Nape na Tendwa wanena kuhusu Kafulila

Wana CHADEMA tunakukaribisha tena KAMBINI ila " KEEP IN MIND THAT" kosa si kosa ila ukilirudia tena ndio kosa,, Ukija kututibua tena tunakuchakachua. WELCOME AGAIN KAFULILA
 
Kabisa. Tena ni kama kuwa promoted vile kutoka CCM B kwenda CCM A.
 
du!!! "watu sio binadamu" kinachotafutwa hapo si kafulila ni ubunge tu, hivi ukiwa mbunge hustahili kumhoji ama kumpinga mwenyekiti wako? hii hamuoni ni hatari na inapelekea wabunge kubaki mihuri kwenye vyama vyao, kwa hofu ya kutimuliwa?. mbunge kachaguliwa na wananchi kwa sifa zake na kwa kiasi kidogo kwa sifa ya chama, ni kwanini basi chama kikimkataa, ambacho hakikumpigia kura kipelekee kuondolewa mamla yake kama mbunge?
Hapa usilaumu uwenyekiti sana sana walaumu wajumbe wasiokuwa na msimamo kwa tamaa zao usiofuata haki baada ya kukatiwa kitu kidogo. waliomwondoa Kafulila ni wajumbe ambao ni waoga walimwogopa mwenyekiti kwani ndie anailea nccr ruzuku haitoshi. Wangemwondoa mwenyekiti ulaji wangepata wapi?
 
Hapa usilaumu uwenyekiti sana sana walaumu wajumbe wasiokuwa na msimamo kwa tamaa zao usiofuata haki baada ya kukatiwa kitu kidogo. waliomwondoa Kafulila ni wajumbe ambao ni waoga walimwogopa mwenyekiti kwani ndie anailea nccr ruzuku haitoshi. Wangemwondoa mwenyekiti ulaji wangepata wapi?

Aliyemuondoa Kafulila ni Mbatia na Ruhuza kwa maslahi yao binafsi na yale ya mabwana wao CCM, wajumbe walikuwa ni rubber stamp tu!!
 
Hebu ngoja kidogo, this guy has a point somewhere.

CCM kweli ni mlezi wa wapora uchumi wasiofukuzika hata kwa kikao cha NEC chao wala CC; yaani mle kwao siku hizi makosa kama haya ya Kafullila wala si kosa tena kwa CCM hii ya leo wala hafukuziwi mtu chamani.

CCM kamfwateni Kafullila haraka ukizingatia kwamba mnakaribia kkukosa wanachama kibao mwakani.

Ni chama imara kisichokuwa na migogoro na ni chama mlezi!
 
“Nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge David Kafulila na nilipata fursa ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa Jamii Forum na kuona mawazo ya Watanzania mbali mbali juu ya jambo hili .Na ninafikiri ninao wajibu kama kijana tena Mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta Mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana Bwana David Kafulila. “ Kwanza kabisa Bwana David Kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo , utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye hekima zaidi kwani katika kila changamoto kubwa Duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea Duniani .
Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa na kwamba “ Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa, Binafsi sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama kinachukuwa taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa, Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini David katika maisha ya siasa na Nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio na hauwezi kuviepuka ndio maana , Mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa “ huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na baadae vifranga watatotolewa ,
Lakini vile vile Mtu huyu mwenye hekima akasema tena “ haijalishi unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia “ kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni muhimu katika kufikia malengo makuu , Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu ? na vile vile tufikirie kama leo Mbunge au Diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu nidhamu ndani ya vyama vyao ,je vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?
NCCR Mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ? Kama nafasi ya Ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ? sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya Ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? nina wasi wasi kuwa siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa na waziri Mkuu wa Uingereza ili muweze kula lakini kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .
Hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio kuwa ni pamoja na nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu, Na ni hatari wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala , kwani ugomvi wetu vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea Taifa madhara makubwa.
Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa David , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha na jambo la kushangaza hapa, ni kwanini watu wameshituka sana Mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini Mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu , hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana ,
Sasa nimalizie kwa kusema David bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi kama, Martin Luther King Jr. alivyopata kunena “ The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.
Naibu Katibu mkuu wetu Mh Zitto nimesoma waraka wake kuwa amekukaribisha Chadema , lakini mimi kwa sasa nakukaribisha Arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama Chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ? kwani kwa mfano ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi Mungu lakini pia itakupasa kwenda Hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama Chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio Mbunge tena. Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa “ THE 21 MOST POWERFUL MINUTES IN A LEADERS DAY “ Kilichoandikwa na na mwandishi maarufu “ John C. Maxwell.
Sasa niseme “Jipe moyo David Kafulila na Hongera NCCR-MAGEUZI.
If you are a leader , it’s not enough to know what to do . You have to know when to act. “ John C. Maxwell.
Godbless Lema . (Mb)



 
Ni kama mama mwenye nyumba anayeogopa changamoto za housegirl wake kwa kuhisi atapinduliwa,
suluhisho housgal kutimuliwa ndio yalomkuta KAFULILA.
Achana na siasa za bongo japo zinalipa,ingia kwa wanaharakati.
 
du!!! "watu sio binadamu" kinachotafutwa hapo si kafulila ni ubunge tu, hivi ukiwa mbunge hustahili kumhoji ama kumpinga mwenyekiti wako? hii hamuoni ni hatari na inapelekea wabunge kubaki mihuri kwenye vyama vyao, kwa hofu ya kutimuliwa?. mbunge kachaguliwa na wananchi kwa sifa zake na kwa kiasi kidogo kwa sifa ya chama, ni kwanini basi chama kikimkataa, ambacho hakikumpigia kura kipelekee kuondolewa mamla yake kama mbunge?
We haumjui huyu sisimizi wewe tafuta habari zake
 
Ni kama mama mwenye nyumba anayeogopa changamoto za housegirl wake kwa kuhisi atapinduliwa,
suluhisho housgal kutimuliwa ndio yalomkuta KAFULILA.
Achana na siasa za bongo japo zinalipa,ingia kwa wanaharakati.
Atakula nini?.clab je?,Totoz? Na shule ndy hvyo tena
 
Yaani huyu aliandika ni Lema (Mb)...?

Sikuwahi sikia huyu jamaa akiongea wala sikuwahi soma chochote alichoandika ...ila ameandika hii kitu kwa umakini iko strong substance hapa ..bravo
 
Bado ni Mbunge Halali kwa sababu
  1. Hakuchaguliwa na Mbatia na Ruhuza
  2. Bado barua haijaenda kwa Supika kumuengua
  3. Yamkini ana fasiri yake ya ya neno mbunge...
  4. Kuna dalili za kurejeshewa uanachama wake
  5. kuna watu wamempa kichwa (CCM bILA SHAKA)
  6. An uhakika wa kushinda tena....anaamini hivyo...........
  7. ......................................................................
  8. ...........................................................................
 
KAMANDA LEMA AMFUNDA 'CHADEMA-CURB- KAFULILA' KWA KUSISITIZA KWAMBA NIDHAMU NI KILA KITU KWA MPAMBANAJI ANAPOPIGANIA UMMA DHIDI YA WAPORA NCHI BILA KUYUMBAYUMBA

"Nimesoma taarifa mbali mbali juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge David Kafulila na nilipata fursa ya kutoa maoni yangu pale vyombo vya habari vilipotaka hivyo kutoka kwangu, nimefuatilia kwa makini sana mijadala mbali mbali haswa katika mtandao wa Jamii Forum na kuona mawazo ya Watanzania mbali mbali juu ya jambo hili.

Na ninafikiri ninao wajibu kama kijana tena Mbunge kutoa maoni yangu na mtazamo wangu kwa kina juu ya jambo hili ambalo limemkuta Mbunge mwenzetu na rafiki yetu kijana Bwana David Kafulila. "

Kwanza kabisa Bwana David Kafulila pole sana lakini kikubwa zaidi jipe moyo kwani changamoto katika siasa mara nyingi ni matukio yasio ya kawaida ambayo yanaweza kushusha heshima ya mtu au kupandisha heshima ya mtu, lakini tambua kuwa matatizo sio msingi mkuu wa kuharibu ndoto ya mtu makini aliyekusudia kutimiza jambo ambalo wajibu wake ni upendo.

Utu na ukweli katika jamii ni imani yangu kuwa changamoto hii inaweza kukufanya uwe kijana mwenye hekima zaidi kwani katika kila changamoto kubwa Duniani hapo ndipo ukombozi ulipotokea Duniani .

Ninatambua wakati unaopitia kwa sasa wewe na familia yako na wapiga kura wako , lakini kwa mtu makini kama mimi ni lazima pia nikipongeze Chama chako kwa uamuzi wake dhidi yako , chama chako cha NCCR-Mageuzi kimechukua hatua muhimu katika maisha yake ya siasa.

Siku zote kumbuka kwamba " Nidhamu katika Chama itakuwa ni msingi mkuu katika kutafuta ukombozi wa kweli katika Taifa, Binafsi sifurahi wewe kufukuzwa katika Chama lakini nimefarijika na jinsi Chama kinachukuwa taratibu kama NCCR kinavyoweza kuchukua maamuzi magumu ya kulinda nidhamu na heshima ndani ya Taasisi ya Chama cha Siasa.

Watu wengi hata mimi ningependa usamehewe , lakini David katika maisha ya siasa na Nyanja nyingine , uvumilivu na nidhamu katika kufanikisha maono au ndoto ni vitu ambayo ni msingi mkuu wa mafanikio na hauwezi kuviepuka .

Ni kutokana na ukweli huu ndio maana , mtu mmoja mwenye hekima aliwahi kupata kunena kuwa " huwezi kupata kifaranga cha kuku kwa kuvunja yai bali kwa kusubiri yai liatamiwe kwa siku kadhaa na baadae vifranga watatotolewa".

Tunapoendelea kuzingati ukweli uliomo ndani y busara zake huyu mtu mwenye busara kemkem, vile vilealiendelea kusema kwamba " haijalishi unampenda mke wako kiasi gani , kuna vitu unaweza kumsaidia na kuna vitu huwezi kumsaidia".

Kwa mfano huwezi kumsaidia mke wako kubeba mimba hata kama unampenda sana , hivyo malengo makubwa katika siasa ni jambo muhimu kwa kijana makini kama wewe kufikiria lakini uvumilivu na kusubiri ni muhimu katika kufikia malengo makuu.

Mimi binafsi ninatofautiana na watu wengi kwamba kupoteza jimbo ni jambo gumu na baya , hapana kupoteza jimbo kwa sababu ya kulinda nidhamu ni jambo jema linalopaswa kufanyiwa hata sherehe , hivi kweli tunaweza kupima nidhamu na ni kitu gani katika maisha ya mwanadamu ?

Tuseme leo hii ikitokea kwamba Mbunge au Diwani akifukuzwa kwa utovu wa nidhamu na sisi tukafikiri ni makosa , je ni halali sasa vyama vya upinzani kutafuta kuunda dola kama vitashindwa kusimamia tu nidhamu ndani ya vyama vyao ,je vitaweza kweli kusimamia nidhamu ya dola pindi vitakapochukua madaraka ?

NCCR Mageuzi wamefanya maamuzi ya msingi na ya uhakika kulinda nidhamu ndani ya chama ambaye yeyoye atakayethubutu kulaani basi ajiulize swali hili ?

Kama nafasi ya Ubunge inathamani kubwa kuliko nidhamu ndani ya chama na jamii , je mtakuwa na ujasiri kweli wa kupinga dhambi dhidi ya utu wa mwanadamu ambapo hivi karibuni mlipewa masharti ya ndoa ya jinsia moja kama mnataka misaada ?

Sasa mkisema nidhamu ipuuzwe dhidi ya nafasi moja ya Ubunge , mtawezaje sasa kuvumilia njaa ,mateso na dhiki dhidi ya kutetea utu wenu ? nina wasi wasi kuwa siku moja pengine mtakubali yale mashariti mliyopewa na waziri Mkuu wa Uingereza ili muweze kula lakini kwa kudhalilisha utu wenu , kwani nafasi ya nidhamu katika maisha ya binadamu haupaswi kupigiwa kura .

Hivyo tukifahamu msingi mkuu wa mafanikio kuwa ni pamoja na nidhamu ya kweli , nafikiri maoni ya wachangiaji yatajikita katika kuutukuza ukweli na wala sio nafasi au cheo cha mtu, Na ni hatari wasomi wakifikiri kwamba lengo la vyama vya upinzani ni kushinda viti vya ubunge , madiwani bila kuzingatia maadili na nidhamu basi ni ukweli kuwa hatutakuwa na sababu ya msingi ya kuwaondoa madarakani chama tawala.

Kimsingi kile kinachotufanya tufikirie kuwangoa wengine madarakani na kubwa zaidi ugomvi wetu vyama vya upinzani na chama tawala hausababishwi na tofauti ya rangi za bendera bali ni msingi katika maadili, nidhamu na uwajibikaji usiozingatia haki na kweli ndio maana kwa sababu hiyo ufisadi,wizi na ubabaishaji umekuwa ukiongezeka kila wakati na kuletea Taifa madhara makubwa.

Aliyekosa akiwa muungwana anaomba radhi na ndio ushauri wangu kwa David , lakini jambo hili limeshitua lakini pia limefundisha na jambo la kushangaza hapa, ni kwanini watu wameshituka sana Mbunge kufutiwa uanachama na sio kwanini Mbunge amekuwa mtovu wa nidhamu.

Hata hivyo sifahamu mgogoro huu kwa kina sana , lakini najua sihitaji ruhusa kuingia chumbani kwangu , mgogoro huu na malumbano yalikuwa wazi tena wazi sana.


Sasa nimalizie kwa kusema David bado unayo nafasi kubwa ya kujirekebisha na kuwa kiongozi mzuri , wako waliopata matukio magumu ya kisiasa kuliko wewe lakini waliweza kurudi kwenye nafasi zao kwa utumishi kama, Martin Luther King Jr. alivyopata kunena " The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort, but where he stands at times of challenge and controversy.

Naibu Katibu mkuu wetu Mh Zitto nimesoma waraka wake kuwa amekukaribisha Chadema , lakini mimi kwa sasa nakukaribisha Arusha kama utapenda kupumzika huku ukitafakari ili upate kujua kuwa unapaswa kuhama Chama au unapaswa kuomba radhi na kujirekebisha ?

kwani kwa mfano ukiuguua ugonjwa wa zinaa pamoja na kutubu dhambi kwa mwenyezi Mungu lakini pia itakupasa kwenda Hosipatalini kutafuta dawa, sioni kama ni muhimu sana kuhama Chama isipokuwa kuomba radhi hata kama wewe sio Mbunge tena.

Sasa ningekushauri utafute kitabu kinachoitwa " THE 21 MOST POWERFUL MINUTES IN A LEADERS DAY " Kilichoandikwa na na mwandishi maarufu " John C. Maxwell.

Sasa nimalizie kwa kusema "Jipe moyo David Kafulila na Hongera NCCR-MAGEUZI. If you are a leader , it's not enough to know what to do . You have to know when to act. " John C. Maxwell.

