Nape: Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, lakini...

Kageuka

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
241
59
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

Tuhuma hizi zimechapishwa leo na baadhi ya vyombo vya habari na hasa TanzaniaDaima zikidai "Chadema wameibua unaoitwa ufisadi wa Mwakyembe wa kuipa CCM zabuni ya kupanua bandari".

Kiongozi huyo wa Chadema alikwenda mbali kwa kuishutumu Wizara ya Uchukuzi na Waziri wake Dokta Harrison Mwakyembe kwa madai ya kukiuka taratibu na kutoa zabuni ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa CCM kinyume na taratibu za manunuzi jambo ambalo ni uongo.

Ukweli ni kwamba Kampuni ya Jitegemee Trading Company ni mali ya CCM, na pia ni kweli kuwa kiwanja kilichotajwa ni mali ya CCM kilichokombolewa kutoka zilizokuwa mali za SUKITA ambayo pia ilikuwa kampuni ya CCM.

Lakini TPA na Jitegemee mpaka sasa hawajaingia mkataba wowote. Eneo hilo limeombwa na wawekezaji wengi wakiwemo TPA na masharti waliyopewa waombaji wote ni kuleta mapendekezo ya mipango yao ya kibiashara kabla ya kufikia uamuzi wa nani anawekeza kwa ubia na Jitegemee kwenye eneo hilo.

Wanachokiita wenzetu wa Chadema kuwa ati ni zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Jitegemee na Mamlaka ya Bandari ni barua ya TPA kwenda Jitegemee wakiomba ridhaa ya kushirikiana kuliendeleza Eneo la kampuni hiyo ya Jitegemee lenye ukubwa wa zaidi ya ekta 100, katika mfumo wa ushirikiano yaani "Joint Venture" kupitia utaratibu wa PPP (Public, Private Partnership) jambo ambalo ni la kawaida sana kwani linafuata utaratibu na sheria zote husika.

Kama nilivyokwisha kusema Chama Cha Mapinduzi kinamiliki Kampuni ya Jitegemee, na kwamba pamoja na umiliki huo, kampuni hiyo imekuwa ikitekeleza shughuli za uwekezaji kwa muda mrefu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi kwa ujumla.

Tunatambua kuwa Chadema kwasasa wanapitia wakati mgumu sana kisiasa kutokana na kuanza kuvuna walichopanda kwa muda mrefu katika siasa za nchi yetu.

Lakini pia tunatambua tabia ya viongozi wa Chama hicho ya kudandia kila gari linalopita bila kujua linakokwenda kwa kugeuza kila kinachofanyika nchini, ilimradi hakifanywi na wao basi ni haramu.

Hata hivyo mazingira haya wanayopitia hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kutofautisha barua ya maombi ya kushirikiana kuendeleza eneo na mkataba!.-

Aidha mazingira wanayopitia kwasasa hayawapi uhalali wa kuwa wavivu wa kufikiri kiasi cha kushindwa kujua kuwa kinachofanyika ni mawasiliano ya awali sana ya kusudio la kuendeleza eneo husika na hakuna taratibu zilizokiukwa.

Umbumbumbu wa aina hii unatia mashaka sana juu ya uwezo wao wa kufikiri na kupambanua mambo. Jambo moja wanaloonekana kulimudu ni uwezo wao wa kutunga uongo na kupanga machafuko. Na hii ndio siri ya watanzania kuwakataa kila kukicha na ndio siri ya kufa kwa chama hicho, kwani njia ya muongo ni fupi.

Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotaka kutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo wa Chadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao. Kutumika huku kunasukumwa na kiu yao ya kushika dola kwa gharama yoyote. Watanzania tuwapuuze na kuwaepuka.

CCM inachukua nafasi hii kuipongeza Wizara ya Uchukuzi kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya chini ya Dr. Harrison Mwakyembe hasa ya kuongeza ufanisi kwenye bandari yetu ya Dar es salaam. Tunawataka wasikatishwe tamaa na mafisadi wachache, wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye, ---
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
04/04/2013
 
Haishangazi kauli ya kinyoya kama hii; lakini ni vyema amekiri kuwa kuna upuuzi unaendelea na CCM kupitia kampuni yake.

Labda ingejulikana ni CCM pekee yenye haki ya kuwa na makampuni ya kushindana kwenye tenda maana neno "vested interest" kwa nafasi ya kuwa chama tawala inawahusu wengine siyo CCM.

Wengine wanabeza vyama vya upinzani kutokuwa na Media zao kama Radio, TV na magazeti; wanasahau kuwa hata hilo kuna mwenye dola mpaka apende.

Nashukuru sana kwa taarifa ya Nape maana alitarajia CHADEMA isimamishe shughuli zake kwa mizengwe yake. CHADEMA itaendelea kuiua CCM kwa maslahi ya wananchi na nchi hii hata kama jua likifa
 
Tanzania Daima mtakosa wanunuzi kwa kuendelea kuutangaza udaku wa Chadema ambao unazidi kupamba moto siku hadi siku huku umaarufu wa chama ukiendelea kuporomoka kwa kazi kubwa!
 
huyu jamaa yupo? nilifikiri kabakia china kucheki fursa za uwekezaji / ujasiliamali..
 
Si ni CCM hii ilokuwa inakanusha kwa nguvu zote kwamba hakuna ufisadi nchini hapa? sasa nape atueleweshe ni mafisadi wapi hao wanaowatumia CHADEMA?

Umbumbumbu mwingine ni wakujitakia.
Lini kuna mtu aliwahi kutoa kauli kuwa nchini hakuna ufisadi? Ukishindwa kujibu hili basi jua kuwa wewe ni MBUMBUMBU unayeongea vitu usivyovijua...
 
Tanzania Daima mtakosa wanunuzi kwa kuendelea kuutangaza udaku wa Chadema ambao unazidi kupamba moto siku hadi siku huku umaarufu wa chama ukiendelea kuporomoka kwa kazi kubwa!

Mkuu, hawawezi kukosa wanunuzi. Unajua magazeti ya udaku ndio yanapendwa zaidi, kwahiyo litanunuliwa sana. Ila swali ni je, nani atalinunua na ujumbe unaoandikwa utaleta impact gani?

Sasa hivi kusoma habari za Tanzania Daima ni sawa na kusoma zile hadithi za Uwazi. Unasoma na kuiacha hapohapo kama movie tu...
 
sisi tulikwambia CCM ina wenyewe akatubishia -- haya tupe mrejesho juu ya wale MAFISADI uliojigamba utawatimua kwa aibu ndani ya chama baada ya siku 30; unafikiri tumesahau?
 
Mwakyembe! Kwani kuweka Bandari kavu ni lazma katika eneo la CCM? TPA ina maeneo mangapi why sukita only? acheni Ufisadi eti Pertinership? safari hii mpaka kitaeleweka....
 
Tanzania Daima mtakosa wanunuzi kwa kuendelea kuutangaza udaku wa Chadema ambao unazidi kupamba moto siku hadi siku huku umaarufu wa chama ukiendelea kuporomoka kwa kazi kubwa!

naona watoto wa Lumumba mewahi kuiweka na kuirukia hii thread, tutawabana eti JITEGEMEE
 
Nape, tatizo unakurupuka bila kujua nini kinaendelea ,

1. Ni kuwa kwenye kikao cha mamlaka ya Bandari kilichoketimwezi Machi tayari walishatenga fedha kiasi cha shilingi bilioni kumi za kitanzania kwa ajili ya kuwalipa CCM na baadhi ya wajumbe walipinga sula hilo kwa hoja kuwa hapakuwa na tenda wala utaratibu uliofuatwa ili kuipatia kampuni hiyo ya CCM tenda , kampuni hii inasimamiwa na Peter MAchunde, Sam Mapande et al, na ndio inajenga ukumbi wa kisasa kule Dodoma ( Jitegemee)

2. Chadema , haiwezi kukaa kimya tena mpaka yatokee yale ya Deep Green , Tangold na wenzake ambao unawajua vizuri, sasa kila hatua itafuatiliwa kikamilifu kuelekea 2015 kwani Chadema wanajua kuwa tangu 1995 mmekuwa mkijichotea fedha za walipa kodi kwa ajili ya chaguzi kama ifuatavyo,

1995 ......Zimbabwe na Malaysia kwa IPTL .....Waliofanikisha dili hilo ni Marehemu Kolimba na Abdalah Kigoda.

2000....... Aggreko, Wartsila, Barrick Gold et all

2005....... BOT kupitia Tangold, Deep Green, Meremeta, wahusika wakuu humu walikuwa Chenge, GRey Mgonja,IMMA Advocates ,et all

2010...... Elections mnajua mlivyochota Hazina, zikaenda Canada kuchapisha mabango, hamkulipia kodi magari bandarini nk.......

2015 ...... Mmeanza na Bandari, Mikataba ya Kichina 17 etc


Yapo mengi nafikiri ni suala la muda tuu.....
 
Back
Top Bottom