Napinga Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Kumekuwa na hoja nyingi za baadhi ya wadau wa kiswahili kuishawishi serikali kufuta kiingereza iwe lugha ya kufundishia hadi VYUO VIKUU na ibaki lama lugha ya kawaida kwa madai kuwa mtu anaelewa zaidi anapofundishwa na lugha anayoifahamu kwa ufasaha. Napinga hatua hii kwa sababu:

1. Tunakwepa kuwajibika kwa kushindwa kufundisha kwa ufasaha Kiingereza, sasa tunakimbilia kiswahili. Tuwajibike, ni rahisi tu, kuwa na walimu wa kutosha wenye motisha na kufundisha kiingereza kama enzi za mkoloni tatizo litaisha. Ni UVIVU tu wa kuona umeshindwa A unakimbilia B. tusikimbie tatizo na kujificha kwenye kishwahili. Mbona wenzetu majirani wanaweza?

2. Kuwa na uwezo wa kumudu lugha zaidi ya moja ( multlingual) ni sifa ya ziada. Ninachoamimi ni kuwa kikiruhusiwa kiswahili tujue kiingereza basi kimekwisha pamoja na kujinasibu kuwa kiingereza kitaendelea kufundishwa Ni siasa tu Watanzania nawafahamu wanapenda mteremko.

3. Angalia Rwanda pamoja na kifaransa chao wanatumia KIINGEREZA sasa kama lugha ya taifa, ni rahisi kufundisha kiingereza sasa kuliko kuhangaika kutafisiri taaluma kwa kiswahili kitu ambacho kitatuchukua miaka mingi na hatimaye utakuta kiswahili kina mambo tele mapya. Fikiria katika computer, keyboard inaitwa baobonye. sasa tasfri kila kitu, kuanzia appilications, software zote, programing , networking n.k halafu uone kama kiswahili kitakuwa chepesi. Tunajidanganya.

4. Sekondari wanaongoza kufeli kiswahii kuliko Kiingereza.

Nawakilisha.
 
Kwa nini tuwe watumwa wa lugha ya watu na ile hali tuna lugha yetu?,kwa nini tunapenda kujiwajibisha kwa kisicho chetu?

Sioni ubaya wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia na pia si vibaya kujifunza lugha ya kingereza lakini kibaya ni kuwa mtumwa wa kuitukuza lugha ya kingereza na kusahau lugha hii adhimu ya kiswahili.

Lazima tujivunie na tutumie lugha yetu kufundishia na pia kujifunza lugha nyingine za kigeni.

WATANZANIA KISWAHILI NI NEMBO YA UTAMADUNI WETU HIVYO HATUNA BUDI KUIENZI LUGHA HII ADHIMU.
 
Kiswahili kitumike lakini English iboreshwe zaidi binafsi napenda kiingereza iwe lugha ya kwanza na kiswahili iwe second language.
 
Ndugu mwanajamvi crome20 shukrani kwa kuchangia hoja. Nami nadiriki kujitosa katika mjadala kwa kuwa hukufanya kosa kama la wengine, kupiga kelele bila kusema chochote. Wewe umechangia kwa hoja. ndiposa nami ninakuja kuzidurusu hoja zako nikiwa naziunga mkono na wakati mwingine nikiwa mpinzani!

Umesema vema katika hoja yako ya kwanza kwamba tumeshindwa kuwajibika kufundisha kwa Kiingereza na sasa tunakimbilia Kiswahili. Pengine ni kweli, lakini hujaonesha namna ambavyo 'kukimbia' kwetu kwenda kwenye Kiswahili kunavyoweza kuboresha kuwajibika kwetu ilhali katika hoja nyingine umeonesha somo la Kiswahili wanafunzi hufeli kuliko English. Kwa hiyo suala hapa ni kuwajibika, lugha tuiweke pembeni kwanza.

Kuwa na uwezo wa kumudu lugha zaidi ya moja ni hoja nzuri na ninakuunga mkono kabisa. Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi ulioutoa kuthibitisha kwamba kukumbatia kwetu Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika ngazi ya Sekondari na Elimu ya juu kumesaidia kuwapata Watanzania mahiri wenye kumudu Kiingereza na Kifaransa au hata na Kiswahili.

Ni jambo la aibu kwamba hata umahiri katika Kiswahili, lugha itumiwayo katika huduma huko gulioni, vijiweni na hata maliwatoni, ni wa mashaka makubwa. Kwa hiyo kimantiki ni kwamba pamoja na kuitumia lugha ya Kiingereza kwa miongo mitano hivi, bado hatujafaulu kupata matunda yafaayo. Hatujawa mahiri wa lugha zaidi ya moja! Mataifa kama Uingereza, Ufaransa, Marekani, Uchina n.k wanatumia lugha zao katika mfumo wao wa elimu ingawa raia wa nchi hizo wa mahiri wa lugha mbili, tatu hadi tano!

Hoja nyingine unayoidokeza hapa ni Rwanda kutumia Kiingereza licha ya kuwa na Kifaransa chao (!). Kwanza pengine ni kwa kutaka kukwepa hoja au pengine ni kwa kutokujua, hukuonesha jinsi serikali ya Paul Kagame ilivyofikia maamuzi magumu ya kukitosa Kifaransa, lugha ya mkoloni wake, na kugeukia Kiingereza.

Kifupi tu niseme tu kwamba Mh. Kagame alikataa mchana kweupe ujinga wa Wafaransa waliokuwa wanaendeleza ukoloni wao kwenye nchi huru Rwanda na pasipo kutafuna maneno akawaambia ikiwa lugha yao waliiona kama mali kitu nchini mwake walikosea. Na kuwadhihirishia hilo akatangaza sasa kutumia Kiingereza mahala pa Kifaransa. Ingawa kimantiki hiyo si kuthibitisha kwamba Kiingereza ni bora kuliko Kifaransa au lugha nyingine yoyote!

Hoja yako ya mwisho uliyoidokeza ni kwamba katika mitihani wanafunzi hufeli sana Kiswahili kuliko Kiingereza. Hoja hii inao ukweli wa kitakwimu ingawa crone20 hujaonesha hoja yako inavyowiana na mjadala wetu. Si kitu, hata hivo! Mimi nataka nipenyeze hoja moja inayohitaji tafakuri. Kwa wenzetu wenye maono, lugha hufananishwa na taifa. Taifa la China huongea Kichina. Taifa la Denmark hutumia Kidenish. Taifa la Ufaransa huongea Kifaransa. Taifa la Ureno wanaongea Kireno. Taifa la Italia wanaongea Kiitaliano. Na lugha hizo ndizo hutumiwa katika mfumo wa elimu katika mataifa tajwa.

Ingawa hiyo haijawahi kulalamikiwa mahala popote kuwa ni kikwazo cha kuwafanya raia wa mataifa hayo kuwa mahiri wa kuongea lugha zingine za kimataifa. Kwa hiyo lugha ni suala la kifalsafa na ambalo watu wenye urazini mpevu hawawezi kulifanyia mzaha asilani!

Vyovyote iwavyo, na tujadili!!!
 
Pamoja na kuwa Lugha ya Kiswahili imefanikiwa kutuunganisha lakini pia kwa kiasi fulani kimesababisha sisi kuwa 'kisiwa' kwa kiasi fulani.Nchi tunazopakana nazo raia wao wengi wanaweza kuwasiliana kwa lugha ya Kiingereza.Hili likiangaliwa kwa undani linaleta shida fulani katika mawasiliano yetu na raia wa nchi jirani.Tunakuwa 'isolated' kwa kiasi fulani.

Ni dhahiri kuwa pamoja na sisi kuwa wazungumzaji wazuri wa Kiswahili tumeshindwa katika upande wa uandishi.Jaribu tu kuchukua vitabu vya hadithi vya kwetu utagundua kuwa waandishi wengi wana shida ya kuandika Kiswahili,ufundi wa lugha haupo au unapotea kwa kasi sana,waandishi wengi wanatumia lugha ya kuongea(informal style) katika uandishi kiasi cha kupoteza ladha ya vitabu.Ndio maana sikushangaa sana baada ya kuona walimu wengi na vitabu vingi vya kiswahili vinavyotumika nchini Uganda ni kutoka Kenya.

Pia nakumbuka tume ya kiswahili TUKI ikishindwa hata kuchukua tenda ya kutafsiri Google na window s na kuishia kuchukuliwa na mwanafunzi wa Kenya(tena asiyesoma hata shahada ya Kiswahili!).Ni dhahiri kuwa tumeshindwa katika suala la uandishi.

Kutumia kiswahili ni kujitenga na majirani zetu na kuzidi kujinyima fursa katika jamii ya kimataifa.Kama China,Japan na Korea pamoja na kuwa na nguvu za kiuchumi bado wanazidi kuongeza juhudi za kujifunza Kiingereza...i
 
Pamoja na kuwa Lugha ya Kiswahili imefanikiwa kutuunganisha lakini pia kwa kiasi fulani kimesababisha sisi kuwa 'kisiwa' kwa kiasi fulani.Nchi tunazopakana nazo raia wao wengi wanaweza kuwasiliana kwa lugha ya Kiingereza.Hili likiangaliwa kwa undani linaleta shida fulani katika mawasiliano yetu na raia wa nchi jirani.Tunakuwa 'isolated' kwa kiasi fulani.
Ni dhahiri kuwa pamoja na sisi kuwa wazungumzaji wazuri wa Kiswahili tumeshindwa katika upande wa uandishi.Jaribu tu kuchukua vitabu vya hadithi vya kwetu utagundua kuwa waandishi wengi wana shida ya kuandika Kiswahili,ufundi wa lugha haupo au unapotea kwa kasi sana,waandishi wengi wanatumia lugha ya kuongea(informal style) katika uandishi kiasi cha kupoteza ladha ya vitabu.Ndio maana sikushangaa sana baada ya kuona walimu wengi na vitabu vingi vya kiswahili vinavyotumika nchini Uganda ni kutoka Kenya.Pia nakumbuka tume ya kiswahili TUKI ikishindwa hata kuchukua tenda ya kutafsiri Google na window s na kuishia kuchukuliwa na mwanafunzi wa Kenya(tena asiyesoma hata shahada ya Kiswahili!).Ni dhahiri kuwa tumeshindwa katika suala la uandishi.
Kutumia kiswahili ni kujitenga na majirani zetu na kuzidi kujinyima fursa katika jamii ya kimataifa.Kama China,Japan na Korea pamoja na kuwa na nguvu za kiuchumi bado wanazidi kuongeza juhudi za kujifunza Kiingereza...i

Lonestriker unaelekea kurudufu makosa ya wengi, kuacha kuongea hoja na kujikuta unapiga kelele au kulalamika. Tunaweza tukawa tumebaki kisiwa kama yalivyo madai yako (ingawa haimaanishi kama nakubaliana na wewe kwa hilo) ingawa hakuna ushahidi kuntu unaothibitisha 'ukisiwa' huo umesababishwa na utumiwaji wa lugha yetu ya Kiswahili. Kimantiki, umejipinga mwenyewe kwa kuwataja Wachina, Wajapani na Wakorea kuwa wana bidii ya kujifunza Kiingereza licha ya ukweli kwamba wana lugha zao. Ningekuelewa kama ungetuthibitishia kuwa hata Wachina, Wajapani na Wakorea wamejikuta kuwa wako kisiwani kwa kukumbatia lugha zao (kama sisi) na sasa wameamua kuchukua hatua ya kujifunza Kiingereza kujiondoa humo kisiwani. Hivyo bado ninaona utetezi wako ni chapwa kwa kiasi kikubwa na hasa kwa kukosa hoja yenye/zenye mashiko kuweza kuthibitisha pasipo kuacha mashaka yoyote kwamba lugha ya Kiswahili Tanzani ni janga!

Na tuendelee kujadili!
 
Unaposema hoja zangu zimekosa mashiko(inaelekea unapenda tu kutumia semi bila maana!) bila kuzipangua kwa hoja zako na mifano hai ni ulemavu wa fikra au uvivu wa kuandika.

1.Nimesema kuwa hatuwezi kutumia lugha ambayo tunashindwa katika uandishi wake.Nimetoa mifano,kwamba ufundi katika uandishi wa vitabu vya Kiswahili haupo au ni wa kiwango cha chini sana kiasi kwamba hata kwenye uchambuzi wa fasihi vitabu vyetu havitumiki sana kwenye zinazojifunza kiswahili kama Uganda na Kenya.Pia nimeandika kwamba hata ukienda Uganda utakuta walimu wa kiswahili ni wakenya kwa sababu sisi pamoja na kuwa wazungumzaji wazuri wa Kiswahili tuna shida kwenye suala la uandishi.Hivyo nami napinga hoja ya kutumika kwa lugha hii kwa sababu kama hatuwezi kuandika vitabu tu vya kawaida sasa tutawezaje kuandika vitabu vya taaluma kama utabibu,uhandisi,uhasibu...vinavyohitajika katika ufundishaji?

2.Ukisiwa wetu.Hauhitaji kwenda mbali kugundua kwamba sisi ndio pekee ambao tunauelewa mdogo wa lugha zenye nguvu na fursa nyingi za kiuchumi.Ukiondoa Burundi ambao wao wanatumia kifaransa ambacho nacho kina nguvu kubwa kimataifa,nchi karibu zote zinatumia kiingereza na hivyo kuwa na 'advantage' kwenye soko la ajira pale wanapokuwa kwenye 'interview' na sisi watanzania.Mara nyingi nimewaona wasomi wetu-mawaziri,ma-profesa,wabunge,wahadhiri wakipata vigugumizi kujenga hoja kwa lugha ya kiingereza (tazama kipindi cha This week in perspective ujionee jinsi tulivyo-general unease with English compared to our fellow counterparts in the region).Hii inatu-isolate kwa wenzetu.Kwenye makongamano,warsha au mikutano ya kanda unakuta sisi watanzania tunajitenga,tunachangia kwa kiwango cha chini katika mazungumzo au kukaa katika vikundi vya watanzania wenzetu kutokana na kutokuwa at ease with English conversations.Hata humu JF,nenda kwenye jukwaa la Kimataifa uone linavyopwaya kwa sisi kushindwa ku-interact na wenzetu wa Kenya na Uganda waliomo,wachangiaji ni wale wale na ni wachache mno.Je huu si ' ukisiwa'?

3.Hoja ya Japan,Korea na China.Nakuomba tu usome historia ya nchi hizi hasa miaka ya 1940-70. Utagundua mchango wa lugha ya kiingereza katika ku-jump start uchumi wao.Katika ulimwengu huu wa utandawazi kujiingiza katika ufundishaji kwa kiswahili hadi vyuoni ni kujizika na kuzidi kujitenga.

4.Sisi wananchi tutasoma kwa Kiswahili humu nchini huku watoto wa wenye wakisoma shule za kimataifa au nje ya nchi then it is only obvious kuwa wakirudi watakuwa na advantage kwenye kazi nzuri au kazi za mashirika ya kimataifa.Tusije tukaanza kulia pale watoto wa wakubwa waliosoma nje ya nchi watakapopewa kazi zote nzuri ambazo nyingi zinahitaji mtu kumudu kuzungumza katika lugha za wafadhili wetu.
 
Kwa nini tuwe watumwa wa lugha ya watu na ile hali tuna lugha yetu?,kwa nini tunapenda kujiwajibisha kwa kisicho chetu?,Sioni ubaya wa kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia na pia si vibaya kujifunza lugha ya kingereza lakini kibaya ni kuwa mtumwa wa kuitukuza lugha ya kingereza na kusahau lugha hii adhimu ya kiswahili.Lazima tujivunie na tutumie lugha yetu kufundishia na pia kujifunza lugha nyingine za kigeni.WATANZANIA KISWAHILI NI NEMBO YA UTAMADUNI WETU HIVYO HATUNA BUDI KUIENZI LUGHA HII ADHIMU.

Naomba unijibu swali hili: kwa nini karibu nchi zote zilizoendelea kuna kozi elimu ya juu zinafundishwa kwa kiingereza? Majuzi chuo kikuu kikongwe kabisa mjini Milan Italia kimeamua kufundisha kozi zake zote kwa Kiingereza, unadhani ni kasumba?
 
Lonestriker;

Hata mimi nina shaka jinsi taifa linavyotaka kuturudisha enzi za ujima kwa kutaka kukibeba beba kiswahili. Ikumbukwe kwamba kama ni kutuunganisha tayari kimetuunganisha sasa ni wakati wa kujua kwa ufasaha lugha za kibiashara na za kimataifa hasa kiingereza.

Tukubali sisi ni wadogo sana na tusijilinganishe na china na ufaransa ya miaka ishirini iliyopita.
 
Last edited by a moderator:
Chemsha vichwa hii kitu ni logic sana..tunaendelea kudadavua kwa kina na vina.

Hapa mie naona mambo matatu ya msingi sana,1 ni watz kwa ujumla kuanzia kwa viongozi kukosa uzalendo(patriotism),tunapokuwa na viongozi waliotayari kuikebehi lugha yao kwa misingi yoyote ile basi hata raia wa kawaida wataidharau lugha yao na kuziona za wengine ni bora kimaandishi,kimatamshi,kimisamiati n.k

2.Nauona uzembe wetu wa kiutanzania ilivyo ada katika kujifunza na kutafuta maharifa kwa ajiri ya maendeleo yetu,haingii akirini miaka 50 ya uhuru watz hawajabobea kuitawala na kuitumia lugha yao ya taifa,mfano,nenda nyumba zote tafuta ni nani ana kamusi ya kiswahili,badala yake watu wanamiliki dictionary kuliko kamusi

3.Uchumi na kujitegemea pia ni tatizo dhidi ya matumizi ya lugha,ikumbukwe lugha ni uchumi,mnapokuwa na uchumi dhabiti na mkaweza kujitegemea basi mtaweza kuikuza lugha yenu pia,mtakuwa na vyuo na wataalamu na waandishi wenye kuandika na kazi zao kununuliwa na kutumiwa,mtatengeneza vitu vyenu na mtaweka majina ya kiswahili na italeta fikra kweli ya taifa la kiswahili dhidi ya lugha zingine

Mwisho,nafikiri iwe lazima kusoma kiswahili kwa watz wote kuanzia primari-vyuo vikuu katika fani zote na kufaulu kwa alama C primary-sekondari na B- katika vyuo vikuu,namaanisha liwe compulsory na mtu afaulu ndo aendelee na ngazi ya juu,mbona kuna TEOFIL huko nje na ili usome pale ni lazima ufaulu hii kitu?kama tukianza na hili ipo siku twaweza kuifanya lugha hii ikatumiwa kwa ufasaha na watu wote na hivyo kurahisisha kujifunzia na kufundishia

Tuendelee na mjadala.
 
jamani wakubwa.kuna mdau anasema sisi tutaendelea kuwa watumwa wa lugha ya kiingereza kwani hata alphabet zinazotumika zimetoka kwa waingereza kwa hiyo tuachane na habari ya kiswahili hatuna hata alphabet zetu.huyu mdau hata akisikia mtu kakosea kuzungumza kiingereza mfano tenses n.k anatamani kuzima radio amefikia mpaka hatua ya kubaki kucheka kila asiyejua kiingereza.ni mtumwa hasa au ulimbukeni.yeye akisikia mtu anaongea kiingereza vizuri huyo atamuita ana akili(hajui hii ni lugha)unaweza kumsikia anasema aah anakuzidi huyo kiingereza.
 
Unaposema hoja zangu zimekosa mashiko(inaelekea unapenda tu kutumia semi bila maana!) bila kuzipangua kwa hoja zako na mifano hai ni ulemavu wa fikra au uvivu wa kuandika.
1.Nimesema kuwa hatuwezi kutumia lugha ambayo tunashindwa katika uandishi wake.Nimetoa mifano,kwamba ufundi katika uandishi wa vitabu vya Kiswahili haupo au ni wa kiwango cha chini sana kiasi kwamba hata kwenye uchambuzi wa fasihi vitabu vyetu havitumiki sana kwenye zinazojifunza kiswahili kama Uganda na Kenya.Pia nimeandika kwamba hata ukienda Uganda utakuta walimu wa kiswahili ni wakenya kwa sababu sisi pamoja na kuwa wazungumzaji wazuri wa Kiswahili tuna shida kwenye suala la uandishi.Hivyo nami napinga hoja ya kutumika kwa lugha hii kwa sababu kama hatuwezi kuandika vitabu tu vya kawaida sasa tutawezaje kuandika vitabu vya taaluma kama utabibu,uhandisi,uhasibu...vinavyohitajika katika ufundishaji?
2.Ukisiwa wetu.Hauhitaji kwenda mbali kugundua kwamba sisi ndio pekee ambao tunauelewa mdogo wa lugha zenye nguvu na fursa nyingi za kiuchumi.Ukiondoa Burundi ambao wao wanatumia kifaransa ambacho nacho kina nguvu kubwa kimataifa,nchi karibu zote zinatumia kiingereza na hivyo kuwa na 'advantage' kwenye soko la ajira pale wanapokuwa kwenye 'interview' na sisi watanzania.Mara nyingi nimewaona wasomi wetu-mawaziri,ma-profesa,wabunge,wahadhiri wakipata vigugumizi kujenga hoja kwa lugha ya kiingereza (tazama kipindi cha This week in perspective ujionee jinsi tulivyo-general unease with English compared to our fellow counterparts in the region).Hii inatu-isolate kwa wenzetu.Kwenye makongamano,warsha au mikutano ya kanda unakuta sisi watanzania tunajitenga,tunachangia kwa kiwango cha chini katika mazungumzo au kukaa katika vikundi vya watanzania wenzetu kutokana na kutokuwa at ease with English conversations.Hata humu JF,nenda kwenye jukwaa la Kimataifa uone linavyopwaya kwa sisi kushindwa ku-interact na wenzetu wa Kenya na Uganda waliomo,wachangiaji ni wale wale na ni wachache mno.Je huu si ' ukisiwa'?
3.Hoja ya Japan,Korea na China.Nakuomba tu usome historia ya nchi hizi hasa miaka ya 1940-70. Utagundua mchango wa lugha ya kiingereza katika ku-jump start uchumi wao.Katika ulimwengu huu wa utandawazi kujiingiza katika ufundishaji kwa kiswahili hadi vyuoni ni kujizika na kuzidi kujitenga.
4.Sisi wananchi tutasoma kwa Kiswahili humu nchini huku watoto wa wenye wakisoma shule za kimataifa au nje ya nchi then it is only obvious kuwa wakirudi watakuwa na advantage kwenye kazi nzuri au kazi za mashirika ya kimataifa.Tusije tukaanza kulia pale watoto wa wakubwa waliosoma nje ya nchi watakapopewa kazi zote nzuri ambazo nyingi zinahitaji mtu kumudu kuzungumza katika lugha za wafadhili wetu.

Ninatanguliza shukurani zangu kwako Lonestrike kwa kuendeleza mjadala. Ingawa kwenye mjadala wenyewe umedhihirika kuhama kabisa kuzijadili hoja na kuamua kunishambulia mtoa hoja kwamba ninatumia maneno pasipo kuzingatia maana, nina ulemavu wa fikra na kwamba ni mvivu wa kuandika. Sitadiriki kutoa utetezi, nitawaachia wanajamvi wengine kuhukumu. Mimi nitajaribu kuzikabili hoja zako (kama zitakuwepo zenye uzito) ili mjadala huu uwe na maana.

Utetezi wako wa awali wa lugha ya Kiingereza unaegemea kwenye udhaifu wa Watanzania katika uandishi wa machapisho mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na kwamba hata walimu wa Kiswahili nchini Uganda ni Wakenya! Nimejaribu kulazimisha sana ili ionekane hapa kuwa umetoa hoja ingawa kimsingi hujasema chochote. Udhaifu wa Watanzania kuandika kwa lugha ya Kiswahili hakuwezi kuhalalisha lugha ya Kiingereza labda kama una mifano dhahiri kwamba yapo walau machapisho kadhaa kwa lugha ya Kiingereza ambayo yameandikwa na hawa Watanzania maana tumeikumbatia lugha ya Kiingereza katika mfumo wa elimu kwa nusu karne sasa. Kama hakuna machapisho ya Kiswahili wala ya Kiingereza basi mantiki inaelekeza tatizo haliwezi kufungamanishwa na lugha. Halafu suala la Wakenya kuwa na fursa ya kufundisha Uganda (na kwingineko...) haimaanishi kwamba wao ni wazuri kuliko Watanzania. Napenda kuweka wazi hapa kwamba Watanzania walikuwa wa kwanza kuiingiza lugha ya Kiswahili katika mtandao kupitia mradi ulioitwa Jambo Microsoft mwaka 2005 na ukazinduliwa na Waziri Mkuu wa wakati ule Mh. F. T. Sumaye lakini wakenya wakateka mradi huo na kuutangaza Ulimwenguni kote kwamba ni wao. Na ni Wakenya hawa hawa ambao wameutangaza Ml. Kilimanjaro kwamba uko nchini mwao na kwa muda wakafanikiwa kuiteka jumuiya wa Watalii wa kimataifa kwenda kuutembelea Ml. Kilimanjaro nchini Kenya! Kwa hiyo unapojadili suala linalowahusu Wakenya unapaswa kuwa makini kidogo vinginevyo utatoa hoja ambazo si jalabati.

Umetaja kwamba Watanzani wameonekana kuwa dhaifu kwa matumizi ya Kiingereza ukilinganisha na majirani zao na hivo hii inawanyima fursa katika soko la ajira na mawasiliano ya ulimwengu wa nje. Hapa sijakupata hasa ulilenga kueleza kitu gani. Watanzani waliokumbatia Kiingereza miaka 50 unawaona wa dhaifu, bado unatushawishi kuendelea katika mfumo huo kwa miaka mingine 50 tukitegemea matokeo tofauti? Liko jambo ambalo ama unalijua na unalikwepa kusudi au hulijui na unahitaji msaada. Udhaifu wa Watanzania katika kumudu lugha ya Kiingereza hakutokani na uwepo wa lugha ya Kiswahili, la hasha! Udhaifu huu unatokana na lugha hii kutofundishwa vizuri. Hata lugha ya Kiswahili pia ufundishwaji wake ni mbovu. Kwa hiyo haiwezakani kuimarisha lugha ya Kiingereza kwa kupiga vita lugha ya Kiswahili, badala yake ni lazima ifike mahala ufundishaji wa kweli uhimizwe. Kwa nini Wafaransa, Waitaliano, Wadenish, Wachina n.k wanamudu vizuri Kiingereza pamoja na kuwa na lugha zao halafu uniletee hoja kwamba ni lazima Kiingereza nchini Tanzania kiimarishwe kwa gharama ya kukitekeza Kiswahili. Mvivu kifikra anaweza kunasa katika mtego huo, siyo mimi!

Umenipa changamoto ya kwenda kusoma historia ya Japan, China na Korea toka miaka ya 40 hadi 70. Wakati ninaenda kuifanya 'kazi' hiyo nami nikuombe umsome mwanagenzi nguri Mganda Wadada Nabudere (Mungu amrehemu) uone anazungumza nini kuhusu nchi hizo. Profesa huyo ndiye muasisi wa dhana ya 'localization' alipokuwa anaziasa hizi nchi zetu jinsi zinavyopapatikia 'globalization' bila kujua utamaduni wake. Hebu jaribu kusoma msimamo wake juu lugha na mchango wake katika kukuza maarifa, stadi, teknolojia na urazini. Kwa hiyo ndugu yangu Lonestriker unapojitosa kwenye mjadala, nashauri uandike vitu unavyovijua kindakindaki ili kuepuka kelele!

Umetoa tahadhari kwamba Watanzania wanaweza 'kudanganyika' kuwasomesha watoto wao humu nchini kwa kutumia Kiswahili huku vigogo wakiwasomesha watoto wao nje ya nchi kwa lugha ya Kiingereza. Hoja hii si kama ni dhaifu tu bali pia inaonesha upeo mdogo wa mtoaji anayeilinganisha lugha na elimu. Inaelekea wazungumzaji wa Kiingereza wote ndiyo wasomi kwa mkabala huo! Ikitokea dhana hiyo ikafanya kazi, babu yangu Mantogoyoka ataitwa profesa wakati wowote maana huyu mzee wangu anatapika ung'eng'e yule licha ya kwamba alitumia muda mwingi wa ujana wake akiwa mpishi kwa mzungu mmoja kule Tanga! Kwa hiyo niseme tu kwamba, tunaweza kuwa tuna matatizo fulani katika mfumo wetu wa elimu. Lakini sikubaliani na hoja ya matatizo haya kushikamanishwa na Kiswahili!

Vyovyote, iwavyo na tujadili!!!
 
Wanajamvi wapendwa, sijaridhika kuona hoja hii mnaizika wakati si wake. Tuuendelezeni mjadala jamani mpaka pale tutakapofikia muafaka.
 
[
Hoja yako ya mwisho uliyoidokeza ni kwamba katika mitihani wanafunzi hufeli sana Kiswahili kuliko Kiingereza. Hoja hii inao ukweli wa kitakwimu ingawa crone20 hujaonesha hoja yako inavyowiana na mjadala wetu. Si kitu, hata hivo! Mimi nataka nipenyeze hoja moja inayohitaji tafakuri. Kwa wenzetu wenye maono, lugha hufananishwa na taifa. Taifa la China huongea Kichina. Taifa la Denmark hutumia Kidenish. Taifa la Ufaransa huongea Kifaransa. Taifa la Ureno wanaongea Kireno. Taifa la Italia wanaongea Kiitaliano. Na lugha hizo ndizo hutumiwa katika mfumo wa elimu katika mataifa tajwa. Ingawa hiyo haijawahi kulalamikiwa mahala popote kuwa ni kikwazo cha kuwafanya raia wa mataifa hayo kuwa mahiri wa kuongea lugha zingine za kimataifa. Kwa hiyo lugha ni suala la kifalsafa na ambalo watu wenye urazini mpevu hawawezi kulifanyia mzaha asilani!]
Vyovyote iwavyo, na tujadili!!![/QUOTE]

Bwana Omonto, nimependa ulivyotiririka. Shida yangu kubwa sana ni kuona Kiswahili sasa kinapigiwa chapuo, bila hao wadau kueleza wapi tuliteleza na Kiingereza, na wala hawatoi mkakati wa kuhakikisha kiingereza kinakuzwa ili watoto wetu waache kuingia gharama za kusoma kiingereza. Nadhani unaona jinsi tulivyowatengenezea ajira majirani zetu nafasi katika English-media schools na utitiri wa vyuo vya english courses. Kukinadi kishwahili tu bila kutoa majibu ya kukikuza kiingereza ni dalili tosha kuwa kiingereza kitatoswa na kubaki ni lugha ya matajiri wenye uwezo wa kusomesha watototo nje au shule za Kimataifa. Na hapa tutakuwa tunatengeneza tabaka lingine, maana kama kazi itahitaji mtu aweze kumudu kuongea na kuandika kwa ufasaha kingereza na kiswahili, basi watoto wa makabwela wataachwa mbali sana.

Tatizo letu si kiingereza, la hasha ni tabia ya kufanya vitu bila kufuata viwango, mfumo wa elimu unaoshabikia idadi ya wahitimu bila kujali ubora wa elimu yenyewe. Ndio maana tuna utitiri wa shahada wakati ukimtathimini muhitimu ni sawa na FORM 4 tu. Kwa vile tumekisingizia Kiingereza kwa kutoelewa kwa wanafunzi wetu, bila kutatua hoja ya msingi bado watoto watafeli tu pamoja na kufundishwa kiswahili. Hebu angalia kuna daraja A, na B ngapi katika kiswahili unapochukua sampuli moja katika shule moja? Utakuta ufaulu wa kiswahili ni mdogo sana pamoja na kufundishwa somo hilo kwa kiswahili tunachokililia.

Na mwisho hii hoja ya kusema kuwa kutukuza Kiingereza ni utumwa naishangaa sana. kukazania kiingereza maana yake si kudharau Kiswahili, ni kutia msisitizo maana hii lugha ni ngeni inahitaji mkakati zaidi ya kiswahili kwani kiswahili tunakizungumza na kukisikiliza sana hivyo huitaji msukumo wa ziada kukielewa. Hivi kuchukua jambo ambalo linakusaidia kukabiliana na changamoto za kimaisha nao ni utumwa?. Mbona hatupigi kelele kutukuza mavazi kama suti za wazungu na kanzu za waarabu ili turudi katika enzi za Kaniki na Lubega? maana hata mavazi ni utamaduni.

Jirani yangu mtoto wake anasoma English Media Primary schools pale Tabata. Kwa kweli ukiangalia uwezo wa mtoto kumudu mambo mbalimbali, kujiamini, kujieleza na kujenga hoja utagundua kuwa sio tu Kiingerza kimeyafanya haya bali seriousnes katika kufundisha na kumjenga mtoto kisaikologia.

Kwa wale waliofuatilia mashindano ya urembo mwaka jana, utagundua wale waliojidai kujibu maswali kwa kiswahili walichemsha hata kwa maswali yaliyokuwa na uwanja mpana wa kujieleza. Kiswahili sio suluhisho la kufeli( sijui kama neno hili ni kiswahili) basi tusiingie gharama kubwa kutafsiri, kutunga vitabu vya kiswahili maelfu kwa maelfu bali tuboreshe mfumo wa kufundisha kiingereza, ili tuwe kama wenzetu Zambia, Kenya, uganda n.k. Tuache kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.
 
[
Hoja yako ya mwisho uliyoidokeza ni kwamba katika mitihani wanafunzi hufeli sana Kiswahili kuliko Kiingereza. Hoja hii inao ukweli wa kitakwimu ingawa crone20 hujaonesha hoja yako inavyowiana na mjadala wetu. Si kitu, hata hivo! Mimi nataka nipenyeze hoja moja inayohitaji tafakuri. Kwa wenzetu wenye maono, lugha hufananishwa na taifa. Taifa la China huongea Kichina. Taifa la Denmark hutumia Kidenish. Taifa la Ufaransa huongea Kifaransa. Taifa la Ureno wanaongea Kireno. Taifa la Italia wanaongea Kiitaliano. Na lugha hizo ndizo hutumiwa katika mfumo wa elimu katika mataifa tajwa. Ingawa hiyo haijawahi kulalamikiwa mahala popote kuwa ni kikwazo cha kuwafanya raia wa mataifa hayo kuwa mahiri wa kuongea lugha zingine za kimataifa. Kwa hiyo lugha ni suala la kifalsafa na ambalo watu wenye urazini mpevu hawawezi kulifanyia mzaha asilani!]
Vyovyote iwavyo, na tujadili!!!

Bwana Omonto, nimependa ulivyotiririka. Shida yangu kubwa sana ni kuona Kiswahili sasa kinapigiwa chapuo, bila hao wadau kueleza wapi tuliteleza na Kiingereza, na wala hawatoi mkakati wa kuhakikisha kiingereza kinakuzwa ili watoto wetu waache kuingia gharama za kusoma kiingereza. Nadhani unaona jinsi tulivyowatengenezea ajira majirani zetu nafasi katika English-media schools na utitiri wa vyuo vya english courses. Kukinadi kishwahili tu bila kutoa majibu ya kukikuza kiingereza ni dalili tosha kuwa kiingereza kitatoswa na kubaki ni lugha ya matajiri wenye uwezo wa kusomesha watototo nje au shule za Kimataifa. Na hapa tutakuwa tunatengeneza tabaka lingine, maana kama kazi itahitaji mtu aweze kumudu kuongea na kuandika kwa ufasaha kingereza na kiswahili, basi watoto wa makabwela wataachwa mbali sana.

Tatizo letu si kiingereza, la hasha ni tabia ya kufanya vitu bila kufuata viwango, mfumo wa elimu unaoshabikia idadi ya wahitimu bila kujali ubora wa elimu yenyewe. Ndio maana tuna utitiri wa shahada wakati ukimtathimini muhitimu ni sawa na FORM 4 tu. Kwa vile tumekisingizia Kiingereza kwa kutoelewa kwa wanafunzi wetu, bila kutatua hoja ya msingi bado watoto watafeli tu pamoja na kufundishwa kiswahili. Hebu angalia kuna daraja A, na B ngapi katika kiswahili unapochukua sampuli moja katika shule moja? Utakuta ufaulu wa kiswahili ni mdogo sana pamoja na kufundishwa somo hilo kwa kiswahili tunachokililia.

Na mwisho hii hoja ya kusema kuwa kutukuza Kiingereza ni utumwa naishangaa sana. kukazania kiingereza maana yake si kudharau Kiswahili, ni kutia msisitizo maana hii lugha ni ngeni inahitaji mkakati zaidi ya kiswahili kwani kiswahili tunakizungumza na kukisikiliza sana hivyo huitaji msukumo wa ziada kukielewa. Hivi kuchukua jambo ambalo linakusaidia kukabiliana na changamoto za kimaisha nao ni utumwa?. Mbona hatupigi kelele kutukuza mavazi kama suti za wazungu na kanzu za waarabu ili turudi katika enzi za Kaniki na Lubega? maana hata mavazi ni utamaduni.

Jirani yangu mtoto wake anasoma English Media Primary schools pale Tabata. Kwa kweli ukiangalia uwezo wa mtoto kumudu mambo mbalimbali, kujiamini, kujieleza na kujenga hoja utagundua kuwa sio tu Kiingerza kimeyafanya haya bali seriousnes katika kufundisha na kumjenga mtoto kisaikologia.

Kwa wale waliofuatilia mashindano ya urembo mwaka jana, utagundua wale waliojidai kujibu maswali kwa kiswahili walichemsha hata kwa maswali yaliyokuwa na uwanja mpana wa kujieleza. Kiswahili sio suluhisho la kufeli( sijui kama neno hili ni kiswahili) basi tusiingie gharama kubwa kutafsiri, kutunga vitabu vya kiswahili maelfu kwa maelfu bali tuboreshe mfumo wa kufundisha kiingereza, ili tuwe kama wenzetu Zambia, Kenya, uganda n.k. Tuache kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.[/QUOTE]

Pana kila dalili za wazi ndugu crome20 unapenda kufanya mjadala. Ukifuatilia nyuzi nyingi hapa jamvini, utagundua kuwa watu hawajadiliani, wanapigiana kelele! Mwanzoni mwa mjadala huu ulikuja kasi kidogo na nusura jazba ikuondoe kwenye mjadala kukupeleka kwenye kupiga kelele. Ila umegutuka na umerudi.

Kiuhalisia, mahala palipokozwa rangi nyekundu (nionavyo mimi) ni hoja nzuri tu na ambazo kuzipinga yakubidi uwe kama mwanasiasa mmoja maarufu anayesema hata wanachama wa chama chake wakihama wooooooote, atabaki yeye mwenyewe na chama kitabaki kuwa imara! Teh! Teh! Teh! Teh! Teh! Teh! Teh! Teh! (nimetania lakini...) Lakini pale palipokozwa rangi nyekundu, pakakuzwa kidogo na kuwa katika hati ya kulazwa ndilo tatizo hasaaaa! Na katika hilo, niseme tu ninakuunga mkono kwa asilimia zote (sio kama wabunge wa CCM lakini. Teh! Teh! Teh! Teh! (nimetania tu.)

Palipokozwa rangi ya bluu panahitaji utunduizi wa fikra kabla hatujafikia masuluhisho hayo. Ni hoja zenye kuhitaji kutafitiwa kidogo ili tufahamu pasipo kuacha mashaka yoyote kwa nini hapo pa bluu pako hivo. Vinginevyo, niendelee kutokukuunga mkono moja kwa moja eti tukiwekeza kwenye Kiingereza basi 'umatonya' wetu utatutoka kwa usiku mmoja tu!

Mjadala unaendelea!!!
 
Mtoa mada unaonekana u mvivu wa kupitia machapisho na hizo hoja za ulowaita wadau,mara zote wamekuwa wakisisitiza kuwa kiswahili kikiwa lugha ya kufundishia haimaanishi tutazitupilia mbali lugha nyingine ikiwemo hicho kiingereza unachokiabudu,bali zitaendelea kufundishwa tu kama somo. Ifike mahali tujiamini kuwa tunaweza tusiwe watumwa,tuamke!
 
Sasa kama tumeshindwa kumudu kiingereza wakati ni lugha ya kufundishia sekondari hadi vyuo, je ikibaki kufundishwa kama lugha itakuwaje? Wewe ndo mvivu wa kusoma thread unakimbilia kulaumu tu . Hebu angalia original thread nimesema hivi: 2. Kuwa na uwezo wa kumudu lugha zaidi ya moja ( multlingual) ni sifa ya ziada. Ninachoamimi ni kuwa kikiruhusiwa kiswahili tujue kiingereza basi kimekwisha pamoja na kujinasibu kuwa kiingereza kitaendelea kufundishwa Ni siasa tu Watanzania nawafahamu wanapenda mteremko" kwa hiyo natambua kuwa wanasema kitaendelea kufundishwa, lakini hawatoi namna mkakati utakavyokuwa ndio maana nasema hizo ni porojo tu. Huo utumwa unaoshadidia nimeshaujibu soma, usikariri maneno ya wengine. Ndio kwa kiswahili tunaweza lakini itachukua muda mrefu sana na gharama kubwa. Wakati kwa kiingereza tunahitaji tu kuwa makini katika kukifundisha tu basi, kama enzi zile za mkoloni.
Mtoa mada unaonekana u mvivu wa kupitia machapisho na hizo hoja za ulowaita wadau,mara zote wamekuwa wakisisitiza kuwa kiswahili kikiwa lugha ya kufundishia haimaanishi tutazitupilia mbali lugha nyingine ikiwemo hicho kiingereza unachokiabudu,bali zitaendelea kufundishwa tu kama somo. Ifike mahali tujiamini kuwa tunaweza tusiwe watumwa,tuamke!
 
Kama China,Japan na Korea pamoja na kuwa na nguvu za kiuchumi bado wanazidi kuongeza juhudi za kujifunza Kiingereza...i

Hapo mimi ndipo hasa palipo na hoja yangu. Ikiwa mataifa tajwa hapo juu leo sote tunakiri kwamba yana nguvu kiuchumi, basi hilo ndilo la kuigwa, na sio kuangalia ufanano wetu na watu wengine kwa kutumia lugha zao kisha sisi tukadidimia kiuchumi. Kwanza tuweke maarifa ya kweli katika vichwa vya vijana wetu, waelewe vizuri maarifa ili waweze kuzalisha na kuboresha uchumi wao kwa kukabiliana vyema na mazingira yao ya Tanzania. Hilo ndio la msingi, hayo ya mawasiliano na wenzetu, tutazalisha wenye uwezo huo kwa kiasi tu cha mahitaji yetu kama taifa. Hakuna haja ya Watanzania wote kujua lugha mbili, tatu au nne na kuendelea.
 
Kila lugha huwa na maana kulingana na matumizi, watumiaji husika.. Sijaona logic sana katika hoja yako, kumbuka kwamba hata hicho kiingereza kilianza kama mchicha kikakua taratibu na kufikia hapa kilipo sasa, na keep it on your mind that bado kinaendelea kukua kulingana na maendelea ya dunia..

Kiswahili pia ni lugha yenye kila sifa na kwa kiasi kikubwa inakidhi mahitaji ya watumiaji wake, ni ulimbukeni na uvivu wa kufikiri kusema kwamba kisw hakifai kutumika kama lugha ya kufundishia(medium of instructions) issue ya msingi ni kuondokana na hiyo kasumba ya ukoloni wa kifikra eti kisa Marekani na Uingereza ni mataifa yenye nguvu dunuan basi tuwategemee kwenye kila kitu .. Datz a big No! Kumbuka kwamba hata hicho kingereza kimekopa maneno mengi tu kutoka kwenye kiswahili chetu mf. Safari, ugali etc.. Cha msingi hapa ni kuweka mikakati ya mdamfupi na mrefu na siku moja tutaweza kufika huko waliko wachina, wajapani n.k..
 
Back
Top Bottom