Naona kijana anaanza kuchemka sasa!

Anawaza uraisi kupitia Chadema huku chama chenyewe kiko hoi ile mbaya,nafikiri hayuko serious au labda anaota ndoto za mchana.
 
kila mtu ana malengo yake katika maisha .either uwe muwazi au iwe kwa siri!Zitto ameweka malengo yake wazi!hakuna kosa hapo!

Mkuu hii hapana, nnakukatalia.

Hata kama ana malengo ya maisha lakini si itakuwa yaleyale ya kutaka kufanza biashara Ikulu?

Huyu mheshimiwa bado hajaiva kisiasa na tutofautishe hayati Nyerere alivoanza siasa shuleni na kufika kuanzisha TAA na baadae TANU na kuwa mwenyekiti na huyu mheshimiwa ambae sanasana itabidi arudi CCM ili atimize malengo yake ya maisha.

Suala la kuutaka uraisi linaenda na wito na majukumu makubwa ambayo ni maraisi wachache wa Afrika wamefanya, vinginevyo ni kuwahi kufanya biashara pale ikulu.

Tatizo letu sisi waafrika ni lilelile siku zote na wala hatutabadilika.
 
Mwanasiasa hutakiwi kufikiria, achilia mbali kuongelea, uchaguzi wowote zaidi ya ule ulio mbele yako, kwa sababu unaweza usifike huko kwingine.
Kuwania na kujiandaa kuja kuwa Rais kuna "mkao wa kula" wake wa Kisiasa, au political posturing. Huo "mkao wa kula" kuna wakati hauendani na manufaa ya watu unaowatumikia sasa hivi. Muwania Urais inabidi aanze kujenga mifungamano na nguvu fulani. Katika kujenga hizo alliances kiongozi anaweza kuogopa kutetea maslahi ya watu wake wakati zinatishiwa na hizo nguvu ambazo anajenga nazo mifungamano.

Leo hii Zitto hawezi tena kuwaudhi wachangiaji kampeni ambao atawahitaji siku ya kugombea. Wakitaka kuanzisha mradi Kigoma ambao hauwanufaishi watu wake bali wao wenyewe, Zitto atashindwa ataogopa kuwabana.

Nyingine ya hizo nguvu ni vyombo vya habari. Sasa hivi Zitto anaweza kuanza kujikomba komba kwa Waandishi ili wampambe pambe na kumjengea jina mbele ya Umma. Katika kujali sana taswira yako ndio unaanza kuharibu kazi kwa kutaka kuandikwa vizuri magazetini. Na mara nyingi unaishia kudanganya.

Jambo la tatu, Mbunge ambae anaota ndoto za kuwa Rais kiasi cha kusema hivyo hadharani anaonyesha dharau juu ya kazi yake ya Ubunge. Anaonyesha kwamba hana wasi wasi na kushinda Ubunge uchaguzi ujao. Kama alivyosema, YournameisMINE, akitokea mwanasiasa mzuri atawaambia watu wa Kigoma, jamani eeee, mimi Ubunge ndio ndoto yangu. Mkinipa hii kazi ya huyu muwania Urais nitawatumikia kwa moyo wangu wote, na kwa focus ya kazi hii tu. Watu wa Kigoma wanaweza kusema, kweli, sisi hatutaki mtu ambae yuko bize anajenga alliance za kuwania Urais. Ana dharau ya kusema anafikiria kazi nyingine. Ni watoto wadogo ndio wanaulizwa ukiwa mkubwa unataka kuwa Polisi, Mwalimu, Daktari au Rubani? Anajibu Rais!

Nne, Mwanasiasa mjanja hutangazii adui your next move. Wataanza kujiaanda dhidi yako.

Pia, siku ya kutangaza kugombea hakutakuwa ile suprise ambayo inasaidia kwenye kampeni. Amesha ondoa ile suspense tayari. Hii ni misingi ya kwanza ya sayansi ya Siasa!

Ndio maana tunasema Zitto kachemsha vibaya mno hapa!

Hutakiwi na nani na hiyo ni sheria au kanuni ni ya nani na ilipitishwa lini na wapi?
 
Bora Useme Wewe Kwa Kuwa Nikisema Mimi Ntaambiwa Ni Mzushi Lakini Nakumbuka Kwenye Kikao Cha East Africa Youth Forum Dodoma Mwaka 2001,by The Time Walikuwepo Hebron Mwakagenda,hubert Augustine-wish, Mayunga,nchimbi,nakumbuka Ata Kitila Alikuwepo Bt Sikumbuki Vema,komba Isaya Na Vijana Wengi.mh Zitto Alianguka Kifafa,kwa Kuwa Alivunjika Jino Moja La Mbele Wakati Anaanguka Tulimpeleka Hospitali.walithibitisha Kuwa Kilikuwa Ni Kifafa.najua Sheria Za Nchi Haziruhusu Mtu Mwenye Kifafa Kuwa Rais Sasa Sijui Yeye Ana Mpango Gani.au Amepona Tayari?

....haya sasa bwana Zitto hii ndio gharama ya uliyosema,kabla hata ya kuchukua form tayari umeshakuwa disqualified,kijana umewapatia weapon nzuri sana wapinzani wako na sasa watakuweka in defence mpaka utie akili,yaaani watahakikisha unakuwa offbalance na hata ubunge sijui kama utauweza tena maana itabidi uishie kujibu mambo kama haya ambayo(very disturbing) ....CCM watakufanya issue sasa kuanzia ulafi wa madaraka ,arrogance,afya yako,hujali ubunge wako etc,inabidi uje na strategy nzuri sana kuchomoa hii la sivyo itakuwa death warranty yako kisiasa.
 
Mimi hapa sioni dhambi ya Zitto..kuweka ambition yako ndo iwe dhambi?
Mbona Obama alitoa ambition yake toka akiwa chekechea kuwa anataka kuwa Rais na wenzetu hawakumzonga kama baadhi ya member wachache humu.
 
.....kuna tofauti kubwa sana kati ya mtoto wa chekechea na mwanasiasa wakisema wanataka uraisi,hata hivyo Hillary alijaribu kuileta hiyo issue kwenye debate kama unakumbuka.
 
Mimi nashangaa mnaposema Kijana anaanza kuchemka...kwani kuna wakati alikuwa hachemki? Huyu kijana ni mchemkaji siku zote.
Wanaompa kichwa ni wale wale waliomuharibu Mtikila kwa kumbebabeba hovyo na inawezekana naye alikuwa kati ya waliombeba Mtikilla huyo.
Cha kunishangaza kwenye hii mada ni mchango wa Mwanakijiji aliyeonekana kutoelewa na yeye tofauti ya dreams za maisha na kuwa Rais kama anavyochanganya huyo kijana mwenyewe.
Kwa kifupi ni kwamba huyo kijana ni mchemkaji siku zote, sasa hivi ameleta kichefu chefu tu. Imagine siku moja unaamka nyumbani kwako halafu Rais wa nchi ni Zitto Kabwe.....duhh ama kweli ikulu yetu sasa hivi imekuwa "loose ball" kila mpuuzi atataka kuwa Rais sasa.
 
Binafsi sioni tatizo lolote kwa mheshimiwa zitto kutangaza nia yake ya kuwa Rais hapo siku za usoni. Hakuna bin-adam aliyezaliwa na chapa ya urais usoni. Nadhani ni wivu tu unatusumbua watanzania. Zitto kanyaga mguu twende, songa mbele kijana, usirudi nyuma!!! Tunakutakia kila la kheri katika kukamilisha lengo lako. Unatukumbusha ahadi moja ya mwana TANU: Sema kweli daima, fitna kwako mwiko.
 
Mi naona amejiingiza kwenye nafasi ya hatari.
Amejiweka kwenye nyumba ya kioo, watu watakuwa wanamuangalia matendo yake yote, wenzie wanaotaka kugombea watanakili mambo mazuri anayofanya au hata kuyaziba na kuyachafua. Yeye kwa kuwa hajui ni kina nani na lengo lao nini, atachoka sana kujifunza, kuwakilisha na kufanya mambo mapya mazuri kwa ajili ya kazi anayoitaka baadae.
Si vibaya kusema, ila ni kujitafutia matatizo, na ugumu wa maisha.
Mtu mzima mwenye busara si kila kitu anasema, mengine unaacha yajionyeshe yenyewe kwa matendo,
Kama msemo unavyosema muungwana vitendo.
Zitto anafanya kazi ila pia anaongea sana. Sijafuatilia mahojiano mazima ila pia kuna uwezekano hiyo statement imetolewa katika maelezo mengi mengine ambayo yangepewa uzito tusingekuwa tunajadiliana haya?
manake waandishi (maripota) wetu wa siku hizi nao....
Pia ieleweke kukubalia zitto kila anachofanya si kumpenda wala kumsaidia, inabidi tuwe wakweli na wanasiasa wote wajue kuwa tunawapenda kwa kazi zao tu, si kwa sura wala lugha za kulainishana, wala umri.
ZITTO NI PAMOJA NAO.
 
