Ndugu wanaJF napenda kufahamu kwa nini taasisi ya Agakhan inapewa misamaha ya kodi hapa nchini kwetu. Nina uliza kwa sababu huduma za Agakhan mfano hospital za Agakhan ni ghali kuliko hospitali zote hapa nchini. Mfano mtoto mdogo wa wiki moja ukimpeleka Agakhan ili alazawe lazima uweke deposit ya laki tano za Tanzania ndiyo apewe huduma ya matibabu. Kumwona daktari ni elfu Ths 40,000-70,000. Shule za Agakhan ada zake nazo zipo juu kulinginishwa shule zingine za binafsi. Je kwanini wapate misamaha ya kodi? Je wanastahili kupewa misamaha ya kodi?