazo
chake. Si uchaguzi wa ndani ya
chama. Uchaguzi ulishakwisha
na Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumuachia Mbowe
uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama,” alisema. Alisema kuwa yeye kama mlezi,
hawezi kuruhusu hali hiyo,
hivyo atatumia nafasi yake ya
mjumbe wa CC kuhakikisha
kwamba tabia hiyo ya
kugombanisha viongozi inakoma. “Nikiwa mzazi, mlezi na
mjumbe wa kamati kuu ya
CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto
kutumika kuingiza chama
katika mgogoro. Nitasimama
imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama,”
alisema. Wiki iliyopita, Dk. Slaa
aliwaondoa katika nafasi za
utendaji David Kafulila
aliyekuwa Afisa Habari na
Danda Juju aliyekuwa Afisa
anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile
kinachoelezwa kuwa utovu wa
nidhamu kwa chama na
viongozi wake. Kafulila alinukuliwa na baadhi
ya magazeti kuwa alibeza kikao
cha viongozi wa juu wa chama
hicho kilichofanyika Dodoma
ambapo Mbowe na Dk. Slaa
walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa
chama hicho na baadhi ya
wakurugenzi. Kafulila alisema mkutano huo
wa viongozi haukuwa na
maana; na alifika mbali zaidi
kwa kuufananisha na vikao vya
geto. Ni matamshi hayo na
mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya
kikatiba kumuondoa Kafulila
katika wadhifa huo. Taarifa zinasema hoja ya
kumuondoa Kafulila katika
kikao ilitolewa na Msafiri
Mtemelwa, mmoja wa viongozi
wake na ambaye alikuwa
meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti
wa CHADEMA.
Suorce: MwanaHALISI.
 
Hivi kama Zitto siyo a "force" kama mnavyodai na hatoshinda uchaguzi ndani ya chama kwa nini mnaogopa hata akitangaza tu nia? kwa nini msiache wagombea wote watangaze, wapelekwe kwenye vikao muhimu 9ambako usalama wa taifa na vyombo vingine vya kijasusi vya CCM havitakuepo au kutokua na nguvu) na kura zipigwe kwa haki na mshindi Dr Slaa atangazwe (kwa sababu inaonekana mna uhakika na ushindi wake hapa JF). Hii itakua ni ishara ya CDM kukomaa kisiasa na kidemokrasia na itawapa wapiga kura taswira nzuri ya mgombea aliyepita kwa haki toka CDM (ukichukulia zoezi la CCM lazima litakua na mizengewe mingi) na hii itatupa moyo sisi wapiga kura kua demokrasia yetu italindwa na CDM pindi wakipata madaraka.

Haya mambo ya kubana demokrasia ndani ya chama hayaeleweki vizuri, hizi excuses za nidhamu, chama kidogo n.k basi kama ni chama kinachokua ni kidogo na hakihitaji mitingiso ya ndani basi wasigombanie urais, CDM ikue miaka 10 au 20 jengeni chama na demokrasia kwanza ili mkabidhiwe nchi kuliko kusema hatutaki mamluki au oh nidhamu lazima ifuatwe, nidhamu gani ya kuabudu miungu watu wasioguswa?
 
Nachoshangazwa mimi ni kuwa kwa nini watu wengi ambao si Chadema wanaonekana kushupalia kumuunga mkono Zitto?!! Mfano huyu Hamis Andrea. Yaani katika hali ya kawaida uibuke umuunge mkono hivi hivi mtu ambaye atakuja kupambana na mtu ambaye chama chako kitamsimamisha? Iko namna hapa. Na ndio maana sishangai tuhuma kuwa Zitto anatumika. Wakina Hamis Andrea wanajua kabisa ndani ya Chadema hakuna utaratibu wa kutangaza nia katika ngazi ya Urais na ndio maana wanashadadia kitendo cha Zitto maana wangependa kuiona Chadema inakuwa kama CCM kwa kutengeneza makundi ya wataka Urais. Ndo maana navyoona tarumbeta za kina Hamis Andrea huwa natumia jicho la tatu kupata tafsiri ya wanachomaanisha.

Zitto asiyumbishe watu, kama anataka kuwa rais ni sawa lakini ni lazima awaonyeshe watanzania kuwa atawafanyia nini. Suala sii kutangaza nia tu kila apatapo nafasi ya kuzungumza. Chama chake kiko busy na kujijenga vijijini na hatumsikii kwenye hizo kampeni akimwaga sera zinatakazo mwonyesha kuwa kweli ni kifaa cha kuwa rais. Namshauri afanye kwanza homework yake vizuri na wakati utakapowadia nguzu ya umma utaamua hata kama kwenye chama chake wataona vinginevyo.
 
Mkuu Baba Clara,
Tufafanulie hizo Siasa za Tz, hasa CDM maana Zitto alipendwa sana na wanaCDM hadi kufikia gari yake kusukumwa alipofukuzwa Bungeni, sasa hivi kwa nini hali imekuwa kinyume hata kabla ya kutangaza kugombea Urais? Kilichobadilisha wanaCDM ni kipi hasa?
Pia kinachowafanya baadhi ya WanaCCM kumpenda Zitto kwa sasa ni kipi hasa? Why this U-TURN kwa CDM na CCM (hata JK kusafiri naye huku akiacha M4C ikiendelea)?
Usiishie tu kutoa mawazo ya jumla jumla kuwa watu hawajui siasa za Tanzania/CDM huku wewe unayedai kujua nako husemi unachokijua, kazi kwako sasa!


kaka kama viongozi wa CDM wanapokea pesa za kada wa CCM sabodo ni vipi zzk aonekane anakosa, ukitaka kujua kwann zzk anapingwa sana utagundua kuwa hapo zamani zzk na m/kt walikuwa marafiki sana tena z alikuwa analala kwa m/kt, ila kijana alipokuja kutangaza kuwa anutaka uenyekt hapo ndio mabeef yalipo anza, mara z kafanya vile mara z kawa vile......siendelei
 
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 18 November 2009 SHIDA Salum, mama mzazi wa SHIDA Salum, mama mzazi wa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha Maendeleo na Demokrasia
(CHADEMA), Zitto Kabwe,
ameibuka na kusema mwanaye
anatumiwa kukivuruga chama chake. Akizungumzia taarifa
zinazoandikwa na baadhi ya
magazeti kuhusu kinachoitwa
mgogoro wa uongozi katika
CHADEMA, kati ya Zitto na
viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale,
kuna kikundi cha watu
wanaotaka kumtumia
mwanangu kufanikisha mambo
yao." Akizungumza na gazeti hili juzi
jijini Dar es Salaam, alidai kuna
watu walio nje ya CHADEMA
wanakula njama za
kumgombanisha mwanawe na
viongozi wenzake. Alisisitiza, "kuna baadhi ya
wanasiasa ndani ya CHADEMA
wanaotumiwa na walio nje
kugombanisha viongozi." Akaongeza, "Mambo ya
uchaguzi yalikwisha kitambo na
Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumaliza tofauti zake
na Mbowe (Freeman Mbowe)
ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee
wa uenyekiti." Shida aliwatuhumu watu walio
nje ya CHADEMA akisema ndio
wanaopandikiza mbegu za
chuki kwa lengo la kuwavuruga.
Hata hivyo, hakuwataja. Alisema kila mwenye akili
timamu anajua kinachotafutwa,
na nani mkweli na yupi
anasingiziwa. "Angalia wanaoandika haya.
Kweli Zitto anaweza kutetewa
na magazeti ya Habari
Corporation yanayomilikiwa na
Rostam Aziz halafu ukaamini
kile kinachoandikwa?" alihoji. Aliongeza, "Rostam yupi? Ni
huyu tunayemjua au mwingine?
Kwa wema upi alionao kwa
chama chetu." Wiki iliyopita magazeti ya Rai
na Mtanzania yalinukuu taarifa
zikidai kuwa zimetolewa na
Shida, kwamba anataka
mwanawe aondoke kwenye
chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa
"kumwepuesha na yaliyomkuta
Chacha Wangwe." Katika kujibu hilo, Shida
anasema, "Mimi na Zitto tunajua
katiba ya chama chetu.
Tunafahamu taratibu za
kuendesha chama. Yeye ni naibu
katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini
maana ya uongozi, hivyo
hatuwezi kukurupuka
barabarani. "Kwamba kama kuna
malalamiko au tuhuma
mathalani juu ya uteuzi wa
wabunge wa viti maalum, basi
sote ni sehemu ya hicho
kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya
hatuhusiki na tukatuhumu
kupitia vyombo vya habari, tena
magazeti yanayomilikiwa na
mwanachama wa CCM." Shida alisema anajua kwa
mapana chanzo cha yote
yanayoandikwa na jitihada za
kutaka kumgombanisha Zitto na
viongozi wenzake, hasa Katibu
Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti
wake, Freeman Mbowe. "Yote haya tunafahamu chazo
chake. Si uchaguzi wa ndani ya
chama. Uchaguzi ulishakwisha
na Zitto kwa moyo mmoja
alikubali kumuachia Mbowe
uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema. Alisema kuwa yeye kama mlezi,
hawezi kuruhusu hali hiyo,
hivyo atatumia nafasi yake ya
mjumbe wa CC kuhakikisha
kwamba tabia hiyo ya
kugombanisha viongozi inakoma. "Nikiwa mzazi, mlezi na
mjumbe wa kamati kuu ya
CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto
kutumika kuingiza chama
katika mgogoro. Nitasimama
imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama,"
alisema. Wiki iliyopita, Dk. Slaa
aliwaondoa katika nafasi za
utendaji David Kafulila
aliyekuwa Afisa Habari na
Danda Juju aliyekuwa Afisa
anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile
kinachoelezwa kuwa utovu wa
nidhamu kwa chama na
viongozi wake. Kafulila alinukuliwa na baadhi
ya magazeti kuwa alibeza kikao
cha viongozi wa juu wa chama
hicho kilichofanyika Dodoma
ambapo Mbowe na Dk. Slaa
walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa
chama hicho na baadhi ya
wakurugenzi. Kafulila alisema mkutano huo
wa viongozi haukuwa na
maana; na alifika mbali zaidi
kwa kuufananisha na vikao vya
geto. Ni matamshi hayo na
mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya
kikatiba kumuondoa Kafulila
katika wadhifa huo. Taarifa zinasema hoja ya
kumuondoa Kafulila katika
kikao ilitolewa na Msafiri
Mtemelwa, mmoja wa viongozi
wake na ambaye alikuwa
meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti
wa CHADEMA.
Suorce: MwanaHALISI.


Huo ulikuwa mtazamo wa mzazi wake lakini naye mtoto anamsimamo wake
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom