Naona kijana anaanza kuchemka sasa!

...sioni tatizo katika hili la kutangaza mtazamo au target yake,kubwa ninaloona ni yeye kuamua kutupa nafasi ya kuchunguza mwenendo wake.
......Ukichukulia kwa mtazamo wa siasa za kuchafuana nadhani kweli ni tatizo, lkn yeye kaamua kuonyesha kuwa atazikwepa na kujiweka safi muda wote.

Kila la kheri Nyepesi Jiwe! We're watching you.
 
...katika jamii changa Kisiasa uko sawa!

Hata kwenye jamii zilizokongwe kuwa na ambition na watu wakajua ambition hiyo siyo dhambi au kosa la mtu kuonekana "amechemsha". Kuna mambo ya kuficha hasa nafasi zinazohitaji mtu kuearn au kuwa na professional qualification ya aina fulani. Ndio maana ukifanya kazi usianze kujitangaza kuwa unataka kuwa bosi na bosi wako akajua au watu wengine.

Lakini haya mambo ya kuchaguliwa, hata mtoto mdogo anayo haki ya kusema anataka kuwa Waziri Mkuu au Mbunge, au Rais akiwa mkubwa na wakati ukifika. We should not try to silence the sounds of noble aspirations..

Binafsi ningeona watu wamereact vizuri kama wangeanza kutoa ushauri kwa Zitto kwa vile ni "kijana" jinsi gani asiharibu na kama ana mambo fulani si mazuri aanze kuyatengeneza kama vile mtu afyekavyo shamba kuliandaa kwa kilimo. Badala yake watu wameibuka na kumshushua na kujaribu kumfanya aonekane duni. Ni kama wamejaribu kuzima kibatari cha matumaini kwa vile tu kimeweshwa mapema kabla jua halijazama...
 
I don't blame him, i blame the system. Hii ndio system iliyotukuza, system ya kuropoka kabla hujafikiria. I hope sababu Mh. Kabwe anatembelea hapa every often then he will take action and issue statement concern that statement.

He need to focus katika Ubunge first,
 
Hizo siasa za zamani za kuogopa kuonesha ambition yako. Urais siyo ufalme ambao mtu anaogopa kusema anautaka. Alichofanya Zitto ni kujisababishia standard ya pekee na kuangaliwa na watu kwa ukaribu zaidi. Amejiweka ili achunguzwe na kupimwa. Haya mambo ya kudanganya ati watu hawautaki Urais lakini zikitolewa fomu wanakuwa wa kwanza kuchukua tena kwa mbwembwe yamepitwa na wakati.

Kama kuna mtu anafikiria kuwa Rais mwakani na ajulikane hivyo. Kinachonishangaza ni kuwa ilipoandikwa taarifa ya gazeti la Raia Mwema wiki chache zilizopita na watu waliojipanga Urais hakuna mtu aliyesema neno. Wao wenyewe hakuna aliyekanusha kuwa si kweli wanautaka Urais. Soma HAPA

Kama kuonesha nia ya kuutaka Urais ni kosa kubwa na vibaya watu kujua unautaka Urais mbona leo tuna Rais ambaye alijulikana ana utaka? Au kwa vile kasema Zitto kwa vile tunamjua na ni bwana mdogo na kama utani tunamuita "kijana" (kweli ni kijana lakini imetumika with contempt) basi hastahili kusema nia yake?

Urais ni nafasi ya kuwatumikia wananchi wenzako na Taifa lako na hakuna aibu wala kumfanya awe duni ati kwa sababu ametamka kuwa wakati ukifika angependa kufanya hivyo. Tuje na chuki nyingine lakini hizi za kwa vile Zitto kasema lililomoyoni mwake hazina msingi, kwani kuna baadhi ya watu hapa Zitto hawezi kusema lolote zuri, hawezi kufanya lolote jema, na hata kama ana mawazo yoyote basi asiyatoe kwa vile anaweza "kuchemsha" na kuwatibua wataalamu wa JF!

Kwa hili ni ninyi mmechemsha, leteni hoja nyingine, kijana ana haki zote kama Mtanzania yeyote na kama atakuwa na sifa zote za kuwa Rais basi hakuna kitakachomzuia..! and he'll have my full support if he wants to! Na hilo applies to anybody else who would dare to declare his intention na tutaangalia rekodi yake.

Binafsi nampongeza Mhe. Zitto kwa kusema alilonalo, na hivyo kutupa nafasi ya kumuangalia na kumsaidia asianze kufungwa fungwa na mafisadi, na hivyo amejiweka mwenyewe kwenye chekecheo la wakosoaji na tutampima na kumjaribu kama kwa moto na akipita salama itakuwa fahari kumuona akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri yetu! Yes I said it!

slaaaaash ! urais anaouongelea zitto ni kwamba anataka kugombea urais kwa sababu ni plan yake binafsi au atagombea kwa vigezo gani ? ina maana hata kama kuna watu ambao wana policies nzuri zaidi yake na yeye anajua hilo wazi, ndio kusema atimize tu hiyo ndoto yake kwa kuwa ameanza kufikiria tokea zamani ?? huu ni upupu, and i expected you kumtetea !

unatetea hadi vinavyovunda sasa !

Huu ushabiki na ushambenga mwingine haufai !!
 
I don't blame him, i blame the system. Hii ndio system iliyotukuza, system ya kuropoka kabla hujafikiria. I hope sababu Mh. Kabwe anatembelea hapa every often then he will take action and issue statement concern that statement.

He need to focus katika Ubunge first,

unajuaje karopoka bila kufikiria..? tatizo ni kuwa hakufikiria wewe ulivyotaka afikiri! na mtu yeyote anayefikiria wengine wanavyofikiria basi huyo hafikiri bali anafikirishwa (mmh... mwisho ntajikuta natukana hivi hivi)
 
Hata kwenye jamii zilizokongwe kuwa na ambition na watu wakajua ambition hiyo siyo dhambi au kosa la mtu kuonekana "amechemsha". Kuna mambo ya kuficha hasa nafasi zinazohitaji mtu kuearn au kuwa na professional qualification ya aina fulani. Ndio maana ukifanya kazi usianze kujitangaza kuwa unataka kuwa bosi na bosi wako akajua au watu wengine.

Lakini haya mambo ya kuchaguliwa, hata mtoto mdogo anayo haki ya kusema anataka kuwa Waziri Mkuu au Mbunge, au Rais akiwa mkubwa na wakati ukifika. We should not try to silence the sounds of noble aspirations..

Binafsi ningeona watu wamereact vizuri kama wangeanza kutoa ushauri kwa Zitto kwa vile ni "kijana" jinsi gani asiharibu na kama ana mambo fulani si mazuri aanze kuyatengeneza kama vile mtu afyekavyo shamba kuliandaa kwa kilimo. Badala yake watu wameibuka na kumshushua na kujaribu kumfanya aonekane duni. Ni kama wamejaribu kuzima kibatari cha matumaini kwa vile tu kimeweshwa mapema kabla jua halijazama...

Politics ni kama professional nyingine. What he suppose to focus kwa sasa ni ubunge wake. Hata kama ana vision ya kuwa raisi lakini huwezi kuja public ukasema moja plan zangu in the future ni kuwa raisi.

Unapoanza kutangaza kwamba that is your vision then people put your political status in question mark. That is political strategy 101, you can't set a goal of becoming president in public while your not even junior MP.
 
