Nataka kujenga ghorofa 5, itanigharimu Milioni ngapi?

Kwa sababu umeuliza kikawaida nami ntakujibu kikawaida.....kila gorofa moja kujenga ni tsh 100milioni so kwa gorofa tano ni milion 500........upo!?
 
Uko dunia gani unauliza maswali hewa? mfano nikikuuliza kufunga duka ni shilingi ngapi utaweza kujibu? Tafuta wataalamu kuanzia Architect, Structural Engineer,Building economist na Service Engineer kama kuna special features ila kushauriwa hewani bila kuwa na mchoro ama relevant details ni kutwanga maji kwenye kinu!
 
Umemjibu vizuri Architect. Hata kwa kutumia ile tunayoiita PRO RATA RATES haiwezekwni kwani hajasema hata PLAN DIMENSION za jengo lake kwa kila FLOOR!
 
Kuweka kumbu kumbu sawa hapa kwa wengine fuateni jedwali lifuatavyo as reference:-

  1. Industrial building ina range 450,000 - 650,000 per sq. m.
  2. Agricultural building/Structure 500,000 - 700,000 per sq. m
  3. Commercial building 700,000 -1,100,000 per sq. m
  4. Residential building ranges from 750,000 -1,000,000 per sq. m
  5. Educational facilities ranges from 500,000 -750,000 per sq. m
  6. Medical & social services building ranges from 850,000 - 1,300,000
  7. Recreational building ranges from 450,000 - 650,000
 
Kitu cha kwanza mtoa mada lazima useme matumizi ya ghorofa, je ni commercial, commercial ya maduka,commercial ya hotel au Residential hapo unamsaidia ata architecture kujua anaanzaje kudesign ghorofa yako ukipata I deal ya ghorafa yako unaweza kwenda kwa quantity surveyor kukupatia gharama za awali kabla ya ujapata detail drawings kutoka kwa architect na structure engineer kwa ajili ya kuandaa gharama halisi ya ghorofa yako Agustini
 
Last edited by a moderator:
Kwanza ujue ukubwa wa jengo kwa sq meters, facilities utakazoweka - lift, etc- na location yenyewe. Ni jambo la kitaalam sio kama chumba na sebule
 
Mkuu @Agustini kwa kuanzia zingatia malelzo ya mkuu Horseshoe Arch post #6 na #9 . Ukikwama nitafute mimi ni structural engineer.

Hawa Clients wetu ni kwenda nao mdogo mdogo...wapewe somo kwanza waelewe then ndipo wafanyiwe kazi zao...kuna utitiri wa wataalamu mtaani mathalani UR Planner, Land Surveyors,Architects,Building economists, Civil & Structural Engineers,Electrical/mechanical/Service Engineers, lakini mwisho wa siku unakuta mtu anaskip wote hawa labda kwa kudhani consultation ni aghali lakini guess what? Ni pale nyundo ya relevant body say (AQRB,CRB,ERB na NEMC kwa upande wa mazingira) inapomshukia...mimi wakija kwangu kipindi wamebanwa ni kumlipisha mara tano kwa kuwa hana jinsi!
 
Attachments

  • 1.JPG
    1.JPG
    32.3 KB · Views: 820
  • 2.JPG
    2.JPG
    54.6 KB · Views: 800
  • 3.JPG
    3.JPG
    45.9 KB · Views: 764
Mimi ni fundi ndio.....but refer to the question asked......check na maelezo yangu mkuu . . . .utaelewa tu kama una upeo mpana

Sina uelewa mpana sana
lakini nauliza ili kujua tu
je ukisema gharama za ujenzi ni milioni 100 kwa ghorofa moja unamaanisha pesa ya mafundi na gharama zote
au hapo unazungumzia gharama bila pesa ya kuwalipa mafundi?
je wewe una kampuni inajihusisha na ujenzi?
mtu akisema ana milioni 500 anataka kujenga ghorofa 5 utamsaidia vipi?
 
Hawa Clients wetu ni kwenda nao mdogo mdogo...wapewe somo kwanza waelewe then ndipo wafanyiwe kazi zao...kuna utitiri wa wataalamu mtaani mathalani UR Planner, Land Surveyors,Architects,Building economists, Civil & Structural Engineers,Electrical/mechanical/Service Engineers, lakini mwisho wa siku unakuta mtu anaskip wote hawa labda kwa kudhani consultation ni aghali lakini guess what? Ni pale nyundo ya relevant body say (AQRB,CRB,ERB na NEMC kwa upande wa mazingira) inapomshukia...mimi wakija kwangu kipindi wamebanwa ni kumlipisha mara tano kwa kuwa hana jinsi!

Mkuu hebu tusaidie kimoja
mimi nikiajiri kampuni ya ujenzi si wanapaswa wao kutafuta hao wataalam wote?
au mimi tena mteja nitafute wataalamu woote hao na bado nitafute kampuni ya ujenzi?

je wewe una kampuni ya ujenzi?
au unafanyaje shughuli zako
suppose nimekuja kwako nataka kujenga ghorofa 5 nina milioni 500 tunaanzia wapi hadi wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom