Nape amung'unya majibu na kutupia lawama Chombo cha Habari. Ni baada ya kusema atawashughulikia wa mtandaoni kuhusu Makamu Rais

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waliotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda

Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.

Akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alitangazwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?

Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilichokuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani

Kiuhalisia ukiuliza fulani yupo wapi, ukajibiwa yupo sehemu fulani, kisha ukakataa kwa kusema hayupo huko, weqe unayekataa ndio unatakiwa utuambie yupo wapi na ushahidi utupe.

Lakini ushahidi wenyewe usiwe yule aliyeniambia fulani yupo sehemu fulani aliwahi kunidanganya kabla, huo kwangu sio ushahidi usio na shaka.

Kama ni suala la ugonjwa, tuambie alilazwa hospitali gani lakini sio kelele tu, ambazo kwangu naona zinakuwa motivated na several other factors.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda

Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.

Hapo ndio balaa lilipoanzia, akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alikuja kuwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?

Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilikuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani

View attachment 2841073
Anazingua nae jambo analifanya kama personal issue serikali ina msemaji rasmi akubali aliteleza!
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waliotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda

Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.

Akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alitangazwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?

Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilichokuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani

View attachment 2841073
Huyu anatakiwa afukuzwe kazi mara moja kwa unafiki uliopitiliza

Mbona taarifa zingine alikuwa anaelekeza habari kuwa 'censored'? Uvumi uliovumishwa umetokea ndani ya CCM na serikali wenyewe kisha wakapewa wapinzani kuropoka hadharani maana walikuwa wakisema wana taarifa kutoka 'reliable and credible of high placed officials' kwamba hicho walichokisema ndicho kilikuwa kinaendelea mpaka wakaanza kujipangia nani atakuwa makamu (wakataja majina). Hata walitajwa majina hawajawahi kutoka hadharani kukanusha kuhusu nia ya wao kurithi kiti.

Waliovumisha hawastahili kutolewa kafara (scapegoat) kwa lengo kushindwa kutimia (failed mission)

Case Study ya hayati JPM inawabeba kwa kuwa serikali ilionesha tabia hii iliyojirudia kwa hiyo wanaotuhumiwa wana 'benefit-of-doubt' ya kudhaniwa wamevunja sheria ya mitandao wakati wawezeshaji walikuwa viongozi wa chama na serikali akiwemo waziri mwenye dhamana ya habari.
 
Tatizo lilianza 2020 pale Shujaa Magufuli alipotuchagulia Wabunge na sasa hayupo!
Aliwachaguliaje kama sio unafiki tu unataka kutembea na upepo? Alienda kwenye vituo vya kura na kuwapigia kura? Kama sio aliwachaguliaje wabunge ambo nyie wenyewe ndio mliwaingiza?

Mfumo uliopo ukikinzana na rais aliyepo madarakani ama wanakutengezea kesi, kifo au zamu inayofuata hautapendekezwa kugombea. Je, nani hapendi kula kodi za wananchi wa Tanzania wajinga waoga wa kuhoji na kuwawajibisha viongozi?

Bunge pekee ambalo lilijaribu kujenga 'benchmark' ya mhimili unaojitambua ni la hayati Samuel Sitta tu ndio maana hata kifo chake kina utata mpaka leo
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waliotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda

Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.

Akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alitangazwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?

Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilichokuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani

View attachment 2841073
Kuna shida kubwa mahali fulani, tatizo dogo kama hili kweli liisumbue Serikali?
 
Aliwachaguliaje kama sio unafiki tu unataka kutembea na upepo? Alienda kwenye vituo vya kura na kuwapigia kura? Kama sio aliwachaguliaje wabunge ambo nyie wenyewe ndio mliwaingiza?

Mfumo uliopo ukikinzana na rais aliyepo madarakani ama wanakutengezea kesi, kifo au zamu inayofuata hautapendekezwa kugombea. Je, nani hapendi kula kodi za wananchi wa Tanzania wajinga waoga wa kuhoji na kuwawajibisha viongozi?

Bunge pekee ambalo lilijaribu kujenga 'benchmark' ya mhimili unaojitambua ni la hayati Samuel Sitta tu ndio maana hata kifo chake kina utata mpaka leo
Sikujua kwamba hujui Siasa kwa kiwango hicho 😂😂

Mungu wa mbinguni akubariki
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema yeye atawashughulikia wale waliotangaza Msiba mtandaoni wa Makamu wa Rais baada ya Makamu kutoonekana kwa muda

Anadai sio kila jambo lazima lisemwe hivyo kwa wakati ule hakukuwa na sababu ya kusema alipo Makamu wa Rais. Anaendelea kudai kuwa ilipotokea haja ya kusema, Waziri Mkuu aliongea.

Akaulizwa ilishawahi kutoa hali kama hiyo kwa Rais Hayati Magufuli na Waziri Mkuu aliongea ila baadaye Rais alitangazwa amefariki. Hivyo haoni kuwa Watanzania wameng’atwa na nyoka na hivyo kijiti kikiwagusa wanashtuka?

Badala ya kujibu swali akaanza kutupia lawama Chombo cha Habari kilichokuwa kinamuhoji akidai anashangaa sana kwamba kinataka kuhalalisha Watu kujitangazia msiba iwapo Kiongozi haonekani

View attachment 2841073
Bumunda ameyatimba asianze kutafuta mchawi
 
Back
Top Bottom