Nape na Tendwa wanena kuhusu Kafulila

kafulila,unatia huruma sana,nakushauri mtafute mvungi akushauri na uombe msamaha na uache unafiki,hila na kukubali kutumiwa ovyo ovyo.simamia maslahi ya Taifa na maendeleo ya jimbo lako
 
Pamoja ya kwamba simjui sana Kafulila,inaelekea jamaa ana matatizo ya kutaka kuonekana na kusikilizwa .Hii ilimletea matatizo cdm. Bado hakusoma alama za nyakati ,lakini naamini sasa ataisoma. Ngoma inogile.
 
Haki ya nani? Yaani huyu Kafulila ana bahati kila upande unamtetea bila mwenyewe kuomba msaada. Ana bahati kweli nilidhani ndio Kafulia. Mara hii afanye adabu kwa viongozi wa juu yake.
 
Tendwa is talking strategically on CCM's point of views. Chaguzi ndogo si wimbo ambao CCM kwa sasa wanataka kuusikia ndiyo maana wanataka kupendekeza mfumo wa kuteua wawakilishi wa wananchi badala ya wananchi kuwapigia kura.

Kwanza
Chaguzi ndogo zinatumika kama kipimo cha kuona imani ya wananchi kwa CCM uchaguzi wa Igunga ulitoa jibu kuwa Imani hiyo imeporomoka catastrophically.

Pili chaguzi ndogo ni hela, CCM ili ifute aibu ya kushindwa vibaya katika chaguzi hizi hutumia fedha nyingi sana kiasi kwamba naona wenye akili kwenye chama wanajiuliza je gharama hiyo ni value for money katika kutetea mbunge mmoja ambaye hata wakimkosa bado wana super majority bungeni.

Tatu wimbo wa kufukuzana katika chama ambao ulipachikwa jina la kujivua gamba umeonekana si mzuri sana kwa afya ya CCM. Hivyo vyama kama NCCR vinapouimba CCM haipaswi kuucheza wimbo huo maana, maana ni dalili mbaya kwao, unawakumbusha magamba era ambayo strategically wameachana na mchakato huo.

Nne CCM wanajua kuwa hata kama jimbo hilo litakuwa wazi kulichukua haitakuwa rahisi sana na huenda ikawa ni cheche ya mabadiliko makubwa ambayo wanayasikia Aljazeera na vyombo vingine vya habari tu.

Tano kufukuzwa huku kwa Kafulila kuna undermine hoja yao ya kupeleka uwezo wa kuziba jimbo toka kwa vyama vinavyoyashikilia majimbo hayo, kwani ni dhahiri kuwa kama utaratibu huo utapitishwa basi wengi watakuwa victim kama Kafulila kwa ajili ya kukomoana tu kwa kuwa mtu hakubaliani na wewe.

Kiujumla Tendwa ameongea kama mlezi wa vyama ila kama kada wa chama chake pia ambacho ndicho kinamuweka mjini. Kwani kwa sura nyingine kukubaliana na uamuzi wa Mbatia ni kukubaliana na tuhuma kuwa Mbatia ni CCM B. Kitu ambacho kwa sasa strategically CCM haitapenda ijulikane hivyo wakati ikiendelea na utafiti wa kuua nguvu ya CDM kabla ya 2015.
 
Kasema kitendo cha kufukuzana si cha kiungwana kashauri vikao vya vyama vitumie busara vitumike kukosoana kwa nia ya kujenga na si kukomoana. source redio clouds.
Tendwa hana haki yoyote kuingilia katiba ya vyama, kazi yake ni usajili na siyo kuongoza vyama vya kisiasa, anaweza toa ushauri kama Mtanzania yeyote lakini si kuingilia katiba na maamuzi ya vyama, mbona hajaingilia kujivua gamba kwa CCM? Busara ni wazi itumike na yy kama lilikuwa jukumu lake basi angeingilia mapema haya mambo maana yaliandikwa sana katika vyombo vya habari kabla ya kufikia hapa, nategemea pia kama ni jukumu lake aingilie pia mambo yalivyo CUF ili yasifikie ya NCCR.
 
WANA-JF;
Kupitia Redio-Fm, Nape Nnauye amesema kwamba wao kama CCM wanamkaribisha Kafulila. Na watakapofuata utaratibu na akipita ataruhusiwa kwenda kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Kigoma Kusini.
 
Je huyu kafulila alikuwa na maana gani haswa?
Je ana maslahi ya wanajimbo lake moyoni kweli au ana agenda ya siri?
 
Kwa mujibu wa habari Tbc 1, kafulila amedai pamoja na kwamba amefukuzwa na chama yeye bado ni mbunge halali.
 
punguza spidi ya kutaka kuwa wa kwanza kuleta habari hadi unasahau vitu muhimu. Radio za fm ziko nyingi. Ila nape nae aangalie asijeporwa nafasi yake na mgeni
 
Kama ni wana Kigoma kwanini ulienda na kumpigia Magoti Mwenyekiti wa Chama; yeye sio Wana Kigoma... Ungepanda gari Mpaka Kigoma na Usingeenda Mahakamani kulilia kiti ungeenda mpaka KIgoma na kuitisha mkutano na kulia na kupiga magoti kwa wananchi hao; na sio CCM B James Mbatia-- anakuonea wivu kweli anakuona unavyodundika na Zitto; Zitto Mgojwa uko pembeni Zitto anakunjwa chai Uko pembeni... alikuwa anakuonea wivu kweli.... sasa kakupata...
 
Sasa kama anajua kwamba bado ni mbunge, kwa nini alisema kuwa alikuwa anawalilia wananchi?
 
hata wale madiwani wa arusha walikuwa na kauli hizo baada ya kumwagwa
 
Hata Rostam pamoja na kutangaza apema kujiuzulu ubunge ilichukua siku kadhaa Tendwa na Spika kupata taarifa hiyo.
 
Back
Top Bottom