Naunga Mkono Bunge Kutoonyeshwa Live

Daaah haya mawazo yanatokana na lishe dunii sana tulizopata utotoni,kukosa uji wa ulezi na maziwa,mayai mayai,fat,wanga,protein ni muhimu sana kwa mtoto wa mwaka 0 mpaka 5.. Mtoto akikosa haya akiwa mkubwa lazima awe na IQ ya kukatisha tamaa yaani chini ya 10....Mungu tuokoe watanzania
 
humu jumvini kumekuwa kwa ajabu,kweli,hivi mtu anawezaje kufikiria kuleta topic kama hii?hivi huyu anayeleta anafahamu kwamba katiba ya jamuhuri ya muungani wa tz inaruhusu mtu kupata uhuru habari bila pingamizi yeyote?hivi huyu aliyeleta hii topic anafahamu editing inayofanywa na hiyo feeder na kutuletea kitu ambacho sio kabisa?nadhani tumewatuma watu bungeni na tunahitaji kuwasikia wakituwakilisha kwa kuchangia bungeni,ni vizuri pia mkiwa mnajifunga mambo kutoka kwa nchi zingine za dunia ya 3,maana mkisema UK wao wako dunia ya 1,huenda watu wengi wako busy na shughuli zao kiasi kwamba hawana nafasi ya kufuatilia bunge,lakini sisi walio wengi hatuna ajira,ndo maana utakuta wtu asubuhi wanaamka na pool table,sasa hawa unawanyima kuangalia bunge,at the same time hakuna ajira,hivi mnataka waende wapi hawa watu,juzi nimesikia nchi wanasema wanataka iwe ya viwanda wametenga bn 96 kwenye budget haya ndo mambo tunataka kuyasikia live,watueleweshe maana DAKOTE kiwanda kile kimoja ya cement alitumia kiasi cha 12trillion,sasa tunataka kujua hii bn 96 ni ya kitu gani?so msiwe wepesi wa kusahau we need bunge live and we are ready kulipia ikibidi lirushwe live:(:(:(
 
Inaonekana wewe uliyeleta agenda hii ni JIPU kwani hizi si zama zile za kufunika mambo mgombea mmoja na kivuli. Tafadhari naomba tafakari na kuzipima hoja zako.
 
Bila kujitoa ufahamu vijana wa Lumumba wamegundua huwez ukwaa uongozi,waacheni mapovu yawatoke
 
Kuna wabunge hawawezi kazi kabisa ila wanajua kupangilia maneno kweli. Wanaishi tu kwenye siasa za live bungeni kwakuzungumza mambo mazito kweli kweli na baadhi ni mahodari wa kudandia Hoja za wenzao.

Ukienda Jimboni kwake wananchi wake wanaishi kwenye dimbwi la umasikini, Hawa wabunge hawajitumi kabisa.

Hawaanzishi vikoba, Hawaanzishi miradi ya manufaa kwa wananchi wao,wana diplomatic passport lakini hwatafuti wafadhiri. Hebu tuwadhibiti kabisa waanze kufanya kazi Majimboni.

Napeeeeee futiilia mbali mbali mambo live wabunge wawe wanashinda kwa wananchi wakiwahudumia.
Hupew ukuu wa wilaya!!
 
1461574564463.jpg
Naunga mkono hoja ya Bunge kuto onyeshwa.
 
Cha msingi tunaangalia reaction za wananchi wengi sio kikundi cha mbowe kwani mahitaji muhimu ya wananchi wengi ni nini???? Na tujiulize wananchi wangapi huwa wanaangalia bunge live kila mjadala wa bunge unapokuwepo???lazima ifikie hatua watu tusiishi kwa mazoea kama mazombie serikali imetoa utaratibu mzuri bunge litaonyeshwa via recorded na wakiwa wamehariri hatua ambayo nadhani itapunguza mihemeko na kurejesha heshima ya bunge letu tukufu wale wabunge wa mipasho na wapiga kelele hatutawaona tena Bali tutaoneshwa chenye manufaa kwetu!!!
Masinki boy!!!
 
Kijana Pasco

Hivi nauliza tu, ile degree yako ulifanikiwa kumaliza kule kwa wadosi? au ulikata corner baada ya kukimbizwa? na ule utapeli wako ushauwacha kule mtaani?
Never mind nimegundua kuwa umekuja na style mpya ya kujipendekeza CCM ili mambo yaende vizuri.
Na ukitaka kujipendekeza lazima ujifanye huna akili.[/QUOT

Tumeshaamua hakuna LIVE !! maneno, kelele, na maandishi yenu hayatunyimi usingizi.
 
that is indirect democracy, badala ya wote kwenda dom tumewatuma wale sio vibaya kumuona uliyemtuma kama anafanya kazi kwa manufaa yako refer the concept of agent na principle
 
Kikao cha bunge ni kikao cha kikazi sio mkutano na waandishi wa habari (press conference).kuna tofauti ya kikao cha kikazi na press conference! Wanaotaka kugeuza bunge kuwa press conference ambamo muda wote waandishi wa habari wamo hawako sahihi

Wabunge wakishakaa na kumaliza kazi ya siku ndio taarifa za yale muhimu ya kazi na matokeo waliyofikia yanawekwa hadharani na maofisa habari wa bunge

Taarifa hizo haziwi na vitu vya kipuuzi kama vile vya mbunge gani amemtukana waziri au mbunge fulani kwa kumwita Kibaka nk.Zinakuwa na zile taarifa muhimu tu za kazi waliyofanya kwenye vikao.

Ikumbukwe pia kuwa Vikao vya kamati za bunge huwa havirushwi Live sababu ni vikao vya kikazi.Na kikao cha bunge ni kikao kikuu cha kikazi sio press conference .Sasa hivi wabunge watafanya kazi barabara kuliko zamani ambapo mara ingine mtu anaomba kuchangia ili tu auze sura kwenye TV aonekane.Wachangiaji unakuta wako msururu wakipigania tu kuonekana!!! Sasa hivi bunge litakuwa na wachangiaji very serious ambao wana hoja za nguvu na si wauza sura kwenye TV

Bunge la Tanzania litakuwa bunge la mfano la kuigwa duniani kwani litatoka na vitu serious vilivyofanyiwa kazi barabara na wabunge serious na habari zitakazotolewa ni zile za HAPA KAZI TU na si zile za mara mbunge kapigwa picha anasinzia bungeni nk


Pia Kazi kuu ya mbunge (Major duty) ni kuleta maendeleo kwenye jimbo lake anakotokea na si kuongeaa sana na kuchonga sana mdomo bungeni na kuanika sura sana kwenye kamera za Televisheni akiwa bungeni.Kuna wabunge majimboni hata kuwaona na kuwakuta ofisini kwao majimboni ni shida.Wao husubiri tu muda ufike wa bunge wachonge midomo na kuuza sura kwenye TV.

Siku Magufuli akisema Bunge lionyeshwa live mara moja,nina uhakika utakuwa wa kwanza kupiga makofi.Hongera lakini.Wengine tunataka tusikie live waongeayo.
 
Back
Top Bottom