Natafuta kazi nimesoma computer science pia nina uzoefu wa ualimu

Hudhaypher

New Member
Feb 12, 2023
1
0
Habari ndugu zangu!!
Natafuta kazi ili nijikwamue kiuchumi maana mtaani ni kugumu sana.

Elimu:
Degree ya Computer Science

UWEZO
1. Programing (C++, Python, Visual basic)
2. Computer Mantainance and troubleshooting
3. Photocopy Mantainance and troubleshooting
4. Printer Mantainance and troubleshooting
5. Computer graphics
6. Data analysis ( Data science)
7. Artificial intelligence nk

UALIMU ( Uzoefu)
1. Kufundisha physics ( form I - VI)
2. Kufundisha Mathematics (form I - VI)
3. Kufundisha ICT
4. Kufundisha science and technology (primary)

Maeneo niliyofanya kazi
1. Shule (primary na secondary)
2. Kampuni
3. Vyuo vya ufundi na ualimu


Uzoefu
1. Miaka 5+ ( kufundisha)

Nipo tayar kufanya kazi mkoa wowote
Mshahara ni makubaliano

Tuwasiliane
0754824790

Natanguliza shukran za dhati

Ahsants
 
Nenda jeshi... TISS au Migration watakuchukua ukawe mzalendo rasmi.

Mnahitajika sana watu wa fani yako. Sisi bado tuko nyuma ingawa si nyuma sana ila ajenda yetu mpaka kufikia mwaka fulani tuwe vizuri kweli! Kweli! Kwenye maswala ya kiusalama na ulinzi hasa kwenye upande wa maswala ya tehama.



Kama una uzoefu wa kufundisha au kipaji nenda shule za Upanga wanataka sana vijana wa kujitolea kufundisha hasa fani za Sayansi... nazungumzia shule kama "Shaaban Robert, Aga-Khan, Al-muntazir...n.k"

Jaribu bahati yako kuomba kazi au intern shule za kimataifa zilizopo nchini pia nazungumzia shule kama IST, Braeburn, HOPAC, LAUREATE, AGA-KHAN yenyewe n.k"
 
Kwa level yako ya elimu na kitu ulichokisomea ulipaswa ujiajiri au uwe na project zako zinazohusu jambo ulilosomea.. Hii itakuwa rahisi sana kumshawishi muajiri, au kupata kazi za moja kwa moja bila kuajiriwa. Mimi bado natafuta certificate ya computer science ila nina projects tayari za web development(Full stack) na sasa hivi nipo mbioni kuikamilisha project yangu ya Mobile App development. Nina uhakika nikimaliza project hizi itakuwa rahisi kwangu kumshawishi mtu anipe kazi bila kuniajiri. Kwa sasa kazi inayoniingizia kipato ni videography na animation.

Nilichogundua Freelancing inapesa kuliko kuajiriwa, ila tu uwe na kazi nzuri na uwe competitive. Kama uko tayari naweza kupa muongozo
 
Mi nadhani ulipaswa kuomba kisaidiwa kuliko kutaja na uzoefu wa kufundishia maana ni wazi wewe siyo Mwalimu kwa taaluma na ni mgumu kupata kazi kwenye shule inayoeleweka itakayokulipa vizuri.

Ushauri wangu: Ebu jikite ktk taaluma uliyisomea ya compyuta na utafika mbali. Kwenye Ualimu huko Hilo wazi ondoa na serikali haitakuajili km Mwalimu wakati siyo taaluma Yako unless ukaji updrade kwa kozi ya Ualimu.

Na Nikuambie tu, km unaweza nenda kasome hata Diploma ya Ualimu na omba kuajiliwa km Mwalimu. Baadae kapeleke vyeti vyako ya degree ya komputa ktk Halmashauri utakayoajilwa. Nakwambia utakuja kunishukuru.
 
Back
Top Bottom