Nashauri vyeo hivi vifutwe!

Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.

Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.

Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.

Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?

Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.

Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.
pamoja na wakuu wa wilaya& mikoa wanafanya nini pale ofisin!kwan watendaji hawawez kufanya kaz bila hao!upande mwingine idadi ya wizara ipunguzwe zibaki walau saba halafu 2bakie na idara tu
 
Nadhani imefika wakati tupunguze vyeo vya kisiasa na kuamini watendaji (civil service) kufanya kazi zao. Nchi kama Ufaransa baada ya vita kuu ya pili ya dunia hali ya kisiasa ilikua tete sana kwa sababu hakuna serikali iliyo kuwa inadumu lakini nchi iliendelea kwa sababu covil service yake ilikua na nguvu. Inabidi tuchukue maamuzi magumu na kuwa disappoint baadhi ya watu kwa kufuta vyeo vyao visivyo vya lazima wala tija kwa taifa.
 
Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.

Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.

Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.

Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?

Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.

Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.

Hapo kwenye red nimepapenda, kwa mawazo yangu ni kuwa hapa kwetu tuna "mgogoro" wa kisiasa ambao ni kuwa tuna wapinzani wanaolazimika kupewa hayo madaraka (Wazanzibar) ili kuwe na balance ya muungano
 
nakubaliana nawe kabisa katika hili mkuu.
Na isiishie hapo, naona hata wabunge nao tuwatoe pia. kwani kuwepo kwake hakuan manufaa yeyote kwa jimbo iwapo tuna hawa wafuatao:
Mjumbe wa nyumba kumi, mwenyekiti wa serikali ya mtaa,mtendaji kata/katibu kata, kasatibu tarafa, diwani, mkurugenzi wa H/wilaya na mwisho mkuu wa wilaya.
hawa wote kazi yao ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika vijiji waliopo na wilaya kwa ujumla. sasa basi kazi ya mbunge hapa inaangukia wapi??
najua mtasema Bunge linatunga sheria! ili hali waliomo humo hata hizo zilizopo hawazijui!!!!
kazi hiyo waachiwe watu wa sheria(MAHAKAMA)
kwa leo ni hayo......
 
Na mimi napendekeza cheo cha waziri wa mambo ya nnje kifutwe ili kupisha raisi ndiye anafaa awe na cheo hicho! namaanisha kua tuwe na raisi na hapohapo awe ni waziri wa mambo ya nnje.
 
Hata cheo cha mkuu wa wilaya pia , hakina tija coz ded ndio afanyae shughuli zoooooote wilayani!
 
naona mnapotea kabisa kama ingetokea mmeona mapungufu ya veo hivi basi mngeshauri ni namna gani kuviboresha na si kuviondoa, cheo cha makamu wa rais ni cheo ambacho hakiwezi kuepukika kwani kinaondoa migongano na pia ni namna a kufanya pengo linaloachwa na rais anaposafiri kupungua na pia kuweza kuongeza ushirikiano wa pande mbili ani bara na visiwani

nadhani kitu cha muhimu ni kuboresha na kutafuta watu wene uwezo katika nafasi hii na si kukimbilia kuvifuta, watu wengi sana wanadhani kufuta kitu ni njia ya kukimbia tatizo badala ya kukaa chini na kuboresha mapungufu yaliyojitokeza
 
Mi naonelea pia hata mawaziri wasitokane na wabunge. Nafasi ya uwaziri iwe ya kuajiriwa tena kwa mkataba wa miaka 5 ili itakapotokea unakuwa na waziri kama Ngeleja, Wasira a.k.a wakulala, Lukuvi inakuwa rahisi kuwawajibisha. Na pia mawaziri wawe wanafanyiwa performace evaluation kila mwaka akishindwa kufikia kiwango mkataba unasitishwa watu wangefanya kazi kuliko ilivyo sasa mawaziri wanaingiza siasa na ushabiki wa vyama katika technical issues.
 
Nakubaliana na hoja, ila tunaweza kufuta cheo cha waziri mkuu na tukawa na ufanisi mkubwa kama South Africa&USA ikiwa mawazr watakuwa wenye ujuzi ktk wzara husika na si lazima awe mbunge pia kuwe na perfomance appraisal na contract ili kuwabana. au tunaweza kufuta cheo cha makamu wa raisi tukawa na raisi kama head of state na waziri mkuu head of government hapa waziri mkuu atachaguliwa na wabunge na mara nyingi atatoka kwenye chama chenye wabunge weng kama Germany& Israel. Pia tufanye restructuring kwa kuwaondoa wakuu mikoa/wilaya na kuwa na province ambazo kutakuwa na magavana watakaochaguliwa na wananchi. Mwisho kupunguza idadi ya majimbo ili kuwa na uwakilishi mzuri kwa kuwa na mbunge mmoja kwa kila halmashauri kwa mfano halmashauri ya manisipaa/wilaya/jiji ili kuleta ufanisi.
 
