Natangaza rasmi kujivua CCM na kuwa mwanachama wa CHADEMA; wewe je?

Japo imekuchukua mda mrefu kufika pahala sahihi; HONGERA KWA UHAMUZI SAHIHI. Mungu akupe nguvu maana na amini tukiwa pamoja ukombozi utaifikia Tanzania na Watanzania.
 
Hata huko ambako unasema umehamia kwa kuona kuna Vision ya maedeleo, ikitokea wakashindwa kuwa na vision ya kulisaidia taifa katika maendeleo, usije ukatutangazia kuwa umeamua kuwatosa. Tanzania yetu hii, usidanganyike, hakuna chama hata kimoja chenye vision ya kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa watanzania. Narudia tena, hakuna chama hata kimoja chenye lengo la dhati la kuinua uchumi wa Tanzania. Nakaribisha matusi kutoka...
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".

I do wish ningekuwa mtaalamu wa hayo matusi!

But sikutukani ila nataka uelewe kuwa ni "afadhali kujaribu usilolijaribu kuliko kukaa chini na kulaumu lililokushinda". Watu wengi wanashindwa kuendelea kwa sababu ya kukosa uthubutu. Kwa sababu eti "hawana mitaji" wakati wanawaona wenzao walioanza biashara na vigenge vya 10000!............... Ni hivyohivyo tunaendelea kuwa masikini kwa sababu hii nchi hatuiwezi kama tulivyosadikishwa na "chama Twawala" kwa hiyo tuwape wawekezaji-wachukuaji,wanaoweza wajichukulie bila gharama,wasilipe hata kodi! .........Alafu uje na wewe ueneze huo ugonjwa wako wa ajabu wa kutisha Watanzania waogope kubadilisha Ubovu.... Una roho gani wewe? mbona humhurumii hata mama yako,kama siyo dada yako au mkeo? Hivi unajua yaliyomfika alipokuwa anakwenda kliniki wewe? Unajua alivyoipata kule "leba" kwa ajili ya sera mbovu zinazozorotesha huduma za afya?..kamwulize. Halafu mwambie hayo maneno unayobwabwaja humu uone atakwambiaje!. Then urudi humu uandike upya!

Amka ndugu yangu. Hii siyo nchi ya Wagaga-gigi-koko. Wala Siyo Kusadikika! Hii Nchi ipo, inaishi. Kama ina hali mbaya wacha wanojaribu kutafuta tiba waendelee we lala kimya. Wakifanikiwa amka Sherehekea nao! Ila uwe na aibu yako pembeni kwani uliwakana wakati wanasaka maziwa na asali!

Wala sijaribu kusema Kujiunga CDM ndiyo ukombozi wa Tanzania! Ila naamini Kuiondoa Serikali ya CCM ni Sehemu muhimu ya Tiba ya Tanzania. Then tuangalie nani mwenye nafuu japo kidogo ya ki-mwelekeo tumpe dhamana aongoze matibabu yaliyobakia.! Am I reaching You?

Sisemi zaidi....
 
Umenikumbusha kitu kimoja kuhusu vision ya rais wetu juu ya nchi kimaendeleo, nakumbuka mwaka 2010 kwenye maswali ya papo kwa papo aliulizwa kuhusu hilo mheshimiwa rais akajibu "ninataka watanzania wanikumbuke kwa kuwatoa hapa na kwapeleka pale"
Kwanza nilipigwa na butwaa kisha nikasema basi tena ishakula kwetu lakini bado alichaguliwa tena licha ya kutoonesha vision yoyote.
 
Back
Top Bottom