Naomba tenda ya kusafirisha abiria mjini Dar es Salaam.

Kidzude

JF-Expert Member
Jul 14, 2011
4,424
1,361
1. Nitaomba TAZARA na TRL wanikodishe reli zao zote zilizo ndani ya mji wa DSM;
2. Nitawaomba wenye daladala kuanzia Kumi wanunue hisa za kampuni mpya ili kununua mabehewa ya abiria na mizigo;
3. Nitaomba jiji itoe sheria ya hakuna kontena kusafiriswa kwa kutumia maroli na maeneo ya kuwekea makontena yawe nje ya mji kama Kibaha pwani;
4. Nitaomba mwekezaji ajenge reli toka ubungo mpaka Tegeta/boko;
5. Asubuhi kuanzia saa kumi na moja mpaka saa mbili usafiri wa treni utafanya kazi na kuanzia saa tisa mpaka saa moja usiku.
6. Nitaomba kituo kimoja pale karibu na quality plaza kingine Tazara kingine tabata dampo, airport,banana, gongolamoto , pugu kajiungeni ubungo maziwa ambapo kutakuwa na daladala za kuanzia maeneo hayo;
7. Itapunguza gharama ya mafuta na usumbufu ambapo uchumi utaimarika kwa pesa ya mafuta kutumika kwa ajili ya shughuli nyingine.
Kama una mawazo zaidi karibu.
 
ningeanzisha route kwa njia ya bahari kuanzia Bagamoyo mpaka kivukoni kupitia tegeta, kawe, msasani, oysterbay n.k..
 
huu mradi wa Dart ningeupiga marufuku kwa sababu hautekelezeki..
 
All the Best...ntakuunga mkono soon ngoja kwanza nilipe ada za watoto
 
Hivi hii ilikiwa kabla au baada ya treni ya mwakyembe. Basi jf naiheshimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom