Giza la Serikali ya Awamu ya Tano Kutoonyesha Bunge Live Dodoma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Na Kilawa the Iron

Ndugu zangu watanzania najua wengi wetu hatujui kuwa tumewekwa katika dimbwi lililojaa uchafu wa kila aina ilihali aliyetuweka katika dimbwi hilo akitudanganyishia asali kwa muonekano wa nje na wananchi wengi tumeamini kuwa tupo kwenye dimbwi lilojaa asali la hasha.

Hivi ni kweli sisi sote takribani watu karibu milioni hamsini hatuoni kuwa tupo katika lindi la giza nene ambalo linaweza kuathiri kuona kwetu kuwaza na kuwazua kwetu na fikra zetu ? Hivi ni kweli kwamba sisi sote hatujui kusoma na hata picha tu hatuoni?
Haiwezekani.

Japo wahenga walisema mwenye macho haambiwi ona lakini mm nadhani ni bora na ni vyema nikakutonya Mtanzania mwenzangu ili uone tu, maana haya yanayoendelea yataathiri kizazi hiki na kijacho tena kwa kasi ya mlipuko wa ebola, dengue au kipindupindu. Hata hivyo kwanini usione ndugu yangu wakati tunaambiwa macho hayana pazia? Funguka chukua hatua.

Ukilinganisha kwa haraka haraka tu, mtanzania yeyote akiulizwa swali kuwa je serikali ya awamu ya nne na ya tano ni serikali ipi inaonekana ni bora katika kuwatumikia wananchi? Najua asilimia kubwa hawatasita kusema serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli ipo vizuri zaidi, kwakuwa washaramba asali kwenye dimbwi la uchafu bila wao kujua, na pia watasema serikali ya mh Kikwete haikuwatumikia vyema japo utasikiwa wakiendelea kulalamikia ugumu wa maisha kila kukicha utawasikia afadhali ya jana,lakini hawakomi kusema hapa kazi tu.

Hata kama watajibu hivyo lakini ningependa watanzania wenzangu mkae chini kwa utulivu mjiulize maswali haya machache.
Kama serikali ya awamu ya tano inawatumikia wananchi vyema bila longolongo ni kwanini waweke zuio la kuoneshwa bunge moja kwa moja kama ilivyokuwa vipindi vilivyopita?
Je serikali hii inaogopa nini kitafichuliwa na wabunge wetu?
Inaficha jambo gani kwa wananchi wake ?
Kwanini wanaminya uhuru wa vyombo vya habari tena habari za kutoka bungeni ambako wawakilishi wetu wanakaa na kujadili yanayotuhusu moja kwa moja?
Ukiwa una mitazamo hafifu yaani yenye uwalakini hutanielewa kwa haraka.

Naomba ukumbuke kuwa mwanzo Mh Nappe Nnauye Waziri mwenye dhamana ya maswala haya ya habari alisema matangazo ya bunge hayataoneshwa live kwa sababu TBC inatumia pesa nyingi kurusha matangazo hivyo akasema watarekodi na vyombo vingine vitachukua kwao. Lakini waziri huyu hajiulizi kwamba serikali hiyo hiyo inayosema kurusha matangazo moja kwa moja kupitia television yetu ya taifa TBC ni gharama hadi sasa inakimbiza kitu kinachoitwa mwenge wa uhuru tena kwa gharama kubwa zaidi ya kurusha matangazo hayo moja kwa moja. Hii tabia kwa wataalamu mnaiitaje? Wanasaikolojia wataniambia kimya kimya.

Japo Mh Nappe alisema hivyo lakini wadau walijitokeza na kusema hapana si vyema wananchi hawa kukosa haki ya kuona wawakilishi wao wanachosema bungeni wakajitolea, wakasema watatoa pesa kufadhili matangazo hayo moja kwa moja, lakini serikali yetu haikukosa kisingizio na kukataa hilo mara oooh bunge litarekodi lenyewe na kuwapa kile inachoona kinafaa. Sasa swali je ni jambo gani ambalo mbunge aliyeaminiwa na watanzania kutoka jimboni kwake akachaguliwa kuwawakilisha ataongea lisiwe na maana au lisifae? Kama sio mazingaombwe ya serikali tukufu ni nini?

Serikali hii tukufu inayoturambisha asali wakati imetuweka kwenye dimbwi chafu haijaishia hapo imefikia hatua ya kusema hata waandishi wa habari ni marufuku kurekodi moja kwa moja wakati wa mjadala, hivyo wanapaswa kusubiri Television ya bunge iwape yale yatakayoonekana yanafaa wao kupata. Hivi ndivyo tulivyopigwa upofu wa akili hadi sasa.

