Nape Nnauye: Wizara ipo mikono salama

pitapiti

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
398
261
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amemuhakikishia aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji kuwa amekabidhi Wizara katika mikono salama na kumuahidi kuwa yeye binafsi pamoja na Naibu wake, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu ni wanataaluma wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA hivyo pasipo shaka anaamini wanakwenda kutimiza matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Samia Suluhu Hassan na watanzania kwa ujumla.

Sambamba na Makabidhiano ya Mawaziri hao yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba pia yalifanyika makabidhiano ya Ofisi baina Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jim Yonazi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula na kushuhudiwa na Menejimenti ya Wizara hiyo.

Mhe. Nnauye amewapongeza Dkt. Kijaji na Dkt. Chaula kwa kazi nzuri walioifanya na kuwaahidi kuendeleza yale yote waliyokuwa wameanza kuyatekeleza katika harakati za kuboresha na kuendeleza Sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA nchini.

Dkt. Kijaji ameishukuru Menejimenti ya Wizara hiyo kwa ushirikiano na uwajibikaji katika kipindi cha takribani miezi minne aliyohudumu katika Wizara hiyo na kuwasisitiza kufanyia kazi masuala yote yaliyokuwa katika hatua za utekelezaji kwa kuhakikisha yanafika mwisho mzuri unaotoa majibu na utatuzi uliokusudiwa.

Kwa upande wa Dkt. Jim Yonazi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema kuwa Dkt. Kijaji na Dkt. Chaula ni wadau muhimu wa Wizara hiyo, hivyo wataendelea kushirikiana, kushauriana na kupeana fursa mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuboresha Sekta ambazo wameteuliwa kuzisimamia

Aidha, Dkt. Chaula ameishukuru timu ya Menejimenti ya Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa kwake ambapo pamoja na kuwa ni Daktari wa binadamu lakini amekuwa na weledi mkubwa wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA na ataendelea kuwa mdau mkubwa wa Wizara hiyo huku akiwausia watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kuwa wazalendo, kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama.
 
Hiyo wizara ina mtu mmoja muungwana sana, Dr. Jim Yonazi, ambaye ni katibu mkuu. Mungu awaongoze
 
Nape hujisifu ana misimamo isiyoyumba lakini kwangu mara nyingi misimamo hiyo humfurahisha bosi wake haiwafurahishi wananchi, kule kufungia magazeti kisa yameandika habari wasiyoipenda kusijirudie.
 
Napenga mpuuzi sana... Asidhani tumemsahau... Alizima bunge live na kukatisha ubunifu wa vijana kwenye ICT na photo/videography

Alafu ghafla leo anatishia waajiri wa marehemu as if ajali imetokana na wao kutokulipwa mishahara kwa wakati...
Shame on him!!
 
jamanie mie hata sijuagi tu ina maana haka kajamaa kamerudi???.........hivi wale majamaa waliotumwa mnyooshea Bastola wanajisikiaje!!....ila nape bana anawajua atapiga kimya tu! km hawajui vile!!!!
 
Back
Top Bottom