Naomba watu wenye ushauri wa busara wanisaidie hili, ni muhimu sana

UKI

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
691
172
NAITWA FRANK (sio jina halisi) nimetokea kumpenda binti Jane(sio jina halisi) tulisha do mara moja tu tukapanga kuchumbiana na tukakubaliana sasa jambo moja limejitokeza nilikuwa simjui ni mtoto wa nani ingawa kumbe mama yake ninamjua vizuri na hii kwa kutomjua mama yake ni kwa sababu alikuwa anasoma mwanza na mimi nilikuwa nafanya kazi zangu shinyanga so sikuwahi kwenda kwao pande za dar, ila dar ndiko wazazi wangu wapo na kumbe ninamjua huyo mama anapokaa dar. siku alipokuwa likizo na mimi nilienda dar na nikaenda mpka kwao dah nilipokaribia nilishtuka sana nikamuambia hapa ninapajua sana na mama huyu namjua namuita kama mama basi tukaongea kwa sana kipindi hicho mama yake hakuepo alikuwa ameenda town basi siku ikapita ikabidi suala la kuwashirikisha ndugu na jamaa kuwa mungu akijalia nitaoa kwa fulani story hii nilimueleza baba yangu wa ubatizo kwani baba yangu alifariki siku nyingi, huwezi amini mzee kwanza alianza kunipongeza kwa sana akasema umechagua penyewe alianza kutiririka kuwa huyo mama yake alikuwa ana mapenzi na baba yangu kwa sana tu (ina maana walikuwa wanado kabla hajampata mama yangu) na mimi nilikuwa sijazaliwa dah nilichoka na akasema hata huyo mama anajua hilo na ndio anakuita kama mtoto wake, nilichoka sikuvumilia nikaenda kutiririka kwa mpenzi wangu akaniambia ngoja na yeye ahakikishe hilo akamueleza mama yake kuhusu hilo mama yake alikuwa happy kwa hilo nae akamueleza kila kitu,tupo bado kwenye uchumba bahati mbaya sasa hivi nimepata kazi huku botswana mkataba miaka miwili ndio narudi now namaliza mwaka bado mwaka mmoja ndio nirudi, swali langu kwa wana JF je hapo sio kwamba namuoa dada yangu? na wazee wa waliokuwa kipindi hicho watasemaje?? naombeni mniondoe haya mawazo kwa kweli na sitaki nionekane muaribifu mtoto wa mtoto wa watu bila sababu maana ni sehemu tunayoheshimiana sana naombeni tafadhali kwa hili mnishauri niendelee au nisiendelee
 
Hapo hakuna shida muoe tu kwani baba yako na huyo mama si walikuwa wanaiba tu!

Usijali sana oa mtoto huyo kama unampenda.hila usicheze na mama.
 
Acha kutafuta sababu za kumuacha huyo binti, kama uko serious fanya search ya mahusiano yote ya nyuma ya baba yako ili ujihakikishie hautotemper na dada zako (kama unavyosema wewe).

Huyo sio dada yako, nakutakia kila kheri.
 
dah hiyo fasihi simulizi ni noumer , anyway history never repeats itself wee umempenda huyo mdada ama? kama umempende muoe basi ili msiendelee na usherati wenu , don't bother about the past bana you can never change it , yesterday have already forgotten you ,if you talk more of the past means you haven;t done anything worth today , afu huyo baba wa ubatizo mkuda tu asa alikwambia hivyo ili iweje , kama umefall kiukweli muoee tu life comes once only afu uje kupata demu cku hizi ishu ohhoo
 
hapo wa kukaa naye na kuzungumza kwa kinagaubaga ni huyo mama wa huyo binti ili athibitisha kuwa huyo binti hakuzaa na baba yako. kwanza mumuulize kama anamfahamu bwana fulani?(yaani baba yako wewe) halafu muelezeni tena lengo lenu na hiyo hofu kuwa msije kuona mtu na dada yake, sasa hapo mumbane awahakikishie na kuthibitisha kuwa huyo binti sio wa kwake ili muendelee na mipango hiyo ya kufunga ndoa...msije ingia katika ndoa halafu kwa kuwa hamkumshirikisha huyo mama mkaja kujua ukweli kuwa huyo binti ni baba mmoja na wewe...kuwa makini sana na muombe sana Mungu wako awafanyie wepesi katika suala hili...kila la kheri Inshaallah!
 
"..............umechagua penyewe........."Nimenukuu maneno ya baba yako wa ubatizo,songa mbele kijana.
 
  • Thanks
Reactions: UKI
Sioni shida mradi kuna uthibitisho kuwa huyo sio dada yako yaani sio zao la kukutana kwa baba na mama yake na binti
Usitafute visingizio kama unampenda muoe huyo dada wala usitake kutafuta kingine
 
jane angekuwa ni dada yko huyo mama asingewapa baraka....
hakuna kinachozuia kumuoa huyo binti....
unless kama humtaki...
 
Usimuoe kabisa sababu umeisha cheza naye kamchezo kabla ya ndoa.

Bora uendelee kujilia tu hapo afu tafuta mwingine wakuoa ambaye hagawi K yake kabla ya ndoa.

Sio hagawi kwako tu hata kwa wengine mana mgawa K akisha igawa K kabla ya ndoa ni hasara kubwa kwa anaye owa.
 
NAITWA FRANK (sio jina halisi) nimetokea kumpenda binti Jane(sio jina halisi) tulisha do mara moja tu tukapanga kuchumbiana na tukakubaliana sasa jambo moja limejitokeza nilikuwa simjui ni mtoto wa nani ingawa kumbe mama yake ninamjua vizuri na hii kwa kutomjua mama yake ni kwa sababu alikuwa anasoma mwanza na mimi nilikuwa nafanya kazi zangu shinyanga so sikuwahi kwenda kwao pande za dar, ila dar ndiko wazazi wangu wapo na kumbe ninamjua huyo mama anapokaa dar. siku alipokuwa likizo na mimi nilienda dar na nikaenda mpka kwao dah nilipokaribia nilishtuka sana nikamuambia hapa ninapajua sana na mama huyu namjua namuita kama mama basi tukaongea kwa sana kipindi hicho mama yake hakuepo alikuwa ameenda town basi siku ikapita ikabidi suala la kuwashirikisha ndugu na jamaa kuwa mungu akijalia nitaoa kwa fulani story hii nilimueleza baba yangu wa ubatizo kwani baba yangu alifariki siku nyingi, huwezi amini mzee kwanza alianza kunipongeza kwa sana akasema umechagua penyewe alianza kutiririka kuwa huyo mama yake alikuwa ana mapenzi na baba yangu kwa sana tu (ina maana walikuwa wanado kabla hajampata mama yangu) na mimi nilikuwa sijazaliwa dah nilichoka na akasema hata huyo mama anajua hilo na ndio anakuita kama mtoto wake, nilichoka sikuvumilia nikaenda kutiririka kwa mpenzi wangu akaniambia ngoja na yeye ahakikishe hilo akamueleza mama yake kuhusu hilo mama yake alikuwa happy kwa hilo nae akamueleza kila kitu,tupo bado kwenye uchumba bahati mbaya sasa hivi nimepata kazi huku botswana mkataba miaka miwili ndio narudi now namaliza mwaka bado mwaka mmoja ndio nirudi, swali langu kwa wana JF je hapo sio kwamba namuoa dada yangu? na wazee wa waliokuwa kipindi hicho watasemaje?? naombeni mniondoe haya mawazo kwa kweli na sitaki nionekane muaribifu mtoto wa mtoto wa watu bila sababu maana ni sehemu tunayoheshimiana sana naombeni tafadhali kwa hili mnishauri niendelee au nisiendelee

Baba yako mlezi kafurahi na mama yake mzazi kafurahi huku wote wakijuwa uhusiano wa baba yako na mkweo mtarajiwa, sasa wewe una hofu nini? Huyo si ndugu yako hata kidogo unless uupange wewe huo undugu. Halafu si mshamaliza kila kitu? Tatizo nini tena? Owaneni tu hakuna ubaya.
 
Nipo salama kabisa tunapambana
namshangaa jamaa hapo juu anaanza visingizio
Sijui huko Botswana kashaona mtu mwingine anatafuta visingizio vya kumuacha huyo dada

inawezekana maana maisha ya sasa upendo/mapenzi yamekuwa ya mashakamashaka au pengine ni hofu baada ya kupata taarifa za wazazi wao.....nafikiri aondoe mashaka/wasi kama anampenda kweli na hataki kumchezea kama alivyosema mwenyewe
 
pole sn mkuu hapo kinachokupa tabu unahisi wewe na father mtakua mmekula poli moja hapana hizo ni hisia tu wewe muoe huyu binti na utapata upendo mkubwa kutoka kwa mama mkwe na familia kwa ujumla.
 
watu wanapenda kutafuta visivyoonekana kabisa, ona sasa umem-zoom sisimizi wee hadi umeanza kumuona tembo.

Haya ngoja akukimbize.
 
Back
Top Bottom