Ndugu zangu wananchi tufunguke tuamue kwa pamoja tudai uhuru wetu usiminywe kwa maslahi yao wao waliowachache.
Hivi kweli kuanzisha tv ya bunge itakayorekodi sio gharama kuendesha? Hata kama sio gharama kwani ITV, Star tv na vyombo vingine vikiamua kurusha matangazo hayo moja kwa moja serikali itapata hasara gani jamani?
Kwani kurusha matangazo hayo ni hasara kubwa zaidi ya kashifa ya Lugumi, Escrow Mabehewa hewa n. k?

Mimi nadhani serikali iliyostahili kuyafanya haya ilikuwa ni serikali ya awamu ya nne kwakuwa madudu tuliyaona mengi sana tena yale ya wazi. Lakini imekuwa kinyume chake, yelewiiiiiiiii hii sasa ni shidaaaaaaa kilonga Ole Sosopi ni Shidaaaaaaaaaah

Katika hili serikali yetu inatupa picha ya wazi kuwa itafanya madudu mengi zaidi ya yale ya awamu zilizopita na haipo tayari kukosolewa, haipo tayari kuona inaanikwa kwa wananchi, haipo tayari kuona maovu yao watu wanayajadili popote, je huu ni utawala bora au uongozi bora? Ikumbukwe bunge ni muhimili unaojitegemea na bunge lina mamlaka ya kujiendesha.

Serikali yoyote yenye nia ya kuwa na utawala bora, utawala wa kisheria katika nchi ya kidemokrasia haina haja ya kuhangaika na kujificha kichakani kwa kuminya uhuru wa habari. Uhuru huu ambao ni haki ya msingi kikatiba.

Kwa wenzangu mimi waliosoma shule za St Kayumba bila shaka mnakumbuka tulisoma kitabu chenye stori moja ya mzee Tola, mzee aliyekuwa na tabia ya kula chakula gizani wakati watoto wake wakiwa wamelala. Lakini siku moja alijikuta kala konokono na kuaza kutapika. Hivyo serikali yetu imeamua kulia chakula gizani sisi watoto tuliomasikini tusione hicho chakula sasa imesahau kuwa chakula hicho kina konokono, tabia ya mzee Tola itawaumbua.

Ni aibu kubwa sana serikali inayojitanabaisha ulimwenguni kote kuwa inatumbua majipu kwa watumishi wa umma tena hadharani kwa tuhuma tu halafu yenyewe iogope kutumbuliwa bungeni na wabunge.

Serikali hii kama imeshauliwa na chama au watafiti au kutoka katika kundi lolote au mtu yeyote kwamba wasipoonesha bunge basi ni rahisi sana nchi kutokujua maovu ya serikali basi mmedanganywa zaidi mnajidharirisha tu kwa wananchi na mataifa mengine kwa hofu na woga mnaouonesha

Kama serikali ya awamu ya tano ni ya viwango vya juu hofu hii ya kuzuia bunge lisirushwe live inatoka wapi?

Naomba nisiende mbali zaidi, naomba niishie hapa ila tu serikali itafakali mara mbili na iangalie kwa jicho la kumi ione umuhimu wa bunge hili kurushwa moja kwa moja watu tupime kama tuliochagua wanatuwakilisha ipasavyo.
 
Tundu Lissu ndie anasababisha Bunge lisitangazwe live. Kwa sababu yeye ndie anayesema,'nafurahi zinapotokea vurugu pale Bungeni,watazamaji wanapata msisimko'
 
Wameidhibiti mitandao,wakadhibiti media na Mawio likawa mhanga..
wamedhibiti Bunge..
who is next ?
hizi ni dalili za kujitambua kutokubalika..
kama unapendwa huwezi kuogopa wakupendao..
 
Ipo video moja ya jamaa mmoja anaigiza watu kama Stephen Nyerere. Ile video naitafuta sasa nadhani imepotea. Labda haikuwapendeza Ikulu wameiondoa Facebook. Lakini naweza kuinukuu kidogo. Yule mtu anawaigiza watu wengi mwisho anamuiga Waziri wa Ujenzi,Magufuli. Kwanza mbunge anauliza ni lini serikali itajenga barabara kijijini kwake. Halafu Spika Anne Makinda anasema,'Waziri wa Ujenzi,tafadhali majibu,kwa ufupi....John Mnyika,kaa chini tafadhali. Haya,Ndugu waziri,majibu...nimesemaJohn Mnyika,kaa chini.Haya,Ndugu Waziri,jibu tafadhali.' Halafu Waziri wa Ujenzi anajibu,'Mheshimiwa Spika,ile barabara tumeshaanza kuijenga. Mpaka hivi sasa tumeweka pale kokoto 54,695,846 ,muwe na subira,ile barabara itatengenezwa.
 
Naona UKAWA jana walisononeka sana wakati wametoka Bungeni bila ya kuonyeshwa "Live"!
 
Tunapojadili haya mambo ni bora kutenganishi mihili husika, bunge ni mhimili wake peke yake. Hivyo ni bora ukajadikiwa wenyewe kama wenyewe. Tatizo ninalo liona ni kuwa na waziri aliyezoea siasa badala ya maslahi mapana ya nchi na wananchi. Kichwa chake kimejaa ushindani wa kisiasa kama baada ya wadau humu ndani, anahangaika kupambana na wapinzani wakati nchi ina angamia. Huyu jamaa ni jipu na anafaa kutumbuliwa kwani analeta mtafaruku usio wa lazima bali kwa maslahi ya wachache.
 
Naona UKAWA jana walisononeka sana wakati wametoka Bungeni bila ya kuonyeshwa "Live"!
Je! Wewe hukusononeka kwa kukosa kusikiliza hotuba ya waziri mkuu kuhusu bajeti ihusuyo wizara zake?!

Usitumie makalio kuwaza, ewe ndugu yangu!
 
Je! Wewe hukusononeka kwa kukosa kusikiliza hotuba ya waziri mkuu kuhusu bajeti ihusuyo wizara zake?!

Usitumie makalio kuwaza, ewe ndugu yangu!
Hotuba yake ipo kwenye mtandao wa Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu. Wewe useme kuwa hauna laptop, deskop au simu ya uhakika ya ku download hiyo hotuba! Vichwa vingine ni kama matikiti maji kama hicho chako!
 
Tundu Lissu ndie anasababishwa Bunge lisitangazwe live. Kwa sababu yeye ndie anayesema,'nafurahi zinapitokea vurugu pale Bungeni,watazamaji wanapata msisimko'
ha ha ha kwa kweli wacha tucheke tu nadhani hasara inaangukia kwa ccm na serikali yake kwa sababu wananchi hawaoni watakachooambiwa na wapinzani watakiamini au kitakaacha andikw n magazeti watakiamini
sasa tumejua magufuli ni mtu asiyefuata utawala wa sheria hata kidogo na hana maono ya uongozi wala kusimamia taratibu kwanza hana mpango kazi wake wala hajazielekeza wizara zake kazi za kufanya baada ya kuziunganisha zingine kuzifuta
Anatumbuwa fedha za serikali bila kibali cha wawakilishi hatumii budget act
bajeti yake kuu hajaonyesha vyanzo vyake kwa maana hiyo ni bajeti ya kufikirika
Amepoka madaraka ya bunge na spik naibu na secretariat ya bunge wanacheka chek tu sasa mvunja sharia antaka wenzake waonekane wavunja sheria
 
Hotuba yake ipo kwenye mtandao wa Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu. Wewe useme kuwa hauna laptop, deskop au simu ya uhakika ya ku download hiyo hotuba! Vichwa vingine ni kama matikiti maji kama hicho chako!
Ni watanzania asilimia ngapi wana desk top, laptop au Ipad?

Kama asilimia 70% ni maskini wanaoshi karibia na chini ya dola moja, pesa ya kwenda mtandaoni wataipata wapi?

Njia nzuri kwao kusikia ni kupitia redio au Tv ambazo naamini wengi wanazo.

Akili zingine bhana..!
 
Ni watanzania asilimia ngapi wana desk top, laptop au Ipad?

Kama asilimia 70% ni maskini wanaoshi karibia na chini ya dola moja, pesa ya kwenda mtandaoni wataipata wapi?

Njia nzuri kwao kusikia ni kupitia redio au Tv ambazo naamini wengi wanazo.

Akili zingine bhana..!
Nimekuambia akili zako ni kama tikitimaji! Hivi unafikiri watanzania wote wana TV za kuwaangalia wabunge wanaosusa vikao vya Bunge lakini wanataka posho? Muda wa Bunge wenzako wapo shambani wanalima!
 
Hotuba yake ipo kwenye mtandao wa Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu. Wewe useme kuwa hauna laptop, deskop au simu ya uhakika ya ku download hiyo hotuba! Vichwa vingine ni kama matikiti maji kama hicho chako!
Umepaniki mkuu, serikali ya awamu ya tano ni Pasua kichwa. Haijajipanga, haikujipanga na haijipangi.
 
Nimekuambia akili zako ni kama tikitimaji! Hivi unafikiri watanzania wote wana TV za kuwaangalia wabunge wanaosusa vikao vya Bunge lakini wanataka posho? Muda wa Bunge wenzako wapo shambani wanalima!
Hujielewi wewe ... Nimesema either Redio au Tv.

Nimeona unaleta ubishi usio na maana.

Nakupuuza, nishajua kuwa wewe sio mjinga bali mpumbavu..!
 
Back
Top Bottom