Nashindwa kupanga bajeti ya mwezi, nifanye nini ili niweze?

tatizo kubwa ni watu tunaoishi nao akiwepo mke. Hawataki kuorodhesha matumizi ya kila siku. Ukiuliza fedha imetumikaje unataka mchanganuo ndo unaanzisha balaa lingine. Maana utajikuta fedha haikutosha na kukopa amekopa.

Ukijaribu kuweka records hata za mwezi 1 tu utakuja kugundua unadanganywa kwenye matuzi maana utashtuka mitungi 3 ya gesi, kila 45 za mchele, unga kilo 30, tambi paketi 25, sukari kilo 15. sasa unajiuliza unalisha shule au ni familia ya watu wasiozidi watu8. Hii inatia hasira sana. Bahati nzuri nyama za ina zote nanunua mwenyewe kwa jumla.

Nidhamu, uadilifu na kumcha Mungu pia vinasaidia sana. Bila uaminifu kupangabajeti ya nyumbani ni shida sana
 
Pole sana mkuu. Hakuna kitu kinacho tesa kama madeni. Ukiamua unaweza. Ila jaribu kwanza kuguta madeni yote. Ukiweza yote kwa pamoja na ukubali kuteseka angalau kwa mwezi mmoja tuu au miwili. Baada ya hapo utakuwa huru na tayari utakuwa umejipa somo la ku bajeti.
 
Ndugu zangu mie ni ni mfanyakazi kama siyo kibarua, nalipwa 500,000 kwa mwezi lakini kila nikijitahidi kupanga bajeti nashindwa. Najikuta nikipewa mshahara tarehe 24 kufika tarehe 10 ya mwezi unaofuata ni shughuri nzito. Mie sinywi pombe, sivuti sigara, kwa sasa nimeacha na soda lakini bado hali si shwari.

Nina mpango wa kuacha chai ingawa sijui kama itasaidia, najikuta siku zinapopita madeni yanaongezeka mpaka imefikia kiasi cha kukopa kwa watu wapya ili niwalipe wale walionikopesha mwanzo.

Naomba msaada wa mawazo.
Yawezekana hutoi zaka na sadaka hiyo lazima itokee
 
Kinachotukumba watanzania wengi ni kuwa, tunataka tuonekane tukiwa level flani ya maisha kama akina flani wanavyoishi au zaidi ya hivyo. Mfano, asubuhi unafika ofisini, muda wa chai mnaenda cafe, wanaume wenzako wanaagiza supu, wanawalipia ladies kuonyesha wanazo. Wewe unaangalia ukiagiza chai rangi utaonekana unajishusha. Na wewe unaagiza supu. Hilo ni kosa kubwa sana. Vijana wengi wanaumizwa na maisha ya kuigiza. Mimi nilikuwa affected na hilo tatizo muda mrefu, nina bajet ya kunywa chai rangi alafu nikifika nakunywa supu.

Pia, epuka manunuzi ya kukurupushwa. Kuna watu wanafanya biashara za kutembeza maofisini. Hukuwa na bajet ya kununua nguo au bidhaa yoyote ile, anapita mtu ofcn, anakushawishi. Unasema huna hela, anakuambia chukua utalipa mwisho wa mwezi. Hapo andika maumivu.

Pia, hakikisha unatafuta kipato cha ziada. Siku zote mshahara hautoshi. Kwa mfano mimi nina mshahara wa 1.5m lakini ilifika hatua, ikifika tarehe 10 akaunt imekauka. U know what? Unaweza ukadhani 1.5m ni hela kubwa. Ila ukipigia mahesabu, lipa ada za watoto wako, ada za watoto wa relatives, mafuta ya gari, service, rent, nguo, chakula, bills, etc. Hapo bado kadi za harusi, michango ya misiba. Nikaamua kuanzisha shughuli zingine kama ufugaji wa kuku na shamba work. I tell you sasa hivi walau nafika mwisho wa mwezi na pia nabakiza chenji kidogo.

Bongo unaweza kuwa Milionea lakini bado ni masikini. Pesa yetu ipo chini sana. The word Million is thrown very loosely. Nchi nyingine ukisikia mtu anataja milioni, amenunua gari la milioni kadhaa, amenunua nyumba kwa milioni kadhaa anakuwa ni mtu wa upper level Fulani tofauti na asilimia kubwa ya watu wengi sio kwetu. Yaani ulichosema ni kweli kabisa, mshahara wa mfanyakazi Bongo unakuwa haukidhi hata asilimia 45 ya mahitaji yake kwa mwezi. Kitu kingine wengi hawana financial discipline kama ulivyosema. Una mke na watoto 3 au 4 unataka kuspend pesa kama vile bado single. Hivi ni kwa nini hatuna utamaduni wa kufungasha breakfast au lunch afu unalia job muda wa break? Watu wengi duniani wanafanya hivi na si kwa vile hawalipwi vizuri kuliko Wabongo. Hakuna aibu kufungasha mlo toka home kama mshahara hautoshelezi mahitaji.
 
Ndugu zangu mie ni ni mfanyakazi kama siyo kibarua, nalipwa 500,000 kwa mwezi lakini kila nikijitahidi kupanga bajeti nashindwa. Najikuta nikipewa mshahara tarehe 24 kufika tarehe 10 ya mwezi unaofuata ni shughuri nzito. Mie sinywi pombe, sivuti sigara, kwa sasa nimeacha na soda lakini bado hali si shwari.

Nina mpango wa kuacha chai ingawa sijui kama itasaidia, najikuta siku zinapopita madeni yanaongezeka mpaka imefikia kiasi cha kukopa kwa watu wapya ili niwalipe wale walionikopesha mwanzo.

Naomba msaada wa mawazo.
achana na vigoli na vimidoli! kwani hivyo ndivyo vinatafuna mchumi wako!
 
Ndugu zangu mie ni ni mfanyakazi kama siyo kibarua, nalipwa 500,000 kwa mwezi lakini kila nikijitahidi kupanga bajeti nashindwa. Najikuta nikipewa mshahara tarehe 24 kufika tarehe 10 ya mwezi unaofuata ni shughuri nzito. Mie sinywi pombe, sivuti sigara, kwa sasa nimeacha na soda lakini bado hali si shwari.

Nina mpango wa kuacha chai ingawa sijui kama itasaidia, najikuta siku zinapopita madeni yanaongezeka mpaka imefikia kiasi cha kukopa kwa watu wapya ili niwalipe wale walionikopesha mwanzo.

Naomba msaada wa mawazo.
Tatizo kubwa hapa sio mshahara mdogo wala matumizi makubwa; tatizo ni kutokujua maana halisi ya budget. Mashuleni tunafundishwa kwa ajili ya kujibu mitihani lakini tukija kwenye vitendo ndo inakuwa ngumu sana.
Budget ni nini?
Huu ni mpango wa matumizi na mapato kwa kipindi maalumu.

Hapa nimeanza na matumzi then mapato ni kwa sababu maalum; hutaweza kupata ni mpaka utumie.
Anza na jambo muhimu (Akiba); baadae horodhesha matumizi muhimu (Chakula, Malazi, Mavazi). Baada ya hapo horodhesha mahitaji muhimu (Nauli, umeme, maji n.k); baada ya hapo weka yasiyo ya lazima (zawadi, mitoko n.k)

Ukishafanya mambo hayo kwa maandishi - naamini utaishi bila wasi na ikitokea ukawa under budget utajitahidi kufanya marekebisho ( utapunguza matumizi au utaongeza mapato)

Utafanya hivyo vipi! .......
1. Fanya overtimes
2. Anzisha biashara ndogo ..
3. Omba msaada kwa ndugu / marafiki
4. Ji- attarch kwa mtu / olewa
 
Bongo unaweza kuwa Milionea lakini bado ni masikini. Pesa yetu ipo chini sana. The word Million is thrown very loosely. Nchi nyingine ukisikia mtu anataja milioni, amenunua gari la milioni kadhaa, amenunua nyumba kwa milioni kadhaa anakuwa ni mtu wa upper level Fulani tofauti na asilimia kubwa ya watu wengi sio kwetu. Yaani ulichosema ni kweli kabisa, mshahara wa mfanyakazi Bongo unakuwa haukidhi hata asilimia 45 ya mahitaji yake kwa mwezi. Kitu kingine wengi hawana financial discipline kama ulivyosema. Una mke na watoto 3 au 4 unataka kuspend pesa kama vile bado single. Hivi ni kwa nini hatuna utamaduni wa kufungasha breakfast au lunch afu unalia job muda wa break? Watu wengi duniani wanafanya hivi na si kwa vile hawalipwi vizuri kuliko Wabongo. Hakuna aibu kufungasha mlo toka home kama mshahara hautoshelezi mahitaji.

Hapo kwenye bold mkuu umeongea kitu kikubwa sana! Eti mtu ananunua maji ya kunywa wakati ameyaacha nyumbani yamechemshwa!

Mi asubuhi huwa nabeba chupa yangu ya maji, lakini wasiojua wanahisi nina hangover naenda kupoza!
 
Nimependa sana michango ya wadau hapo juu. ila kwangu mimi naona tofauti kwani kupunguza matumizi ili hela itoshe sio kutatua tatizo kinachotakiwa hapo ni wewe kuongeza chanzo kingine cha mapato ili upate hela nyingi zaidi ya unavyotumia kwa mwezi. Ingawa ni vizuri kuanza na ushauri uliotolewa hapo juu ili kufikia malengo.

“It’s more important to grow your income than cut your expenses. It’s more important to grow your spirit that cut your dreams.
 
Umenifurahisha moja;unakopa kwa mtu mpya kumlipa wa zamani!!na ndio system nzuri;dawa ya deni ni kulipa na usiogope madeni!!lakini kubwa linalokukabili mie lilishanikuta miaka miwili imepita!!Kwanza heshimu 500;000 ukiamini ni kama 250;000 then 250;000 ipangie bajeti kwa udogo wake;ukihakikisha chakula kipo home;maji;nauli na umeme plus Kodi ya nyumba!then inayobaki 250;000 amini ndio saving yako hapo utaitumia where necessary!!lakini ya yote ukishajiaccomodate na 250;000 basi maisha yatakuwa kawaida na sio ya stress!!pambana uongeze kipato maana 500;000 ni ndogo pia so kupambana huko kuwe kusaka ajira ingine yenye kipato zaidi ya hicho
 
Back
Top Bottom