Naunga mkono Zitto kuwania urais - Kigwangalla

Kwanini umfukuze udiwani/ uanachama mtu aliyepiga kura kwenye uchaguzi wa halmashauri ya jiji/manispaa? Does that make sense to you? Au umfukuze mbunge aliyesema mwenyekiti hafanyi la maana? (Hamad).
Hivi filikunjombe angekuwa CDM si angefukuzwa kwa kutokuwa na imani na PM?
Kwanini basi, hamkumfukuza Zitto kwa kutosusia hotuba ya rais ambaye baadae mmemkubali?
Na mzee mwanakijiji acha kugeneralize swali lako la kichovu, ni vizuri ungespecify characteristics za wabunge na viongozi wa CCM wanaomkubali Zitto...... Young and rebellious unlike the status quo....old, fake, misinformed, unpatriotic, partisan and above all BORING!!!

ukijifunza kuzungumza kama mtu wa kuheshimika utaheshimika. Kama swali ni la kichovu unajaribu kulijibu la nini kama siyo kuthibitisha uchovu wako mwenyewe wa kufikiri?
 
ukijifunza kuzungumza kama mtu wa kuheshimika utaheshimika. Kama swali ni la kichovu unajaribu kulijibu la nini kama siyo kuthibitisha uchovu wako mwenyewe wa kufikiri?
Unajua kabisa kama ungeliframe swali lako kuwa "Kwanini wabunge wengi vijana wa CCM ....." jibu lingekuwa tofauti.
Ila kwa makusudi umesema kwanini wabunge na viongozi wa CCM (kwa ujumla au kwa wingi). Sasa huo ni uchovu na inabidi uelezwe ukweli. Heshima is a relative term na unafiki au uchochezi hauwezi ku-earn heshima.
Come again, that was a lazy question.
 
Kigwangala karibu chadema kaka naona umeona mbali kuwa 2015 CCM hutoki, njoo huku kwa waungwana wanao jua nini maana ya demokrasia. Hongera kwa kumuunga mkono Zitto
 
Unajua kabisa kama ungeliframe swali lako kuwa "Kwanini wabunge wengi vijana wa CCM ....." jibu lingekuwa tofauti.
Ila kwa makusudi umesema kwanini wabunge na viongozi wa CCM (kwa ujumla au kwa wingi). Sasa huo ni uchovu na inabidi uelezwe ukweli. Heshima is a relative term na unafiki au uchochezi hauwezi ku-earn heshima.
Come again, that was a lazy question.
Ahhh mkuu wangu sio wewe unayepingana siku zote na swala la ku generalize, Ujana vs Wazee, mara leo imetokea vijana wawili sijui watatu wa CCM unataka isomeke vijana wengi wa CCM...Kwa nini mkenge huu wanaupandisha kwa ZZK badala ya wao wenyewe vijana ambao wapo CCM kusiko kuwa na matatizo ndio wamsemee ya CDM kusiko wahusu - Think mkuu wangu think..
 
Kobello,
Penigne tuandike wa ufupi ya kwamba KATIBA ya Jamhuri inasema wazi kwamba mgombea Urais lazima awe na umri wa miaka 40. Zitto hatakuwa na umri huo. Hatari yake ni pamoja na kwamba hivi sasa hata chama chake kikishinikiza umri ushushwe hadi miaka 35 itaonekana wanafanya hivyo ili kumwezesha Zitto agombee. Hivyo Chama kinapendekeza sheria kutokana na mgombea wake sio kuafiki ukweli kwamba Umri sio kigezo cha uongozi..Hivi unataka kunambia ZZK anaweza kuhamia CCM kwa sababu anataka kusimama kugombea kiti cha Urais, hivyo anakaribishwa?. Mnaijua CCM ama basi tu mnasema ili mradi malengo yenu yatimie kupitia The weakest link hii..

Watu wengi tunachomshauri ZZK ni kujijenga na wenzake ili kuwe na msimamo mmoja kutoka chama chake na sio kila mtu anataka nini pasipo utaratibu. Tumeyaona haya wakati wa Chacha Wangwe na nakumbuka Kafulila aliandika mengi sana kuhusu ukosefu wa NIDHAMU wa kiongozi yule marehemu lakini maajabu ikafuatiwa na yeye mwenyewe, halafu leo tunamuona ZZK pia akifuata mkondo ule ule..Hakuna mtu anayepinga uwezo wa ZZK ktk uongozi, na ndio maana yupo meza kubwa, lakini njia anazotumia kutafuta nafasi hiyo ndio haifai, hivyo kutofaa kwa njia zake haina maana tunasema ZZK hafai..

Bro
unamaanisha kuwa Hadi 2015 ZItto atakuwa hajafikisha miaka 40?
 
Bro unamaanisha kuwa Hadi 2015 ZItto atakuwa hajafikisha miaka 40?
Bado na ndio maana kawachanganya wengi maana swala hili lingesimikwa na Bavicha au UVCCM kwanza ili umri upitishwe halafu ndipo mtu/watu wanajipanga nyuma ya hoja yenyewe..
 
I can not support a person who is all about himself and full of meandering ways and a cohort of ccm....an enemy from within...
asante
 
Ahhh mkuu wangu sio wewe unayepingana siku zote na swala la ku generalize, Ujana vs Wazee, mara leo imetokea vijana wawili sijui watatu wa CCM unataka isomeke vijana wengi wa CCM...Kwa nini mkenge huu wanaupandisha kwa ZZK badala ya wao wenyewe vijana ambao wapo CCM kusiko kuwa na matatizo ndio wamsemee ya CDM kusiko wahusu - Think mkuu wangu think..
Ukifikiria sana, hata samaki huwezi kumla. Haya mambo ya vyama mnayakuza mno.
Ndiyo, mimi sipendelei ku-generalize mambo na nikauliza, hivi kweli mtu unaweza kusema wabunge na viongozi wengi wa CCM wanataka Zitto awe rais? Where did you get that?
Kuna aina ya watu regardless of their party affilliation, wanakubali azma ya zitto. Azma inaweza isifikie level ya rasmi.
Na rasmi bila ridhaa ya wanachama wenzako, au rasmi bila ridhaa ya wananchi kwa ujumla baada ya kukubaliwa na wanachama wenzako haitakupa madaraka unayoyawania.

My problem is, kutaka kuuaminisha umma kuwa Zitto yupo kuiangamiza CDM, simply because he often cross the aisle. Thats really dumb.
 
Mkuu wangu labda nikukumbushe tu kwamba aliyeanzisha swala la next Presidaa kuwa kijana ni JK akiwania kura za wananchi wa Kigoma ktk kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2010 akiwa jukwaani. Aliahidi mengi sana kuibadilisha Kigoma kuwa Dubai..Usanii ambao ZZK mwenyewe inaonyesha alitayaamini na hata mtazamo wake ukageuka ghafla kwa matumaini alopewa..Na toka siku ile ZZK ameiweka hoja hiyo kuwa mada kuu ya mtazamo wake ktk sera. Sasa tunajiuliza kwa nini JK ayaseme hayo akiwa Kigoma, sio Nzega wala Bumbuli halafu wapambe wengi wa CCM wanamyooshea kidole ZZK kama muweza badala ya WanaChadema wenyewe kumtunuku ZZK..

Sisi wengine tumejaribu sana kumshauri, ajitazame upya na kwa habari tulizonazo ni kwamba ZZK anatumiwa makusudi kuweza kukibomoa chama. Why cross the aisle when you have your seat - a designated seat?..

Mkuu wangu hivi kweli wewe unaona hakuna Ubaya mbunge yeyote kuhama kiti chake bungeni akenda kukaa upande wa chama kingine halafu akizunguza kama mwakilishi wa upande ule na akapigiwa makofi?... This is what ZZK is doing hivyo hata siye tunaompa support kubwa ktk uwezo wake tunashindwa kumtetea esp. anapoutaka Urais kabla ya sheria kupitishwa wala kujadiliwa na chama chake kupendekeza.

Ndio maana niliwahi kusema hakuna ugonvi baina ya ZZK na Mbowe isipokuwa majungu yanapikwa makusudi kiasi kwamba ZZK anaamini na anazidi kumezwa na unafiki ulopikwa makusudi. Na imefikia wakati ZZK sasa haaminiki kwa haya haya mambo madogo sana kufikia kutengwa na baadhi ya watu hivyo yeye anajiengua na anajenga mahusiano ya karibu na upande wa pili tena Kisiasa...Kuna mawasiliano mabaya sana kati ya ZZK na wanaCDM na yote hii inatokana na ambition yake badala ya yeye kukitumia chama kuwa nyuma yake..Sorry mkuu wangu tumejaribu lakini yaonyesha wazi ZZK kesha amua - LIWALO LIWE....
 
Mkuu Mkandara,

I was really interested na ile Interview ya Makamba Jr. In fact huwa nikibahatika kumuona katika kipindi achojieleza kwa lolote lile sikosi kumsikiliza. Mkuu Mkandara nakubaliana na wewe kuwa Makama Jr katumia busara za hali ya juu sana katika majibu yake ila ni wazi kuwa circumtances za Makamba na Zitto ni tofauti (hio ni IMO yangu). Wote ni vijana, ila Zitto katoka mbali compared to Makamba ambae kwa mtindo wa mfananisho wapo tofauti… Naweza hata sema kuwa January ni mdogo kwa Zitto Kisiasa.

Kwa kuzingatia yale ambayo kaongea January, naweza sema kuwa basi Zitto hajakosea kuweka wazi hilo wazo na takwa lake kuu la kuwa raisi. Sababu mtu wa kwanza Makamba Jr. kusema kuwa ana ‘mkubali’ (not the exact word) ni Zitto akitoa baadhi ya sababu ya kumkubali Zitto kama Kujituma kwake, consultation-seeing behavior toka wa wadau na wazee mbali mbali bila kujali wa chama gani, na tabia yake Zitto ya kusimamia lile ambalo analiamini.

Judging Zitto katika matamshi yake ya kuwania urais kwa mtindo wa comparative analysis Vs January kwa mtazamo wangu itakuwa SIO fair… Kwa misingi ya kuangalia umri, nguvu, uimara, sera na sababishi za uwepo wa vyama vyao (CCM Vs CDM) ni tofauti. Je nasapoti Zitto’s nature of Politics? That is another issue… Hapa what am trying to do is calling a spade a spade.

Umezungumzia taratibu za chama... Hizo taratibu za Chama (CDM) ndizo hasa am interested in. Mkuu Mkandara CDM hawana mzaha katika utendaji na upotofu wa nidhamu kwa jinsi nionavyo hadi sasa. Naamini hujasahau kuwa hapa juzi tu wametowa adhabu kali kwa wanachama wawili tena waliokuwa viongozi kwa kuwanyang’anya uwana chama. Hicho sio kitu kidogo mkuu… Wamethubutu na kuweza kuonesha mfano wa kulinda nidhamu ya hali ya juu kwa wavunjifu wa sheria. Hizo sheria naamini kuwa ni applicable kwa kila mwanachama haijalishi kuwa ni kiongozi.

Nabaki najiuliza, kama yooote ambayo huwa nayasoma hapa na pale kwa members hasa wale ambao hujibu hoja kwa hoja ni kweli mbona sijawahi kusikia tamko ama mahala popote pale kuwa Zitto kakalishwa maybe kiti moto na chama ili aweze eleza tuhuma mbali mbali? Kwa nini tushangae la Zitto kutangaza Uraisi lakini tusishangae kwa Zitto kutoa hoja nyingine independently (ziwe za kujenga ama kubomoa tegemeana na observer e.g. hili la Gas na Oil). Mie sina shida kabisa kuwa Zitto katamka ama kuto tamka… Ila napeda nielewe why the remarks against him zipo so very fierce toka kwa wana CDM…

My analysis ya Zitto (strictly kwa mtazamo wangu) ni kuwa ni mtu ambaye anajuwa kuwa anaweza na kwamba kwa uwezo wake nafasi aliyopo na anayotumikia sasa ni chini ya uwezo wake. Yaani yeye ni overqualified for the position he is holding… Nafikiria kuwa anaamini kuwa CDM kuna watu wengi wanaweza kuwa viongozi, ila anaona kama yeye kawiva kwa hio nafasi kuliko wote na he deserves it more. Naamini kuwa anaamin kuwa kaijenga CDM kuliko mtu yeyote Yule…

Naona kama anaona wanaompinga ni wale tu ambao wameijua CDM ya leo tena kwa mtutu wa M4C, naamini anaamini kuwa majority ya wana Tanzania waliopo CDM wanamkubali vilivyo na kwamba akichaguliwa yeye kuwania uraisi kuna nafasi kubwa ya CDM kushinda uraisi kuliko mtu yeyote Yule. Naweza sema pia kuna some sort of desperation akiamini kuwa kama CDM itashindwa kushukua ushindi 2015 basi hakuna hope hadi 2025 ambapo kwa yeye ambae ana dreams za kuwa juu ya alipo ni mbali mno! Na inakatisha tamaa kwake.

Am I right/wrong? sielewi... Ila linalobaki hapa ni swali kuwa hizo assumptions nilizonazo, ni mimi peke yangu ninazo ama wana CDM pamoja na baadhi ya viongozi wanayo pia? Na zaidi kama wengi wanazo hizo assumptions hapo juu je wanaziamini? Maana kama wanaziami… That would explain the explosion toka kwa majority kila itokeapo Zitto katajwa in the lines of politics…

Inabaki tu kujiuliza mtu ana watu wanamkubali toka kambi zote CCM vs CDM... Viongozi mbali mbali hasa wapinzani wanam support Zitto. Kama tulivoona January, sasa Kigwangalla naamini na wengine wengi. Ni ajabu tu kuwa hakuna linalotamkwa na viongozi wenzake wa CDM, whether sababu wanaogopa kash kash kama iliyotokea mara ya mwisho Kigoma kwa akina Mdee, Nassari, Filikunjobe et al or for what ever reasons, viongozi wa CDM pekee ndio wanaelewa hilo...

Take note sitaki ni assume kuwa Zitto analaumiwa na kuitwa msaliti kwa sababu fulani fulani... Ila naona ingekuwa bora zaidi wale ambao wanachukia hizo tabia na kutomkubali Zitto waeleze hasa kuwa huyu mkuu ana tatizo wapi hasa, nje ya hiyo makala aliyonipa Matola hapo nyuma.

AshaDii labda nikikumbushe kuwa Zitto ameshasema kuwa hataki kugombea tena ubunge kwa sababu yale ambayo hajaweza kuyafanya katika nafasi yake ya ubunge hataweza tena kuyafanya hata akipewa muda zaidi, sasa iweje utuambie eti nafasi aliyo nayo sasa ni chini ya uwezo wake?
 
zito awe rais haaingii akilini ubunge ndo saizi yake na hata chadema wote wajue tu watakuwa wabunge urais ni hell NOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Ngoja nimsaidie Kigwangala kama Zitto atagombea urais basi mgombea mwenza awe Hussein Bashe.
Mimi nadhani HK ana sababu zake za msingi za kumunga mkono ZZK...tumuulizeni atwambie kuliko kumshambulia namna hii

Hata hivyo kila mtu ana haki ya kuamua amuunge mkono nani kwenye nini , hussein basha nimeona kuna post inaelezea uraia wake sasa atakuwaje mgombea mwenza???
 
Mkuu wangu labda nikukumbushe tu kwamba aliyeanzisha swala la next Presidaa kuwa kijana ni JK akiwania kura za wananchi wa Kigoma ktk kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2010 akiwa jukwaani. Aliahidi mengi sana kuibadilisha Kigoma kuwa Dubai..Usanii ambao ZZK mwenyewe inaonyesha alitayaamini na hata mtazamo wake ukageuka ghafla kwa matumaini alopewa..Na toka siku ile ZZK ameiweka hoja hiyo kuwa mada kuu ya mtazamo wake ktk sera. Sasa tunajiuliza kwa nini JK ayaseme hayo akiwa Kigoma, sio Nzega wala Bumbuli halafu wapambe wengi wa CCM wanamyooshea kidole ZZK kama muweza badala ya WanaChadema wenyewe kumtunuku ZZK..

Sisi wengine tumejaribu sana kumshauri, ajitazame upya na kwa habari tulizonazo ni kwamba ZZK anatumiwa makusudi kuweza kukibomoa chama. Why cross the aisle when you have your seat - a designated seat?..

Mkuu wangu hivi kweli wewe unaona hakuna Ubaya mbunge yeyote kuhama kiti chake bungeni akenda kukaa upande wa chama kingine halafu akizunguza kama mwakilishi wa upande ule na akapigiwa makofi?... This is what ZZK is doing hivyo hata siye tunaompa support kubwa ktk uwezo wake tunashindwa kumtetea esp. anapoutaka Urais kabla ya sheria kupitishwa wala kujadiliwa na chama chake kupendekeza.

Ndio maana niliwahi kusema hakuna ugonvi baina ya ZZK na Mbowe isipokuwa majungu yanapikwa makusudi kiasi kwamba ZZK anaamini na anazidi kumezwa na unafiki ulopikwa makusudi. Na imefikia wakati ZZK sasa haaminiki kwa haya haya mambo madogo sana kufikia kutengwa na baadhi ya watu hivyo yeye anajiengua na anajenga mahusiano ya karibu na upande wa pili tena Kisiasa...Kuna mawasiliano mabaya sana kati ya ZZK na wanaCDM na yote hii inatokana na ambition yake badala ya yeye kukitumia chama kuwa nyuma yake..Sorry mkuu wangu tumejaribu lakini yaonyesha wazi ZZK kesha amua - LIWALO LIWE....
Pole Mkandara kwa ushauri wako kutokufuatwa.
kwani kuna ubaya gani zzk akiamua kutangaza nia yake ya kugombea urais? na kwa nini useme kuwa akiutaka urais tu basi ndo anakuwa adui wa mbowe ama wa dkt.? mimi nadhani nyie mnaomshauri asigombee na mnaomchukia mna wagombea wenu na yeye mnaona kama threat kwa mgombea wenu hivyo mnajidai kumnasihi asigombee kwa kuogopa atawafunika wagombea wenu. mimi nawashauri wote mmuache aendelee na nia na mchakato wake wa kugombea na ikifika kwenye vikao halali ashindwe lakini siyo kumkandya na kumuona amekuwa adui maana kufanya hivyo ni kuua demokrasia ndani ya chama na nchi
 
Hoja : Wana ccm wanaomuunga mkono zitto
kutangaza nia ya kugombea urais "je,
wanampenda zitto kabwe au wanamhofia dr.
Slaa?".
Mimi binafsi simuungi mkono zzk lakini pia sidhani kama Dkt. Slaa ni candidate mzuri sana wa nafasi ya urais. nafikiri chadema watafute mgombea mwingine wa urais. Mbowe angekuwa a bit serious angeweza kuwa right candidate wa nafasi hiyo ila nadhani bado kiadogo
 
Mkuu wangu labda nikukumbushe tu kwamba aliyeanzisha swala la next Presidaa kuwa kijana ni JK akiwania kura za wananchi wa Kigoma ktk kampeni zake za uchaguzi wa mwaka 2010 akiwa jukwaani. Aliahidi mengi sana kuibadilisha Kigoma kuwa Dubai..Usanii ambao ZZK mwenyewe inaonyesha alitayaamini na hata mtazamo wake ukageuka ghafla kwa matumaini alopewa..Na toka siku ile ZZK ameiweka hoja hiyo kuwa mada kuu ya mtazamo wake ktk sera. Sasa tunajiuliza kwa nini JK ayaseme hayo akiwa Kigoma, sio Nzega wala Bumbuli halafu wapambe wengi wa CCM wanamyooshea kidole ZZK kama muweza badala ya WanaChadema wenyewe kumtunuku ZZK..

Sisi wengine tumejaribu sana kumshauri, ajitazame upya na kwa habari tulizonazo ni kwamba ZZK anatumiwa makusudi kuweza kukibomoa chama. Why cross the aisle when you have your seat - a designated seat?..

Mkuu wangu hivi kweli wewe unaona hakuna Ubaya mbunge yeyote kuhama kiti chake bungeni akenda kukaa upande wa chama kingine halafu akizunguza kama mwakilishi wa upande ule na akapigiwa makofi?... This is what ZZK is doing hivyo hata siye tunaompa support kubwa ktk uwezo wake tunashindwa kumtetea esp. anapoutaka Urais kabla ya sheria kupitishwa wala kujadiliwa na chama chake kupendekeza.

Ndio maana niliwahi kusema hakuna ugonvi baina ya ZZK na Mbowe isipokuwa majungu yanapikwa makusudi kiasi kwamba ZZK anaamini na anazidi kumezwa na unafiki ulopikwa makusudi. Na imefikia wakati ZZK sasa haaminiki kwa haya haya mambo madogo sana kufikia kutengwa na baadhi ya watu hivyo yeye anajiengua na anajenga mahusiano ya karibu na upande wa pili tena Kisiasa...Kuna mawasiliano mabaya sana kati ya ZZK na wanaCDM na yote hii inatokana na ambition yake badala ya yeye kukitumia chama kuwa nyuma yake..Sorry mkuu wangu tumejaribu lakini yaonyesha wazi ZZK kesha amua - LIWALO LIWE....
Unavyofikiria wewe ni tofauti kabisa.
Yaani mtu awe CCM halafu atake kumwajibisha PM? .. au wewe ulikuwa unaona ni acting tu?
Kuhusu Mbowe na Zitto, usipende kuudanganya umma hao watu wawili hawapatani kisiasa wala usijidanganye mkuu.
'Labda nikuulize, unafikiri Mbowe au Zitto ni yupi yupo karibu na Ikulu? .... think!
 
Mkuu Mkandara,

Nimekupata kabisa… Naona pia hujanipata vema ama sijajieleza vizuri. Bado nasimamia utofauti wa Makamba Jr. na Zitto katika wao kutaka kugombea Uraisi. January is well articulated mkuu na napenda the way huwa anajenga mazingira ya msikilizaji kujenga ‘Imani' na ‘Amani' juu yake na maelezo ya maelezo yake ya vitendo dhidi ya wananchi… Na aliongea kitu kizuri sana. Akasema kuwa katika nchi hii hakuna mtu ambae ni kiongozi hana watu wanamwambia kuwa anafaa kuwa rais na kumshawishi agombee.

Mkuu sikubali na wala siamini kuwa Zitto ni mjinga na haelewi atendalo, kwamba hajaona impact ya hoja zake za kugombea zinavyoleta mzozo na jinsi zinavyo zua mijadala mbali mbali mingi ikiwa kinyume. Hapa kati kati kuna tatizo sio bure! Kama ulivyosema kwa mfano wake mwenyewe kuwa kuna kijana alitaka kugombea na akamjibu jibu la msingi kabisa… Kuwa wanachi ndio waamuzi; swala ambalo halina upingamizi.

Nimependa ulivyoeleza hapa… Kuwa Zitto ni mkweli mno… Sijui… Ila naweza sema kuwa Zitto ni mkweli katika yale ambayo anapigania yaende na yawe vile atakavyo. Siamini kuwa huwa anatoa ukweli wote wa mambo kadha wa kadha. Na kusema kweli wa Mungu sioni kuwa ni tatizo la yeye kutangaza kutaka kuwania urais na niya yake ya kutogombea tena ubunge 2015 kwa kuamini kuwa kisha fanya ya kutosha chini ya ubunge na sasa inabidi asonge mbele tena.

Alafu mkuu sijui kama nakosea, ila ninavyofahamu so far yupo vizuri tu na vijana wenzio (else hio habari iwe imenipita pembeni). Mwisho wa yoote Mkuu, hadi sasa sijapata sababu za Msingi za Zitto kupingwa saana na wana CDM kuwa ni msaliti…. Tena anapingwa na wafuasi ila hatujasikia Mh. Mbowe ama Dr. Slaa kuzungumzia swala lolote kuhusu usaliti wa Zitto. What really rattles them up?

Kwa nini hafai kugombea kwa mtazamo wako nimekupata kwa misingi ya haya;

  • Zitto hatangazi sera za Chama isipokuwa ni yake yay eye ataweza kufanya nini.
  • Zitto anajinadi na kujisifia (not the exact words) inatakiwa asubiri awe appointed sio yeye kujisemea.
  • Zitto ni mkweli mno! Hivo hafai kuwa raisi kiongozi inabidi awe mnafiki kidg ili kuweza ongoza wananchi wa aina yote.
  • Zitto anatakiwa kujifunza siasa ingawa ana niya nzuri na chama chake…

Mkuu Mkandara naomba niwe wazi… Hizo sababu zako hapo juu siamini kuwa ndio sababu ambazo wanazo wanao mpinga. Na sioni kuwa sababu hizo hapo juu ndio zinawez m'disqualify kuonekana hafai kuwa kiongozi na kupelekea mijadala mikubwa juu yake na assumptions juu ya nia yake.

My Take on Zitto na takwa lake la kugombea

Naona anafaa sana kuwa raisi sababu yupo aggressive, focused, hateteleki, hababaishwi na anajua nini ataka tena ni kijana ana nguvu ya kutosha. Kwa mtu wa namna hiyo faida kwa Tanzania ni kubwa sana… Hasara yake inakuja tu pale kama ni mbinafsi na si mzalendo. Hapo WaTanzania ni lazima tujibebe ikiwa kaingia kwa ajili ya tamaa na sio kwa ajili ya for a better Tanzania. Naomba pia niwe wazi kuwa eneo moja ambalo siwezi bet on him ni ‘Uzalendo' hapo sielewi kuwa Zitto ni Mzalendo ama sio… Kuna watu ni rahisi kujua but with Zitto kazi ipo. Yupo so calculative…

Na support kutangaza kwake kuwa anapeda awe rais ila tu huwa anani disappoint once in a while kwa tabia yake ya kufanya mambo yake independently nje ya Chama. Sijui ndani ya chama ikoje, ila mimi personally kwa mtazamo wangu naona kama vile yupo mbali kidogo na chama chake; inawezekana ni mtu wa namna hio kuwa anafanya kazi vizuri akiwa peke yake or what ever... Na pia naamini kuwa CDM wangeona hafai basi wangemtena, na kama hawawezi mtema na hali wameona wazi hafai basi Zitto would be right in thinking kuwa kwa kiasi kikubwa nguvu ya Chama ipo reliant kwake. Pia napenda the way anajichanganya na wazee wa pande zote zote (CCM na CDM) for naamini kuwa one a the qualities of a good leader ni kujichanganya hata na adui kujua hasa ana deal na mambo gani.

Pamoja na kusema kuwa naona anafaa kuwa rais, naona kuwa 2015 ni mapema sana, he will be a better one chaguzi kubwa zingine zaidi ya 2015. Nikiamini kuwa atakuwa zaidi ya alipo, more mature in politics as well as decisions za msingi zinazo faa dhidi ya jamii nzima katika nyanja mbali mbali nje ya maeneo yake of interest katika kuboresha, for instance mikataba na sera za Oil and Gas.

All in all, ni moja ya wanasiasa you never get bored ku observe nini linafuata.
 
Hahaa umemmaliza kigwangala akisikia hilo jina la Bashe nywele zinamsimama.
teh teh teh Kwenye chaguzi za CCM Kigwangalah kamsambaratisha Bashe vibaya sana...kasome FB yake jinsi anavyojifagilia mimi sidhani kama anamuogopa kiasi hicho
 
Back
Top Bottom