Nashauri motisha ya Rais itolewe kwa timu za taifa na siyo vilabu

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
13,405
19,069
Kutokana na vilabu kusheheni wachezaji wa kigeni, nashauri motisha ya rais itolewe kwa timu zetu za taifa zikiwemo ile ya mabinti iliyofanya vizuri sana kwenye mashindano ya soka la kimataifa na wanamichezo wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya olympiki ili wajitahidi kupata medali.

Motisha kwenye vilabu binafsi waachiwe wafadhili wa hizo timu.

Ni hayo tu kwa leo.​
 
Kutokana na vilabu kusheheni wachezaji wa kigeni, nashauri motisha ya rais itolewe kwa timu zetu za taifa zikiwemo ile ya mabinti iliyofanya vizuri sana kwenye mashindano ya soka la kimataifa na wanamichezo wanaoenda kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya olympiki ili wajitahidi kupata medali.

Motisha kwenye vilabu binafsi waachiwe wafadhili wa hizo timu.

Ni hayo tu kwa leo.​

Kwani akitoa motisha kwa klabu, hatakuwa na uwezo tena wa kutoa motisha huko kwenye timu za taifa?
Au kwa kuwa klabu zimesheheni wageni, huo ushindi unaopatikana unakuwa diverted to nchi wanakotokea hao wageni?
 
Kwani akitoa motisha kwa klabu, hatakuwa na uwezo tena wa kutoa motisha huko kwenye timu za taifa?
Au kwa kuwa klabu zimesheheni wageni, huo ushindi unaopatikana unakuwa diverted to nchi wanakotokea hao wageni?
Ukimsikiliza mtangazaji anapokuwa anaelezea wachezaji utasikia mara kenyan international, mara congolese international nk, yaani klabu ya kitanzania imejaa wakongoman
 
Tunawekeza kwenye kuandaa timu bora za taifa ili ziletee nchi heshima ikiwemo michezo kama riadha kama ilivyo kule kenya.
Miaka yote motisha imetolewa Kwa timu ya taifa ila imeshindwa kufanya lolote,
hivi umesahau juzi tu hapa waliahidiwa milioni 500 wakifuzu chan? Matokeo yake tukachabangwa na Uganda hapa uwanja wa taifa na umeme ukazimika uwanjani..

Acha utopolo wachukue izo ela maana ndio pekee wameonesha wanaweza kutoa kimasomaso
 
WIVU, UCHOYO NA UBINAFSI HUTOKA MOYONI

Reference;Biblia Takatifu

Nukuu; Je, Siwezi kufanya nipendavyo na Mali yangu, au unaona wivu kwa kuwa nimekua mkarimu?

Matayo 20=
Mfano Wa Wafanyakazi Katika Shamba La Mizabibu

20 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu mwenye shamba la mizabibu aliyeondoka alfajiri kwenda kutafuta vibarua wa kufanya kazi shambani kwake. 2 Wakapatana kuwa atawalipa msha hara wa kutwa, yaani dinari moja, akawapeleka shambani.

3 “Mnamo saa tatu akaondoka tena akawakuta watu wengine wamesimama sokoni bila kazi. 4 Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu na nitawalipa haki yenu.’ Kwa hiyo wakaenda. 5 Mnamo saa sita na pia saa tisa alion doka tena akafanya hivyo hivyo. 6 Mnamo saa kumi na moja akaon doka tena akawakuta watu wengine bado wanazurura. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’ 7 Wakamjibu, ‘Ni kwa kuwa hakuna aliyetuajiri.’ Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la miza bibu.’

8 “Ilipofika jioni, yule mwenye shamba akamwita msimamizi wa vibarua akamwambia, ‘Waite wafanyakazi uwalipe ujira wao, ukian zia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’ 9 Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akalipwa dinari moja. 10 Basi wale wal ioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipewa dinari moja. 11 Walipoipokea, wakaanza kumlalamikia yule mwenye shamba wakisema, 12 ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu. Ime kuwaje wewe ukawalipa sawa na sisi ambao tumefanya kazi ngumu na kuchomwa na jua mchana kutwa?’

13 “Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sija kudhulumu. Je, hatukupatana kwamba utafanya kazi kwa dinari moja? 14 Chukua haki yako uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu ali yeajiriwa mwisho sawa na wewe. 15 Je, siwezi kufanya nipendavyo na mali yangu? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’ 16 Hali kadhalika, wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”
 
Back
Top Bottom