Natafuta mashamba na bei zake huko morogoro au pwani

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
habari wakuu,naomba mnisaidie bei za mashamba huko pwani na moro zikoje kwa wale wanaofahamu.natanguliza shukrani zangu.
 
pwani - wilaya ya bagamoyo kuelekea msata - inategemea - kuna maeneo mengine ni 400,000/- kwa acre moja; pengine 250,000/= inategemea muuzaji.

All the best
 
mashamba ya 20,000 utaambiwa mbele ya dumira ambako hata maji huwezi kupeleka, ila kama mnataka kuwa na mapori tu ambayo badae vitakuwa viwanja, hayo yapo!. ulizia vizuri mie niliwahi ambiwa kuna ekari arobaini zinauzwa 3.5M nikafurahi lakini nilipoambiwa maeneo na kuhadisiwa mazingita hata hamu iliniishia!. uliza vizuri mie siyo mzoefu wa morogoro!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
pwani - wilaya ya bagamoyo kuelekea msata - inategemea - kuna maeneo mengine ni 400,000/- kwa acre moja; pengine 250,000/= inategemea muuzaji.

All the best

nashukuru mkuu kwa taarifa hii,bila shaka itanisaidia sana katika kufanya maamuzi.
 
Mashamba basi wanaJF, ni polini tena huko morogoro kwa watani zangu wanaosema "sima taa" badala ya "zima taa" utapelekwa polini, ila vizuri kujionea na kufanya maamuzi sahihi. Huko pwani hata mimi nayataka.
 
Sasa mkuu unawatania wenzako wanasema 'sima taa' mbona wewe unakosea unasema polini badala ya porini, toa kwanza kibanzi kwenye jicho lako mkuu.....
 
kaka umeuliza mashamba moro na pwani. Hujatuambia ni kwa ajili ya kilimo gani kwa moro kuna kilimo cha mpunga, mahindi na mazao mengine, au unataka mapori kwa ajili ya kupanda miti ya mbao. naona umekuwa interested na bei ya 20,000.pls fafanua unataka ardhi kwa ajili ya nini mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom