Natangaza rasmi kujivua CCM na kuwa mwanachama wa CHADEMA; wewe je?

WANAJF:
Kwa heshima na taadhima napenda kuutangazia Umma wa Watanzania popote walipo chini ya Jua kwamba nimeamua kwa dhati kabisa bila kushawishiwa na mtu yeyote bali ni kwa msukumo wa Uzalendo na upendo nilionao kwa nchi yangu ya Tanzania, ambayo imekuwa na hali mbaya sana na inazidi kuwa mbaya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisiasa kila kukicha. Na mbaya zaidi hali ya maisha kwa wananchi walio wengi inazidi kuwa mbaya, kwani gharama ya maisha inazidi kupanda kila sekta.

Nimekuwa mwanachama wa CCM mwaminifu toka nilipozaliwa na sasa yapata miaka 33 na tawi langu ni Ubungo. Mwaka 2005 nikiwa chuoni, nilikuwa kati ya watu waliomfanyia kampeni Rais wangu Kikwete ili kuweza kuwa Rais wa Tz. Kwanza kabisa katika harakati za kupata mgombea wa CCM kule Chimwaga Dodoma, siku hiyo nilishinda kwenye TV nikiomba JK Kikwete ashinde. Na siku hiyo hata vipindi sikuweza kuhudhuria kwasababu ya msisimko niliokuwa nao na kutaka hasa Kikwete aweze kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, na ndivyo ilivyotokea. Hakika nilifurahi sana na mara moja nilianza kuhamasisha vijana wenzangu na hata ndugu zangu vijijini ili kumpigia Kikwete kura. Mwisho wa siku alishinda na hakika ilikuwa furaha yangu kuu sana, LAKINI, LAKINI, LAKINI!!!

Mara tu Rais wangu alipoingia madarakani na nikaanza kupima uwezo wa utendaji wake, teuzi zake ambazo nyingi hazizingatii vigezo bali zimejaa walakini, na mwelekeo wa nchi kiujumla, hakika nilianza kupoteza matumaini na Rais wangu na serikali yake kwa ujumla. Hatahivyo, niliendelea kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu nikiwa na matumaini kwamba ipo siku Rais wangu akipata Uzoefu katika ngazi ya Urais, ndipo ataanza kuleta mabadiliko makubwa katika ngazi zote hasa za kiuchumi na maendeleo. Nilitoa kama miaka 3 kwa Rais wangu ili apate Experience, lkn sikuona faida ya huo uzoefu na hata sasa ana uzoefu wa miaka karibia 7 kwenye Urais lkn hakuna faida,na badala yake Tz imefanikiwa kuingia kwenye 3 Bora ya nchi zinazoongoza kwa Ombaomba Duniani,tukiwa na Iraq na Afghanistan.

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu OMBAOMBA hasa TZ yenye rasilimali lkn sipati majibu, je ni kweli hatuna kabisa watu makini ambao wanaweza kusaidia uchumi wetu kuimarika? Jibu nililo nalo ni kwamba TZ ina watu wazuri sana lkn tatizo liko kwenye mfumo wa taasisi zetu mbalimbali na serikali yetu kiujumla. Pia nikasema na ninaamini kwamba RAIS wangu hakuwahi, hana, na hatakuwa na VISION ya wapi anataka kuipeleka Tanzania.

Ndg. Wanajf naomba nisiwachoshe na maneno mengi lkn naomba niseme hili, kwamba naomba msamaha kwa wana-CCM wenzangu ambao nimekuwa nao kwa kipindi chote hicho akiwemo marehemu baba yangu aliyewahi kuwa Kiongozi wa CCM na serikali katika ngazi ya Kata na Kijiji kuhusu maamuzi haya ya kuachana na CCM na kujiunga CHADEMA, chama ambacho kinaonekana kuwa na vision ya kuibadilisha Tanzania. Naomba wale wote nitakaowakwaza kwa maamuzi yangu haya wanisamehe na kamwe wasinilaumu kwasababu si mimi niliyeamua BALI NI MSUKUMO WA UZALENDO NA UPENDO KWA NCHI YANGU TANZANIA ndiyo maana nimeamua Kuvua Gamba na Kuvaa GWANDA.

KWAHIYO: Kuanzia leo tarehe 01.06.2012, Mimi TELO, nikiwa na akili zangu timamu na kwa uwezo wangu wote na kwa upendo na Uzalendo nilionao dhidi ya nchi yangu Tanzania, Natangaza Rasmi kwamba Nimekuwa Mwanachama wa CHADEMA.

WITO: Nawaomba Watanzania wote popote mlipo chini ya JUA, tuungane kwa pamoja kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Na huo muungano ninauongelea hapa ni kwa kujiunga na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

Natanguliza shukrani sana, kwani hatimaye NIMEKUWA HURU; TENA HURU KWELI KWELI baada ya kuachana na maumivu ambayo nimekuwa nayo tangu mwaka 2005.

Ni mimi,
TELO
01.06.2012

Kujivua CCM katangazie M4C, hapa siyo mahali pake
 
Ndugu usije ukauachie moyo wako 100% kuamini Chadema, chama hicho kimejawa na viongozi wenye utashi wa kutumia matatizo yanayoikumba Tanzania hivi sasa ili kujijengea UMAARUFU wa kisiasa kwa nia ya kutumia migongo yenu wanemeeke,

Dr. Slaa ni mbinafsi ambaye anajizoelea posho nyingi huku watz wakilala njaa

Mbowe amediriki kupiga chenga mapesa ya walalahoi aliyokopeshwa na NSSF.

Hayo ni mafupi tu ya viongozi wako wa Chadema
unadhani kama matatizo haya nyinyiemu mlosababushia tungejua habari ya chadema.usimtishe mwenzuo anajua analifanya.najua nawewe unatamani sana tu,
 
Ukitaka na kadi nitakupa

Sent from my BlackBerry 9300 using Jambo Adverts Tanzania Networks.
 
Welcome Telo kwenye gari kubwa la wapenda haki za wananchi,waache hao wachache wasioelewana lakini muda wao ukaribu
 
Nadhani Iran kuwemo siyo muhimu, alitaka kuonyesha kuwa Tz imo kwenye ukanda huo.

JF ni shule sio sehemu ya porojo kama wewe huoni muhimu sio wote sijui kwa nini Pro-Chadema JF hata kwenye mambo ya udaku wanakuwa kitu kimoja...kama wewe unaambiwa Iran ni omba omba wa tatu duniani na wewe unakubali kazi kweli kweli.
 
Kujivua CCM katangazie M4C, hapa siyo mahali pake
M4C Haina mipaka ndugu ndiyo maana hata waliosema Dar ina wenyewe sasa hivi wako ICU!
Utashanga matangazo hadi kwenye NEC ya CCM we subiri utaona!.
 
JF ni shule sio sehemu ya porojo kama wewe huoni muhimu sio wote sijui kwa nini Pro-Chadema JF hata kwenye mambo ya udaku wanakuwa kitu kimoja...kama wewe unaambiwa Iran ni omba omba wa tatu duniani na wewe unakubali kazi kweli kweli.
Hoja ikiwa nzito watu mnaanza kuwa wanafunzi, Duhh .................! pata somo sasa TZ ni moja kati tatu ombaomba wenzi Iraq na Afghanistan.
Rudi kwenye mada!
Je inakubali kuwa GAMBA ulilomo na wenzio ndio mmetufikisha huko?

Ingia huku panakufaa zaidi, ukirudi tutajadili hoja upya!!
Jukwaa la Elimu (Education Forum)
 
M4C Haina mipaka ndugu ndiyo maana hata waliosema Dar ina wenyewe sasa hivi wako ICU!
Utashanga matangazo hadi kwenye NEC ya CCM we subiri utaona!.

Ahsante ndugu yangu kwa kunjibia tena majibu mazuri sana. People Powerrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kumbuka CDM ni chama cha wachache, wateule, wanajuana kwa vilemba. CCM ni kimbilio la wote
 
Kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa mpaka uwe na KADI ya uanachama. Tafuta KADI mdogo wangu!
 
Kumbuka CDM ni chama cha wachache, wateule, wanajuana kwa vilemba. CCM ni kimbilio la wote
Rekebisha, CCM haiwezi kuwa kimbilio tafuta neno jingine,
Watanzania wote kabla ya kurudi kwa vyama vingi utake usitake kwao ilikuwa CCM.
Hivyo hakuna mtu anakimbilia kwao ila ana........... kwao.
Kimbilio ni sehemu nyingine tofauti na kwenu, kama kwenu unaona hapakukufai.
 
Jamani mi nina tatizo kubwa sana na sijui kama wanasheria wanaweza kunisaidia. Nilimpa kura mgombea wa Urais wa Nyinyiem, Jakaya Kikwete, akashinda. Alitoa ahadi kemkem. Ajabu hajatekeleza hata moja ukiacha hii ya juzi ya kukabidhi sh milioni 10 kwa familia ya Kanumba. Sasa swali. Je, naweza kumshtaki yeye na chama chake nikidai kurudishiwa kura yangu, kuombwa radhi na kulipwa fidia kwa kuniharibia kura yangu na pia kuiomba mahakama imwamuru Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kutangaza upya matokeo ya Urais kwa kupunguza kura yangu? Ushauri jamani naumia sana!
 
Pole sana! wengi tulizipoteza mkuu!.
Hayo yalitabiriwa na nabii wa siasa nchini Pro.J tukamwita mhuni. Tafuta mistari ya NDIYO MZEE usome!.
Kuhusu msaada subiri KATIBA mpya maana matokeo unayozungumzia ni ya Urais.
Unaweza ukajikuta unavunja Katiba kwa sasa.
 
Jamani mi nina tatizo kubwa sana na sijui kama wanasheria wanaweza kunisaidia. Nilimpa kura mgombea wa Urais wa Nyinyiem, Jakaya Kikwete, akashinda. Alitoa ahadi kemkem. Ajabu hajatekeleza hata moja ukiacha hii ya juzi ya kukabidhi sh milioni 10 kwa familia ya Kanumba. Sasa swali. Je, naweza kumshtaki yeye na chama chake nikidai kurudishiwa kura yangu, kuombwa radhi na kulipwa fidia kwa kuniharibia kura yangu na pia kuiomba mahakama imwamuru Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kutangaza upya matokeo ya Urais kwa kupunguza kura yangu? Ushauri jamani naumia sana!

Pole sana ndugu kwa hayo yanayokuumiza. Usiwe na wasiwasi kwani ni wengi tu wanaojuta sasa kwa kura zao, kwani matokeo yake hawayaamini mpaka leo wala kesho. Lkn mimi nina habari njema kwako, Jiunge CHADEMA leo na kamwe hutajutia maamuzi yako, kwani mimi toka nijivue gamba-CCM na kujiunga CHADEMA asubuhi ya leo, hakika nina furaha kubwa sana na najisikia vizuri sana kwasababu nimetua mzigo niliokuwa nao karibia miaka 7 sasa wa kumpigia kampeni na kura Rais JM Kikwete. Usisite ndugu, fanya maamuzi leo na nafsi yako itakuwa HURU KWELI KWELI.
 
WANAJF:
Kwa heshima na taadhima napenda kuutangazia Umma wa Watanzania popote walipo chini ya Jua kwamba nimeamua kwa dhati kabisa bila kushawishiwa na mtu yeyote bali ni kwa msukumo wa Uzalendo na upendo nilionao kwa nchi yangu ya Tanzania, ambayo imekuwa na hali mbaya sana na inazidi kuwa mbaya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisiasa kila kukicha. Na mbaya zaidi hali ya maisha kwa wananchi walio wengi inazidi kuwa mbaya, kwani gharama ya maisha inazidi kupanda kila sekta.

Nimekuwa mwanachama wa CCM mwaminifu toka nilipozaliwa na sasa yapata miaka 33 na tawi langu ni Ubungo. Mwaka 2005 nikiwa chuoni, nilikuwa kati ya watu waliomfanyia kampeni Rais wangu Kikwete ili kuweza kuwa Rais wa Tz. Kwanza kabisa katika harakati za kupata mgombea wa CCM kule Chimwaga Dodoma, siku hiyo nilishinda kwenye TV nikiomba JK Kikwete ashinde. Na siku hiyo hata vipindi sikuweza kuhudhuria kwasababu ya msisimko niliokuwa nao na kutaka hasa Kikwete aweze kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, na ndivyo ilivyotokea. Hakika nilifurahi sana na mara moja nilianza kuhamasisha vijana wenzangu na hata ndugu zangu vijijini ili kumpigia Kikwete kura. Mwisho wa siku alishinda na hakika ilikuwa furaha yangu kuu sana, LAKINI, LAKINI, LAKINI!!!

Mara tu Rais wangu alipoingia madarakani na nikaanza kupima uwezo wa utendaji wake, teuzi zake ambazo nyingi hazizingatii vigezo bali zimejaa walakini, na mwelekeo wa nchi kiujumla, hakika nilianza kupoteza matumaini na Rais wangu na serikali yake kwa ujumla. Hatahivyo, niliendelea kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu nikiwa na matumaini kwamba ipo siku Rais wangu akipata Uzoefu katika ngazi ya Urais, ndipo ataanza kuleta mabadiliko makubwa katika ngazi zote hasa za kiuchumi na maendeleo. Nilitoa kama miaka 3 kwa Rais wangu ili apate Experience, lkn sikuona faida ya huo uzoefu na hata sasa ana uzoefu wa miaka karibia 7 kwenye Urais lkn hakuna faida,na badala yake Tz imefanikiwa kuingia kwenye 3 Bora ya nchi zinazoongoza kwa Ombaomba Duniani,tukiwa na Iraq na Afghanistan.

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu OMBAOMBA hasa TZ yenye rasilimali lkn sipati majibu, je ni kweli hatuna kabisa watu makini ambao wanaweza kusaidia uchumi wetu kuimarika? Jibu nililo nalo ni kwamba TZ ina watu wazuri sana lkn tatizo liko kwenye mfumo wa taasisi zetu mbalimbali na serikali yetu kiujumla. Pia nikasema na ninaamini kwamba RAIS wangu hakuwahi, hana, na hatakuwa na VISION ya wapi anataka kuipeleka Tanzania.

Ndg. Wanajf naomba nisiwachoshe na maneno mengi lkn naomba niseme hili, kwamba naomba msamaha kwa wana-CCM wenzangu ambao nimekuwa nao kwa kipindi chote hicho akiwemo marehemu baba yangu aliyewahi kuwa Kiongozi wa CCM na serikali katika ngazi ya Kata na Kijiji kuhusu maamuzi haya ya kuachana na CCM na kujiunga CHADEMA, chama ambacho kinaonekana kuwa na vision ya kuibadilisha Tanzania. Naomba wale wote nitakaowakwaza kwa maamuzi yangu haya wanisamehe na kamwe wasinilaumu kwasababu si mimi niliyeamua BALI NI MSUKUMO WA UZALENDO NA UPENDO KWA NCHI YANGU TANZANIA ndiyo maana nimeamua Kuvua Gamba na Kuvaa GWANDA.

KWAHIYO: Kuanzia leo tarehe 01.06.2012, Mimi TELO, nikiwa na akili zangu timamu na kwa uwezo wangu wote na kwa upendo na Uzalendo nilionao dhidi ya nchi yangu Tanzania, Natangaza Rasmi kwamba Nimekuwa Mwanachama wa CHADEMA.

WITO: Nawaomba Watanzania wote popote mlipo chini ya JUA, tuungane kwa pamoja kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Na huo muungano ninauongelea hapa ni kwa kujiunga na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

Natanguliza shukrani sana, kwani hatimaye NIMEKUWA HURU; TENA HURU KWELI KWELI baada ya kuachana na maumivu ambayo nimekuwa nayo tangu mwaka 2005.

Ni mimi,
TELO
01.06.2012
Ndugu yangu Telo nakupongeza kwa uamuzi huo mzuri uliofikia , mimi marehemu baba yangu enzi zile mwaka 1995 alikuwa mwanachama wa Chadema mzuri sana ila mimi nilijiunga CCM baada yakuona Chadema hakina mwelekeo .Lakini kwa mujibu wa mambo yanavyokwenda naona kwa dhati kabisa mimi kuendelea kuwa mwanachama wa CCM ni kupoteza muda wangu kwani sioni la maana kilichonifanyia zaidi ufisadi,ujinga,siasa majungu .ninashawishika nami kujiunga Chadema kwani ni tumaini la wengi.natanguliza shukrani za dhati kwakunipa mwamko .

Ni mimi
Alice
 
Back
Top Bottom