Natamani kurudiana na mke wangu wa zamani

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Nilikutana na huyu dada kipindi nimemaliza chuo, sikua nikimpenda tangu mwanzo kwani nilijua kabisa si mtu wa hadhi yangu. Lakini kwakua nilikua na shida na nilimuona kama mtoaji niliamua kuendelea naye. Mara ya kwanza nilimtongoza tu kwakua nilikua na hamu ya kufanya mapenzi, sikujali mwanamke yeyote aliyekuja mbele yangu, yeye alikua anauza matunda stendi, kwa wenyeji wa dar nadhani mnafahamu wale wadada wanaouza matunda usiku na vibatari.

Nilinunua ndizi kwake na kuomba namba ya simu, siku iliyofuata nilimtafuta na kumuita kwenye getto la mshikaji, hakuja alitaka tuonane sehemu nyingine, sikua na pesa hivyo nilizuga niko bize. Lakini jioni yake nilipita ile sehemu aliyokua anauza matunda na kumsalimia, tuliongea na nilimuona kama ni mchanmgamfu, nilimuambia kuwa mimi nimemaliza chuo na nasubiri ajira. Tuliopngea mengi na siku ile aliniacha nikachukua ndizi bila kulipa.

Tulianza kuwa marafiki, mimi bado nilikua naishi kwetu, urafiki wetu mkubwa ulikua ni wa mimi kwenda kuchukua matunda bure, kumdanganya danganya kuwa nampenda nakula ndizi zangu naondoka. Sikumoja alinikaribisha kwake, nikiamini kuwa itakua ni sehemu ya hovyo nilishangaa sana kuona kuwa alikua akiishi katika nyumba nzuri, nikisema nyumba nzuri namaanisha nyumba yake aliyokua amejenga. Haikua kubwa sana lakini ilikua ya kisasa flani.

Vyumba vitatu, na sebule, jiko zuri na vitu vingine vingine vingi vizuri ambavyo mimi hata sikua na uwezo navyo, hata kwetu hatukua na hivyo vitu, tena sisi wenyewe nyumba ilikua ya urithi inakaribia kudondoka. Aliniambia nikwake, nilishtuka nikiamini kuwa labda kapangishiwa na mwanaume, lakini aliponielezea namana livyojenga kwa shida nilimuamini. Hakua na ile biashara tu ya ndizi, hapana, ile ilikua ni biashara yake ya usiku, mchana alikua zake Karume anahangaika na mtumba.

Pia alikua na kijana mwingine kamuajiri soko la tandika, aliniambia namana livyokua akichaprika, namna alivyokua akitafuta nilichoka kabisa. Nilianza kujiona fala na nilianza kumpenda nikitamani maisha yake, kipato chake kwa mwezi kilikua ni kikubwa kuliko mfanyakazi wa serikali na digrii zake. Alikua ni binti tu wa miaka 25 lakini. Alikuja Dar akiwa na miaka 16, alianza kufanya kazi za ndani na alikusanya mtaji wake kwa kuuza icecream akitumia friji la bosi.

Bosi alioona anapata pesa alimfukuza kazi lakini hakurudi kijijini, aliingia barabarani akawa anauza ndizi usiku, aliifanya hiyo biashara kwa mwaka mzima, akafanikiwa kununua kiwanja, lakini hakutaka kujenga, aliraka kufungua biashara nyingine, alitafuta sehemu Karume na kuanza mtumba, akaanza kujenga taratibu na nyumba yake ilichukua takribani miaka mitano kukamilika. Hapo alikua akisomesha waodgo zake watano na mmoja tayari yupo chuo kikuu.

Kwa kusikiliza nilijua kuwa ana akili sana na akipata mtu msomi kama mimi basi tutafanikiwa zaidi. Nilijilazimisha kumpenda, nikaanzisha naye mahusiano, kweli alinipenda na kwakua mimi ni msomi basi aliniamini zaidi. Nilikaa mtaani kwa mwaka mmoja bila ajita, mara nyingi nilikua nikila na kulala kwake, alikua akinipa pesa ya matumizi na kila mara alinisisitiza kufanya biashara. Alinisukuma sana akanitafutia mataji nikaanza biashara ya duka la vyombo, alikua anacheza mchezo na alipopokea alinipa Shilingi milioni tatu, akanitafutia na fremu na kunifungulia biashara.

Wakati huo nyumbani kwetu walishanichoka, ile kuombaomba pesa kila siku iliwachosha na hakuna aliyekua wakijali kama nipo au sipo. Hata nilipowaambia nimepata mchumba hakuna aliyejali na nilipotangaza ndoa hakuna mtu aliyechangia, Mama yangu mzazi alikua hata hataki kusikia naoa. Waliniona kama hasara kwani lengo la kunisomesha ilikua ni mimi kuja kuapta kazi serikalini na kuwahudumia wadogo zangu hivyo mimi kuhudumiwa na mwanamke ilikua kama dharau kwao.

Nilifunga naye ndoa ya kiislamu, ingawa yeye alikua ni mkristo lakini alikubali kubadilisha dini kwani alikua ananipenda sana na alikua tayari kufanya chochote kile ninachotaka. Maisha ya ndoa yalianza, ndugu walikataa hatakuja kwangu wakisema kuwa nimeolewa mpaka niwe na kwangu ndiyo watakuja. Lakini sikujali, mke wangu alinipa moyo na kunisukuma kufanikiwa. Mara zote alinifanya kujisikia vizuri, hakuninyanyasa kwakua ana kipato kikubwa, kwakua amenipa mtaji, alinifanya kuwa mwanaume na aliniacha kufanya maamuzi mengi.

Aliniambia biashara ya duka la vyombo iwe yangu nisimamie mpaka isimame yeye ahudumie kila kitu. Pamoja na kunipa zile milinio tatu za mwanzoni lakini bado alikua akipata pesa ananipa ananiambia ongeze amtaji, kutokana na mimi kusota sana mtaani sikuzembea, nilismimamia biashara mpaka ikasimama. Mungu alitujaalia kupata mtoto wakiume, wakati huo huo na mimi nilikua ninajenga, nilinunua kiwanja kimya kimya bila kumuambia mke wangu na kuanza kujenga, nyumba ilipokamilika ndipo nilimuambia.

Nilimuambia nilitaka iwe surprise kwani sikutaka anisaidie, alinielewe, tulihamia katika nyumba ile kubwa na tukanunua gari yetu. Ndugu zangu baada ya kuona nimeanza kufanikiwa walianza kujileta kwangu, alianza kuja Mama kisha dada zangu wawili, nyumba yetu ilikua kubwa hivyo haikua na shida sana, baada ya muda familia nzima ilihamia Mama akilalamika kuwa nimfanyie ukarabati nyumba yetu ya zamani ndiyo arudi, kwa wakati huo sikua na pesa za kufanya ukarabati.

Mwanzoni maisha yaliendelea vizuri lakini kama mnavyojua ndugu, mkishaanza kuishi pamoja basi maneno hayakosekani, mke wangu mimi ni mchumi, anaijua pesa na ndugu zangu wao ni watu wakutumia, ni wale watu wanaweza kutoa samaki kwenye friji mpaka wanaharibika hata hawjaali. Walianza kukorofishana kwani mke wangu alikua anawaambia, walianza kusema anawanyanyasa na kulalamika kwangu. Yakaanza kuzuka maneno kuwa hanifai na mambo mengine kibao.

Kila siku maneno yalizidi, mke wangu alivumilia ikashindikana akawa ananiambia na kunilalamikia. Mimi nilimuambia kuvumilia kwani ni wazazi wangu. Kuna kipindi Mama mkwe wangu aliumwa na kuja kukaa pale, alikuja kutibiwa lakini hakukaa hata mwezi, aliondoka kutokana na masimango ya ndugu zangu. Binafsi nilianza kushika pesa zangu, nilianza kujiona mwanaume na nilianza kumuona mke wangu kama siku niliyomuona kwa mara ya kwanza, nilimuona kama vile hafai kuwa na mimi kwakua si msomi.

Kabla ya kukutana na mke wangu nilikuaga na mpenzi wangu, yeye nilisoma naye chuo, sikuwahi kuachana naye, nilishamtambulisha mpaka nyumbani kwetu na hata wakati naoa bado alikua ni mpenzi wangu, nilimpa ujauzito na kupata mtoto ambaye alilingana kama mtoto wangu. Yeye alikua anafanya kazi na nilikua bado nampenda, kipindi sina kazi alipata mwanaume mwingine tukawa tumetengana kwa muda na alikuja baada ya mimi kuwa na biashara niliyofunguliwa na mke wangu.

Nilijua kabisa kuwa pesa ndiyo zimemleta kwangu kwani huko nyuma alikua na mwanaume mwingine mwenye pesa kidogo ambaye alimuacha. Lakini baada ya kuona maneno maneno yanazidi na kwakua alikua ni msomi mwenangu niliamua kuishi naye, nilimpangishia nyumba nikawa natumia muda mwingi sana kwake, mwanzo mke wangu hakujua lakini baadaye alijua na ndugu zangu nao walijua kwani walikua wakiwasiliana kila siku hata Mama yangu alikua akienda nilipokua nimempangia.

Msukumo ulikua mkubwa kutoka kwa ndugu zangu na kwakua sikua nikimpenda mke wangu kihivyo nilitafuta sababu mpaka kauchana naye. Nilimuambia turudi katika nyumba ya zamani niliyomkuta nayo na pale niwaache ndugu zangu kwani ni kelele nyingi, tuliporudi nilimleta yule mwanamke mwingine na kuanza kuishi naye, nilifunga ndoa nyingine kimya kimya na alipojua alikasirika, nilijua kuwa ataondoka alikubaliana na mimi kuoa mke wa pili.

Lakini mimi sikua tayari kuwa na wake wawili, nilimuambia kuwa nibora kauchana na kulea mtoto kwani sikua na mapenzi tena naye, aliomba msamaha na kulia sana lakini sikujali. Nyumba na vitu vingi nilivyokua nachuma nilikua nimeandika majina ya mtoto wangu yule ambaye nilizaa na yule mpenzi wangu mwingine hivyo tulipoachana alibaki na nyumba yake ambayo nilimkuta nayo na maisha kuendelea. Mke wangu alitaka kubaki na mtoto, lakini nilikataa na ndugu zangu nao walikataa.

Tulisumbuana sana lakini kwakua mke wangu mpya hakua akimtaka mtoto nilimuacha kuondoka naye. Hapo ndiyo ilikua mwisho wa mawasiliano yetu, nilikata kabisa mawasiliano na mke wangu na kuanza upya maisha na mke wangu mpya. Niliamini kuwa nitakua na furaha nilimuoa mwanamke ambaye alikua na elimu kama mimi, mwanamke niliyekua nampenda na kikubwa kabisa hata ndugu zangu nao walikua wakimpenda.

Nyumba ilikua na amani kwa miezi mitatu tu, lakini baada ya hapo yalianza malalamiko, mke wangu alikua hataki ndugu zangu, walikua wakimpangia maisha, mama alikua akiingilia kila kitu chake na kutaka kumuendesha. Tayari walishazoea kumuendesha na kumnyanyasa mke wangu wa zamani hivyo yeye alikua makini, alikua akiwalalamikia na pale nilipokua sichukui hatua basi alikua akitukanana nao na hata kufikia hatua kupigana na waodgo zangu. Mambo yalipozidi kuwa mabaya nilijitahidi na kufanyia ukarabati nyumba yetu ya zamani na kuwapeleka ndugu angu kusihi kule.

Baada ya ndugu zangu kuondoka nyumba ilikua na amani kwa muda, lakini likaja tatizo jingine, mke wangu mpya alikua ni mtu wa kutumia tu, hakua akijua kutafuta, nilikua nikimuacha dukani wiki moja nikirudi ni kama duka limefilisika, mimi nililazimika kusafiri mara kwa mara kununua mzigo, mara nyingi nilikua nikienda China, lakini nikirudi nakutana na mambo ya ajabu ajabu. Wakati huohuo ndugu zangu nao matatizo yalizidi, kila siku kuniomba pesa, biashara ilianza kuyumba kwa kukosa usimamizi.

Wateja walikua wananikimbia kila siku, mara nyingi biashara zote alikua akisimamia mke wangu wa zamani, alikua na wateja wake na alikua akijuana na karibu kila mtu, mimi nilikua kama picha tu sijui chochote ingawa nilijiona msomi ndiyo mwenye akili. Hali ilikua ngumu na kulazimika kuchukua mkopo, niliweka rehani nyumba tuliyokua tukiishi, nikapata mkopo wa kama milioni tisini, hapo sasa nilijua kama nitafanikiwa kwani nilipanga kupanua biashara yangu na kujipanga upya.

Lakini baada ya kupata zile pesa mke wangu alianza kulalamika kuwa anataka gari, sikuona kama ni kitu cha muhimu kwa wakati huo lakini alilalamika sana nikamnunulia gari ya milioni 20, hivyo kubakia na milioni thabini. Nilienda China kuchukua mzigo, nilitaka kuanza kuuza vyombo vya jumla na nilishapata wateja ambao wlainiagiza mzigo. Nilienda na kuleta mziogo mkubwa lakini tatizo lilikuja katika kuuza, biashara ilianza kuangumu, wale walioniahidi kununua walikua wakilalamika kuwa wana mzigo mkubwa na hauna wateja, nilikaa na mzigo ule kwa miezi mitatu bila kurudisha hata nusu ya pesa niliyokua nimechukua, nilihitajika rejesho na matumizi nayo yaliongezeka.

Hali ile iliendelea na kwa mwaka mmoja nilikua nimebaki sifuri, biashara ilishakufa, nilisharudi nyumbani kwetu kukaa na ndugu zangu kwani ile nyumba niliyoweka rehani ilichukuliwa na benki, mimi na mke wangu tulirudi kwa wazazi wangu, tukalazimika kuishi hivyo kwa kugombana kila siku. Nilikua sijafunga biashara kabisa lakini nilikua kama naenda tu kuangalia vitu ambavyo havina wateja TRA nao walikua wanasumbua kwani nilishaahau kulipa kodi na nilikua na deni kubwa tu ambalo niliomba kulipa kwa awamu ingwa nilikua siwezi.

Baada ya kuachana na mke wangu yeye hakuka akuomboleza, alijinyanyua na kutafuta fremu jirani tu na mimi, alichukua wateja wangu wote, hakua na mtaji mkubwa lakini kwakua alikua anafahamiana na watu na walikua wanajua bado ana biashara kubwa alipata mzigo kwa mali kauli na hatimaye kufungua duka lake kubwa. Wakati mambo yangu ni mazuri nilikua sipiti dukani kwake, nilikua sitaki hata kumsikia hata mtoto sikumuulizia, lakini sasa kila mara napita dukani kwake kumuangalia na kuona namna anavyoendelea.

Naumia sana kumuona jinsi anavyoendelea na maisha yake bila mimi, nilishampa talaka hivyo si mke wangu tena lakini najutia kwani ingawa hakusoma ana akili sana ya biashara. Mimi nimeshaharibu kila kitu, kila siku ni ugomvi mimi na mke wangu, ndugu zangu nao ni kero kila siku, masimango, matusi na kila kitu ni changu, sujii hata nifanye nini, natamani kumuacha mke wangu wa sasa nitrudiane na mke wangu wa zamani lakini ndiyo hivyo haiwezekani nimechanganyikiwa sijui hata nifanye nini na haya maisha!

Copy & paste
 
Hahahaa kwakweli wew umevurugwa km siyo kurogwa. Yani unaacha wanawake unavyoweza tu, akikushinda huyu unataka kurudi kwa huyu. Ndio ujue akili ya darasani sijui usomi siyo maisha. Akili ya darasani mara nyingi inaandaliwa ije iajiriwe tu, wachache sana wanakuwaga na akili za maisha halisi. Pole! Ure a big loser, huna mbele wala nyuma. Nenda kaombe huyo mtalaka wako akuajiri hata hapo dukani kwake upukute vumbi bidhaa jioni akulipe kitu kidgo, labda atakuonea huruma punguani wew
 
Mimi nashauri amuombe Radhi Mke wake wake za zamani na Aache tamaa maana alitamani Mali alokuwa NATO Mke wake
Pili familia yake ndiyo inayomhalibia inatakiwa awe mbali nayo naaisaidie pale inapowezekana watu wa mhimu kusaidiwa hapo ni wazazi tu hawo wengine wadogo zake watafute za kwao sio kusubili kutafutiwa wakishindwa wakaolewe
 
Back
Top Bottom