Nape: Wanachama wengi CCM mamluki; Asema asilimia 80 ya Wananchi ni Wanachama Wa CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, 04 May 2011 08:36
Rachel Balama na Rose Itono, Jijini

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeazimia kuandaa mkakati wa kuangalia ubora wa wanachama wake kuliko kuendelea kuwa na mamluki ndani ya chama hicho. Kauli hiyo imetolewa jana usiku na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye, katika kipindi maalumu kinachorushwa na televisheni ya ITV kuhusu kujivua gamba kwa wanachama wa CCM.

Amesema chama hicho kina wingi wa wanachama wasio na sifa wala ubora ambao wamekuwa wakisababisha makundi ndani ya chama na kukivuruga chama.

Amesema CCM asilimia 80 ya wananchi ni wanachama wa CCM lakini baadhi yao hawana ubora, jambo ambalo lililosababisha chama kupoteza majimbo mengi katika uchaguzi uliopita.

“Wanachama wa CCM ni wengi, lakini ubora wa wanachama ni mdogo ambao umesababisha wananchi kukosa imani na chama,” amesema Nnauye.

Nnauye amewataka wana-CCM waliotakiwa kuwajibika wasiwe na chuki kwa kuwa hizo ni taratibu walizojiwekea katika chama.

“Kuna watu wanafikiri kuwa kujivua gamba ni kwa ajili ya watu wawili au watatu. La hasha! Hiyo ni kwa ajili ya wanachama wote,” amesema Nnauye.

Nnauye amewaomba wana-CCM kushikamana kuhakikisha kuwa chama kinaimarika na kurudisha imani kwa wananchi ambao walikuwa wameonesha kukatishwa tamaa na serikali ya chama hicho.

“Nawaomba wananchi waliokuwa wamekata tamaa na chama kurudisha imani yao sasa hivi. Chama kimeshaanza kuimarika na hali ya kukiimarisha zaidi itaendelea hadi ngazi za chini,” amesema Nnauye.

Ameongeza kuwa chama hicho kimekubaliana kutoa elimu kwa wanachama kabla ya kupewa kadi ili kuwawezesha wanachama wa chama hicho kukomaa kisiasa.

Amesema awali chama kilikuwa kikotoa kadi kwa wanachama kama njugu hali iliyopelekea chama hicho kupata wanachama wasio na sifa ndani ya chama.

Amewataka Watanzania kutarajia mabadiliko makubwa katika chama kwa maendeleo katika jamii kwa ujumla.

Nnauye ameongeza kuwa ndani ya sekretarieti yao wamekubaliana kuunda tume ya kumtafuta mgombea bora wa kiti cha Urais ambaye anakubalika ndani ya chama na jamii.
 
CCM inawanachama milioni 5 hivi.. Tanzania ina karibu watu milioni 45... asilimia 80 ya milioni 45 ni milioni 5! well according to Nape.
 
Kuna mtindo wa baadhi ya Watanzania kuwa na kadi ya CCM just in case.
 
Watanzania tuachane na hawa watoto wa mafisadi ni wamechanganyikiwa. Wanachoongea ni pumba Baba zao wamewapa vichwani mwao na wanafikiri bado Watanzania wanaudhaifu wa kufikiria kama mababu na mabibi huko vijijini. Mtu yeyote yule akifanya simple analysis ataona how ignorant this boy is,
1. Arusha, Mbeya, Dar, Moro, Mwanza, Songea, Mara, Shinyanga, Bukoba, Moshi, Tanga, Pwani, Rukwa, Kigoma, Dodoma ndipo population kubwa zilipo kutokana na ajira na kazi. Wananchi wangapi kwenye hii miji wanasikiza na kuamini pumba za kikwete na ccm?
2. Huko vijijini wamebaki wananchi wangapi zaidi ya mababu na mabibi wanaosaidiwa na vijana mijini?
3. What's percentage if Tanzanians still uninformed kama wakina Nnape na January?

"Nape endeleeni kuwandanganya wajinga na familia zenu, mwisho wenu msipoangalia utakuwa kama mtoto wa Gadaffi"
 
Yeah I remember Mimi ilibidi niwe na kadi ya CCM kupata pasipoti wakati huo wazazi wangu walisha fariki so one of the proof they wanted to see my CCM Card inaonyesha bado wananijumlisha kwenye hiyo orodha ya chama cha Mapinduzi
 
Kudadaki, mzimu wa ticha utazidi kuwatafuna mpaka....!!
Alafu hiki ki2ko, jamaa kwa2c kikubwa wameuchuna, yani 80% ni mamluki 20% ndio Mr.clean, alafu bado anasisitiza washikamane, teeh! I ain't get ze concept hapa!? Yaelekea jamaa alienda shule kuesabu madawati na kufuta ubao.
 
Kuna mtindo wa baadhi ya Watanzania kuwa na kadi ya CCM just in case.
Na hawa ndio wengi,hizi kadi wanakuwa nazo ili waweze kuzitumia pindi inapohitajika, wanachama hawa ndio wanatakiwa watimuliwe haraka sana
 
Hivi kasema asilimia 80% ya watanzania ni wanachama wa CCM au mwandishi ni kanjanja? Naamini angesema 80% ya wanachama wao ni waaminifu.
 
Nape mwenyewe ni Mamluki tu vilevile...............

wote tu hawa ma-opportunist kama magonjwa nyemelezi ya Ukimwi.............

Hiyo 80% nina wasiwasi itakuwa ni ya wananchi ndugu wa vigogo vya magogoni na sio wananchi wa Tz.......
 
hivi hiki chama kina mwenyekiti kweli...maana mi sielewi mara mafisadi ndo gamba mara wanachama wote ni magamba mara mamluki.....hahaaaa kazi kweli kweli
 
Nafuu kagundua huo ukweli.

Wa-Tanzania wengi sana walikizika CCM miaka mitano tu baada ya Baba yetu wa Taifa kupatwa na mauti na mambo kuanza kwenda kombo mithili ya 'PAKA AKIONDOKA PANYA HUTAWALA' hadi kero zikatufikia pomoni bila kiongozi yeyote mle kujali wala kuonekana kutujali sie mayatima wa utawala wa Mwalimi.

Ukweli wa mambo ni kwamba hizo kadi Kkibao wanazobeba wananchi mikononi ni geresha tu kusaidia kupata baadhi ya huduma za kiserikali ambazo ni siku nyingi tu zimekua zikitolewa kwa kuzingatia mmegemeo wa mtu kisiasa nchini.

Tofauti na hapo, waaalla!!!
 
Wednesday, 04 May 2011 08:36
Rachel Balama na Rose Itono, Jijini

Amesema CCM asilimia 80 ya wananchi ni wanachama wa CCM lakini baadhi yao hawana ubora, jambo ambalo lililosababisha chama kupoteza majimbo mengi katika uchaguzi uliopita.

Kwa kweli "gamba" ni baya sana na inachukua muda kulivua!

45,000,000 mil x 80% = 5,000,000mil !

I hope Katibu Itikadi anahitaji kurudi Darasani kusoma Hesabu badala ya kukaa na kuropoka! Shame on you Nape!
 
Kumsikiliza Nape ni sawa na ujinga,mbona hasemi tena kuwashughulikia akina EL,LA na AC na siku 90 baada ya Mkama kumzima domo yeye anyamaze kelele za nini kwani yeye ndio mwenyekiti?
 
Hivi kasema asilimia 80% ya watanzania ni wanachama wa CCM au mwandishi ni kanjanja? Naamini angesema 80% ya wanachama wao ni waaminifu.

kwa iyo 80%*41mil=32.8mil. Wakati mwaka jana kufikia tar30 june 2010 kumbukumbu zinasema walikuwa na wanachama 3,520,136. Sasa mil.3 na nusu imekuwa ghafla mpaka mil 32??? Watawala wetu wanafanya hesabu za whitehouse eti tukiwalipa wafanyakazi lak3.5 tutatumia trilioni6. Kwa kweli kukimbia hesabu shuleni ni dhambi.
 
Nape's speeches are always filled with lamentations. The man is so much confused now he can't even remember what decisions got decided upon in his party's vikaos.
Besides, he's too ignorant and bling to the eminent party's downfall whilst spending much of his time to 'bleach' the much stained president's family.
 
Heheeeeee, ccm bwana wamapata vuvuzela lingine baada ya makamba, no difference, no actions. Afadhali ccm kabla ya magamba kuliko hii inapoelekea, nape kakabidhiwa jembe la kuichimbia kaburi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom