Natangaza nia yangu juu ya kutengeneza filamu ya kipelelezi, ila naomba msaada wa yafuatayo...

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,302
Habari wanajamvi na wapenzi wa filamu, nina nia ya kutengeneza filamu ya kipelelezi ila kuna vitu nahitaji kuvijua hasa vitengo vya usalama ndani Serikali, mfano ninajua kwamba kuna kitengo kinahusika na ufuatiliaji wa pesa haramu nadhani kipo BOT au WIZARA YA FEDHA kwa anayefahamu anisaidie na jina lake pia, na katika vikosi vya usalama wa Taifa nafahamu TISS peke yake, na je ndani ya TISS kuna vitengo vingine au la? Na kutokana na ugumu wa kupata mavazi ya polisi hapa Nchini katika moja ya Scene zangu kuna sehemu mauaji yametokea na nia yangu ni kufanya watu wa usalama wa Taifa (ambao sijajua ni Division gani) wanaiwahi ile maiti na kutaka polisi wasijue kitu kama vile wafanyavyo CIA, MI6 na vikosi vingine vya kijasusi kwenye Movie au Novel za mbele sasa tatizo langu sijajua je vikosi kama hivyo vipo hapa Nchini na je vinafanya kazi chini ya order kutoka mamlaka gani?
Kingine ni jina la kitengo cha kuzuia dawa za kulevya ndani ya jeshi la polisi (sio tume).
Natanguliza shukrani zangu na mwenye kufahamu anisaidie hayo, na baada ya kukamilisha story na kupanga script naahidi kuiweka hapa baadhi ya Scene wadau mnisaidie tuweze kuisogeza tasnia ya filamu Nchini.
 
Mkuu kwanza nikupe hongera kwa wazo lako
Pili hivi ndivyo wenzetu mbele wanavyotengeneza movies zao kwa kutafuta washauri kutokana na aina ya movies

Naamini JF ni kisima cha maarifa utapata wajuzi toka kona hizo kwa ushauri zaidi

Nahisi ningeijua stori kamili ningekuwa katika nafasi nzuri ya kukushauri maana nimewahikupitia moja ya vitengo ulivyotaja
 
Kiongozi asante kwa kunipa matumaini ukweli ni kwamba nimekuwa na hili wazo muda mrefu na tayari hata location nimeshaandaa kwani sehemu kubwa ya upigaji picha itakuwa studio (Blue au Green screen), kwa ufupi story inahusu mmoja wa wahamasishaji wa mauaji ya kimbari kule Rwanda baada ya kutafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio hatimaye TISS wakapata taarifa kwamba yupo Nchini Tanzania na wakati huo huo BOT wakapokea taarifa kutoka bank kadhaa hapa Nchini kwamba kuna mzunguko fulani wa hela usio wa kawaida hivyo ikabidi BOT watoe taarifa sehemu husika (NDIO HICHO KITENGO CHA FEDHA HARAMU NINAPOTAKA KUKIJUA) na tayari kukawa na matukio kadhaa yaliyotokea yanayofanya watu wa usalama washtuke.
Lengo la huyo mhalifu hasa ni kufanya biashara haramu na kutaka kuichonganisha Tanzania na Mataifa mengine jirani ili ionekane Tanzania tunawasaidia waasi wa Nchi fulani, bado naendelea kuhangaika na mtiririko wa story lakini kama nilivyosema nitataka sana ushauri wa wadau kama nyinyi ili angalau tuukaribie ukweli wa filamu, asante Mkuu.
Vp ulishaipata Glory na kuiangalia?
 
Ok mkuu nimekupata, nipo napoza kiu mida hii natumia simu nikitulia home kwa pc ntajaribu kukupa kaushauri

BTW nimeiangalia GRORY majuzi tu mkuu, niliipenda sana hasa Denzel alivyo act mtata fulani hivi
Lakini it has a very sad ending aisee
 
Kiongozi asante kwa kunipa matumaini ukweli ni kwamba nimekuwa na hili wazo muda mrefu na tayari hata location nimeshaandaa kwani sehemu kubwa ya upigaji picha itakuwa studio (Blue au Green screen), kwa ufupi story inahusu mmoja wa wahamasishaji wa mauaji ya kimbari kule Rwanda baada ya kutafutwa kwa muda mrefu bila mafanikio hatimaye TISS wakapata taarifa kwamba yupo Nchini Tanzania na wakati huo huo BOT wakapokea taarifa kutoka bank kadhaa hapa Nchini kwamba kuna mzunguko fulani wa hela usio wa kawaida hivyo ikabidi BOT watoe taarifa sehemu husika (NDIO HICHO KITENGO CHA FEDHA HARAMU NINAPOTAKA KUKIJUA) na tayari kukawa na matukio kadhaa yaliyotokea yanayofanya watu wa usalama washtuke.
Lengo la huyo mhalifu hasa ni kufanya biashara haramu na kutaka kuichonganisha Tanzania na Mataifa mengine jirani ili ionekane Tanzania tunawasaidia waasi wa Nchi fulani, bado naendelea kuhangaika na mtiririko wa story lakini kama nilivyosema nitataka sana ushauri wa wadau kama nyinyi ili angalau tuukaribie ukweli wa filamu, asante Mkuu.
Vp ulishaipata Glory na kuiangalia?
Seen this useful post very late but i think i'll something!!
 
Back
Top Bottom