Nape kauli zako na vitendo havioani ni kama Lila na Fila visivyotangamana

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Nape,
Siku ya jana tarehe 06 Machi 2023 nimekusikiliza kwa kituo kila hoja uliyokuwa unaijibu katika kipindi cha Dk. 45 ambapo ulikuwa unatoa fafanuzi kwa masuala kadha wa kadha.

Kwanza nikupongeze kwa kutimiza mwaka mmoja kwenye wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Ni mwaka mmoja wenye matukio mengi chanya na hasi kwenye utendaji wako.

CHANYA
  1. Kufungullia vyombo vya habari vilivyofungiwa kupitia sheria ka damizi.
  2. Ongezeko dogo la uhuru wa maoni
  3. Serikali kushirikisha wadau wa utangazaji kwenye mchakato wa marekebisho ya sheria inayohusu vyombo vya habari.
  4. Tanzania kuwa mwenyekiti wa eneo la mawssiliano kwenye Jumuiya ya Madola
  5. Uwezo na uamuzi wako wa kuinterract na wananchi kupitia social platforms zako na wizara.
HASI
  1. Kushindwa kudhibiti ongezeko holela la gharama za mitandao hususan internet.
  2. Kusimama upande wa service providers kwa kuwatetea wazi wazi bila kuweka uwiano au hata kupokea maoni ya walaji
  3. Katika rasimu ya marekebisho ya sheria ya vyombo vya habari, wizara imeshindwa kuwatambua wachora vibonzo na watu wa maudhui ya picha jongefu (animators) kwenye sheria hivyo wataendelea kupambana na hali zao. Yaani hawalindwi kisheria.
  4. Kutokuwa mkweli kwenye issue ya kuwsshtaki wanaoikosoa serikali hususan tukichukulia jaribio la hivi karibuni kule Mbeya ambapo Mdude_Nyagali alikamatwa na kuzuiwa polisi kwa tuhuma za kutoa contents ambazo pia zinamhusu kiongozi aliyeasisi slogan ya Bao la Mkono ambapo kama siyo wasamaria kupiga kelele basi Mdude angekuwa historia leo.
  5. Serikali kuwashughulikia watumishi wsnaofichua maovu sugu ndani ya utumishi wa umma. Mfano yule mtumishi aliyefichua matumizi mabovu ya MRDT zilizoisha muda wake kwenye hospitali ya umma.
  6. Manunuzi ya mtambo ws kudukua mawasiliano ya wananchi kama ambavyo viongozi mmekuwa mkutamba kuwa yeyote atakayekosoa kwa lugha kali atakamatwa na kushughulikiwa.
Hayo machache yanatosha kukukumbusha dhima ya nini sisi wenye nchi tunatarajia kutoka kwa nyie waajiriwa wetu ambao mmejipa mamlaka ya HATIMA ya Tanzania mikononi mwenu bila kuzingatia Utawala Bora.

Jana kwenye maojiano, sisi tuliosomea Cuba kuhusu body language tulikuona ulianza kuhamaki na kutufokea wasikilizaji ulipoulizwa swali la uhuru wa maoni na serikali kuwashughulikia wanaokosoa.

Pia napenda kukuelewesha zaidi kuhusu contentwise na privacy.

  1. Nakubaliana nawe kuna contents hazifai kuwa viewed kwenye public kama vile porno, marehemu ktk mauti yake, lugha za matusi na vifananizi vyake
  2. Kwenye lugha za matusi kunahitajika maelezo ya kuelewana hapa. Wewe kama kiongozi kumbuka kuwa uongozi ni eneo ama jukwaa linalokuanika katika jamii ambapo kila tabia yako itamulikwa. Unapaswa kujidhibiti kauli na mwenendo wako kwa sababu pamoja na kwamba hatuna kiongozi malaika lakini ofisi siyo eneo la kuendelea uhuni na tabia mbaya ambazo labda alikuwa nazo kabla ya uongozi. Kama vile kutoa lugha chafu, kutoka na wake za watu, ulevi uliopindukia na kadhalika. Kutukataza kutorekodi matusi kutoka kinywani kws kiongozi ni kulazimisha matumizi mabaya na kukosa weledi kwenye ofisi za umma.
MAONI YANGU
  1. Mtambo wa kufuatilia mawsiliano ujikite kwenye kuimarisha usslama wa Taifa hususani mienendo ya kigaidi, ujambazi, wizi wa mitandaoni na fananizi vyao.
  2. Serikali izingatie Ibara za katiba yetu inapokuja na mipango ya kutunga ama kuboresha sheria yeyote.
  3. Mwandishi wa sheria au idara ya Chief Draftsman kuhamishiwa ofisi ya Katibu wa Bunge kwa sababu mpaka leo serikali imelipora Bunge mamlaka na haki yake ya kutunga sheria.
Naamini wanaJF wanalo la kukushauri na kukukosoa kama uzi unavyojieleza
 
Hivi kumbe yule mtumish wa hospital walimfanyia jambo,dah.

Ukiwa mwema unaonja joto ya jiwe bongo
 
Well
 
Back
Top Bottom