Nape live on Star tv: Anazungumzia uchaguzi wa CCM

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
531
225
Katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye yuko live Star tv anadadavua kwa makini taratibu za uchaguzi ndani ya CCM.
 
watu mna moyo yaani unapoteza muda wako kumsikiliza nape..angalia asianze kuporomosha matusi maana hawachelewi.
 
Hivi sauti ya Nape huwa haiwezi kupungua kwa namna yoyote ile? Jamaa anaongea kama yupo kwenye jukwaa la propaganda
 
nape kuna tetesi zinasema mwenyekiti wa uvccm lazima atoke zanzibar je kanuni za uchaguzi sinasemaje?
 
shida ya chama cha mapinduzi ni kujifanya hawaoni na wanadhani wakifanya hivyo basi wanaweza kufanya watu wengine wasione. shida inakuwa kubwa kama hata wanapokuwa na vikao wanashindwa kujadili misingi ya matatizo ya chama kwa sababu tayari wamejifanya hawaoni.

Chama kimekosa uwezo kwa sababu ya hofu ya mijidala. wanachama waliojaribu kuona matatizo ya chama walitishwa na wenye madaraa ndani ya chama, kwa sababu mara nyingi wenye madaraka wamekuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya chama ama kwa kutenda ndivyo sivyo au kwa kutokutenda yaliopaswa kutendwa, unapojadili matatizo ya CHAMA NI SAWA NA KUJADILI UDHAIFU WAO.

HAYA YOOTE NI KWA SABABU YA NGUVU YA FEDHA YA WALIOFANIKIWA KUKITEKA CHAMA. UKIJUA HIVYO UTAFAHAHAMU KUWA UCHAGUZI WA CCM NI NAFASI YA WALIO NA FEDHA KUJIPANGA KIMKAKATI KUELEKEA KWENYE MALENGO WALIOJIWEKEA. HAKUNA WAKUZUIA NDANI NA NJE YA CHAMA, SABABU ZIPO WAZI CHAMA KIMETEKWA NA NGUVU YA FEDHA BADALA YA NGUVU YA UMMA
SIDHANI KAMA KUNA MTU ANAWEZAKUOMBA USHAHIDI WA HAYA ISIPOKUWA VIPOFU NA VIZIWI WAKUJITAKIA WA HALI HALISI
 
Mkuu unataka magamba wafe mara ngapi? Mbona tayari wanaendelea kuzikwa na M4C.

Amesema wanajipanga kwa umakini wasije kuanguka 2014 & 2015 halafu wawe wapiga kelele!!!

Kuna mchangiaji mmoja (Ruhuza) kamtahadharisha wajitahidi kurudisha vijana chamani maana kiuhalisia asilimia kubwa sana wamekimbilia CDM.....jambo ambalo mwenzake (katibu wa ccm Kinondoni) kalipinga kwa nguvu akidai yeye anafahamu hali halisi mitaani kwamba vijana karibu wote bado ni ccm!!! Maajabu ccm hayaishi
 
Sikio la kufa halisikii dawa!
 
Ccm ni chama kizuri na sera zake ni nzuri tatizo ni baadhi ya watu wake
 
Back
Top Bottom