Nape: Msimamo dhidi ya ufisadi hautabadilishwa

Ccm inaongoza kwa kuwa na viongozi waongo na wasioeleweka kuanzia kwa mwenyekiti mpaka balozi wa nyumba 10
 
Kwanza U-DC nlishaacha siku nilipoteuliwa katibu wa NEC. Kwahiyo kupanda majukwaani kwasasa si tatizo.
Kuhusu nilichofanya Masasi, sijisifu lakini nenda leo au tafuta mtu aliyeko Masasi atakuambia, na hakika si rahisi kunisahau pamoja na kukaa miezi nani tu.
Maneno gani yanageuzwa? Hata hiyo siku ya kikao na wahariri, tulielezea kilichotokea,tatizo watu wanachukua maneno ambayo hayajatolewa ufafanuzi, na jana nimesisitiza UAMUZI na MJADALA WA NEC VIME REKODIWA kwa MOVING kamera na ndo maana wanaosema ni maamuzi ya Nape na Chiligati si wajumbe wa NEC. Bado nashauri subirini tushindwe kuwafukuza....

Nape, nakupongeza kuwepo ktk nafasi hiyo amabyo inakupa popularity impact, lkn mm kama ndugu yk nakushaurini kuwa, kama mnaamua kufanya bora mngefanya wakati ule, lkn kwa sasa nashauri kuwa kusameheana katika mambo kama haya ni kukijenga chama kuliko kuendeleza migogoro, kuwafukuza sababu ni maneno ya watu, wakisema na Nnauye afukuzwe sababu ya kufumaniwa na mke wa mtu wakai ushahidi haupo? nakushauri tu amueni kuwa pamoja nakuacha ugomvi, mkijua kuwa hakuna msafi duniani kila mtu anamakosa, kwakufnaya hivyo jamii itasema yake lkn mwisho mtakuwa timu moja na mafanikio yataonekana,
kitu kingine nashauri kuwa makundi ktk chama ni janga, kwani kila kundi linasema yake nakuonekana linasema kweli, ukijua kuwa uongo na ukweli vinatenganishwa na mstari mwembamba sana huwe utofautisha sn.
jambo lingine, ndugu ningeomba chama kishike hatam kuondoa rushwa kikianzaia mipakani na airport, chana kifundishe vijana wakipewa vifaa maalumu kuwtega wara rushwa, vifaa hivyo kama kalamu za camera, cha zaidi, ukiwa kama msemaji wa chama, ukae kwenye kuondoa kero zinazo semwa humu kuliko kujibu na kuacha watu waendelee kuteseka. Elewa kuwa siyo dereva tu atalaumiwa kwa mwendo mbaya hata conda anahusika kuleta ajari kwa abiria wasio na hatia.
 
Funika kombe mwana haramu apite lakini kwa CCM hapiti anaendelea kuwatafuna watanzania...na swali letu kwa Nape ni kamati kuu haja kaa bado au siku 90 hazijaisha au alisema miaka 90 hatukumwelewa watanzania nape huna jeuri ya kuwavua magamba wakongwe wa CCM maana hata wewe ni sehemu ya walionufaika na rushwa....
 
View attachment 74040
Hili la msingi kabisa wameshindwa itakuwa swala la kompyata mashuleni sahau....bado huja pita mashuleni kuna shule moja hapa Bunju B nilipita juzi nilishangaa kweli ni Dar lakini watoto wana kaa chini na hakuna sakafu halafu wana leta propaganda za kipumbavu eti wataleta kompyuta....
Hawa jamaa (ccm) na kinara wao ni opportunists. Hawajali wananchi wana matatizo gani ya msingi. Wanachojali ni namna gani wanaweza kupata umaarufu kupitia utendaji wao bila kujali impact kwa wananchi. Ndiyo maana siwezi kushangaa kusikia eti serikali ya ccm imenunua laptop kwa ajili ya wanafunzi wote nchini na kuacha hospitali hazina madawa na vitendea kazi muhimu. Usanii wa aina hii unafanana sana na ule wa mkuu wa nchi kukaa kwenye mkeka na kujifanya anamsikiliza kwa umakini mlemavu. Anachotafuta hapo ni kuonekana "mtu wa watu" na siyo kumsaidia mlemavu.
 
Wasihangaike na kujivu gamba. Hawana uwezo huo. Hebu waanze tu kidogo na ule ufisadi wa jengo la UVCCM. Mbona kimya. Kimya kabisa. Wakaja kwa maneno mengi, kumbe Wasaka Vyeo. Sasa tuna Wasaka tonge na Wasaka Vyeo. CCM na Ufisadi ni sawa na binadamu na ngozi yake. Unatenganishaje bila huyo binadamu kufa. Ukishapambana kuuondoa ufisadi maana yake umeingia kwenye vita tamu ya kuiondoa CCM.

Ndiyo maana tunasema maadui wetu sasa ni watano, wale wa asili watatu na wawili ha walioongezeka, CCM na ufisadi ambayo ndani yake kuna rushwa. Wote watano wanahusiana sana na kutegemeana.
 
Ndugu Zitto ziarani Ulaya

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ndugu Zitto Zuberi Kabwe ameanza ziara ya kikazi nchini Ujerumani ambapo atahudhuria na kuhutubia Mkutano mkubwa wa masuala ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Africa. Mkutano huo "Economic Conference: Commitment to Africa Initiative" utafanyika Jijini Berlin kuanzia tarehe 9 – 11 Desemba 2012 na umeandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Ujerumani.

Katika ufunguzi wa Mkutano huo ndugu Zitto atatoa mada kuhusu mgongano wa maslahi kati ya Kampuni binafsi na Jamii ambapo ataongelea suala zima la makampuni makubwa ya kimataifa yanavyonyonya rasilimali za Afrika bila kuwajibika kulipa kodi na kuendeleza jamii zinazozunguka shughuli zao. Atazungumzia pia mitaji kiduchu inayokuja Afrika na fedha nyingi inayotoroshwa Afrika kupitia rushwa, ukwepaji kodi na wizi wa rasilimali. Afrika inapoteza zaidi ya dola za kimarekani 583 bilioni kila mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha unaofanywa na makampuni ya kimataifa kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa Afrika. Hata hivyo Afrika inapokea takribani dola za Kimarekani 80 bilioni tu kwa mwaka kutokana na Uwekezaji (FDI) na Misaada (foreign Aid). Tanzania ni moja ya nchi inayopokea misaada mingi kutoka nje na moja ya nchi ambayo rasilimali zake zinatoroshwa na baadhi ya viongozi wake kutorosha fedha na kuzihifadhi kwenye mabenki ya Ulaya kama Uswiss.

Mnamo tarehe 11 Desemba ndugu Zitto atakuwa kwenye jukwaa moja na Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani kuzungumzia namna bora ya kushirikiana kati ya Ujerumani na nchi za Kiafrika. Miongoni mwa mapendekezo ya Zitto ni kuondokana na mfumo wa sasa wa ushirikiano wa misaada na badala yake kuwe na ushirikiano wa kujengeana uwezo ili kila nchi iweze kuhimili maendeleo yake yenyewe.

Katika ziara hii Zitto atakutana na Mawaziri Wakuu wa majimbo ya Nord Rhein Westphalen jimbo ambalo limefanikiwa sana katika vita dhidi ya ukwepaji kodi unaotokana na raia wa Ujerumani kuficha fedha kwenye mabenki ya Uswiss na wa jimbo la Lower Saxony kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ukarabati wa Meli ya Liemba na kujenga mahusiano kati ya Mkoa huu na Mkoa wa Kigoma pia kati ya mji wa PapenBurg na Manispaa ya Kigoma.

Zitto anatarajiwa kutembelea baadhi ya nchi nyingine za Ulaya na kukutana na watu mbalimbali katika kuimarisha mtandao wa kimataifa dhidi ya utoroshaji wa fedha kutoka Afrika (illicit money transfer). Pia atakutana na watu binafsi wenye ujuzi na weledi katika masuala haya ya kupambana na watoroshaji wa fedha. Zitto anataraji kurudi nchini mnamo tarehe 16 Desemba 2012. Kwa namna itaakavyowezekana umma utapewa taarifa kuhusu ziara hii kupitia akaunti ya twitter na facebook ya ndugu Zitto. Pia mada zote atakazowasilisha zitawekwa kwenye blogu ya zittokabwe.com kila itakapowezekana.

Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni anawatakia Watanzania wote kila la kheri katika Sikukuu ya Uhuru wa Tanzania Bara. Utu, Uzalendo, Uadilifu na Uwajibikaji ni silaha muhimu sana za kujenga Taifa lenye heshima na jamii ya watu wenye fursa za kuendeleza maisha yao kwa haki na amani. Tutimize wajibu wetu katika kuijenga Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini
8 Desemba 2012, Dar es Salaam
 
Nimeamua kuja mwenyewe. Nashangaa wakati mwingine maana ni hapa ndo watu walisema Nape kashazibwa mdomo kama vile yale ni maamuzi ya Nape binafsi.
Jana nimewakumbusha tu watuhumiwa na wapambe wao si busara kujifariji kuwa maamuzi yatabadilishwa nje ya vikao, na vikao vyenyewe ni lazima iwe ama NEC au Mkutano Mkuu(Congres) na si vinginevyo.
Kuna hoja hapa eti kwamba Nape anabwabwaja tu, hakuna vitendo, let's be objective,hivyo vitendo ni vipi? Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi haya itatolewa kwenye kikao kijacho cha NEC na si siku 90 kama wanavyojaribu kueleza hapa. Tumelieleza sana hili la siku,WAANDISHI TENA BAADHI ndo walitafsiri siku tisini kutoka kwenye ratiba ya vikao vya NEC ambavyo Dodoma tulikubaliana tentively tunaweza kukutana July ndo wakahesabu na kusema siku tisini. Lakini hakuna kikao kinakutana exactly kwa muda ulopangwa,kuna flexibility.
Ushauri subirini NEC ikutane mtuseme tukishindwa kufukuza.

soma mwenyewe haya maelezo unayaelewa. yaani hata kujieleza vizuri huwezi. hakika hiki chama kinaongozwa na vilaza umeshindwa kupanga hoja vizuri plz take time 2think before u decide. sasa nafahamu kwanini matausi ndo ngao yako. maelezo haya na mtu asiyeenda shule ndo matatizo ya kusoma India.
 
NAPE naamini kabisa ya kuwa wewe ni kijana wa chama tawala unaekubalika kwa watanzania kwa kiasi kikubwa hilo halina ubishi. NINGEFURAHI SANA kama ungetoa ufafanuzi kwa kile kinachoaminika ya kwamba umenyanyapaa kabila fulani mbele ya waandishi wa habari. SIO SIRI hizi taarifa za kunyanyapa kabila fulani zimetushtusha hata sisi ambao tumekuwa tukikuamini ya kuwa wewe ndio kijana pekee ndani ya CCM mwenye kuweza kuvuta kadamanasi (ORATOR)

unanuka unafiki!hata ujisugue kwa dodoki la chuma hautakati tena!
 
Nape tunaomba ufafanuzi wa kauli kama ilivyohapo juu. Au ww jambo kubwa na la maana ni kadi ya CCM aliyonayo Dr. Jambo la kijinga unakomaa. Fukuza hao magamba wenzako tuone kweli unawajali watz sio porojo na elimu yako ya INDIA.
 
Unajua mimi siamini sana katika kuzomea na kuzodoa tu , hivi humu JF hatuwezi kumchukulia hatua yoyote huyu ndugu Nape Nnauye ? namaanisha kama vile kumpa ban ya nguvu ! au labda hata hatua zingine zinazofaa ? Maana ametuongopea kuhusu magamba hali akijua hana uwezo huo ! Analeta hoja bila utafiti mwisho wa siku anaumbuka (rejea hoja ya Hon. Mnyika ) ! Hivi hana hata aibu ! Yaani full uongo , kwani hiyo ndiyo kazi ya katibu mwenezi ?
 
  1. Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
  2. John Samwel Malecela
  3. Philip Mangula
  4. Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali
  5. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
  6. Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
  7. Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina
  8. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa
  9. Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge
  10. Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
  11. Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
  12. Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM)
  13. Rais mstaafu, Benjamin Mkapa
  14. Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete
usimsahau kinana mzee wa meno ya tembo...
Umejaa pumba wewe, sasa wanangoja nini kumvua hilo gamba?
 
Itakuwa hivi - Lowasa mgombea Urais, Chenge waziri mkuu mtarajiwa, Rostam mshauri, Kinana waziri wa wanyamapori n.k., Karamagi usafirishaji -sera kuu ufisadi kwa kwenda mbele!
 
Nape,

Suala la Lowassa ni kubwa na kusema ukweli liko nje ya uwezo wako. Mimi ningependa kama ungeshughulikia suala la afya yako, kwa kufanya mazoezi na kupunguza hiko kitambi.
 
Itakuwa hivi - Lowasa mgombea Urais, Chenge waziri mkuu mtarajiwa, Rostam mshauri, Kinana waziri wa wanyamapori n.k., Karamagi usafirishaji -sera kuu ufisadi kwa kwenda mbele!

ikitokea hivyo naanzisha kundi la kigaidi ama nijiue kama nitawashindwa kuwamaliza kuliko kushuhudia nchi ikiteteketea kwa kiwango kile..
 
Kwanza U-DC nlishaacha siku nilipoteuliwa katibu wa NEC. Kwahiyo kupanda majukwaani kwasasa si tatizo.
Kuhusu nilichofanya Masasi, sijisifu lakini nenda leo au tafuta mtu aliyeko Masasi atakuambia, na hakika si rahisi kunisahau pamoja na kukaa miezi nani tu.
Maneno gani yanageuzwa? Hata hiyo siku ya kikao na wahariri, tulielezea kilichotokea,tatizo watu wanachukua maneno ambayo hayajatolewa ufafanuzi, na jana nimesisitiza UAMUZI na MJADALA WA NEC VIME REKODIWA kwa MOVING kamera na ndo maana wanaosema ni maamuzi ya Nape na Chiligati si wajumbe wa NEC. Bado nashauri subirini tushindwe kuwafukuza....

Mh. N. Nauye pole sana na majukumu, naomba kuuliza na mimi nipate ufafanuzi, kuna wkt mh Lowassa aliwahi kunukuliwa akisema mwenyekiti wenu anaujua mchongo mzima wa richmond which implies naye ni sehemu ya dili, vp naye mtamfukuza au ndo mtaonea hao wachache tu? Na pia vp mh mkapa naye mtamtimua chamani? Orodha ya watuhumiwa ni ndefu so hatutatarajia watu 3 tu kufukuzwa, pia zipo vumi mbalimbali juu ya uadilifu wa riziwani kwa msingi huo mtihani ni mzito sana kwa upande wenu. Nashukuru kwa ufafanuzi mh Nauye.
 
Back
Top Bottom