Napendekeza kuwe na governing body ya manunuzi katika industry ya Telecom

haibreus

JF-Expert Member
Oct 1, 2009
295
106
KUTOKANA NA UZOEFU WANGU KTK INDUSTRY YA TELECOM YAFUATAYO YANAHITAJI SERIKALI IINGILIE KATI
1. Mabadiliko holela ya bei kutoka makampuni ya simu na washirika wake ( Huawei na Helios towers ) yanaelekea kuua makampuni ya mawasiliano ya wazawa kwa mfano :
Gharama ya kujenga link moja mwaka
1.2005-2007 ilikuwa ni hadi Tsh 5 millioni
2.2013-2014 link hiyo hiyo ikawa ni Tsh Milioni moja
3.2016-2017 link hiyo hiyo imekuwa ni Tsh laki 7
Gharama ya kusimamisha mnara
1. 2005-2007 ilikuwa ni hadi 70 millioni
2. 2010-2013 ilikuwa ni hadi 50 millioni
3. 2015- 2017 Imekuwa ni hadi 35 millioni

Huo ni Mfano mdogo tu wa kile ninachotaka kukisema , ila Wizara husika ikitaka kufuatilia kwa undani itagundua uozo mwingi ambao unafanywa na hizi kampuni za kigeni chini ya vivuli vya Vodacom(Vodaphone) , Tigo( MIC) na Celtel ( Airtel or Zain ).
Kampuni ya Helios towers Tanzania ambao ndio walionunua minara ya Tigo na Voda , ilikuwa ikifanya kazi na kampuni za Watanzania hapo awali kuanzia 2012 kwa bei angalizi ambazo zilikuwa ni maridhiano yao na kampuni za wazawa , hili lilisaidia sana kuchangia ktk pato la Taifa.
Baada tu ya muda mfupi Kampun hii ya Helios a.k.a HTT ikatoka mikononi mwa Waingereza na kuhamia mikononi mwa Mfaransa , ambae nae amekuja na masharti yake mapya ...
- Kuleta kampuni za kifaransa kufanya kazi zake zote
- Kufuta makampuni asilimia 90 ya wazawa na kwamba yakitaka kazi basi yaombe kwa kampuni mpya zilizosajiliwa na wao yani za kifaransa
- Kupunguza bei zote kwa asilimia zaidi ya 50 , kwa kauli ya Take it or leave it
- Kuhusu nafasi za managers wengine(kutoka nje ya Tanzania = hili sitalisema )

2. Makampuni ya simu na washirika wake ( helios Towers na Huawei)
Mapato ya serikali yatapungua sana au kupotea kutokana na kuharibiwa kwa fursa ya kampuni za wazawa kuendelea kustawi kwa sababu punguzo la bei angalizi ( supply ) hadi chini ya 50%
Hii itasababisha kampuni nyingi kushindwa kujiendesha na hatimae kufa kabisa

ANGALIZO
Natoa ushauri kwa wizara husika kuwa na tabia ya kutembelea kampuni kama hizi na kufuatilia uendeshaji wake kwa kufanya ulinganifu wa mapato kwa miaka iliyopita na sasa na kuangalia chanzo hasa ni nini
Serikali iweke bei angalizi ktk sekta hii nyeti ili kusaidia makampuni ya wazawa yaweze kuendelea kutoa fursa za ajira kwa Watanzania wengi zaidi .
Kwa leo naishia hapo labda kama kuna maoni zaidi
 
Serikali isiishie hapo tu,ifatilie na uendeshaji wa hizi kampuni za wazawa,zenye kuchukua kandarasi za kuhudumia minara ya simu(power ),
Makampuni haya mengi,yanaajiri watu wasio na sifa na elimu ya kutosha ya kufanya kazi za uhandisi,mishahara duni,na ukiukaji mwingi wa sheria za kazi,
Baadhi ya makampuni,yalikufa,na kupoteza ajira nyingi,sababu kubwa unakuta ni ugomvi,binafsi wa wakurugenzi na wadau wao,mfano Linksoft,
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom