Nashauri magari yote ya Serikali na Taasisi za Umma yapakwe rangi za nembo zao kupunguza ukiritimba

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Maelekezo ya ukamataji magari yasiyo kuwa na nembo wapewe trafiki ili waanze msako wa kukagua kadi za gari feki na dereva atakayekamatwa ahukumiwe kesi ya hujuma.

Hili litasaidia uwajibikaji ili wanainchi waone nani mharibifu wa Mali ya umma, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali

3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima

4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!

Updates
IMG-20220612-WA0002 (1).jpg
 
Kuna kipindi fulani kama sijasahau enzi za J,Nyerere ilikua siku za weekend kama Jumapili hivi ni marufuku gari za serikali kuonekana Barabarani,anayekumbuka zaidi hii issue atujuze zaidi.
 
Ukiondoa magari ya IKULU na yale ya Viongozi wa kitaifa;

Naishauri ofisi ya waziri mkuu ikiongozwa na Mh Majaliwa Kassimu kwa kushirikiana na Tamisemi chini ya Bashungwa!

Waelekeze magari yote ya serikali yapakwe rangi ya nembo ya taasisi husika kama ilivyo kwa taasisi chache kama (Polisi,Tanesco, NHC, NSSF n.k)

Na hili lisiishie tu kupaka magari ya SITE na kuacha mashangingi au magari mengine ya mameneja na wakurugenzi pasipo kuwa na rangi za nembo zao!

Ili wanainchi waone nani mharibifu, nani anakimbia mbio za hatari barabarani, nani kaenda kulewa muda wa kazi, nani yuko gesti mida ya kazi, nani kabebea mbuzi wake kwenye shangingi la serikali! N.k

Watu wa masijala wahakikishe kila chombo cha moto cha serikali kiwe na rangi za nembo husika ili kuongeza uwajibikaji na kupunguza ukilitimba.

Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali
3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima
4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)

Nasema hivi kwasababu nimeshuhudia mashangingi kadhaa ya serikali STL au DFPA lakini wakifika mtaani wanabandika namba binafsi mfano DZA!

Kwahiyo mtu kama huyu akiuza kipuli gereji yoyote hakuna atakaye mshitukia!
Kila gari la serikal huwa Linakuwa na namba ya usajili wa gari wa kawaida. Matumiz ya kiserikal ni mengi jombi.
 
Hili litasaidia mambo kama haya!
1. Madereva wa serikali siku hizi wamebuni mbinu ya kuwa na namba za usajili feki (fake plate number) ambazo hubandika siku za weekend na kutumia gari jambo linalochangia uchakavu wa haraka na kuighalimu serikali kufanya matengenezo

2. Madereva wanapokuwa na hayo magari yasiyo na nembo (waliyoweka feki namba binafsi) ni rahisi sana kuuza au kubadilisha vipuli orijino kwenye gereji bubu na kuitia hasara serikali
3. Matumizi ya mafuta yako juu kwasababu magari yasiyo na nembo yanashawishi mizunguko isiyokuwa ya lazima
4. Magari yasiyo na nembo hayaoneshi uwajibikaji kwa wananchi (hili lipo kisaikolojia zaidi)
Kuna ukweli mwingi kwenye hili jambo, kuna magari mengi ya serikali yanaonekana yakirandanranda barabarani usiku na weekend yakiwa na namba tofauti na zile zinazoonekana siku za kazi na moja ni kwa jirai yetu huku kitaa
 
Back
Top Bottom