Naota nadanganywa

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,194
Wapenzi wa JF, ni miezi sita kamili tangu Mamsapu wangu apate ajira katika kampuni moja ya umma hapa jijini Dar. Siku tu ya kwanza amekwenda kuripoti aliporudi home aliniambia kwamba hajaona kampuni ambayo ina wakaware wengi kama hiyo. Katika miezi mitatu ya kwanza akiwa hapo kila aliyetaka kumletea mazoea mabaya alinipa taarifa. Hata wale waliomkonyeza, waliompa offer za lunch akazitolea nje, waliomtekenya kwenye kiganja wakati wakisalimia kwa mkono, waliojipitisha pitisha ofisini kwake kumtaka mazungumzo yasiyo na kichwa wala miguu, wote hao nilipewa taarifa zao. Mamsapu muda wa kufika nyumbani toka kazini katika hiyo miezi 3 ya mwanzo ilikuwa kabla ya saa 12 jioni.

Baada ya miezi mitatu kumalizika, mambo naona yamebadilika kabisa. Zile taarifa za wakware sipati hata moja (siuji kama wale wakware wote walishaacha kazi ama la!) na wife "amekuwa na kazi nyingi sana" kiasi kwamba muda wa kufika nyumbani ni saa 3 hadi saa 4 usiku, Kazini anakwenda hadi week end na kwenye pay slip sijawahi kuona amepata malipo ya overtime!

Hiki kimya kinanipa wasi wasi kwamba labda sipati taarifa kwa kuwa sasa tayari kuna maridhiano tofauti na hapo mwanzoni. Je ninyi mnafikiriaje juu ya hili???
 
my wife wako teyari kashapata mtu,jiandae na visa zaidi ya hivyo. Ila tatizo halikimbiwi unatakiwa ulisolve. Nalog off
 
Kuna uwezekano mkubwa IKULU imeshazingirwa na maharamia mkuu!Hayo madiliko siyo bure kuna kitu.
 
Sitaki kuzungumza mambo kwa mazoea ila,Jifunze kumwamini mkeo,kama humwamini achana nae,ni kazi ngumu kuishi na mtu usiemwamini,
 
Kuna unalolitafuta una kifua cha kubeba au ndio yaleyale unataka kila taarifa ya kutongozwa mkeo akupe ..............usipende kufukunyua sana
 
usimchunguze we muache tu,ata akimegwa nje haiezi isha
Ushauri wako unanitia machungu sana, hasa ikizingatiwa unatolewa na mwanamke mwenzake. Asije akawa labda ni shoga yako unafanya u-advocate kijanja.
 
Nashangaa kuona comments za wachangiaji wanawake wote zina mfumo unaofanana. Wote pamoja na kutumia maneno tofauti tofauti lakini ujumbe wao ninaoupata ni kunishauri "nimwache amegwe tu kama anamegwa"
 
Ushauri wako unanitia machungu sana, hasa ikizingatiwa unatolewa na mwanamke mwenzake. Asije akawa labda ni shoga yako unafanya u-advocate kijanja.

sio kwamba nam-advoketia,ukimchunguza sana bata humli
 
Nashangaa kuona comments za wachangiaji wanawake wote zina mfumo unaofanana. Wote pamoja na kutumia maneno tofauti tofauti lakini ujumbe wao ninaoupata ni kunishauri "nimwache amegwe tu kama anamegwa"

ee uo ndo ushauri unles uwe tayari kumuacha,otherwise ata umkanye vp ka ni wa kugawa atagawa tu
 
hahahaha......mkuu tayari kuna issue hapo.....hebu muulize imekuwaje usikie kauli yake na vile atakujibu...akikujibu kwa nyodo imekula kwako mazee.
 
Back
Top Bottom