Kaliro X
JF-Expert Member
- Apr 18, 2013
- 749
- 438
Naomba unijibu swali hili: kwa nini karibu nchi zote zilizoendelea kuna kozi elimu ya juu zinafundishwa kwa kiingereza? Majuzi chuo kikuu kikongwe kabisa mjini Milan Italia kimeamua kufundisha kozi zake zote kwa Kiingereza, unadhani ni kasumba?
Acha utumwa wa kifikra sio kila kinachofanywa na watu wa Italia au taifa lolote kubwa duniani kiko sahihi kuigwa, kumbuka formula na nadharia nyingi za masomo ziligunduliwa na Wagiriki pamoja na Warumi sasa kama English people waliweza kuzitranslate kwenda kwenye lugha zao kwann sisi tusiweze kuzileta kwny kisw??.. Enzi utamaduni wako kwa manufaa yako na ya vizazi vijavyo.. Mbona Wachina kwa kiasi kikubwa wameweza!