Nape: Wanachama wengi CCM mamluki; Asema asilimia 80 ya Wananchi ni Wanachama Wa CCM

Miaka ile ya 80S ilikuwa ni muhimu kuwa na kadi ya ccm na hata mimi nilikuwa nayo kwa sababu mzee wangu alikuwa mwasisi mzuri na mwalimu wa siasa. Watoto wote wakubwa tulikuwa na kadi na watu walikuwa wanafundishwa siasa za ujamaa na kujitegemea.

Baada ya mwalimu kuFariki mzee wangu hakuendelea tena na siasa za ccm maana zilipoteza mvuto. Na ilifika mahali akahama hata chama japo upinzani wakati huo hata haukuwa na maana sana.

Kimsingi ni kwamba ccm iliondoka na mwenyewe mwalimu kilichobaki ni kivuli cha ccm. Kimebaki kichaka cha kuficha ufisadi wa serikali na maswahiba wao.

Ccm ilikuwa chama cha wanyonge na kiliwapigania na kuwatete hata kufa.
Hakika hakuna atakayeweza kukunusuru chama hiki labda mwalimu arudi.

Nape hatakama unania njema ya kurejesha ccm ya mwalimu kamwe hutaweza maana ccm uliyonayo si ile ya mwalimu hilo ni jina tu brother, the chama cha mapinduzi kimepumuzi na mwenyewe baba wa taifa.
kama unataka ccm ya mwalimu ondoka ccm ya leo(chama cha mafisadi )na uanze upya.

Lakini kama wewe ni just opportunist tu unayetaka kupata manufaa ya baadaye kupitia hiki chama kichafu kamwe you will die holding it!
Endelea na kile ulichotumwa but we are advising you, hujui kinachoendelea you are just a vuvuzela wenyewe wapo. Amini usiamini hutakaa uwatoe akina Rachel kwenye chama maana ndiyo wenye chama chao wewe umedandia pasipo kujua kama hiki ni chama kingine kabisa na wala si cha akina mzee Mnauye tena.

Wewe mgeni tu ndani ya hiki chama kwanini uwasumbue wenye chama watakuondoa dogo jiangalie!
Huo ndo ushauri wangu kwakwo kama uko humu unafatilia.
 
waacheni wajiparue...unaukumbuka "wenyewe kwa wenyewe wameanza kugombana?" sikio la kufa halisikii dawa. kwaherini ccm. jaribuni kubadili fikra na kuanza kutafakari namna ya kuwa chama cha upinzani bora chenye nia ya dhati kurudi madarakani...kwa kutetea maslahi ya wananchi na kudosarisha watawala
 
Kijana wa marehemu Brigedia Moses Nnauye ni mchemkaji tu!

Mkuu nimeona picha uliyobandika kwenye ile thread nyingine akijimwaga na sebene. huyu ni msanii tu hana jipya. kweli Nchimbi aliona mbali kumfuta uanachama wa uvccm huyu kijana, maana angeupata uenyekiti ingekuwa ameshaimaliza uvccm.
 
CCM inawanachama milioni 5 hivi.. Tanzania ina karibu watu milioni 45... asilimia 80 ya milioni 45 ni milioni 5! well according to Nape.

Wakati Namaliza Chuo Vijana wengi walichukua Kadi za CCM eti Wakifikiri Kwamba ni Moja Kati ya Maswali ya Intreview ( Kimsingi wengi hata si Wanachama wa CCM)

Actually Vijana wengi sasa si Wanachama wa Vyama vya Siasa Wengi ni Wanaharakati
 
Hajatofautiana sana na TAMBWE HIZA, labda kimaumbile cause mmoja mnene sana na mwingine ana mwili wa kawaida.Ila kwakuropoka wote ni mavuvuzela tu.
 
Wednesday, 04 May 2011 08:36
Rachel Balama na Rose Itono, Jijini

"Kuna watu wanafikiri kuwa kujivua gamba ni kwa ajili ya watu wawili au watatu. La hasha! Hiyo ni kwa ajili ya wanachama wote," amesema Nnauye.

CCM nashauri msifukuze mtu, itaharibu umoja na mshikamano ndani ya chama. Shikamaneni, it is good for the party.
 
Hongera Nape kwa kuliona hilo la wana-CCM ni makapi, kwani tunaona hata mchango wa hoja za wabunge wa CCM bungeni ni ZERO, serikali ya CCM ktk kutatua matatizo ya msingi ya mtanzania pia ni ZERO.
 
Kwa kweli "gamba" ni baya sana na inachukua muda kulivua!

45,000,000 mil x 80% = 5,000,000mil !

I hope Katibu Itikadi anahitaji kurudi Darasani kusoma Hesabu badala ya kukaa na kuropoka! Shame on you Nape!
Angalia hapo kwenye red, nafikiri hata China hawajafika hapo
 
Ukikabidhiwa uongozi ccm hata kama ulikuwa makini inabidi ufuate upepo tu,maana linalosemwa leo linaweza kubadilishwa kesho na mtu huyo huyo au likakanushwa na mwingine.
 
Nafasi aliyopewa Nape huko CCM hata angepewa mtu makini vipi,angepwaya tu na kuonekana kituko.Nape angekuwa smart angeikataa hiyo post na ku concentrate kwenye ukuu wake wa wilaya
 
Kijana wa marehemu Brigedia Moses Nnauye ni mchemkaji tu!

Light travels faster than sound, that's why some people appear to be bright/smart until when they speak.

Kwa mahesabu ya Nape, asilimia 19.5 (80 - 60.5) ya wana-CCM walimkataa JK katika uchaguzi wa 2010.


In retrospective, labda Nape yuko sahihi.

Waliojiandikisha kupiga kura 2010 tuliambiwa kuwa ni 19 milioni. Waliopiga kura ni 8 milioni, kutokana na majumuisho ya NEC. Waliompigia JK/CCM ni 4.8 milioni ambao ni takribani sawa na asilimia 25 ya watu 19 milioni waliojiandikisha kupiga kura.

Kweli CCM imejaa mamluki.
 
kama wapo wanachama wa ccm basi ni wazee wetu waliokua wanalazimishwa kuwa na kadi ya ccm ili wapate mgao wa sukari RTC.WENGINE ni watoto wa waliowahi kukulia na kuifaidi ccm kama nape maisha ya baba yake yalitegemea ccm!
 
Back
Top Bottom