Nape: Rais Samia alinikataza kujibizana na Watu Mitandaoni

Sasa hata mama kakuambia acha mipasho. Unapenda mambo ya kujibizana mzee wa oil chafu
Ona ulivoingia aibu hata kwenye msiba wa mzee Lowasa. Ulikua baridiiiiii sababu ya mipasho.
Sasa bila aibu eti unawaambia watu huo ugoro. Aibu yako
 
Ye muda mwingi alikuwa anautumia mitandaoni kutukanana ba watu, sio kujibizana.
 
Bora alivyomdhibiti maana Nape alikuwa ana majibu ya hovyo sana Tena ya kishamba
 
Hivi kuna siku huyu Waziri keshawahi simama sehemu akaelezea Mipango ya Tanzania kwenda na Kasi ya teknolojia, akatoa nondo namna tumepiga hatua na mauvumbuzi ya uhakika hivi, maana simuelewi, yeye kila siku ni story tu ambazo sidhani kama zinatusaidia.

Unaenda mbali sana Mkuu, zoezi la anwani, waliita post code liliishia wapi?
 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan alimsihi kuacha kujibizana na watu mitandaoni na badala yake asimamie falsafa ya R4.

Nape ameyasema hayo leo Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika kilele cha kurasa 365 za Mama zikiangazia mafanikio ya Rais Samia tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Nape amesema mara kadhaa Rais Samia huchafuliwa lakini amekuwa kimya huku asisitiza yasichukuliwe maamuzi yatayowadhuru raia wengine.

“Kuna wakati fulani, kuna jamaa fulani walimshambulia sana Rais na familia yake kwenye mitandano, huku ndani wakaanza kusema sasa waziri tunafanyaje? Mjadala ukawa mkubwa tuwachukulie hatua, tena kali! Tukasema kwa hawa au kwa jukwaa lote lililotumika?”

“Lakini wakati majadiliano yakiendelea, habari zilivuja na kumfikia Rais Samia ambaye aliamua kuniita na kuniambia nataka utatue jambo hili kwa busara,” amesema Nape na kuongeza

“Mama akaniita bana, akaniambia Nape…nimesikia mnajadiliana, lakini naomba nikukumbushe, nilitangaza 4R, mojawapo ni kuvumiliana, akasema hata kama mnataka kufanya lolote, hakikisheni hamuingilii uhuru wa watu kujieleza,” amesema

R4 za Rais Samia ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga taifa.

View attachment 2946314
Yaani kwa akili zako NAPE ulifikiri kujibizana kungekusaidia nini!?

Viongozi wa aina yako yawezekana uongozi siyo karama kwenu.
 
Yooooo nimesikiliza hotuba mbili za PM,wakati wa kuipokea ndege na Clouds tv ,jina la Dr.Samia amelitaja zaidi ya mara 20,je it's necessary?mtu anatukuzwa kama semi God!nchi inahitaji TAASISI IMARA na sio strong state person
Taasisi zipo,sema watu wake wengi siyo imara!!
 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan alimsihi kuacha kujibizana na watu mitandaoni na badala yake asimamie falsafa ya R4.

Nape ameyasema hayo leo Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika kilele cha kurasa 365 za Mama zikiangazia mafanikio ya Rais Samia tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Nape amesema mara kadhaa Rais Samia huchafuliwa lakini amekuwa kimya huku asisitiza yasichukuliwe maamuzi yatayowadhuru raia wengine.

“Kuna wakati fulani, kuna jamaa fulani walimshambulia sana Rais na familia yake kwenye mitandano, huku ndani wakaanza kusema sasa waziri tunafanyaje? Mjadala ukawa mkubwa tuwachukulie hatua, tena kali! Tukasema kwa hawa au kwa jukwaa lote lililotumika?”

“Lakini wakati majadiliano yakiendelea, habari zilivuja na kumfikia Rais Samia ambaye aliamua kuniita na kuniambia nataka utatue jambo hili kwa busara,” amesema Nape na kuongeza

“Mama akaniita bana, akaniambia Nape…nimesikia mnajadiliana, lakini naomba nikukumbushe, nilitangaza 4R, mojawapo ni kuvumiliana, akasema hata kama mnataka kufanya lolote, hakikisheni hamuingilii uhuru wa watu kujieleza,” amesema

R4 za Rais Samia ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga taifa.

View attachment 2946314
Na, huyu jamaa ni kubwa, jinga tu, yaani huna busara ya, kujua kujibishanq na watu iwe hadharani au mitandaoni ni ujinga,
 
Huyu Nape Nnauye ana wenge sana
 
Back
Top Bottom