Kwa muktadha huu "URAIS" ni wa CCM 2015...

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,080
Habari wana JF,

Kawaida kama wanadamu huwa tunakuwa na matarajio ya vitu mbali mbali, na matarajio hayo huegemea tokana na viashiria vinavyowezesha haya matarajio ku materialise. Tumetofautiana katika kusoma viashiria hasa pale amapo viashiria hivyo kuwa ni vya ku donoa donoa! Ingawa kuna viashiria vingine ambavyo huonesha WAZI kabisa kuwa matarajio ni haya iwe kwa kupenda ama kutopenda kwa watazamaji wote. Tokana na nyenendo, habari na matukio yanayotokea siku zote nchini kwetu hasa kwa yale yanayohusiana na masuala ya Siasa yananipa kutoa mtazamo huu nilotoa katika makala hii.

Ni wazi kuwa idadi kubwa ya Watanzania (na hata mataifa mengine baadhi) tunasubiri kwa hamu kuona na kushuhudia shughuli za uchaguzi mkuu 2015. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania toka ipate uhuru mwaka 51 iliyopita itakuwa na idadi kubwa zaidi ya wanaharakati, wakereketwa na wafuasi wa vyama, wananchi wa kawaida kuvutiwa na kuwa na hamu kubwa kujua hatma ya uchaguzi na kama uongozi mkuu wa nchi utachukuliwa na Chama Pinzani ama bado kitabaki Chama tawala madarakani. Ni matumaini yangu hata idadi ya wapiga kura itaongezeka kuliko miaka ya nyuma.

Hakuna ubishi kuwa uchaguzi mkuu wa 2015 utakuwa ni kabambe, wenye kuvutia na wa muhimu pengine kuliko chaguzi nyingine zote zilizowahi kutokea. Ni uchaguzi ambao kubwa litakalotawala ni kutaka kwa shauku kuona ni nani hasa atashinda kiti cha Urais. Kwenye akili na fikra za wengi pengine hata haitajalisha na wala kutokuwa na nguvu huyo rais atakuwa ni nani; bali lenye nguvu ni kuona rais huyo atakuwa wa chama gani. Je, Chama Cha Mapinduzi bado kitakuwa kinashikilia nchi ama Wapinzani? 2015 baada ya uchaguzi ndiyo tutapata jibu kamili la swali hilo!

Hata hivyo licha ya kuwa baada ya Uchaguzi huo mkuu ndiyo tutakuwa na jibu kamili. Ukweli unabaki kuwa kuna vitu/viashiria/matendo ya vyama husika ambavyo hutoa picha kwa Wanaharakati, Wanasiasa, Wakereketwa na Wafuasi; ya kuwa Chama gani kinaonekana kinara na wana nafasi ya kuweza kushinda kiti hicho katika Uchaguzi.

Kila mmoja toka katika hayo makundi tajwa huwa na vigezo na sababu ambazo humpelekea aamini ushindi ni wa nani. Kwa mantiki hiyo siyo ajabu ukikutana na watu wawili wakawa na mawazo tofauti huku kila mmoja akiamini wazo lake ndiyo sahihi. Katika hili ambacho kinaweza toa mwanga na sababu ya kuamini mmoja kuliko mwingine ni tokana na sababu zake ambazo ataainisha kwa hoja ambazo yastahili ziwe nzito.

Maandalizi na mikakati ya kushika Uongozi wa juu wa Serikali huwa ni mzito na wakimahesabu na kwa maandalizi thabiti yaliyo jipanga vyema. Maandalizi hayo hayafanywi kwa siku moja, hayafanywi in Isolation na wala hayawezi fanikiwa kwa kubahatisha. Inahitaji nguvu ya Chama, nguvu ya uongozi wa Chama na kubwa zaidi nguvu ya wanachama ambao ndiyo Umma na ndiyo wana wajibu wa kumweka mtu katika kiti hicho kwa njia ya kura wakati wa Uchaguzi.

Hivyo basi kuna makundi matatu (Tokana na Mtazamo wangu) yanayotoa picha ya uchaguzi utakuwa vipi hasa:

A]. Kundi la wapiga Kura ambao ndiyo wananchi.
B]. Kundi la Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio chama tawala.
C]. Kundi la wapinzani wakuu; kwa maana ya CHADEMA ambao wamekuwa ni wapinzani wakuu.


KUNDI LA WAPIGA KURA

Historia Kujirudia (hasa ya 2005)

Kuna kila dalili kwamba historia ya 2005 inaweza kujirudia i.e. watanzania wengi watakuwa wamejiandikisha kupiga kura ila wachache watakaopiga kura. Hata hivyo izingatiwe kuwa hili linaweza epushwa ama kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kama: Kwanza iwapo Vyama pinzani, Vyombo Vya habari na Wanaharakai wa Demokrasia wataweza kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwa nguvu zaidi, na Pili ni kwa CHADEMA kuja na candidate mzuri, mashuhuri, mwenye experience ya kutosha ambaye ataweza himili na kushindana vyema na mgombea urais wa chama pinzani.

Kutokujifunga kwa wapiga kura

Watanzania wengi ambao ni wapiga kura na wanao kuwa na vitambulisho vya kupiga kura kwa nia hiyo ya kujiandikisha hawapo katika chama chochote, ni wachache ambao wapo katika vyama kwa maana ya kuwa yupo chama Fulani. So far, tunaona CHADEMA nguvu ya kuongeza wapiga kura ipo katika kubanana na hao ambao tayari ni wanachama wa CCM na wale wasio na chama ambao wanawapata pia. Tokana na furaha ipatikanapo pale wanapo faulu kuwavuta wana CCM wengi kuja Chadema inapelekea kuonekana kana kwamba Strategy yao ipo katika kuhakikisha wanachama wa CCM wanahamia CHADEMA badala ya nguvu katika kuhakikisha wanajenga &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];loyalties' kwa kuwavuta wale wasio na chama.

Woga wa Mabadiliko

Kura nyingi zipo vijijini, na wengi wao ni CCM ingawa inaenda inapungua na ni kwa sababu sio tu kwa sababu hawana upeo au elimu ya uraia bali by default, watu maeneo ya vijijini huwa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];conservatives'. Hawapendi mabadiliko na ni waoga wa mabadiliko, wapo katika hali mbaya lakini bado wana amini kuwa uongozi mwingine unaweza waangamiza zaidi na kabisa.

