Nataka nijenge Five ghorofa sijajua itanigharimu Milioni ngapi za Kitanzania!
Itakugharimu tsh milioni 50,babu yangu aliwahi kujenga ghorofa 6 hapa moshi na alitumia sii zaid ya 50m
Umemjibu vizuri Architect. Hata kwa kutumia ile tunayoiita PRO RATA RATES haiwezekwni kwani hajasema hata PLAN DIMENSION za jengo lake kwa kila FLOOR!Uko dunia gani unauliza maswali hewa? mfano nikikuuliza kufunga duka ni shilingi ngapi utaweza kujibu? Tafuta wataalamu kuanzia Architect, Structural Engineer,Building economist na Service Engineer kama kuna special features ila kushauriwa hewani bila kuwa na mchoro ama relevant details ni kutwanga maji kwenye kinu!
Kwa sababu umeuliza kikawaida nami ntakujibu kikawaida.....kila gorofa moja kujenga ni tsh 100milioni so kwa gorofa tano ni milion 500........upo!?
Mkuu samahani wewe ni fundi?
umewahi kujenga ghorofa?
unawajua waliowahi kujenga kwa bei hizo?
au itakua kama ya baba yake na 20%Itakugharimu tsh milioni 50,babu yangu aliwahi kujenga ghorofa 6 hapa moshi na alitumia sii zaid ya 50m
Mkuu @Agustini kwa kuanzia zingatia malelzo ya mkuu Horseshoe Arch post #6 na #9 . Ukikwama nitafute mimi ni structural engineer.
Mimi ni fundi ndio.....but refer to the question asked......check na maelezo yangu mkuu . . . .utaelewa tu kama una upeo mpana
Hawa Clients wetu ni kwenda nao mdogo mdogo...wapewe somo kwanza waelewe then ndipo wafanyiwe kazi zao...kuna utitiri wa wataalamu mtaani mathalani UR Planner, Land Surveyors,Architects,Building economists, Civil & Structural Engineers,Electrical/mechanical/Service Engineers, lakini mwisho wa siku unakuta mtu anaskip wote hawa labda kwa kudhani consultation ni aghali lakini guess what? Ni pale nyundo ya relevant body say (AQRB,CRB,ERB na NEMC kwa upande wa mazingira) inapomshukia...mimi wakija kwangu kipindi wamebanwa ni kumlipisha mara tano kwa kuwa hana jinsi!