Hakika Uwaziri mkuu wa Watanzania ni vyema ufutwe,manake imekuwa kama kichocheo,kuyumbisha shughuri za maendeleo,manake kwa walio wengi waliopata kuwa mawaziri wakuu wa Tanzania ni mmoja tu ndiyea laiyefanikiwa kuwa Rais wa Tanzania na mwingine japo angeweza kuwa Rais lakini hakungangania na angekuwa kinganganizi angeweza lakini kwa kujua urais ni nini akamludishia Rais mhusika.

Waliobaki wali wengi wao wamekuwa ving'ang'anizi wa kutaka wawe Marais bila kujali kanuni na mpangilio mzima.Wanapoingia kwenye cheo hicho hawaangaiki na kuhudumia Wananchi kama ilivyokuwa kwa JK na RK.Wanachoshughurika nacho ni kuhangaika huku na kule ili wajenge mfumo [System] ya kuwasupport kuchukua Urais.

Kidogo JSW sikupata kusikia kuingia kwenye vuguvugu la kuwania Urais lakini waliosaria wengi wao walichaluka kama mbogo,kukitaka kiti cha enzi cha Watanzania.Waliokuwa na busara walikaa pembeni baada ya kukikosa wakatumia busara zao kujiengua,wasio na busara wamekuwa na kero mpaka inachefua.

Hakika Kama Mzee huyu JM akuhupata Urais wa Tanzania,basi hakika haitatokea Waziri mkuu mwingine yoyote kinganganizi awe na pesa asiwe na pesa kuweza kuwa Rais wa Nchi hii,bali ataingia kukubalika tu kama Wananchi watataka au wanampenda kuona anakuwa Rais wao.

Kuna jadi na kama utamaduni wa asilia [nature] na kama Mama Tanzania imekuwa kitu ambacho waliopata kuwa Mawaziri wakuu wa Tanzania, ambao wameshika nafsi hiyo ni JK tu ndiye aliyepata kuwa Rais,basi kwa utamaduni wa Mzee RK kukabidhi tena madaraka kwa aliyekuja kuwa Rais aliasisi jadi ya kufunga ufunguo wa mtu aliyepata kuwa Waziri mkuu kuwa Rais.

Japo wakiwa kwenye cheo hicho wanapumbazika na kamwe hawaioni jadi hiyo asilia [nature] wala hawajifunzi kwa kwa kuona wenzao walio watangulia.Na kwa kuwa hawana macho wala masikio basi wanabaki kupigana na vivuli vyao kila siku ya Mungu ili wawe Marais.

Kuna mmoja yeye inasemekana alipendwa na Mwalimu sana kiasi kuwa alitamani kumuona kawa Rais wa Watanzania lakini Mwalimu akupata kutimiza ndoto yake hiyo na hivyo kudhibitishiwa na kanuni asilia ambayo walio wengi ukiizungumia awawezi kujua unazungumzia nini.

Hivyo kuendele kuwa na cheo hiki kinachoshabikia mbinu na mikakati ya kuangalia nafasi ya Urais na si kusimamia shughuri za maendeleo na Taifa kwa ujumla ni mzigo mkubwa kwa Taifa letu.Na pamoja na mbinu zote na michakato na matumizi ya rasimali ya umma yote na bado wasichukue Urais,inakuwa ni kuyumbisha Taifa na watu wake.

Na mchezo mwingine umezaliwa kwenye Wizara ya mambo Nchi za Nje, kuanza kuhalalishwa kuwa ni kituo cha kumuandaa Rais mtarajiwa.Upofu huu wa kinasaba ya kimfumo ni hatarishi sana kwa usalama wa Taifa.Tusifike sehemu Watanzania wajue Rais anaweza kutoka sehemu yoyote ile ndani ya Serikali au Nje ya Serikali ili tu awe na uwezo na mfumo [system] unajua ni mzalendo na atasimamia kujenga na kulinda Nchi kwa kadri ya maono yake na kukubalika kwake kwa jamii.
 
Back
Top Bottom