Nape: Rais Samia alinikataza kujibizana na Watu Mitandaoni

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan alimsihi kuacha kujibizana na watu mitandaoni na badala yake asimamie falsafa ya R4.

Nape ameyasema hayo leo Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika kilele cha kurasa 365 za Mama zikiangazia mafanikio ya Rais Samia tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Nape amesema mara kadhaa Rais Samia huchafuliwa lakini amekuwa kimya huku asisitiza yasichukuliwe maamuzi yatayowadhuru raia wengine.

“Kuna wakati fulani, kuna jamaa fulani walimshambulia sana Rais na familia yake kwenye mitandano, huku ndani wakaanza kusema sasa waziri tunafanyaje? Mjadala ukawa mkubwa tuwachukulie hatua, tena kali! Tukasema kwa hawa au kwa jukwaa lote lililotumika?”

“Lakini wakati majadiliano yakiendelea, habari zilivuja na kumfikia Rais Samia ambaye aliamua kuniita na kuniambia nataka utatue jambo hili kwa busara,” amesema Nape na kuongeza

“Mama akaniita bana, akaniambia Nape…nimesikia mnajadiliana, lakini naomba nikukumbushe, nilitangaza 4R, mojawapo ni kuvumiliana, akasema hata kama mnataka kufanya lolote, hakikisheni hamuingilii uhuru wa watu kujieleza,” amesema

R4 za Rais Samia ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga taifa.
Nape hakujua kama yy ni waziri na hana sababu ya kujibizana na watu mitandaoni na kama Rais ndiye aliyemkataza basi Rais kwa katazo hilo alikuwa anamwambia Nape huna Akili.Waziri gani poyoyo unabishana na watu mitandaoni bila kushtuka na bado ni waziri.Nchi inalewa wapumbavu tu.yaan mpaka akwambie ww huna Akili kabisa ya kuwaza.
 
Hivi inawezekana vioi watu kama hawa kupata nafasi ya kuwa kiongozi mkubwa kiasi hiki hali upeo wake hata mwanafunzi alie ngazi ya elimu ya msingi anautoa kasoro?
 
Mjukuu wa Nyerere? Utakuwa huna taarifa sahishi kuhusu Yerico Nyerere.Hata hivyo kama mwanachama wa CDM ni haki yake kikatiba kugombea nafasi yoyote ndani ya Chama chake, sisi tusiyo na Vyama tutaendelea kuwa wapenzi watazamaji.
 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan alimsihi kuacha kujibizana na watu mitandaoni na badala yake asimamie falsafa ya R4.

Nape ameyasema hayo leo Machi 27, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika kilele cha kurasa 365 za Mama zikiangazia mafanikio ya Rais Samia tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021.

Nape amesema mara kadhaa Rais Samia huchafuliwa lakini amekuwa kimya huku asisitiza yasichukuliwe maamuzi yatayowadhuru raia wengine.

“Kuna wakati fulani, kuna jamaa fulani walimshambulia sana Rais na familia yake kwenye mitandano, huku ndani wakaanza kusema sasa waziri tunafanyaje? Mjadala ukawa mkubwa tuwachukulie hatua, tena kali! Tukasema kwa hawa au kwa jukwaa lote lililotumika?”

“Lakini wakati majadiliano yakiendelea, habari zilivuja na kumfikia Rais Samia ambaye aliamua kuniita na kuniambia nataka utatue jambo hili kwa busara,” amesema Nape na kuongeza

“Mama akaniita bana, akaniambia Nape…nimesikia mnajadiliana, lakini naomba nikukumbushe, nilitangaza 4R, mojawapo ni kuvumiliana, akasema hata kama mnataka kufanya lolote, hakikisheni hamuingilii uhuru wa watu kujieleza,” amesema

R4 za Rais Samia ni maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga taifa.

View attachment 2946314
Kuna tweet yake fulani alimwambia mwananchi "acha usng😂😂" aseme ukweli hii labda ndio ilifanya Rais akamkanya.
 
Kuna Waziri mwingine wa familia ile isiyoridhika na mipesa....kila kitu wanataka wao.....huyo mtoto nae simuoni nadhani nae ameshauriwa kuacha mihemko ya dini na vita Israel na matusi kwa wafuasi imani tofauti.....mitusi yake...mara shiga mara uharo....mitusi tu kutoka waziri ambae.....abaempa kibri siku skilala na yeye sihasa ....ndio mwisho wake
 
Back
Top Bottom