Kama ni hivyo basi, ajitahidi apewe majukumu kadhaa kama ya uwaziri na kadhalika ili atape uzofu wa mambo kama ya kushiriki "cabinets meetings" au hata ukuu wa mkoa.

Tukumbuke hata senator Obama ni kijana ndio, lakini ameishi ndani ya Congress kwa muda na jimbo lake la Illionis ni kubwa na ametumikia kamati mbalimbali za senate za nchi hio ikiwemo kamati ya mahusiano ya kimataifa kwa muda mrefu tu.

Sasa Mheshimiwa Zitto nae afanye kazi na kamati ya madini na nyingine ambazo atachaguliwa ili apate uzoefu wa kazi na halafu tuone na Kigoma maefanya nini ndio tuanze maneno mengi.

Akae kama miaka mitatu hivi! bado sana kwa sasa.
 
Binafsi sioni tatizo lolote kwa mheshimiwa zitto kutangaza nia yake ya kuwa Rais hapo siku za usoni. Hakuna bin-adam aliyezaliwa na chapa ya urais usoni. Nadhani ni wivu tu unatusumbua watanzania. Zitto kanyaga mguu twende, songa mbele kijana, usirudi nyuma!!! Tunakutakia kila la kheri katika kukamilisha lengo lako. Unatukumbusha ahadi moja ya mwana TANU: Sema kweli daima, fitna kwako mwiko.

Mwanamalundi inawezekana hutaona tatizo kabisa. Kwa sababu kwanza unachanganya mambo. Zitto hakutangaza nia yake ya kuwa Rais. Ameweka hadharani ndoto zake za kuwa Rais. Kabala ya kuendelea unajua tofauti ya haya mawili??!
 
ZITTO KABWE FOR PRESIDENT 2015!

Go Zitto go! fanya ile kitu roho yako inapenda, nia unayo na uwezo unao. Okay?

Mama
 
Mi naona amejiingiza kwenye nafasi ya hatari.
Amejiweka kwenye nyumba ya kioo, watu watakuwa wanamuangalia matendo yake yote, wenzie wanaotaka kugombea watanakili mambo mazuri anayofanya au hata kuyaziba na kuyachafua. Yeye kwa kuwa hajui ni kina nani na lengo lao nini, atachoka sana kujifunza, kuwakilisha na kufanya mambo mapya mazuri kwa ajili ya kazi anayoitaka baadae.
Si vibaya kusema, ila ni kujitafutia matatizo, na ugumu wa maisha.
Mtu mzima mwenye busara si kila kitu anasema, mengine unaacha yajionyeshe yenyewe kwa matendo,
Kama msemo unavyosema muungwana vitendo.
Zitto anafanya kazi ila pia anaongea sana. Sijafuatilia mahojiano mazima ila pia kuna uwezekano hiyo statement imetolewa katika maelezo mengi mengine ambayo yangepewa uzito tusingekuwa tunajadiliana haya?
manake waandishi (maripota) wetu wa siku hizi nao....
Pia ieleweke kukubalia zitto kila anachofanya si kumpenda wala kumsaidia, inabidi tuwe wakweli na wanasiasa wote wajue kuwa tunawapenda kwa kazi zao tu, si kwa sura wala lugha za kulainishana, wala umri.
ZITTO NI PAMOJA NAO.

Kwa vile kaweka lengo lake wazi lakini haina maana lazima aje kugombea nafasi hiyo. Mambo hubadilika na mawazo hubadilika. Hilo la kuangalia matendo yake yote si baya hata kidogo. Viongozi wote wa kitaifa inabidi tuwe tunawaangalia kwa ukaribu iwe wanagombea nafasi kubwa au la. Huo ni wajibu wa jamii nzima.
 
Mimi nafikiri kila mtu ana haki ya kutaka kuwa yeyote katika nchi yetu, ikiwemo urais. Zitto pia ana haki ya kuutaka urais wa nchi yetu au hata Ukatibu Mkuu wa Umoja wa mataifa, mpaka hapo hakuna shida wala mushekeli. Kwamba anaweza au la hilo ni jukumu la wapiga kura kuamua.

Je amefanya a strategic mistake kuweka intentions zake wazi tena mapema namna hii, it is highly debatable.

Mambo mawili muhimu ya kuzingatia kwa mwanasiasa. Kwanza, mwanasiasa hujengwa na kubomolewa kwa maneno yake. Pili, wanasiasa wengi strategic wanazingatia sana kanuni na 3 na 4 za political strategist maarufu duniani anayeitwa Robert Greene. Inasemekana wanasiasa wengi maarufu duniani wanatembea na kitabu chake hiki popote waendapo, kinaitwa "48 laws of power".

Nazinukuu hizi kanuni namba 3 na 4 hapa chini.

Law 3: Conceal your intentions. Keep people off- balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions. If they have no clue what you are up to, they cannot prepare a defence.

Law 4: Always say less than necessary. When you are trying to impress people with words, the more you say, the more common you appear, and the less in control. Even if you are saying something banal, it will seem original if you make it vague, open- ended, and sphinxlike. Powerful people impress and intimidate by saying less. The more you say, the more likely you are to say somthing foolish.

So, kwangu mimi alichosema Zitto sio ujinga lakini pia sio ujanja katika siasa!

So, why are people making a big deal out of it?
 
Mwanamalundi inawezekana hutaona tatizo kabisa. Kwa sababu kwanza unachanganya mambo. Zitto hakutangaza nia yake ya kuwa Rais. Ameweka hadharani ndoto zake za kuwa Rais. Kabala ya kuendelea unajua tofauti ya haya mawili??!

Whatever the case. Bado sijaona tatizo. Yeye ameamua kuwa muwazi katika ndoto zake, ambazo ndizo zinazomshawishi kuwania kiti cha urais. Mbona mdogo wake karume alishatangaza kule zanzibar!!! Mbona hilo hamkulivalia njuga???
 
Viongozi wa CHADEMA kuropoka kwao ni jambo la kawaida sana, msishangazw na hii. Zitto inawezekana anamikakati mizuri, ingawa kulikuwa hakuna haja ya kuanza kuropoka sasa hivi. Mimi niko very curious kumuona kama huo ubunge 2010 atauacha kama alivyosema. Akigombea atadhihirisha kuwa ni another CHADEMA mropokaji, kama mwenyekiti wao Mbowe.
 
Mwanamalundi (na wengine msiiona tatizo),

Kutoona tatizo sio dhambi wala si kosa la jinai. Swali ni kwamba mnataka? au hamlioni tatizo, hamtaki kuliona na hivyo mnadhani kuwa hakuna tatizo!!
 
Whatever the case. Bado sijaona tatizo. Yeye ameamua kuwa muwazi katika ndoto zake, ambazo ndizo zinazomshawishi kuwania kiti cha urais. Mbona mdogo wake karume alishatangaza kule zanzibar!!! Mbona hilo hamkulivalia njuga???

Bado tofauti ipo mkuu.

Mdogo wake Karume alitangaza nia(sio ndoto) hio na akaenda TZ akachukua fomu na akashindwa katika mchujo.

Mheshimiwa Zitto ameongelea kuhusu anayoota kuwa raisi siku moja.
 
Viongozi wa CHADEMA kutopoka kwao ni jambo la kawaida sana, msishangazw na hii. Zitto inawezekana anamikakati mizuri, ingawa kulikuwa hakuna haja ya kuanza kuropoka sasa hivi. Mimi niko very curious kumuona kama huo ubunge 2010 atauacha kama alivyosema. Akigombea atadhihirisha kuwa ni another CHADEMA mropokaji, kama mwenyekiti wao Mbowe.

mtu kutangaza nia ni kuropoka? acheni jamani, tunazidi vipimo. Hivi leo hii mimi mama hapa nikaamua kutangaza nia ya kugombea urais si ndio mtasema natapika maneno na sio kuropoka tena! kwa hiyo mtu kama ana ndoto zake basi anyamaze tu kuwaridhisha watanzania?! duh kazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom