Nataka kumiliki kiwanja ila kipato changu ni cha kwa siku...

Mdigokhan

JF-Expert Member
May 2, 2022
843
1,923
Khabari zenu ndugu zangu.

Naomba mnipe mawazo katika Hili.

Mimi ni kijana miaka 28 hivi, kipato changu sh 30k kwa siku but nikifanya matumizi yangu katika familia Yaweza baki 10 au 15 inategemea na siku.

Nataka kununua kiwanja nina mawazo na kiwanja huu ni mwaka sasa kinanitia mawazo. Nawaza kuweka hela mpaka ifike million 2 au 3 Dah Nashindwa,sina mshahara ni kipato cha siku tu.

Je, Mmewezaje wezaje kumiliki viwanja na kujenga?

Naombeni mbinu,nawaza sana kiwanja.

Niliwahi jaribu kuweka mpk laki 9 ila ikapatapata majanga weeeee sijaiona hata ilivoisha isha.

Kwanza ni kiwanja mawazo ya kujenga ni baada ya kiwanja.

Nipeni mawazo, nifungueni akili labda nimelala msinikejeri..
 
Mkuu hapa cha msingi ni mipango yako na kuweka savings mara kwa mara, Nakuhakikishia kwa hicho kipato chako ndani ya miezi sita au mwaka utakuwa umeshapata hela ya kununulia kiwanja!

Amua kujibana inawezekana vizuri tu, kuna watu wengi wamenunua viwanja na wana vipato vidogo kuliko hat hicho chako, Kila la kheri!
 
Kwanza ushukuru Mungu una kipato cha kuuweza kubaki na elfu 10 mpaka 15 baada ya matumizi yako..

Fanya hivi daily weka elfu 15,elfu 10 ya kiwanja, buku 5 kuna dharura Inaweza kutokea, kkwa mwezi hukosi 450000(laki 3 kiwanja, 150k ni kwa ajili ya hizo emergency).

Jibanebane haswa upate hiyo 15 daily, sababu ukiweka elfu 10 itatokea emergency utadonyoa humo humo ya kiwanja, sababu ni kidogo kidogo ukidokoa dokoa mwaka utaisha bila kufikia lengo.

Ndani ya miezi 10 tu hutokosa milioni 3 mpaka 4.5 kutegemea na ulivyoweza kujizuia kutumia ile elfu 5 5 ya dharura, ama kama hakuna dharura yoyote kubwa iliyokutokea.

Kila la kheri mzee.
 
Mkuu hapa cha msingi ni mipango yako na kuweka savings mara kwa mara, Nakuhakikishia kwa hicho kipato chako ndani ya miezi sita au mwaka utakuwa umeshapata hela ya kununulia kiwanja...
Asante sana ndugu...
 
Hongera mpendwa kila hatua dua pesa inayobaki cheza mchezo ukipokea tu unaenda kununua kiwanja tena huko chanika vipo viwanja vya million 2 unapata
 
mungu atakusaidia utapata kiwanja kikubwa na kizuri haita fika 2024 trust me
Mpe mbinu ndo umwambie kwenye hizo mbinu mungu atakusaidia.. sa unamwambia tu atapata kiwanja kikubwaa mungu atamsaidia alafu hujaishia hapo na ukamwambia trust me,

Unamchanganya pia aaenze kumtrust mungu au wewe uliemwambia
 
Una miaka 28...

Unaishi Gongolamboto...

Kipato chako 30k/siku...

Na bado unapata tabu ni vipi utamiliki kiwanja NJIA YA CHANIKA.?!!!

Kuna tatizo mahali!
 
Kama upo Dar nifuate bobo nikueleweshe kitu mana mimi kipato changu ni 18k lakini mwezi uliopita nimenunua tayari sasa kama upo tayari followme
 
Khabari zenu ndugu zangu.

Naomba mnipe mawazo katika Hili.

Mimi ni kijana miaka 28 hivi, kipato changu sh 30k kwa siku but nikifanya matumizi yangu katika familia Yaweza baki 10 au 15 inategemea na siku.

Nataka kununua kiwanja nina mawazo na kiwanja huu ni mwaka sasa kinanitia mawazo

Nawaza kuweka hela mpaka ifike million 2 au 3 Dah Nashindwa,sina mshahara ni kipato cha siku tu.

Je, Mmewezaje wezaje kumiliki viwanja na kujenga?

Naombeni mbinu,nawaza sana kiwanja.

Niliwahi jaribu kuweka mpk laki 9 ila ikapatapata majanga weeeee sijaiona hata ilivoisha isha.

Kwanza ni kiwanja mawazo ya kujenga ni baada ya kiwanja.

Nipeni mawazo, nifungueni akili labda nimelala msinikejeri..
Kuna watu /kampuni wanauza viwanja na sio lazima kulipa yote kwa mara mmoja
 
Mipango tuu! kama utaweza kujima kidogo tuu kwa siku tumia elfu10 na jiwekee akiba ya 20k ndani ya muda mfupi tuu utakuwa na Akiba ya kukuwezesha kununua viwanja………...
 
Back
Top Bottom