Ukichanganya hili na kwamba tangia kupata uhuru wengi wanaishi maisha ya kujitosheleza (pa kulala, chakula, nguo) hivyo wao hawaguswi sana na matatizo ya kiuchumi kama wale wananchi ambao wapo mijini wanaotegemea formal, monetary and market based economy kuendesha maisha yako ya kila siku. Vijijini ni moja ya sababu CCM itaendelea kushinda urais na kama katika ngazi ya ubunge, ikitokea upinzani unapata kura za vijijini basi ni kutokana na wananchi husika kuvutiwa na mgombea ambae ni msomi, makini n.k. Ikiwa ni sifa ya kutukuka miongoni mwao (mfano labda Mnyaturu) kuonesha hata wao pia wana wasomi wa kuwang'arisha katika anga za siasa za nchi na siyo tu Wanyakyusa, Wachaga, Wahaya n.k wanaweza kuwa hivo.

KUNDI LA CHAMA CHA MAPINDUZI

Ni mengi ambayo Serkali ya CCM imewakosea na inaendelea kuwakosea wananchi wake, kukiwa na matukio ya kuudhunisha, sikitisha, katisha tamaa kila kunapo kucha! Hakuna unafuu popote pale na Serkali imekuwa kama imefuzu katika kupiga kote kote kwa wananchi tena panapo uma! Haya yamekuwa yakiendelea siku zote na bado yanaendelea kwa miaka kadhaa sasa.

Kwanza tujiulize ni kwa namna ipi CCM wame survive hadi hapo walipo?! Tuache yote hayo na tuanzie pale ambapo tulipata orodha ya "List of Shame" toka kwa Dr. Slaa, Orodha iliyotikisa na kusababisha viongozi hao wa juu kumaka kumfungulia kesi Dr. Slaa - suala ambalo halijafanikiwa hadi leo. Ile Orodha ilikuwa ni tosha kabisa kuwa hamasa kwa wananchi na wanaharakati kuing'oa CCM kwenye uchaguzi wa 2010. Lakini haikuwa hivyo...

Katika miongo ya miaka kumi kumekuwa na transparency kwa kiwango cha jamii nzima kujua madhaifu ya Serkali ya CCM juu ya Ufisadi uliyo kithiri kama pesa za Uswizi, Mikataba ya Madini yenye walakini kama vile wa Buzwagi, Magumashi na rushwa zilizokithiri katka utendaji kama masuala ya EPA na Richmond.

Kumekuwa na kuongezeka kwa matukio katika jamii dhidi ya wanajamii na vyama pinzani. Tumeona ni namna ipi Serkali imekuwa ikitumia vyombo vya Ulinzi na Usalama wa wananchi kwa kuharibu huo huo usalama wa wananchi na ni suala la kusikitisha kuwa tumepoteza watu katika jamii kwa kuonewa, kimakosa ama kukosa umakini wa utendaji wa vyombo hivyo vya usalama. Hali zinazidi kuwa mbaya karibu katika taasisi zote za ambazo Serkali ina wajibu wa kusimamia na kuhakikisha hali ni nzuri na huduma stahili zinatimizwa na kuwafikia wana nchi. Elimu, Uchumi, Afya, Usalama na mengine mengi yanazidi kuzorota huku Serikali ikizidi kujitazama yenyewe pamoja na viongozi wake wakuu. Kazi na nguvu yao ya Ziada kubwa imeelekezwa katika kuhakikisha wapo katika uongozi huo wa juu daima. Hili linafanya Serikali kufanya kila wanalo weza katika kuhakikisha wanafanikiwa.

Mbaya zaidi kumekuwa na kuongezeka kwa kasi juu ya suala la "Udini", tena basi udini huo ukisababishia ukosefu wa amani, uharibifu wa mali na kupoteza kwa maisha ya wananchi na viongozi wa dini. Chuki kati ya Waislamu na Wakristo inaenda kukuzwa tena kwa kubembeleza sababu tu Serkali kwa udhaifu mkubwa imeshindwa kabisa kudhibiti na kukomesha udini huo. Hali na sasa inaonesha kuwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];future' na usalama wa nchi ni walakini sana. Sad.

Hawajali kuwa wanawaumiza wananchi, hawajali kuwa inatoa implication gani kwa Wanasiasa, Wanaharakati, Wakereketwa na Wafuatiliaji wa mambo. Inafanya kutoa maamuzi ya kujikoroga kama vile la kujadili Bungwe lisiangaliwe 'Live' na mra tena kubadilisha msimamo. Na pia inafanya Serikali kutoa maamuzi ambayo kimsingi na kimantiki hayaeleweki; kama vile kuvunjwa kwa POAC. Ukichukulia uzito na umuhimu wa Kamati yenyewe ikiwa ilikuwa inaangalia na kufuatilia asset zenye thamani ya trillion za shilingi, inafanya kuamini kuwa ni mtu asiye na akili tu ndiyo anaweza futa ama kukubali ifutwe LA SIVYO zinatakiwa sababu za Msing sana kuwakilishwa.

Hata hivyo pamoja na matendo ya kidhaifu hayo yote, ukweli (kwa mtazamo wangu) unabaki kuwa kwa hali ilivyo sasa kisiasa ikiambatanishwa na matendo, attitude za wananchi na baadhi ya Viongozi pia na matukio infanya niamini kuwa 2015 CCM bado wana uwezo wa kuwa vinara wa Uraisi hata kama ni kwa asilimia ndogo kuliko siku zote za chaguzi kwa sababu hizi zifuatazo;

Wamejipanga Vyema

Kujipanga haijialishi ni njia ipi unatumia, kama ni chafu/safi, halali/si haliali, haki/siyo haki - inachojalisha ni mipango yako kuweza kufanikisha azma ya malengo ya mipango hiyo. Serikali ya CCM imekuwa hodari katika kuhakikisha inatengeneza mazingira wezeshi kwa wao kuweza kushinda uchaguzi mkuu ujao. Wamejitosheleza vyema katika Nyanja mbali mbali, tokana na vita baridi waliyo nayo dhidi ya wapinzani wao wakuu CHADEMA. Wamejikita katika kujizatiti kuwanyong'onyeza nguvu CHADEMA kwa kila namna inayowezekana hasa kwa kutumia madhaifu yao.

Viongozi wao wamekuwa wakijitahidi na kuweza kufanya kazi hiyo ya kwa bidii, Tumeona namna shutuma za CHADEMA kuingia mikataba na Wafadhili wa mabillioni ya shilingi (Sijui hii kesi iliishia wapi?); Tumeona suala la Kadi ya CCM ya Dr. Slaa vile ilisambaa katika vyombo vya habari ambayo mwanzo ilichukuliwa kwa wepesi na hatimaye kuweza ku 'divert' attention ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwa kulitatua tatizo badala ya kuangalia mambo mengine ya msingi na yalo na tija kwa shughuli za Chama.

Wapo juu ya Taasisi

Wamekuwa wapo juu ya taasisi mbalimbali ambazo ni mhimu, msingi na kugusa jamii kwa upana. Tukiacha taasisi nyingine zote tuangalie taasisi ya Bunge letu tukufu kwa namna ambavyo limekuwa likiendishwa kwa matakwa ya Chama Cha Mapinduzi. Kumekuwa na sarakasi nyingi Bungeni hadi kupelekea lawama zilizo kithiri dhidi ya Madame Anne Makinda na ndugu Job Ndugai tokana na matendo yasiyowaridhisha wabunge wengi na wananchi kwa ujumla. Kubwa kuliko hapa karibuni kumefutwa na kuvunjwa kwa Kamati mbili (1) Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje iliyokua inaongozwa na Edward Lowassa na (2) Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa inaongozwa na Zitto Zuberi Kabwe ambayo ilifutwa kabisa. Inaleta uwalakini sana 'timing' ya events hizi hasa tokana na kuwa ripoti za kamati hizo zilikuwa zikae wiki chache baada ya tukio. Ikumbukwe ripoti ya mwisho ya Zitto ilipeleka kura ya kutokuwa na Imani kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na hivo kusababisha kusimamishwa kwa mawaziri 8.

Katiba (ya sasa) inasimama upande wa Serikali iliyopo Madarakani

Katiba mpya ilitakiwa ipatikane walau 2010 ili kuwe na miaka walau mitano ya utawala chini ya Katiba mpya ili kufikia 2015, mabadiliko mengi yawe tayari yamejitokeza katika kila Nyanja hivyo kuisaidia CHADEMA na vyama vingine pinzani. Vipengele vingi vya katiba ya sasa vinakumbatia na kulinda nafasi za Uongozi uliyopo madarakani tokana na wajibu na majukumu yaliyo ainishwa kwa mujibu wa katiba. Nje ya nafasi ya Rais ambazo ni nzito na nyeti (Kama vile Mkuu wa Serikali nan chi; Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya usalama na Ulinzi; Ana mamlaka ya kutaifisha mali yoyote; Ndiye anayeteua viongozi wakuu akiwemo na Jaji mkuu, wakuu wa vyombo ya ulinzi na Usalama n.k); Pia ndiye ambae anawajibika kuteua Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo ndiyo tegemezi katika chaguzi kuu.

Madhaifu ya Rais Jakaya Kikwete

Katika ila tatizo, kila uozo, kila ufisadi ama uchemvu uliotokea lawama zote zimekuwa zikienda kwa Rais JK. Hilo limepelekea kutamkwa kwa wengi wa wanaharakati, wanasiasa, wananchi na wakereketwa kuwa ni 'Udhaifu wa Kikwete'. Hii kauli inatowa picha kuwa katika akili za wengi matatizo yoote tuliyo nayo ni kana kwamba yalikuwepo tu baada ya JK kushika Urais na hayakuwepo awali. Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa kwa matatizo yote yaliyopo toka Ufisadi, Kutowajibika, Kuangamiza nchi kuliko Serkali yake ya CCM. Kwa maana nyingine hili linaweza kupelekea Kingozo Mkuu (rais) toka CCM akapokelewa kwa mikono miwili kwa kuamini kuwa atairudisha CCM katika mstari.

KUNDI LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Chadema wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanatambua umuhimu wa Demokrasia hasa kwa njia ya mikutano na harakati za Movement for Change (M4C) ambazo zimekuwa zikifanywa katika kila maeneo ya nchi. Jitihada zao na 'results' ya hizo harakati zimekuwa wazi kiasi kwamba zimefanya viongozi wa CCM (hasa wa kitengo hicho) kuhangaika usiku na mchana namna ambayo wanaweza kuwachafua na kuwanyong'onyeza Chadema.

Imefanya kuwajengea baadhi ya Wanachadema kuamini kuwa CCM wanatishika na Slaa to the extent ambayo they are potraying, Imefanya kuzuka kwa kashfa mbali mbali dhidi ya Dr. Slaa nyingi zikiwa hazina tija wala mantiki.

Imefanya wajikite na kwa kiasi Fulani kuweza kuwayumbisha Chadema kwa kuingilia kupitia vipandikizi wao maslahi ya Chama. Kwa kiasi kikubwa Chadema wamefaulu katika kuwawezesha viongozi wengi wa CCM na serkali yenyewe kukosa usingizi. Hiyo ni 'achievement' kubwa sana; Lakini hata hivyo Chadema wanatakiwa wajitazame upya kuweza kuhakikisha wanajipanga, jikita na kuhakikisha kuwa wanashinda uchaguzi mkuu 2015.

Bado tuna miaka miwili hadi Uchaguzi mkuu kama mambo yataenda inavyostahili. Ni muda tosha wa Chadema kuweza kufanya mabadiliko. Ninachoweza kusema, hadi hapa tulipo kwa mtazamo wangu Chadema bado wana kazi kubwa kuweza kuhakikisha inafanikiwa, naamini kuwa ni muhimu wajitazame wapi nut zimelegea na wakaze katika maeneo yote husika ili kuhakikisha yanatolewa ama kufutwa kabisa.

Wameingia mtego "Siasa za Ligi na Mipasho" dhidi ya CCM

CCM ikiwa kama chama ambacho ni kikongwe na kimejijenga kuliko CHADEMA ambayo ni changa, wana nafasi kubwa, watu wa kutosha na walio jidhatiti hapo kwa ajili ya kuendesha ligi za mipasho na kushindana kwa kutafuta kwa udi na uvumba kitu gani kinaweza ivunja nguvu CHADEMA ambayo inakuwa siku kwa siku na kuonekana dhahiri kuwa ni tishio kwa CCM.

Tatizo ni kwamba CCM ni mabingwa wa Siasa za FITINA, wana uzoefu mkubwa sana katika hili hata katika siasa za ndani ya chama; CHADEMA hawana ujuzi huu na hilo litawagharimu kwani kuna kura nyingi sana ambazo zinapatikana kwa fitina, sio kwa kupitia tu nguvu ya hoja au ukweli diama fitina mwiko, kwani watanzania wengi ni mashabiki wa siasa za matukio na vituko CHADEMA wameshindwa kuja na counter strategy ya siasa za fitina kama vile za akina Nchemba, Nape na wengineo. Wananchi wengi hasa vijijini ambako ndio kuna kura nyingi - wananunua hoja za Nchemba (haijalishi wamepewa Tisheti ama lah) kuliko tunavyofikiri kwani wengi ni illiterate and ignorant.

Centralisation ya Uongozi toka Kaskazini

Inawezekana kabisa hili halikuwa kwa lengo mbaya; Lakini ni muhimu tukaelewa kwamba kwa kipindi kufikia 2010, inawezekana ilikuwa ni lazima CHADEMA kufanya hivyo kwani bado kilikuwa hakina true loyalists wengi kutoka maeneo mengine ya nchi wenye uwezo na uzoefu katika masuala ya uongozi. Ni suala ambalo CHADEMA haiwezi sema kwa jamii LAKINI ni muhimu pakawepo na mbinu mpya ya kuhakikisha hii imani ya kuwa ni "Chama cha Kaskazini" inatutwa na kufa kabisa.

Pia waeleze kuwa sasa wameshapata watu wengi wenye uwezo na muda ukifika Watanzania watajionea ni namna ipi CHADEMA itadhihirisha kwa uma kuwa Chama siyo cha Kaskazini bali cha Watanzania wote. CHADEMA wakiwa makini na wakajipanga wanaweza tumia dhaifu hili la ukanda "Kaskazini" kama strength, huku waki appeal kwa umma kwamba wawapatie watu makini toka maeneo mbali mbali ya Mkoa ili wawe msaada kwa Chama na wananchi ambao wanawataumikia. Kama ilivyo wazi hapa karibuni, Umaaruru wa Chadema umekuwa ukikuwa na kusambaa karibu nchi nzima. Hili pia linaweza punguzwa kwa kuangalia nafasi za viongozi na wajibu walio nao hasa katika Chama. Naamini kuna Watanzania wengi wana uwezo wa kuwa viongozi, inakuwa haina mantiki mtu mmoja anapokuwa na vyeo ziaidi ya Vitano na hali anaweza saidiwa na kupunguziwa majukumu.


Mapungufu makubwa ya Movement for Change (M4C)

Madhaifu ya M4C ambayo inaonesha inatokana na upungufu wa mfuko wa pesa kuweza kuendeshea. Namna harakati za M4C zilianza ni tofauti na sasa. Pengine tokana na kuchafuliwa kwake kwa kuhusishwa na vurugu ama lah, ila kama CHADEMA wana niya ya kushika Urais inabidi kuongeza nguvu na kasi katika harakati hizi.

Pia M4C imekuwa ikitumia nguvu kubwa katika kuichongea serikali ya CCM kwa uma kuliko kuhakikisha na kupigania idadi ya wapiga kura inaongezeka; Lengo ilitakiwa iwe kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura huku chama kikijenga uwigo mpana na kukuwa idadi ya wana CDM na pia kujenga database yake mpya ambayo ingetumia katika tathmini za uchaguzi mikuu iliyopita nay a sasa


Kujenga kwa maadui wasio na Tija

CHADEMA wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nidhamu inafanyika na viongozi wao na dhidi ya viongozi na wananchi pia. Hata hivo kwa mtazamo wangu wamekuwa haraka sana katika maamuzi ya kuchukua hatua ya kufukuza mara moja viongozi wao hadi pengine kutilia mashaka kama kweli huwa kuna chunguzi za dhati huwa zinafanywa dhidi ya watuhumiwa hao. Tayari tumeona reactions za akina Chriss Lukosi, Juliana Shonza, Mtela Mwampamba - Hawa watu walikuwa ni viongozi wa CHADEMA, hivo ina maana wanawajua vema. Ni wazi kuwa mtu ambaye ni adui mkuu ni Yule akujuae vema, maana anajua wapi pa kubofya.

Kupokea kwa Oil Chafu toka CCM

Ni ajabu sana kuwa CHADEMA wapo haraka sana katika kupokea viongozi toka chama kingine (hasa cha wapinzani wao wakuu CCM) kwa mbwembwe na matangazo. Utata unakuja pale ambapo huyo aliyejitoa CCM ni Kiongozi na akifika CDM anapewa uongozi; Hiyo ni hatarishi kama huyo mtu ni pandikizi, pia kwa namna moja ama nyingine kuwanyima haki wale ambao wanaweza hiyo nafasi nje ya huyo mgeni. Hili litatokea na ni moja ya mambo ambayo yataigharimu CHADEMA urais 2015; CHADEMA wanaweza kuepuka kuwa chama chakupokea wale wote ambao wanaogopa kusimama kama wagombea wa CCM e 2015 kutokana na nguvu ya CHADEMA

Bahati mbaya siyo kutokana na Mapenzi juu ya CHADEMA na taifa, bali kwa nafsi na ubinafsi wao. Ni muhimu CHADEMA wakaliangalia upya hili; pengine CHADEMA waje na tamko kwamba mtu yeyote ambaye atahama kutoka CCM dadika ya mwisho hatopata nafasi ya kugombea kwani ni kuwanyima haki loyalists. Chama kije na kanuni kwamba ni lazima ujiunge na CHADEMA miaka miwili kwa mfano before uchaguzi ili uweze kupata experience na chama etc

My General Take

Hadi hapa naamini kuwa Kuna kila dalili kuwa CCM itashinda, hata kama itakuwa kwa asilimia 51% za kura zote; Tofauti itakayokuwepo katika ushindi huo ni kuwa CCM itashinda kwa margine ndogo kuko zote katika historia za Chaguzi Tanzania. Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshima Freeman Mbowe yeye kishajiapia kuwa ikishinda CCM 2015 atajiuzuru na naomba nimnukuu "Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa". Ni kauli ya kutia moyo ya kuwa Chama kimejipanga vipi, kuwa kina uhakika wa Kazi na nguvu zake na kuwa Chama kitaikomboa nchi ifikipo 2015.

Vile vile iwapo kutakuwa na ushindi wa CHADEMA kama vile wengi wa Watanzania, Wanaharakati na Viongozi wa Chama hicho wanavyo dhania na kuamini; basi ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hasa iwapo CHADEMA watapata kura nyingi ngazi ya Urais na wabunge wengi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ila nikiri kuwa tatizo ni kwamba suala la ndoa za vyama, CHADEMA walishajifunga na umma unajua fika na kwa kiasi kikubwa namna gani CHADEMA hawakubaliani a wazo la 'Government of National Unity' kule ZNZ. Swali linabaki je ikitokea uwezekano wa GNU Tanzania bara na ikaonekana ndiyo suluhu pekee, CHADEMA watakula matapishi yao wenyewe? Hata hivyo naomba hili niliache hapa kwani ni mjadala mwingine mpya kabisa. Wanachadema... Hii nakala ni katika ku challengiana na kujitazama upya kuweza kufanikisha safari ya Ikulu.

Naomba nitumie hii nukuu ya vita from the Legendary Sun Wu. Naamini kuwa hii nukuu, inatumika vema na CCM katika tactics zake zake chafu za kisiasa hasa hizi za &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Gutter Politics' ambazo ndio sababu pekee bado wapo hapo walipo. It is time Chadema start doing the same... (IMO).

"If your enemy is secure at all points, be prepared for him. If he is in superior strength, evade him. If your opponent is temperamental, seek to irritate him. Pretend to be weak, that he may grow arrogant. If he is taking his ease, give him no rest. If his forces are united, separate them. If sovereign and subject are in accord, put division between them. Attack him where he is unprepared, appear where you are not expected."

Pamoja Saana,

AshaDii.

 
Unachosema kina mantiki AD ingawa mara nyingine kinaumiza masikioni kukisikiliza...mimi sidhani kama ni uoga wa watu kupokea mabadiliko nndio utakipa chama tawala ushindi....ila ni namna nzima ya kujipanga na kudhihirisha kama kweli kuna mbadala zaidi ya CCM. Kwanini nisumbuke na chama ambacho kinasubiri walioachwa na CCM ili kiweze kujinadi kwa wananchi?
 
Wakuu AshaDii na SINA JINA1,naomba niwajibu:

Kwanza AshaDii umesahau kuwa mwaka 2015,uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge utafanyika chini ya Katiba mpya. Kwahiyo,hoja yako ya kwamba Katiba ya sasa inaipendelea CCM na hivyo itashinda kiti cha Urais inashindwa na kuanguka.

Pili AshaDii yawezekana umebaki Dar es Salaam na kuandika uchambuzi huu.Unasikiasikia tu kuwa watu wa vijijini wanaogopa mabadiliko au wanaipenda sana CCM. Hiyo si kweli. Wakati wa likizo zangu za kikazi,hutembelea mikoa mbalimbali hususani inayoonekana kama imesheheni vijiji. Watanzania wamebadilika. Songea vijijini kabisa huko kuna CHADEMA,NCCR na CUF tena yenye nguvu. Unapotaka kuandika uchambuzi 'sensitive' kama huu,ni vyema ukatembea kidogo na kujionea. Usipofanya utafiti,huna haki ya kusema. Hoja hii pia haina mshiko.

Tatu, si CCM pekee waliojipanga. Hata CHADEMA,CUF,NCCR na vyama vingine vimejipanga. Unaijuaje nguvu ya vyama vyote nchini kuelekea 2015 kwa vijimambo unavyoweza kuviona tu? Maneno kama yako yalisemwa Kenya juu ya nguvu ya KANU.Hatahivyo,KANU iliondolewa madarakani kwa aibu mwaka 2003. Wananchi ndio imara kuliko vyama. Wakiamua wasiibiwe kura wanaweza.Watazilinda. Usitishwe na uyaonayo...sasa CCM iko madarakani;wacha itambe iwezavyo. 2015 ni tofauti.

Nne,Mapungufu unayoyaona kwa CHADEMA hata kwa CCM yapo.Kwanini uyaone ya CHADEMA kama ya madhara zaidi kuliko ya CCM? You are biased here!

Kimsingi,hakuna uchambuzi au utafiti wowote utakaozidi nguvu ya wananchi mwaka 2015. Watanzania watachagua mabadiliko au mazoea. Wao ndio waamuzi wa mwisho.Wakisema,wamesema.

Asante Mkuu AshaDii
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @Petro E. Mselewa,

Mkuu majibu ya masuala yako manne ni haya;

La kwanza;

Naelewa kuwa katiba itakuwa mpya, ila ZINGATIA kuwa hadi dakika hii hiyo "Katiba Mpya" bado haijapatikana tukiwa bado miaka miwili tu kwenda huo Uchaguzi mkuu! Kumbuka kuwa siyo kila mahala ambapo wewe, viongozi ama wananchi wanataka mabadiliko – yatakuwepo hayo mabadiliko. Kuna anae elewa na mwenye uhakika wa vipengele vinavyo ‘favor' Uongozi uliyo madarakani kama vitatolewa?

La Pili;

Suala la wananchi wa Kijijini, hiyo ni maeneo na maeneo… CCM siku zote huko nyuma walikuwa hizo ndio ngome zao, hivyo bado maeneo mengi ya vijijini humo ndani bado ni ngome yao. Chadema wanajitahidi katika kuwafikia wananchi ila naelewa bado hawajafanikiwa kufika vile ipaswavyo kwa kuweza wagusa wote.

La tatu;

Sijakataa kuwa vyama vingine havijajipanga… Ila naamini kuwa CCM wamejipanga vema zaidi. Kama hapa tulipo Chadema wataona wamejipanga vya kutosha tayari, then ndilo hilo lingine nililogusia, kuwa Chadema wanajiamini mno! Suala ambalo halistahili unapo kuwa una deal na kitu chochote kilicho jidhatiti na kuota mizizi hadi to the epicenter.

La nne;

Mapungufu yaliyopo kwa Chadema yanaweza yakawepo na CCM… Lakini nikuulize swali, Chadema inapokosea kitu ambacho CCM nao wanakosea – Does it make it right? Kwa hiyo Chadema wakosee na kurudia makosa yale yale ya CCM?

Hapo mwisho ndipo ambapo sasa IMO naona ni dalili za kuchemka! Chadema watakazana nguvu ya umma kwa kutegemea kura za Wananchi huku CCM wakijipanga kwa nguvu ya Ujangili na Wizi wa kura hizo hizo za "Nguvu ya Umma" kwa kutegemea kufanya jitihada zozote zile kufanikisha ushindi wao. Mwisho wa siku CCM inashinda na tunarudi kulee kulee...
 
"Ukichanganya hili na kwamba tangia kupata uhuru wengi wanaishi maisha ya kujitosheleza (pa kulala, chakula, nguo) hivyo wao hawaguswi sana na matatizo ya kiuchumi kama wale wananchi ambao wapo mijini wanaotegemea formal, monetary and market based economy kuendesha maisha yako ya kila siku. Vijijini ni moja ya sababu CCM itaendelea kushinda urais na kama katika ngazi ya ubunge, ikitokea upinzani unapata kura za vijijini basi ni kutokana na wananchi husika kuvutiwa na mgombea ambae ni msomi, makini n.k. Ikiwa ni sifa ya kutukuka miongoni mwao (mfano labda Mnyaturu) kuonesha hata wao pia wana wasomi wa kuwang'arisha katika anga za siasa za nchi na siyo tu Wanyakyusa, Wachaga, Wahaya n.k wanaweza kuwa hivo."

Unaweza ukarudia kusoma ulichoandika hapo? Umeandika kwa sababu ya kuandika au unadata zake? Hata bila kuzunguka vijijini unaweza ukajiuliza kama kweli hao wananchi wa kijijini unaowazungumzia,tena bila ridhaa yao, kama kweli wanamaisha ya " kujitosheleza(pa kulala, chakula na nguo) " kwa nini kila siku wanakimbilia mijini hasa dsm wakati wamejitosheleza?

Anyway sina imani katika demokrasia hasa hii ya kiafrika, warudi CCM au waje CHADEMA hakuna jipya watakaloleta hawa wanasiasa, Tanzania yetu hii ni kama jamii ya kwenye allegory of the cave ya Plato, watu wasiojua kusoma na kuandika (wajinga), nchi inayozalisha sifuri nyingi kwenye mitihani, wananchi wanaoshinda kusoma udaku na ushabiki wa vyama vya siasa wana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kweli?
 
AshaDii,

I have said it in the past and I will say it again here potelea mbali hata kama nikitukanwa. Those who are looking forward for changes in 2015, they better go back and regroup. Hakuna kuna kitu kama changes in 2015. We still have got a long way to go.

Malcolm X said that “Usually when people are sad, they don’t do anything. They just cry over their condition. But when they get angry, they bring about a change.” Now AshaDii tell me are you sad or angry with what is happening in the country right now? In particular, are you sad or angry with the yesterday’s form four results? Be honest.

People believe things have fallen apart and that "It is no Longer at Ease". But either they're doing nothing because they strongly believe that "A Man of the People" will come and rescue them or believe that "The Beautiful Ones are not yet Born", kwa hiyo wanasubiri mpaka wazuri wazaliwe kwanza. But the majority are afraid of "The Petals of Bloods" ndiyo maana tunasizitiza amani na utulivu. We're still afraid to face "The Trial of Dedan Kimathi".

So, the biggest reason that Tanzanians do not make positive change in their lives is fear. Fear of the unknown, fear of persecution, fear of alienation and so on. There are also people who have become very comfortable with their lives and do not want to change, even if it is a positive change. They are also known as indifference, laziness or apathy. Tumekubali matatizo yanayotukabili kuwa integral part ya maisha yetu.

Another fundamental reason is that most Tanzanians have been programmed. We have people who have been educated or coerced to "believe" that their negative belief systems are correct and do not need to be changed. They are also known as delusion or brainwashed. Then, we have people with ego who believe that they are beyond the need for any change.

Of course, there are people who really want things to change. But people have always wanted things to be better than they are anyway. No matter how good we ever have it we will always want it to be much better. Don't you AshaDii?

But the other side of the coin is the people's willingness to change for themselves. This is the clincher. This is where it gets really tough because despite how good it could be people are very rarely willing to change for themselves.

Take, for instance, the frog in water comparison, a frog will jump out of a pot of boiling water but if the water starts at room temperature and is brought to a boil what will you have? A cooked frog. Thus, the water in the pot is boiling up, but we don't want to jump out of it yet. Instead, we are blaming the pot. We will end up being cooked in the pot just like the frog.
 
Sijasoma makala nzima ya AshaDii nataka kulala nitaisomna kesho, ila EMT acha mara moja ku under estimate Watanzania kiasi hicho, mimi na Familia yangu CCM haina kura hata moja, subilini tu lile bomu alilolisema Lowasa liotakavyofanya kazi yake vyema.

Wengi humu licha kuwa ni wachambuzi wazuri lakini mnashindwa kufanya calculation ya wapiga kura wa 2015 ni wa rika gani. hawa hawadanganywi kwa lugha ya amani na utulivu bali wanataka kuishi kama binadamu na siyo porojo za kwamba Chadema ni chama cha ukanda wa kaskazini wakati CCM ndio ina Wabunge wengi Kaskazini, this is ridiculous.

Naamka mapema kesho nitamsoma vizuri AshaDii ndio nitoe comment zangu.
 
Last edited by a moderator:
Mtaji wa CCM kubaki madarakani 2015

1. Siasa za maji taka
2. Kampeni za vitisho, vurugu, mauaji, umafioso na uharamia kwa kusaidiwa na vyombo vya dola
3. Kubariki au kufadhili chokochoko za kidini kuwachanganya wananchi
4. Kulivuruga bunge kwa kuwakandamiza wabunge wa upinzani waonekane hawana maana mbele ya wananchi

Hizi vurugu zinazoendelea sasa sio bahati mbaya hata kidogo...CCM wanajua wanachofanya na zitazidi zaidi! Mazingira yanatengenezwa kuvuruga wananchi na kuvuruga uchaguzi kwa ujumla ili wabaki madarakani!!!
 
Unaweza ukarudia kusoma ulichoandika hapo? Umeandika kwa sababu ya kuandika au unadata zake? Hata bila kuzunguka vijijini unaweza ukajiuliza kama kweli hao wananchi wa kijijini unaowazungumzia,tena bila ridhaa yao, kama kweli wanamaisha ya " kujitosheleza(pa kulala, chakula na nguo) " kwa nini kila siku wanakimbilia mijini hasa dsm wakati wamejitosheleza?

Anyway sina imani katika demokrasia hasa hii ya kiafrika, warudi CCM au waje CHADEMA hakuna jipya watakaloleta hawa wanasiasa, Tanzania yetu hii ni kama jamii ya kwenye allegory of the cave ya Plato, watu wasiojua kusoma na kuandika (wajinga), nchi inayozalisha sifuri nyingi kwenye mitihani, wananchi wanaoshinda kusoma udaku na ushabiki wa vyama vya siasa wana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kweli?

Mkuu Mourinho,
Hebu acha maslaha bana! Nimeandika sababu ya kuandika? Ukitaka data hapa tutadanganyana tu mkuu… Ila nina vigezo; Kabla hujajibu post yangu hii naomba jitazame wewe na watu walio kuzungua (hasa colleagues na marafiki) – Acha kabisa kundi lile ambao labda wao ni familia za kisomi ama wazawa wa mujini ambao baba, babu na nyanya ni wa mjini ama wasomi wa hapa toka enzi hizo..

Angalia kila mmoja wenu (lets say mpo kumi) mkianza kuainisha familia zenu za akina bibi na babu, Shangazi na Wajomba, Mabinamu na ndugu na jamaa… Idadi yenu kubwa inatoka wapi? ‘Utakuta kila mmoja wenu kwa kiasi kikubwa wanandugu ambao kweli wapo mjini ni asilimia ndogo ukifananisha na walio vijijini.

Suala hilo la Imani yako juu ya demokrasia hasa za Kiafrika nakuunga mkono.
 
Naungana na AshaDii, kuwa CCM inaweza kushinda tena uchaguzi kwa sabubu zifuatazo-


  • Nguvu nyingi sana za makusudi za kutumia vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha CCM inashinda na inaendelea kukaa madarakani.
  • Kutumia au kufuja fedha nyingi sana kuwapita wapinzani, rushwa, kununua vitambulisho vya kupigia, kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura vya watu ambao hawa'exist n.k
  • Vyombo vya usalama kuingizwa katika siasa ya kuhakikisha ccm inashinda kwa mbinu yeyote....badala ya vyombo hivyo kulinda wanachi, kulinda mali zao....hivyo kutoa picha kuwa, hali ya umasikini iliopo, hali ya migogoro ya kidini inayo endelea, hali ya kuporwa rasilimali zetu, vyombo hivi vya ulinzi na usalama vinanufaika.
  • Kuwatishia wapiga kura kutojitokeza kwa wingi ya kuwa; siku ya uchaguzi kunategemewa kuwa na vurugu, hivyo kuweka askari wengi wenye uniform na silaa za kivita.
  • Vifaa vya kupigia kura kuchelewa kufika katika maeneo husika, kwa makusudi, hasa zile sehemu zenye ngome kubwa ya upinzani.
  • Kuwakatisha tamaa wapiga kura kwa kuwaambia kumbukumbu za daftari ya mpiga kura jina lake halipo, au zinaonyesha ameshakufa.
  • Tume ya uchaguzi kutokuwa huru, na inatia mashaka kuiamini inapotoa matokeo ya mshindi kama ni ya kweli au laa...tumeona zanbar, cuf walishinda...tume ilitangazaje...hadi leo kuna serikali ya uwk?! Kuna kipindi Zanzbr ilibidi nyerere aende ili yatangazwe tofauti na uhalisia.

Watawala wana kila kitu cha kuwafanya waendelee kutawala kupitia CCM, fedha zipo mikononi mwao, ulinzi na usalama upo mikononi mwao, tume za uchaguzi ni zao, bunge ni lao na wanam'remote tu spika na naibu wake watakavyo, vyombo vya habari wamevishika na vinavyoleta ubishi wanavifungia, mahakama zipo chini yao...nini kimebaki?

My take ni kuwa, until that day watawaliwa tutakapo amua (inaf is inaf) kwa kuandamana nchi nzima dhidi ya dhuluma za viongozi wetu wanaodhani nchi ni mali yao ya mfukoni. Lini sasa wananchi tutaamua kukiambia chama tawala kuwa inatosha, mimi nadhini itakuwa 2015 kama tume itaamua kutoa matokeo tofauti na maamuzi ya wananchi wote.
 
Mkuu Mourinho,
Hebu acha maslaha bana! Nimeandika sababu ya kuandika? Ukitaka data hapa tutadanganyana tu mkuu… Ila nina vigezo; Kabla hujajibu post yangu hii naomba jitazame wewe na watu walio kuzungua (hasa colleagues na marafiki) – Acha kabisa kundi lile ambao labda wao ni familia za kisomi ama wazawa wa mujini ambao baba, babu na nyanya ni wa mjini ama wasomi wa hapa toka enzi hizo..

Angalia kila mmoja wenu (lets say mpo kumi) mkianza kuainisha familia zenu za akina bibi na babu, Shangazi na Wajomba, Mabinamu na ndugu na jamaa… Idadi yenu kubwa inatoka wapi? ‘Utakuta kila mmoja wenu kwa kiasi kikubwa wanandugu ambao kweli wapo mjini ni asilimia ndogo ukifananisha na walio vijijini.

Suala hilo la Imani yako juu ya demokrasia hasa za Kiafrika nakuunga mkono.

Kama umesoma vizuri mchango wangu utajua kuwa sijakataa kwamba watanzania wengi wanaishi kijijini, nakataa maneno yako kwamba wananchi wa kijijini wamejitosheleza( kula, mavazi, malazi)
 
Mkuu Petro E. Mselewa,

Ningependa kujibu maoni yako kwa mujibu wa bandiko lako namba 10 kama ifuatavyo:

Wakuu AshaDii na SINA JINA1,naomba niwajibu:

Kwanza AshaDii umesahau kuwa mwaka 2015,uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge utafanyika chini ya Katiba mpya. Kwahiyo,hoja yako ya kwamba Katiba ya sasa inaipendelea CCM na hivyo itashinda kiti cha Urais inashindwa na kuanguka.

Kwenye kijani hapo juu ndio tatizo; ni rahisi sana kwa CCM kujenga hoja kwamba tumepata mgombea mzuri na tuanze upya chini ya katiba mpya kama taifa, and many people will buy this statement; Katiba mpya ilitakiwa ije kabla ya uchagzi mkuu suala ambalo lingekuwa a major defeat to CCM; Ni kama ilivyotokea mwaka 1992 ambapo CCM ilifanikiwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi huku ikiacha uchaguzi mkuu uendelee katika ratiba ile ile ya ki-ccm ya kila baada ya miaka mitano; CCM ilijifunza kutoka kwa UNIP kwani wao waliruhusu uchaguzi ndani ya muda mfupi sana baada ya mageuzi ya kisiasa; Pia tazama Kenya, tayari they are experiencing katiba mpya kwa muda kabla ya uchaguzi; Tukirudi kwa CCM, Mwaka 1992, CCM ilipata muda wa kujipanga dhidi ya upinzani kwa kutumia ratiba yake tangia uhuru, na mwaka 2015 kuhusiana na katiba mpya, itakuwa hivyo hivyo;

Pili AshaDii yawezekana umebaki Dar es Salaam na kuandika uchambuzi huu.Unasikiasikia tu kuwa watu wa vijijini wanaogopa mabadiliko au wanaipenda sana CCM. Hiyo si kweli. Wakati wa likizo zangu za kikazi,hutembelea mikoa mbalimbali hususani inayoonekana kama imesheheni vijiji. Watanzania wamebadilika. Songea vijijini kabisa huko kuna CHADEMA,NCCR na CUF tena yenye nguvu. Unapotaka kuandika uchambuzi 'sensitive' kama huu,ni vyema ukatembea kidogo na kujionea. Usipofanya utafiti,huna haki ya kusema. Hoja hii pia haina mshiko.

Nakubaliana na wewe katika hili vinginevyo the general atmosphere huko vijijini bado ni pro ccm ingawa upinzani unazidi kuimarika; ukiangalia political map ya nchi based on takwimu za ubunge za 2010 ambazo kwa kiasi kikubwa zina reflect ukweli kwani hapakuwa na uchakachuaji mwingi, CCM ina nguvu kubwa sana bado vijijini, na nguvu kubwa haina maana ni absolute strength, even relative stength is still a strength; na hapa ndipo hoja ya asha dii kwamba ccm itapit alakini kwa kura chache kuliko miaka mingin yote, comes handy;

Tatu, si CCM pekee waliojipanga. Hata CHADEMA,CUF,NCCR na vyama vingine vimejipanga. Unaijuaje nguvu ya vyama vyote nchini kuelekea 2015 kwa vijimambo unavyoweza kuviona tu? Maneno kama yako yalisemwa Kenya juu ya nguvu ya KANU.Hatahivyo,KANU iliondolewa madarakani kwa aibu mwaka 2003. Wananchi ndio imara kuliko vyama. Wakiamua wasiibiwe kura wanaweza.Watazilinda. Usitishwe na uyaonayo...sasa CCM iko madarakani;wacha itambe iwezavyo. 2015 ni tofauti.

Ni kweli hata wapinzani wamejipanga lakini suala kubwa hapa ni katika hiyo green niliyo underline; uchaguzi wa 2010 watanzania milioni 18 walijiandikisha kupiga kura lakini waliojitokeza walikuwa less than 50%; unazungumziaje experience hii na hoja yako kuhusu watanzania kuamua? Kabla kwanza ya kuamua wasiibiwe, ni lazima waamue kujitokeza kupiga kura kwa wingi; Inachofanya Chadema kupitia M4C ni kinyume na ilivyotakiwa kama anavyojenga hoja asha dii - M4C ilitakiwa iwe ni movement ya ku deal na swing voters bila ya kujali kama wanakuwa wanachama wa chadema au wanaamua kuendela kutokuwa na interest ya kuwa na political affiliation kama kigezo cha wao kuamua kwenda kupiga kura; kama alivyosema asha dii, swing voters ndio wengi kuliko wanachama wa CCM na Chadema combined;

Nne,Mapungufu unayoyaona kwa CHADEMA hata kwa CCM yapo.Kwanini uyaone ya CHADEMA kama ya madhara zaidi kuliko ya CCM? You are biased here!
Ni kweli hata CCM ina mapungufu mengi sana lakini hoja ya asha dii kama ukiamua kuisoma in between the lines ni kwamba CCM ni mabingwa wa ku - turn its weakness into a strenght kutokana na uzoefu wake wa siasa za fitina n.k;

Kimsingi,hakuna uchambuzi au utafiti wowote utakaozidi nguvu ya wananchi mwaka 2015. Watanzania watachagua mabadiliko au mazoea. Wao ndio waamuzi wa mwisho.Wakisema,wamesema.

Asante Mkuu AshaDii

Kimsingi ilitakiwa uje na counter arguments kwamba - Kwa Mwaka 2015, Bado urais ni Wa Chadema; Vinginevyo sio lazima mtu ufanye utafiti wa kina kubaini hoja alizoleta asha dii, isitoshe, aliyaleta kama mawazo yake binafsi, na sote tuna nafasi ya kuyaboresha, au kuyapinga kwa hoja, na ili kuwa na nafasi nzuri ya kujibu hoja zilizo makini, ni lazima kichwani tuanze na uelewa wa hoja iliyo mbele yetu objectively kwanza kisha ndio tujipange kuzijibu subjevtively au in party lines;

Vinginevyo hiyo niliyo highlight blue hapo juu ndio changamoto kwa chadema 2015 kwamba mwaka 2010 kulikuwa na voters registered milioni kumi na nane, waliopiga kura walikuwa less than 50% kama sikosei; 2015, tunaweza kuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 21, je watajitokeza? au watakaa nyumbani kama 2010? Kumbuka, from experience, a low voter turn out ni ushindi kwa CCM!!!;
 
Back
Top Bottom