National Health Insurance Fund (NHIF) - Kero za wananchi

Mkewangu alienda pale kwa huduma ya kliniki, ikabidi aelekezwe regency, nadhan tunamfumo mbovu kabisa wa afya,
 
Mifuko yote: LAPF, PSPF, NSSF, GEPF etc wanakula bata ilhali wanachama ziiiiiiiiii.

Nina hasira nao sana hao watajwa hapo juu,haiwezekani mie nachangia mwaka wa tano huu halafu sijachukua hela na wala hawanikopeshi lakin manji anaenda na kukopa fedha ndefu kwenye hayo mashirika,katiba mpya lazima hilo swala liangaliwe,pili haiwezekani hela yangu wanafanyia miradi wanaingiza faida lakini mimi mwanachama sipati hata sumni ya faidi katiba mpya lazima waweke sawa hili swala
 
hii ndiyotanzania halisi! tusipoandamana, mambo hayatabadilika!
hali ni mbaya zaidi mikoani, ukienda kutafuta dawa wakiona tu bima,
utaambiwa hakuna, na utatembea mji mzima! kisa NHIF hawalipi madeni yao!
kwa nini watanzania tusubiri kufa kimyakimya ilhali ni haki yetu na yunaichangia??

TWENDENI BARABARANI TU!
 
Wana utani hawa watu,
kama mwajiri amepeleka hundi bima ya afya
wakuambie hakuna matibabu inakuwaje,
ni vizuri wale waajiri wababaishaje wafuatiliwe
na kama bima wamekula hela zetu wafuatiliwe,
wanataka watu wafie njiani sasa.
 
Mdogo wangu ambaye ni mwanachama wa Bima ya Afya aliniambia kuwa amenyang’anywa kitambusliho chake na maofisa wa mfuko waliomkuta hospitali ati kwa sababu kimechakaa. Hivyo kwa sasa hawezi kutibwa pamoja na kuwa yeye ni mwanachama na anaendelea kukatwa michango ya kila mwezi! Amekwenda kufautilia Kurasini ziliko ofisi za Bima ya Afya bila mafanikio ambapo ameishia kuambiwa kuwa vitambulisho vyote anavyo Mkurugenzi ambaye ameambiwa anaitwa Mikongoti na havitoki bila yeye.

Nikaona bora nimsaidie mdogo wangu kufuatilia kitambulisho chake kwani kwa niaba yake kwani yeye ni mdhaifu kiafya, hata hivyo sijafanikiwa hadi leo! Nimefika kurasini mara tatu na kuambiwa mhusika ambaye Bwana Mikongoti aidha yuko kwenye vikao au hayupo ofisini! Siku ya kwanza niliomba kuwaona wasaidizi wake, nikaambiwa kuwa kuna maelekezo kwamba suala la vitambulisho linashughulikiwa na Mkurugenzi peke yake. Nikauliza kuwa mbona sasa Mkurugenzi mwenyewe hapatikani? Nikajibiwa kuwa niendelee kusubiri kwani nikilazimisha nitawatia watu matatizoni.

Nikashawishika kuomba kumwona Mkurugenzi Mkuu. Hapo nikaambiwa huyo ndio asingeweza kunisaidia kitu. Nikashauriwa kuwa mvumilivu tu. Kumbe pale tulikuwepo watu zaidi ya wanne tuna tatizo linalofanana na wote tunamtafuta Mikongoti. Tulichoambulia pale ni kujua kuwa yale mambo ya kusumbuliwa kwa wanachama yameanza kujitokeza tangu huyu Bwana Mikongoti aliporudishwa makao makuu kutoka mwanza na kuchukua nafasi ya ukurugenzi wa operesheni. Kwa mantiki inaonyesha kuna mtu alikuwa anashikilia hiyo nafasi ambaye hatukuhitaji kujua yuko wapi? Kwani sisi tulichokuwa tunataka ni kutatuliwa matatizo yaliyotupeleka pale.

Wana-jf hadi leo mdogo wangu ninalazimika kumlipia matibabu ilhali yeye ni mwanachama wa mfuko. Sasa naomba ushauri kwani ninaona mdogo wangu anatesekea haki yake. Hivi kitambulisho kuchakaa ni kosa la aliyepewa? Je, sheria inasemaje? Maana ninataka kulichukua hili suala kisheria kwavile ningetaka Bima ya Afya wanirudishie fedha zangu nilizotumia kumtibia mwanachama wao.

Ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu wa bBima ya Afya, Bwana Mikongoti na wakurugenzi wengine wajenge utaratibu wa ku-delegate kazi hasa kwenye taasisi kama hiyo inayoshughulikia mambo ya watu wengi.
 
HIi NHIF ifutwe tu haina tija kwa mtanzania, kwanza wana kadi za aina mbili. ya Kijani na ya pink km sikosei, hii ya kijani inathaminika sana ndo viongozi wengi wanatumia lkn hii ya pink ambayo ndo watu wengi wanayo maskini kwenye mahospitali mengi hawaitaki kabisa kuiona. sa NHIF mpo kwa ajili ya viongozi tu au? na hawa watu wa chini wanaotoa michango yao kila mwezi pesa zao zinakwenda wapikm hawapati huduma?
 
Hawa Bima ya afya ni matapeli na wababaishaji wakubwa. Nimeanza kukatwa mshahara toka August Mwaka jana na nikajaza fomu za kujiunga Oktoba lakini mpaka leo sijapata hiyo kadi na huku wanaendelea kunikata mshahara, gharama za matibabu najilipia mwenyewe kwani mwajiri alishasitisha huduma hiyo toka michango ilipoanza kupelekwa NHIF.
 
mie nakatwa toka september 2006 mpaka leo sijapewa kadi! kimsingi hawa watu ni wezi tu
 
Msaada jamani, NINA MAMA MGONJWA ANATIBIWA TAASISI YA MOYO KAANDIKIWA DAWA KWENDA BIMA WAMESEMA WANAUPDATE PRICE ARUDI BAADA YA WIKI MBILI SASA MARADHI YATASUBIRI WIKI MBILI AU NDIO UFISADI WA MAKATO YETU. NAWAKILISHA
 
Mkuu heshima yako.
Mbona bima ya afya hua hawatoi dawa? Ila kama ni dawa za kununuliwa ambazo zinahitaji kibali kutoka bima ya afya waweza kwenda pale makao makuu kurasini na ukashughulikiwa mara moja.

Sijawahi kwenda pale na mgonjwa nikapewa excuse yoyote labda wewe ulishindwa kujieleza vizuri.
 
Makato ya matibabu yako kisheria hivyo kinachotakiwa kwa mtumishi anayechangia ni kujaza fomu na kuziwasilisha katika ofisi yoyote ya Mfuko kisha utaratibu wa kuandaliwa kitambulisho utafuatwa na kwa haraka zaidi hivyo kama hujajaza fumo jitahidi ujaze ili uepukane na lawama kwa Mfuko.
 
Hawa Bima ya afya ni matapeli na wababaishaji wakubwa. Nimeanza kukatwa mshahara toka August Mwaka jana na nikajaza fomu za kujiunga Oktoba lakini mpaka leo sijapata hiyo kadi na huku wanaendelea kunikata mshahara, gharama za matibabu najilipia mwenyewe kwani mwajiri alishasitisha huduma hiyo toka michango ilipoanza kupelekwa NHIF.

Mkuu mi sidhani kama bima ya afya kuna utapeli wowote.
Moja ya mashirika yanayojitahidi kujali wateja ni pamoja na bima ya afya ukizingatia wao wana deal na wagonjwa ambao wengi wao hua wanakua na stress.
Sasa basi kuhusu kitambulisho maybe hujafuatilia sehemu ulipowasilisha form yako ....ILA ushauri ni vyema ukahakikisha form yako inawasilishwa kwenye ofisi zao zilizopo kanda maana sometimes waajiri wetu hua hawapeleki form zetu bima ya afya mapema ndo maana hua vitambulisho vinachelewa.
 
Ni moja ya mashirika yanayofatunyonya watanzania. Sitaki hata kulisikia hili shirika!!

Siku ukiumwa au ndugu yako akiumwa ndo utajua umuhimu wa kua na bima ya afya........mbona hua unakata insurance za magari na miaka nenda rudi hujawahi kupata faida yoyote?.
Mi nakushauri ujaze form upewe vitambulisho na vya wategemezi wako na siyo lazima wewe binafsi uugue ila bima ya afya ukiwa nayo yaweza hata kumsaidia mzazi wako au mtoto wako kwa maana NHIF wanaongoza kwa kutoa mafao mengi ya matibabu kuliko bima zingine za afya kwa africa nzima.
 
Mkuu mi sidhani kama bima ya afya kuna utapeli wowote.
Moja ya mashirika yanayojitahidi kujali wateja ni pamoja na bima ya afya ukizingatia wao wana deal na wagonjwa ambao wengi wao hua wanakua na stress.
Sasa basi kuhusu kitambulisho maybe hujafuatilia sehemu ulipowasilisha form yako ....ILA ushauri ni vyema ukahakikisha form yako inawasilishwa kwenye ofisi zao zilizopo kanda maana sometimes waajiri wetu hua hawapeleki form zetu bima ya afya mapema ndo maana hua vitambulisho vinachelewa.

Mkuu, nina uhakika na ninachokisema, Bima ya afya ni wababaishaji kwani Meneja Rasilimaliwatu (HRM) wa ofisini kwetu amekuwa akifuatilia kila wiki lakini bila mafanikio. Inatia hasira kukatwa makato kila mwezi pasipo kupata huduma. Wafanyakazi wengi wa ofisi yetu hawajapata hivyo vitambulisho lakini makato kama kawaida, kama sio utapeli ni nini mkuu?
 
Kwa upande wa WIZI BIMA YA AFYA halina ubishi. Hata Mkurugenzi Mkuu Humba analitambua na kukiri kuhusu hili. Hapa tunaongelea wizi ambao madhara yake ni makubwa na yanaweza kupelekea NHIF kushindwa hata kufanya malipo. Katika uozo wa NHIF ni kulipa malipo hewa kwa mahospitali. Ninamfahamu mwenye Hospitali hapa Dar es Salaam anasema NHIF imemsaidia sana kwani kuna upenyo wa kufanya madai yasiyo halali. Hili ndilo Bima ya Afya ingeanza kulishughulikia.

Mtu unaweza kuwa na kitambulisho safi lakini wenye hospitali wanafanya madai hewa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ndani ya mfuko. Bwana Mikongoti angesimamia kuona mfuko unalipa malipo halali na sio kusumbua wagonjwa mahospitalini na kuwanyang'anya vitambulisho ati vimechakaa! Kama kimechakaa si angeamuru nipatiwe kingine kipya! Ni ushauri wa bure tu BWana Mikongoti.
 
Back
Top Bottom