...Kama kawaida, lundo la maneno kwa kitu ambacho kipo obvious!! ama kweli kipenda roho hula nyama mbichi.
...Zitto kachemka, na si suala la siasa za kizamani au za kisasa!! lakini hapa tupo kwenye gumzo na baraza lazima liendelee!!!! MIE PIA NAKUBALI KWAMBA ALICHOFANYA NI SAHIHI....Big Up ZITTO KABWELA, way to GO dude!!
...sio kila kitu,"leteni hoja" huo ni utoto!! unaweza ku-argue for or against kitu chochote hata kama si cha kweli. mara nyingi kwenye mazingira ya namna hiyo lengo linakuwa ni ushindi pasipo kujali facts!! kwa mwendo huo.....kweli tutafika?? hivi kwa akili yako deep deep inside, unaamini kwamba politically, Zitto Kabwela hajachemsha!!?? labda sina hoja......nanawa mikono, yamenishinda!!.

hawa watu utasema ni married couple, wanateteana hata kwenye kusiko ! ujinga mtupu ! nia ya kugombea urais ya zitto inaonyesha dhahiri ni ulafi, sijui anatumia vigezo gani ! na watu wanamtetea kwa huu upuuzi !

Early symptoms are showing folks ! Hapa hamna lolote, ndio wale wale !!!!!!!!!!
Watu wanatia kichefuchefu humu kwa kutetea upuuzi ! wamezidi sasa ! Huwezi ukasema utagombea urais just because una interest ya kugombea urais, bali that comes with events ! Nafikiri hapa ndio mwanzo wa kwa nini watoto wa vigogo wanagombea uongozi, tena wa ngazi za juu !
 
slaaaaash ! urais anaouongelea zitto ni kwamba anataka kugombea urais kwa sababu ni plan yake binafsi au atagombea kwa vigezo gani ? ina maana hata kama kuna watu ambao wana policies nzuri zaidi yake na yeye anajua hilo wazi, ndio kusema atimize tu hiyo ndoto yake kwa kuwa ameanza kufikiria tokea zamani ?? huu ni upupu, and i expected you kumtetea !

unatetea hadi vinavyovunda sasa !

Sidhani kama wewe unapinga yeye kuweka malengo yake hadharani. Unachopinga wewe ni kuwa yeye hafai/ hana sifa. Mambo mawili tofauti kabisa!!
 
unajuaje karopoka bila kufikiria..? tatizo ni kuwa hakufikiria wewe ulivyotaka afikiri! na mtu yeyote anayefikiria wengine wanavyofikiria basi huyo hafikiri bali anafikirishwa (mmh... mwisho ntajikuta natukana hivi hivi)

Politics like other business ina do's zake and don't. Politics sio kwamba watu wanazaliwa nayo, but they learn. There is nothing wrong kwa Zitto kuwa na desire ya kuwa raisi siku moja, however there is something wrong kwa yeye kutoa straight comment kwamba anataka kuwa raisi siku moja. I should understand kama angesema uraisi au uwaziri are still option on the table, and as time ellapse we will see what will come first. That is politics 101, I know you have enough knowledge to read between the lines.

Kufananisha politics na michezo ya kuigiza ndio kunapelekea vyama vyetu vinafanya mambo ya ajabu. Politics ni kama proffesional business, kila neno unalolisema linaweza kuwa hold against you. Sasa Zitto anaweza kutoa any other idea then wabunge wenzie wakaona ana throw punch because he wanna be a president. No matter what he is going to do, that picture kwamba he is doing that to win political spin will stay there. Na hilo ndio swala la kutazama, na sio kwamba i force my idea kuwa part of his idea. Naangalia in the big picture.
 
Hoja huwa na nguvu zenyewe ukiona watu wanaanza kuita watu majina ni ushahidi kuwa hoja zao hazina nguvu wanajaribu kuzilazimisha.. but such are some people..
 
Politics like other business ina do's zake and don't. Politics sio kwamba watu wanazaliwa nayo, but they learn. There is nothing wrong kwa Zitto kuwa na desire ya kuwa raisi siku moja, however there is something wrong kwa yeye kutoa straight comment kwamba anataka kuwa raisi siku moja. I should understand kama angesema uraisi au uwaziri are still option on the table, and as time ellapse we will see what will come first. That is politics 101, I know you have enough knowledge to read between the lines.


sasa huo ndio uzugaji ambao watu wamezoea... nimesoma taarifa yenyewe ya mwanzoni na nadhani inajieleza wazi... tatizo ni kuwa tumezoea kuzungushwa kwa maneno na mtu akija straight talking bado tunataka kuzungushwa! why?

Sasa nakubaliana na wewe kuhusu matumizi ya lugha n.k ndio ujana wenyewe huo lakini kwenye siasa watu kusema vitu visivyo sahihi ni sehemu ya siasa yenyewe... lakini kusema kuwa "amechemsha"! ni zaidi ya dharau..

Kama watu wana chuki cha Zitto, Chadema, upinzani n.k go for it.. lakini si kwenye mambo madogo kama haya! Hapa ndiyo kile cha kujaribu kutengeneza mlima toka kwenye kichuguu cha mchwa..
 
sasa huo ndio uzugaji ambao watu wamezoea... nimesoma taarifa yenyewe ya mwanzoni na nadhani inajieleza wazi... tatizo ni kuwa tumezoea kuzungushwa kwa maneno na mtu akija straight talking bado tunataka kuzungushwa! why?

Sasa nakubaliana na wewe kuhusu matumizi ya lugha n.k ndio ujana wenyewe huo lakini kwenye siasa watu kusema vitu visivyo sahihi ni sehemu ya siasa yenyewe... lakini kusema kuwa "amechemsha"! ni zaidi ya dharau..

Kama watu wana chuki cha Zitto, Chadema, upinzani n.k go for it.. lakini si kwenye mambo madogo kama haya! Hapa ndiyo kile cha kujaribu kutengeneza mlima toka kwenye kichuguu cha mchwa..

bado tu unatetea ?? wee kweli umepotea !
 
Uraisi lengo lake siyo kwa ajili ya ulaji, Uraisi ni kazi ya juu kwa ajili ya huduma kwa watu. mtu yeyote mwenye uwezo siyo kosa kujitosa kuuwania. kwa minajili hii kama zitto anajiamini anaweza kuwatumikia wananchi basi ni jukumu letu kumpima pindi wakati muafaka ukifika.lakini siyo hoja eti kwamba katamka wazi kwamba anautaka basi eti hapo kachemsha, kachemsha kitu gani sasa? , mimi mwenyewe sometimes huwa nawaza kuwa raisi oneday na wala sijawahi kuwa hata katibu kata, sembuse Zitto bwana?. acheni mentallity ya kukosoakosoa hata kwa vile visivyokosoleka mtaonekana wanoko bure!
kweli pasipo na hoja vioja hutawala!
 
Jamani muache kijana wa watu na ndoto zake zamchana. Kuna watu wengine wanakuwa wazi hata kama nikujimaliza wenyewe. Kila la heri Nyepesi. Tutakupgia kura ukiamua.
 
tujisenti wewe umesema jambo zuri, kwa sababu sasa hivi watu watampima na kumfuatilia Zitto kwa ukaribu zaidi. La maana ni kumpa nafasi ya kufanya makosa na kujifunza na kusonga mbele, tusiwe watu wepesi kutaka aanguke ili tushangilie!!
 
Mwanasiasa hutakiwi kufikiria, achilia mbali kuongelea, uchaguzi wowote zaidi ya ule ulio mbele yako, kwa sababu unaweza usifike huko kwingine.

Kuwania na kujiandaa kuja kuwa Rais kuna "mkao wa kula" wake wa Kisiasa, au political posturing. Huo "mkao wa kula" kuna wakati hauendani na manufaa ya watu unaowatumikia sasa hivi. Muwania Urais inabidi aanze kujenga mifungamano na nguvu fulani. Katika kujenga hizo alliances kiongozi anaweza kuogopa kutetea maslahi ya watu wake wakati zinatishiwa na hizo nguvu ambazo anajenga nazo mifungamano.

Leo hii Zitto hawezi tena kuwaudhi wachangiaji kampeni ambao atawahitaji siku ya kugombea. Wakitaka kuanzisha mradi Kigoma ambao hauwanufaishi watu wake bali wao wenyewe, Zitto atashindwa ataogopa kuwabana.

Nyingine ya hizo nguvu ni vyombo vya habari. Sasa hivi Zitto anaweza kuanza kujikomba komba kwa Waandishi ili wampambe pambe na kumjengea jina mbele ya Umma. Katika kujali sana taswira yako ndio unaanza kuharibu kazi kwa kutaka kuandikwa vizuri magazetini. Na mara nyingi unaishia kudanganya.

Jambo la tatu, Mbunge ambae anaota ndoto za kuwa Rais kiasi cha kusema hivyo hadharani anaonyesha dharau juu ya kazi yake ya Ubunge. Anaonyesha kwamba hana wasi wasi na kushinda Ubunge uchaguzi ujao. Kama alivyosema, YournameisMINE, akitokea mwanasiasa mzuri atawaambia watu wa Kigoma, jamani eeee, mimi Ubunge ndio ndoto yangu. Mkinipa hii kazi ya huyu muwania Urais nitawatumikia kwa moyo wangu wote, na kwa focus ya kazi hii tu. Watu wa Kigoma wanaweza kusema, kweli, sisi hatutaki mtu ambae yuko bize anajenga alliance za kuwania Urais. Ana dharau ya kusema anafikiria kazi nyingine. Ni watoto wadogo ndio wanaulizwa ukiwa mkubwa unataka kuwa Polisi, Mwalimu, Daktari au Rubani? Anajibu Rais!

Nne, Mwanasiasa mjanja hutangazii adui your next move. Wataanza kujiaanda dhidi yako.

Pia, siku ya kutangaza kugombea hakutakuwa ile suprise ambayo inasaidia kwenye kampeni. Amesha ondoa ile suspense tayari. Hii ni misingi ya kwanza ya sayansi ya Siasa!

Ndio maana tunasema Zitto kachemsha vibaya mno hapa!
 
Slaa, Hamad kusimama upinzani


Zitto kuwaunga mkono


Masha, Membe watajwa CCM

MIAKA miwili tu kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kipindi chake cha kwanza mwaka 2010 na huku serikali yake ikiandamwa na kashfa za ufisadi, wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wale wa upinzani wanajipanga kwa nia ya kujiandaa kushika nafasi hiyo, Raia Mwema imefahamishwa.

Habari zinaeleza kwamba kwa sasa baadhi ya wana CCM wanajenga msingi wa kuwawezesha kumrithi Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao lakini wakishindwa, angalau basi kwa uchaguzi mwingine wa 2015; huku wapinzani wao wakipania kuchukua madaraka mwaka 2010, wakitumia kuyumba kwa nchi katika sehemu kubwa ya awamu ya kwanza ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Kwa mujibu wa habari hizo, tayari mazungumzo na mikakati imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kuangalia wanasiasa wanaoweza kushika nafasi ya urais, lakini pia kuwazuia wale ambao wanahofiwa kuweza kuharibu mikakati hiyo.

Wanasiasa kadhaa wakubwa nchini wa sasa, wastaafu na hata wale walioguswa na kashfa, wamekuwa wakitajwa moja kwa moja kujihusisha katika mikakati hiyo ama kwa kupima upepo kama wanaweza kujitokeza wao au kwa kuandaa watu wanaowaunga mkono.

Kwa upande wa upinzani, wanasiasa wapya kabisa wanatajwa kuweza kuibuka na kwa kupishwa na wanasiasa waliogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiwa ni mkakati unaoelezwa kujaribu kuwavuta wapiga kura wengi.

Imeelezwa kwamba waliogombea katika chaguzi za nyuma ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2005, kupitia vyama vya upinzani, wanaweza kuwaunga mkono wagombea watakaouzika katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kusimamishwa kwa nafasi ya urais kwa upande wa upinzani ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Bunge, Hamad Rashid Mohamed, ambao wanaelezwa kuweza kukubaliana mmoja akawa Mgombea Mwenza.

Wanasiasa hao wa upinzani wanaelezwa kusukumwa zaidi na wabunge wenzao pamoja na watu wa kawaida wanaofuatilia mwenendo wa kisiasa nchini hasa kutokana na mchango wao ndani ya Bunge ambalo limebadili hali ya kisiasa nchini kwa kurudisha mwamko wa wabunge na wananchi.

Hamad Rashid amelithibitishia Raia Mwema jana kwamba ameshauriwa kujiandaa kuwania urais mwaka 2015 lakini baadhi wametaka aanze mwaka 2010, akiwataja baadhi ya wabunge waliomshauri, wakiwamo hata wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Ni kweli nina nia ya kuwania urais lakini si wa Zanzibar na kwamba nilijiandaa kwa mwaka 2015, lakini wabunge wenzangu baadhi kutoka CCM wamenishauri nianze kujitokeza mwaka 2010," alisema Hamad, ambaye amewahi kuwa ndani ya Serikali ya Muungano katika wizara za Fedha na baadaye Mambo ya Ndani.

Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alisema sasa ni mapema mno kuzungumzia mambo ya urais kutokana na nchi kuwa katika harakati za kupambana na ufisadi unaoihusisha hata Ikulu yenyewe.

Alisema Dk. Slaa: "Bado tuko mbali tukipambana na ufisadi. Nchi haitaki wanaokimbilia Ikulu. Inataka wenye ujasiri wa kusafisha Ikulu. Ukisema nawe unakimbilia Ikulu, unakuwa unataka ukafanye biashara au ukachote Ikulu. Wakati ukifika, hayo tutayajadili."

Kwingineko kumekuwa na minong'ono kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe pia ana nia ya kugombea kwa tiketi ya chama. Nia ya kuwania urais ya viongozi hao wawili huenda ikawagombanisha na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, aliyesimama mwaka 2005 na ambaye inaaminika angependa asimame tena mwaka 2010.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo za yeye kutajwa kuwania urais, Chache Wangwe alisema, "Ni kweli, ikiwa chama changu kitanipendekeza, nitakua tayari kugombea."

Mkanganyiko mwingine wa Chadema unaweza kutokana na habari kwamba Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, akizungumza na Watanzania walioko Houston, Marekani alikokuwa kwa ziara hivi karibuni, alisema atawaunga mkono Dk. Slaa na Hamad kama mazingira ya kisiasa yatawafikisha watu hao wawili katika kugombea mwaka 2010.

Siku za karibuni zimeshuhudia kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa Chadema na hata kumhusisha Zitto na madai ya kuwa na urafiki wa karibu na Rais Kikwete, kiasi cha Kikwete kutaka kumteua kuwa waziri katika Serikali kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ya Februari mwaka huu.

Zitto ameiambia Raia Mwema wiki katika mahojiano kuwa wakati hapingi kuwa ana ukaribu wa kiasi fulani wa siku nyingi na Rais Kikwete, hakuna wakati alipotaka kuingia katika serikali yake.

"Sijawahi kuombwa na Rais Kikwete kuingia katika serikali. Msimamo wangu siku zote umekuwa ni kutumikia taifa bila kujali itikadi. Hata Rais anajua hili, kwamba siwezi kuhama chama au kwenda kinyume na maamuzi ya chama changu. Kwamba Rais Kikwete ni rafiki yangu, si kweli. Ninafahamiana naye kitambo. Ninajua ananiheshimu sana. Lakini hakuwa chaguo langu la urais wakati wa mchakato wa chama chao na hata katika uchaguzi mkuu," alisema Zitto.

Lakini wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanasema Zitto hajawahi kusikika akimshambulia Rais Kikwete katika hotuba zake na mara kadhaa amekuwa akimsifia katika maamuzi yake mbalimbali ambayo yamepingwa na wenzake. Hata kuingizwa kwake katika Kamati ya Madini ya Jaji Mark Bomani kulizua maswali mengi kutoka kwa wanasiasa wa CCM iliyombana alipoibua hoja ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na wa Upinzani.

Wengi hawaamini maelezo ya Zitto kwani anaonekana ni mtu mwenye kujiandaa kutokana na kuwa kwake na mahusiano ya karibu sana na wastaafu kama Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim, watu ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Alipoulizwa kuhusu hili Zitto alisema kuwa yeye anawaheshimu sana viongozi wastaafu na hupenda kujifunza kutoka kwao na mahusiano yake nao hayana maana ya kutafuta kuungwa mkono.

"Nimekuwa na mahusiano na wazee hawa kama viongozi. Sio hawa tu. Ninazungumza na mzee Kaduma (Ibrahim), mzee Butiku (Joseph), mzee Kimiti (Paul) na mzee Jackson Makweta. Pia ninazungumza sana na Spika Samuel Sitta. Huwezi kusema hawa wote wananiandaa mimi kuwa Rais. Huo ni woga tu wa watu. Ni hulka yangu kuheshimu wakubwa na kujifunza ndiyo maana ukinikuta na Hamad Rashid hutaona mahusiano ya kiubunge. Utaona mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi," anasema Zitto ambaye mwaka jana gazeti moja la kila wiki lilimshutumu kwa kujipendekeza kwa viongozi wakubwa.

Kwa upande wa CCM, habari zinaeleza kwamba tayari makundi yameanza kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2010 na wa 2015 kama Rais Jakaya Kikwete atafanikiwa kushinda patashika ya mwaka 2010 na kuendelea muhula wa pili ambao ni wa mwisho kwa mujibu wa katiba.

Makundi hayo yanajipanga mapema na kwa kuanzia imeelezwa kwamba wanasiasa na wafanyabiashara wanajiandaa kuweza kupata wajumbe wa kutosha katika Mkutano Mkuu wakati wa uchaguzi, wajumbe ambao ndio watakuwa waamuzi wakubwa wa mgombea kutoka chama hicho.

Licha ya kwamba kuna fununu za wagombea wengine kujitokeza kushindana na Rais Kikwete katika kinyanganyiro cha ndani ya CCM mwaka 2010, inaonekana uwezekano wa ushindi ni mdogo kutokana na utamaduni wa CCM kuendeleza muhula wa pili wa Rais aliyeko madarakani utaendelea. Hata hivyo, hali inaweza kubadilika kama Kikwete atakumbwa na dhoruba yoyote kubwa ya kisiasa kabla au kuelekea 2010.

Magazeti kadhaa, hivi karibuni, yalimtaja Profesa Mark Mwandosya kama mgombea anayetajwa kuweza kumkabili Rais Kikwete ikifika mwaka 2010. Mwandosya alikuwamo katika hatua za mwisho za mbio za urais mwaka 2005.

Wengine wanaotajwa kwa sasa kwa upande wa CCM kujiandaa ama kuandaliwa kumrithi Kikwete, iwe 2010 au 2015, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrance Masha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.

My Take:

Wengine wanaweza kuonesha nia yao lakini Zitto asioneshe..!
 
tujisenti wewe umesema jambo zuri, kwa sababu sasa hivi watu watampima na kumfuatilia Zitto kwa ukaribu zaidi. La maana ni kumpa nafasi ya kufanya makosa na kujifunza na kusonga mbele, tusiwe watu wepesi kutaka aanguke ili tushangilie!!

Mkuu,

Hapo Zitto akikusikia hatapenda. Umedokeza kwamba ni kweli amefanya makosa na tumpe nafasi! LOL!

Wamarekani wanasema "you are deep doodle"!

Jamani kubalini, mwenzetu leo kachemsha! LOL!

Hatushangilii, lakini alichofanya leo kwa kweli kinachekesha!

Yani hapa sina mbavu!
 
Back
Top Bottom