Godbless Lema . (Mb)


--------------------------------------

NB: Hayo maneno mazito na tena yaliojaa busara tele hapo juu wala si yangu bali ni kwamba nimejaribu kuyapangilia tu japo kidogo - Uwezo Tunao.
 
Kwa kauli hiyo nzito hapo juu, Kamanda Lema arusha kombora hewani kwa wapiganaji wote nchini huku akisisitiza kwamba pindi tunapoendelea kusimamia kile tunachokiamini ni sharti NIDHAMU (si WOGA) itutangulie mbeele kama tai.
 

Monday, 19 December 2011 21:21


tendwa-top.jpg

Msajiri wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa

CHADEMA WAMKARIBISHA, CCM WAPONDA KUFUKUZANA

Waandishi Wetu

MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa amemkingia kifua Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR Mageuzi, David Kafulila ambaye alifukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita.

Badala yake Tendwa katika kauli yake jana alivitaka vyama vya siasa kutumia busara katika kutatua migogoro yake na siyo kutoa uamuzi wa kukomoana kama ya kumfukuza mtu uanachama.

"Kila mara nasema kwamba, vyama viwe makini panapotokea migogoro. Wafanye majadiliano kupitia vikao na sio kuchukua uamuzi wa haraka kufukuzana uananchama," alisisitiza Tendwa. Tendwa alisema hayo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa Mafunzo ya viongozi wa Baraza la vyama vya Siasa nchini. Mafunzo hayo yalihusu uongozi, uwajibikaji na utawala bora. Kauli hiyo ya Tendwa imekuja siku tatu tangu Chama cha NCCR-Mageuzi kimfukuze uanachama Kafulila kwa madai ya kukiuka taratibu za chama hicho.

"Mimi kama Msajili siingilii mamlaka ya chama chochote na sina mamlaka ya kikatiba kufanya hivyo. Lakini, katiba haimruhusu (Kafulila) kuendelea na uongozi (mbunge) hadi awe na chama, hivyo kunatakiwa sasa, kuandaliwe uchaguzi mdogo,"alisema Tendwa na kuongeza: "Kuandaa uchaguzi mdogo ni gharama kubwa. Uchaguzi mmoja gharama yake ni zaidi ya Sh19 bilioni. Kwa suala kama hili tujiulize nani amesababisha gharama, tusiishie tu kuupigia kelele ufisadi, tuangalie na sisi viongozi wa vyama tunaisaidia vipi serikali?"

Alisema unapoitishwa uchaguzi lazima kuwaandaa wasimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kusimamia uchaguzi, polisi kwa ajili ya usalama na mahitaji mengine na kwamba fedha zinazotumika zingeweza kugharamia shughuli nyingine za maendeleo. Alitoa mfano wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambao alisema walioshiriki wanafahamu gharama na usumbufu walioupata.

Hata hivyo Tendwa alisema, Kafulila bado ana nafasi ya kukata rufaa ndani ya chama chake na hata nje ya chama. Alifafanua: "Ana uhuru kwenda mahakamani na akishinda ataendelea kuwa mbunge".

Alifafanua kwamba mbunge huyo ana haki ya kwenda mahakamani kukata rufaa na kwamba makahama ikiona alikiuka sheria na taratibu za chama basi hapo lazima uchaguzi mdogo ufanyike na serikali italazimika kuingia gharama kubwa.

Awali, akizungumza katika mkutano huo uliohusisha viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, Tendwa alisema matatizo yanayotokea ndani ya taasisi, asasi na hata kwenye vyama vya siasa yanatokana na mawasiliano hafifu hivyo viongozi bora wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwasiliana. "Kama kiongozi anatakiwa kutoa onyo au karipio kwa mtumishi ama mtendaji ni vizuri na busara kutoa onyo hilo bila kuonyesha hisia za chuki binafsi,"alisema Tendwa.

Alisema migongano mingi inatokana na udhahifu katika kuainisha ukomo wa madaraka na kwamba busara inatakiwa itumike kutambua yale kiongozi anayotakiwa kuamua na yale ambayo lazima apate ushauri kabla ya kutoa uamuzi wake.

Matumaini ya Kafulila
Kwa upande wake Kafulila alisema hawezi kuzungumza kwa undani kuhusu hatma yake kisiasa na kusisitiza kwamba, jambo hilo litakwisha. Akizungumza Dar es Salaam jana Kafulila alisema, ''Kuna taratibu zinaendelea ndani ya chama, kwa sasa sitaweza kuzungumza lolote, kila jambo liko ndani ya chama (NCCR Mageuzi) na taratibu zinaendelea". Alipoulizwa taarifa kwamba anataka kufungua kesi ya kikatiba kupinga uamuzi wa chama hicho kumfukuza uanachama alisema, ''Unajua nini kuna…, kuna mambo yanaendelea hivyo siwezi kuzungumza kwa sasa, ila ninachopenda kuwaeleza watanzania ni kwamba hili jambo litakwisha tu,''.

Hawezi kukata rufaa

Mwanasheria wa NCCR Mageuzi, Dk Sengondo Mvungi alisema Kafulila hawezi kukata rufaa sehemu yoyote dhidi ya uamuzi wa kumfukuza uanachama kwa mujibu wa kanuni ya 7 (2) ya chama hicho.

Kanuni hiyo ya 7(2) ya nidhamu na usuluhishi sehemu ya (d) inaeleza kuwa, baada ya uamuzi wa mwisho kufanywa, kikao husika kitatoa maelekezo kwa kikao au vikao vya chini vyenye mamlaka ya kuchukua hatua au kutoa adhabu kwa kiongozi au mwanachama husika. Kipengele (f) kinasema uamuzi utakaofanywa kwa mujibu wa kupengele (d) utakuwa wa mwisho ila tu pale unapomhusu Mwenyekiti Taifa na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) ambao uamuzi wa mwisho kuwahusu wao ni Mkutano Mkuu.
Kanuni hiyo hiyo sehemu ya 7(1) inaeleza, ''Mlalamikiwa au mhusika atakuwa na haki ya kukata rufaa kwenda kamati ya nidhamu na usuluhishi iliyo katika kikao cha ngazi ya juu zaidi ya kikao husika, na kamati hiyo itakuwa na uwezo sawa na ule wa kamati ya kwanza, ila tu haitapokea ushahidi mara ya pili''. Hata hivyo, kwa mujibu wa Ibara ya 10(4) ya Katiba ya chama hicho, ''Mwanachama ana haki ya kujitetea mbele ya kikao cha chama kinachohusika katika mashitaka au madai yoyoye, na kuwa na haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo mhusika hakuridhika na uamuzi wa kikao cha chini.''

Chadema wamkaribisha Kafulila
Wakati hayo yakiendelea, Chadema kimemkaribisha mbunge huyo kujiunga na chama hicho baada ya kufukuzwa NCCR-Mageuzi. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook alisema: "Kafulila akumbuke kwamba hakufukuzwa Chadema ila alijiondoa mwenyewe".

"Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama chetu,"alisema Zitto. Hata hivyo, Zitto ameeleza kuwa anaamini NCCR Mageuzi watamaliza matatizo yao kwa mujibu wa katiba ya chama chao na Kafulila atazikabili changamoto hizo kama kiongozi kijana wa kisiasa badala ya kukata tamaa.

"Ifahamike wazi kabisa kwamba David ni mtu huru mwenye mawazo yake na maamuzi yake. Kwamba sisi ni marafiki wa karibu na kwamba tunatoka mkoa mmoja,"alisema na kukanusha taarifa zinazomuhusisha yeye na Kafulila kuhusu mgogoro ndani ya NCCR Mageuzi.

"Napenda kuweka wazi kwamba sihusiki kwa namna yeyote ile na migogoro ya chama kile. Ninaomba nisihusishwe na mambo yasiyonihusu. Ni dhahiri kwamba kuvuliwa uanachama kwa David ni jaribio kubwa kwa mfumo wetu wa demokrasia kama ilivyokuwa huko nyuma wakati kina Erasto Tumbo walipovuliwa uanachama wa chama chao cha UDP."

Zitto alisema haina maana kwamba lolote afanyalo ama Kafulila amemtuma yeye au anahusika na kuongeza kwamba, anaheshimu msimamo wake siku zote na huwa yupo upande wa anayeonewa, kudhulumiwa na mnyonge. "Msimamo huu wa msingi usiwape watu nafasi ya kunihusisha na mambo ya chama dhaifu kisicho na dira kama NCCR-Mageuzi,"alisema.

Nape abeza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye alisema vijana kwenye vyama vya siasa wanatakiwa washauriwe na kupewa maonyo badala ya kufukuzwa. Nape ambaye aliwahi kuingia kwenye malumbano na wazee ndani ya CCM akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu Yusuph Makamba, hadi kufikia hatua ya kumwambia kijana huyo, "alifungiwa duniani hadi mbinguni", alisema vijana waelimishwe.

Alifafanua kwamba hata enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere watu walikuwa wanakosea na wanaelimishwa na kwamba kama Nyerere angekwua na hasira hizo hata wanasiasa wanaoonekana leo wasingekuwepo.

Nape alivitaka vyama vya siasa vijenge utamaduni wa kuvumiliana na kuwalea vijana kwa kuwafundisha, badala ya kuwafukuza uanachama. "Mimi sio muumini wa kufukuza wana siasa vijana lakini kama tukiendelea hivi mwisho wa siku tutateketeza wanasiasa; "Kasi ya wanasiasa vijana ni kubwa lakini inawezekana kasi hii imeanza kuwatia homa wanasiasa wa zamani hasa kama mfano huu wa Kafulila,"alisema.

Alisema pia kama kutafanyika uchaguzi mdogo katika jimbo hilo wanaamini watashinda na kwamba anawashukuru NCCR, kwa kuwarejeshea jimbo hilo.

Habari hii imeandaliwa na Nora Damian, Fidelis Butahe, Gedius Rwiza, Boniface Meena na Keneth Goliama

 
Mbona CCM walifukuzana wakazaa Hamad na CUF; Mrema na NCCR Mageuzi, Mtei na Makani na CHadema

Sasa Hivyo vingine vikifukuzana ni dhambi kwao?
 
Good work.... the expected CDM chairman!!
Hivi wewe huwezi kuchangia kitu bila kugusia uenyekiti wa CDM au Mbowe? jifunze, zamani nilikuwa nakushangaa siku hizi tunashit kiutu uzima. Kila mtu wewe ni expected chairman angeandika Mnyika angekuwa expected angeandika Zitto angekuwa expected chairman, vipi mkuu mbona unakuwa obsessed sana na vyeo.

Back to the topic, binafsi nampongeza sana Lema kwa uandishi ulio balanced amezungumza vitu muhimu kwa pande zote chama NCCR na Kafulila, 'heshima na nidhamu', bila discipline huwezi fanikisha jambo lolote uwe mbunge injinia au daktari. Ni kweli kabisa kwamba vyama havikuanzishwa ili kupata wabunge tu ila kujenga na kudumisha heshima ya jamii katika nyanja mbalimbali, kurudisha nidhamu ya utendaji serikalini, hivyo basi haviwezi kusubiri hadi viingie ikulu ndipo vianze kujenga nidhamu ya wanachama na viongozi wake. Kwa hili nakupongeza, vile vile nitumie nafasi hii kumpongeza Mh. Lema kwa kushinda "Mjengwablog Young Leaders Award,".
 
Back
Top Bottom